Anayeonekana kwenye picha hii ni John Pazia, kijana mwenye vipaji vingi, mcha Mungu na mwenye ndoto na maono makubwa
MFAHAMU MTANGAZAJI JOHN
PAZIA
John Pazia mwenye makazi yake mkoani Arusha ni mmoja baadhi kati
ya watangazaji wenye ushawishi mkubwa Tanzania, na ameinua muziki injili kwa
upande wa kaskazini kwa asilimia kubwa na mchango wake umeonekana. Amekuwa
sauti ya wengi waliokuwa na kilio cha kuinuka na kutambulika. Ni mtangazaji wa
kituo cha radio Radio Habari Maalum kilichopo Jijini Arusha.
MTAZAMO WA JOHN PAZIA KWA MWAKA JANA
2015 NA KINACHOTAKIWA MWAKA HUU
“Mwaka 2015 ulikuwa ni mwaka mzuri
ambao ulileta changamoto kwakuwa kuna waimbaji waliofanya kazi nzuri na kuleta
changamoto kwa waimbaji wengine, video pia audio na matamasha pia” Alisema John
Pazia.
“Pia ulikuwa ni mwaka ambao
umewafanya baadhi ya waimbaji wa Injili kujiingiza katika siasa na kuwagawa
mashabiki wa muziki wa injili kwa kuingia na kuwaimbia wanasiasa na kuleta
gumzo kwa watu na pia gumzo kwa waimbaji wenzao, huenda ikawa walikuwa na
malengo yao siwahukumu” na “pia swala la ngazi maana ya makundi ya waimbaji
wana mashabiki fulani kama wa Sebene na Hip Hop walikuwa hawachangamani lakini
hivi sasa wengi wameanza kuelewa, pia waimbaji wa muziki wa injili wamekuwa
karibu wao kwa wao tofauti na kipindi cha nyuma na pia hata kushirikiana katika
nyimbo zao.
Pia Wachungaji wameanza kutambua
huduma hizi na kukubaliana na kile hususani vijana na kuwaruhusu kumtumikia
Mungu katika madhehebu tofauti tofauti na sehemu nyingine nyingi za huduma”.
Pia kuna waimbaji waliokurupuka na kufanya kazi mbovu na kutokukubali ushauri,
na wengine hawana ushirika mzuri na watangazaji, wengine hutafuta watangazaji wakiwa
na shida tu bila hivyo hawana ushirika wa zaidi, wengine hawakubali kuambiwa
ukweli wakikosea na hawapendi kuthubutu pia kama kushiriki katika tuzo, pia
wengine hawapendi kujitangaza kimitandao, vituo tofauti tofautio vya habari,
pia uongozi (management) husema Bwana ataonekana huku wamebweteka, ni jambo la
kuthubutu.
Waimbaji wasitoe nyimbo ovyo bila
malengo , watazame mbele na pia hii huchangia kutofanya kazi nzuri na zenye
viwango, pia video nzuri na zenye viwango.
Pia waimbaji kuwa na ushirika mzuri
na makanisa na Baba zao wa kiroho, pia kutodharau waimbaji wadogo ama wenzao
lakini ni vyema kuwashauri kwa kutumia njia nzuri ili tuweze kujengana.
Swala muhimu sana ambalo ni vyema
watu waelewe si kama wanavyofikiria, uimbaji wa injili ni swala linaloanzia
rohoni, na ukitaka wimbo wako usikike na kuongea na mioyo ya watu na
kuponya walioumia, wanaohitaji kutiwa moyo. Usifanye kazi kama kuhudumia watu
ila imguse kwanza Mungu na yawe yatokayo kwa Mungu, jenga mahusiano mazuri na
Mungu, Mungu hutoa ili awaguse watu wengine kupitia uimbaji.
1.
Ushirika na Mungu, kuomba sana kuliko kuimba sana. Unaweza kutoa nyimbo nyingi
lakini zisiguse watu kabisa, kama kiukopi nyimbo za duniani na kuweka maneno ya
Mungu kama Mungu haweza kukupa ufunuo.
2.
Waweza kutoa nyimbo nyingi lakini zisiwe na uwepo wa Mungu na Roho Mtakatifu
asionekane . Tunza uhusiano na Mungu wako na pia maneno uyazungumzayo kila
wakati.
Malengo ya mwaka 2016:
“Malengo ni kuendelea kuusukuma
muziki wa Injili na kuwasaidia waimbaji kupitia tasnia yangu, kuwatangazia kazi
zao na pia kuwashauri. Haya yote nitayafanya na walio tayari kupokea na kutoa
panapostahili, kwakuwa wote tunaujenga mwili wa Kristo. Nitatumia taaluma na
kazi yangu kitaifa na kimataifa, nahitaji tu ushirikiano wao” alisema JOHN
Pazia.
No comments:
Post a Comment