Pages

2 March 2015

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MH LAZARO NAYANDU AWA MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI WA ALBAM MPYA YA CHRISTINA SHUSHO-DAR ES SALAAM




              Waziri na Nyarandu sambamba na Christina Shusho, wakimtukuza Mungu

Kazi ya Bwana ilifanyika katika viwanja vya kanisa la Pentekoste Tabata Kisiwa jijini Dar es Salaam Tanzania na kuhudhuriwa na watu wengi sana. Tamasha la uzinduzi wa albamu ya mtumishi wa Mungu Christina Shusho lilianza saa nane mchana siku ya Jumapili 02/03/2015. Watu walikaa pamoja wakifurahia uwepo wa Mungu uliotanda eneo hilo. Mungu alionekana akiwa mlinzi kwa wana wa Mungu waliofika siku hiyo. 

Mgeni Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lozaro Nyarandu aliweza kuserebuka na kuacha watu wakiwa wameachama mdomo wazi wakishangaa kuona hata viongozi wa serikali wanaweza kuserebuka na kumtukuza Mungu. Hii inatokana na vile nyimbo za mwadada huyu kuwa na kibali kwa kila mtu na upako alionao. 

Mh. Nyarandu ni waziri ambaye amekuwa mstari wa mbele sana katika kuhakikisha kazi ya Mungu inasonga mbele, amekuwa mwepesi pale anapoombwa kushiriki katika sherehe na matamasha mbalimbali ya dini. Uwepo wa Mh. Nyarandu uliwafanya watu kubarikiwa sana kutokana na unyenyekevu wake na upole mbele za watu. 

Mh. Nyarandu hakijizuia na aliweza kutoa dola zake mfukoni na kumponeza Christina Shusho wakati akiimba, hii inatokana na kuguswa na uimbaji wake.




 Huu ndio umati wa watu waliojitokeza katika tamasha la shusho

Christina Shusho ni mwimbaji anayefanya kazi kwa bidii kuhakikisha kazi ya Mungu inakwenda mbele ikiwa katika viwango vya kimataifa machoni pa watu na mbele za Mungu.

John Shabani na team nzima ya blogu hii tunasema
" Mungu azidi kukuinua na kukubariki, ili uwe baraka kwa wengi".
 

No comments:

Post a Comment