Mwl. John Shabani akitoa darasa
kwa watoto wa Shalom Orphanage
Nilitembelea
kituo cha Shalom Orphanage Centre mwaka 2014, hakika nilijifunza mambo mengi,
huku nikijaribu kuona tofauti iliopo kati ya vituo mbalimbali vya watoto yatima
nilivyowahi kuvitembelea Tanzania na nje ya mipaka yetu.
Mlezi wa
kituo hicho Mama Warra Nnko, kwanza ni Mjane, pili baada ya kuguswa na haili ya
maisha ya watoto yatima, aliamua kusahau hali yake ya ujane na kujiona kuwa
anayo nafasi kubwa ya kufanya lolote awezalo ili kuyakomboa maisha ya mtoto
yatima Tanzania. Ndipo Mama huyo alipoamua kutoka katika Jiji la Arusha, huku
akiacha makazi yake mazuri na kujielekeza huko karatu, ni takriba kilomita 160
kutoka Jiji la Arusha. Tangu mwaka 2004 Mama huyo akilea watoto yatima
katikamakazi aliyofanikiwa kuyapata huko karatu. Ukifika Shalom Orphanage Centre
hakika huwezi kuyazuia machozi yako, hasa bale unapoona zaidi ya watoto 60, wengine
wachanga, wengine wenye ulemavu, wengine walioathirika na ukimwi, wote hao
humwita Mama warra jina moja tu (Mama)
Ikumbukwe,
jirani na wilaya ya karatu ndiko kunakoongoza kwa vivutio vya utalii
Tanzanzania, hivyo, kwasababu ya habari zilizoeneo kote duniani kuhusu kituo
hicho, watalii na wasamaria wengi wanaotembelea Ngorongoro, Serengeti, n.k,
mara nyingi pia hukitembelea kituo hicho.
Niliposikia
habari za kituo hicho, nikiwa mwana harakati wa haki za Binadamu, nilifunga
safari na kutembelea shalom Orphanage, nikajisikia kunzisha program ya kuibua
vipaji hasa vya uimbaji. Kwa kuanzia, tayari mapema mwaka huu wa 2015, tumerekodi
Albam ya kwanza na maandalizi ya mkanda wa video yanaendelea. Naamini kwa
kupitia ujumbe uliomo ndani ya nyimbo hizi utagusa mioyo ya watu wengi ndani na
nje ya nchi. Lakini pia mkanda wa video utakiunganisha kituo na dunia, kwani
nyimbo hizo zitatafsiriwa kwa lugha ya kingereza. Pia nyimbo hizi zitawaingizia
kipato.
Baadhi ya
nyimbo zilizomo katika Albam hiyo ni: Mtoto
wa mwenzio ni wako, Sitaitwa Yatima tena, Nani kama Mama, Baba wa Yatima na
Tanzania.
Endelea kuombea kituo hicho, na pia unaweza ukatoa
mchango wako wa hali na mali ili kuwabariki watoto hao.
No comments:
Post a Comment