Pages

4 June 2015

JOHN SHABANI AUNGANA NA WANAHARAKATI WENGINE WA HAKI ZA BINADAMU KUREJESHA MATUMAINI KWA WAJANE


Baadhi ya wanachama cha wajane Tanzania (Tanzania Widows Association) wakiongozwa na mwenyekiti wa chama Bi Rose Sarwatt pamoja na katibu mkuu John Shabani, wakiwa miongoni mwa waalikwa katika maadhimisho ya miaka 25 ya chama cha wanawake wanasheria Tanzania - TAWLA 



Huwezi kuitwa mtu aliyefanikiwa ikiwa watu waliokuzunguka, ndugu, jamaa, marafiki na jamii kwa ujumla wanaishi katika mazingira magumu.

MAISHA YA MJANE NA YATIMA WA KIJIJINI




Hivyo pamoja na mkakati wa John Shabani wa kujitolea kuwatembelea waatu wanaoishi katika mazingira magumu na kutafuta namna ya kuwasaidia, mwanaharakati wa kujtolea wa haki za binadumu John Shabani; safari hii ameungana na mwanamama mwenye uchungu wa kutetea haki za mjane Bi Rose Sarwatt na kuanzisha chama cha wajane Tanzania.


 Chama cha Wajane Tanzania (Tanzania Widows Association) chenye usajili na S.A. 19708, ni chama kilichoanzishwa rasmi mnamo mwaka 2014, kikiwa na lengo la kuwaweka wajane pamoja, ili kutambuana, kufahamiana, kujua changamoto mbalimbali anazopitia mjane, na kutafuta ufumbuzi wa kutatua changamoto hizo.  Ikiwemo kusomesha watoto, elimu ya sheria, afya, saikologia, biashara na ujasiriamali.   

Vilevile chama kinajihusisha na kutoa elimu kwa jamii juu ya mjane, iwatambue wajane, kuwapenda, kuwathamini na kuwasaidia kwa namna moja ama nyingine, pia kujitoa kwa hali na mali kusaidia kupambana na changamoto anazopitia mjane.  Pia chama kinasimamia sheria inayotetea haki za mjane Tanzania, ikiwemo hati ya mirathi na usimamizi wa mali za familia baada ya kifo cha mume wa mjane.  Hivyo chama hiki kitarejesha matumaini mapya kwa mjane, na wajane watarajiwa.  Pia kwa namna moja au nyingine, kujihusiha na haki za mgane na watoto walioachwa na wazazi (yatima).


Pamoja na kujitahidi  kwa uwezo mdogo tulionao, tumeweza kuzunguka mikoa kadhaa ya ya Tanzania na hasa vijijini na kujifunza hali halisi ya wajane na watoto yatima.Tumegundua asilimia kubwa ya Wajane ni wale wenye kipato cha chini sana na wengine wanaishi kwa kutegemea misaada ya kuwasaidia kujikimu kimaisha. Misaada hiyo ni kama chakula, mavazi, kodi za nyumba ukiachilia mbali ada za watoto.
Wana TAWIA baada ya kuhudhuria semina zinazoendelea katika ukumbi wa TGNP, mada ikiwa ni pamoja na kuingalia sheria inayopendekezwa ikiwa inavifungu vinavyomsaidia mjane na mwanamke kwa ujumla


 Hakika wajane wanahitaji kuwezeshwa kwa hali na mali ili waingie katika hatua ya kujishughulisha au uzalishaji.

Wanachohitaji  wajane ni  imparting skills and education na baada ya hapo ni kuwezeshwa sasa ili kwaanzishe uzalishaji/biashara ndogondogo za mtu mmoja binafsi au vikundi
Mkurugenzi wa kituo cha msaa wa sheria na haki za binadamu, Bi Heleje Kijo Bisimba, akiwa mgeni rasmi katika moja ya makongamano ya chama cha wajane




Kwa hapa kwetu tumegundua biashara muhimu ni kama zile za utengenezaji juice, masuala ya lishe au usindikaji wa chakula, kilimo kama cha, miogo, viazi vitamu ambayo huchukua miezi mitatu hadi mine, tayari kwa matumizi na pia huhitajika kwa mahitai ya kila siku. Pia kilimo cha mboga mboga kama matembele na mchicha ambavyo huchukua wiki mbili au tatu. Lakini pia kilimo kama cha mahindi na mchele kwa kilimo cha kumwagilizia ambavyo huchukua miezi 4 hadi tano. Pia wajane wakizipata mashine za kusindika vifaranga vya kuku pamoja na mayai ambayo huchukua muda wa wiki mbili na mashine zake ni  rahisi kuzipata hapa hapa nchini kwenye viwanda vya SIDO (Small Industries Development Organization), mafunzo mengine ni ya ushonaji na kudarizi ambayo tayari tunaye mjane mwenye uwezo mkubwa wa kutengeneza nguo za maofisini, taasisi na za kawaida pamoa na mashuka  na vitambaa vya kudarizi vya kiafrika.

Mahitaji mengine au mafunzo mengine ni masuala ya Agriculture, Livestock Farming, Fish Farming, basic Computer courses, ufugaji, ushonaji na mapishi na mengine utakayoona yanafaa kulingana na uzoefu wako.


Upande wa afya ambayo ni jambo la msingi kwa maisha ya binadamu, tumekuwa na mawasiliano na taasisi ya MEDA TANZANIA pamoja na BETTER LIFE HEALTH SERVICES ili kuhakikisha wajane wanakua na afya bora.


Upande wa sheria tunawashukuru TAWLA kwa kujitolea kutoa mafunzo ya msaada wa sheria (Para Legal) kwa kikosi cha watu 24 kutoka TAWIA, mafunzo hayo ni ya miezi sita, na baadaye kikosi hicho kitasaidia masuala mbalimbali ya kisheria kwa wajane na jamii kwa ujumla. Mafunzo yaliyopewa kipaumbele ni ya sheria ya ardhi, sheria ya ndoa, talaka au kuachana, sheria ya watoto n.k.

Tuna karibisha wadau mbalimbali wenye moyo wa kuwasaidia wajane na watoto yatima, tushirikiane kwa hali na mali kurejesha matumaini ya maje. Kumbuka kwambawajane ni moja ya kundi la watu ambao Mungu anawaheshimu sana. 

Tunakaribisha mchango wako wa hali na mali ili kuwasaidia wajane Tanzania.

Mawasiliano

CHAMA CHA WAJANE TANZANIA
“Tanzania Widows Association”

P.O.Box 33476,
Dar es salaam
Simu: +255 754 366 530 – Mwenyekiti
  +255 713 778 778 – Katibu
E-mail: widowstz@gmail.com
FACEBOOK: Widows Tanzania
  TWITTER: @TanzaniaWidows
 

No comments:

Post a Comment