Pages

11 October 2014

HATIMAYE CHAMA CHA WAJANE KIMEANZISHWA TANZANIA

Chama hicho kijulikanacho kwa jina la Chama cha Wajane Tanzania 
(Tanzania Widows Association - TAWIA)

lengo lake kuu ni kuwaweka wajane pamoja, ili kutambuana, kufahamiana, kujua changamoto mbalimbali anazopitia mjane, na kutafuta ufumbuzi wa kutatua changamoto hizo.  Ikiwemo kusomesha watoto, elimu ya sheria, afya, saikologia, biashara na ujasiriamali. Vilevile chama kitajihusisha na kutoa elimu kwa jamii juu ya mjane, iwatambue wajane, kuwapenda, kuwathamini na kuwasaidia kwa namna moja ama nyingine, pia kujitoa kwa hali na mali kusaidia kupambana na changamoto anazopitia mjane.
                                     Wajane wkieleza changamoto zinazowakabili

                                       Msaada wa nguo zilizotolewa na mfadhili


Pia chama kitasimamia sheria inayotetea haki za mjane Tanzania, ikiwemo hati ya mirathi na usimamizi wa mali za familia baada ya kifo cha mume wa mjane.  Hivyo chama hiki kitarejesha matumaini mapya kwa mjane, na wajane watarajiwa.  Pia kwa namna moja au nyingine, kujihusiha na haki za mgane na watoto walioachwa na wazazi (yatima).

Zipo changamoto nyingi zinazotokea pale mwanamke anapofiwa na mume wake. Huo kwake ndio wakati anaohitaji sana kupendwa na kutiwa moyo na jamii iliyobaki. Lakini kinyume chake, umekuwa ndio wakati wa kutengwa, kunyanyaswa na ndugu, jamaa na marafiki waliokuwa wakaribu kabisa kabla ya kifo cha mume wake. Ikiwa ni pamoja na  kunyang’anywa mali zilizokuwa za familia, pamoja na kufukuzwa katika nyumba aliyokuwa akiishi na mume wake.  Mjane amekuwa mtu wa kuonewa na kuumizwa katika jamii, wengi wamenyanyasika kijinsia pamoja na kuathiriwa kabisa kisaikologia, na hata wengine kupoteza maisha, muda mfupi baada ya kufiwa na mume wake kutokana na mkandamizo na msongo wa mawazo.

Ikumbukwe kuwa Nchi mbalimbali duniani limeanzisha vyama vya aina hii. Kwasababu ya kuona changamoto anazopitia mjane, ndio maana tarehe 22/12/2010, Umoja wa Mataifa uliridhia kila ifikapo tarehe 23 mwezi wa sita, siku hiyo kuadhimishwa kama siku ya wajane duniani (Iternational Widows Day).

Hapa chini ni ujumbe wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa kuhusu siku ya wajane duniani:



Message from Ban Ki-moon, Secretary-General, United Nations
On International Widows’ Day, 23 June 2013

We commemorate the third International Widows’ Day for the hundreds of millions of women in the world who suffer exploitation, deprivation and exclusion when their husbands die. Today, we call for stronger action to end widespread discrimination against widows because no woman should lose her rights when she loses her husband.

Every human being has the right to live in dignity with equal rights and opportunities to realize their potential. Yet women and girls continue to face gender-based violence and discrimination, and this is the case for many widows around the world.

Many widows are denied their rights—from being evicted from their homes because they cannot inherit property or the land they live on to being forced into exploitative and risky sex work to support themselves and their families because they have no income and nowhere else to turn.
An estimated 115 million widows are currently living in poverty, and 81 million have suffered physical abuse, some from members of their own family. Adolescent girls, many of whom have been married off too early to much older men, are at great risk with very little protection.
It is our collective duty to ensure that widows of all ages and their children are treated as full and equal citizens, with equal opportunities for education, participation in the economy and decision-making, and a healthy life free of violence and discrimination.

We must recognize the role of widows as not only victims of poverty, conflict and natural disasters but as peace-builders and re-builders of families, communities and societies. National laws and policies that protect and promote the rights of widows should be guided by the Convention on the Elimination of Discrimination against Women and the Convention of the Rights of the Child.

UN Women works in partnership with governments and with the private sector, to support the economic empowerment of widows in Asia, Africa and Latin America.

Moja ya mambo ambayo chama kimeanza kuyatekeleza mapema tu baada ya kusaidiwa kupata ofisi ya muda, ni mafunzo mbalimbali yanayotolewa bure kwa wajane na watoto wao. 

Mafunzo hayo ni pamoja na kujifunza kompyuta, ushonaji, lugha, mapishi, ujasiriamali n.k. Mafunzo hayo yanatolewa bure hapohapo ofisini. Pia wajane wenye mahitaji madogomadogo kama mavazi na chakula wamekuwa wakisaidika mara moja. Pia mkakati wa watoto wa wajane kupata elimu bora ni moja ya malengo ya chama.



Chama kinawashukuru watu ambao wamejiguswa na changamoto za ujane na kukubali kujitolea kusaidia. Pia uongozi wa chama unawashukuru wale wote wanaoendelea kutoa ushauri wao ili kukiboresha, pamoja na wale wote wanaoendelea kupongeza wazo hili la kuanzisha Chama cha Wajane Tanzania.

Ili kufahamu mengi kuhusu Chama cha Wajane Tanzania, au labda ungependa kutoa mchango wako wa hali na mali, ushauri, au wewe ni mjane, mgane, mtoto wa mjane au una ndugu, jamaa na rafiki wa aina hii, unaweza kuwasiliana na uongozi kwa simu namba 0716 214 680/0754 366 530, pia unaweza ukatembelea ukurasa wa facebook wenye jina “Tanzania Widows Association”

Umoja wetu ndio mafanikio yetu!

 


No comments:

Post a Comment