Kuna uwekezaji mmoja unaolipa kuliko uwekezaji mwingine wowote. Ukiwekeza vizuri kwenye uwekezaji huu, lazima uwekezaji mwingine utalipa tu. Ukishindwa kuwekeza vizuri kwenye uwekezaji huu, hautafika mbali kwenye safari ya mafanikio.

Uwekezaji huu ni kuwekeza kwako wewe
binafsi. Ni kujitengeneza wewe binafsi. Kuitengeneza akili yako, mwili wako,
roho yako, hisia na mahusiano yako na wengine. Ili uwe na mafanikio makubwa
lazima uwekeze kwako binafsi kwanza.
Kuna maeneo manne ambayo unahitaji
kuyafanyia kazi kila siku ili uwe na ufanisi mkubwa kwenye yale unayofanya.
Haya hapa ni maeneo makuu manne unayotakiwa kuwekeza;
- Eneo la kwanza ni afya ya kiroho au imani.
Hili ni eneo lenye umuhimu sana kwako na ni eneo linalokupa maana halisi ya maisha yako. Kila siku ni lazima ukue kiroho, kila siku ni lazima uhakikishe unakua imani yako. Kila siku unahitaji kujenga imani yako, ili maisha yako yawe na maana. Kila siku hakikisha unaungana na chanzo chako cha kiroho (kwa maombi, sala au tajuhudi (meditation)) na kuwa mtu wa kushukuru kwa kila jambo.

- Eneo la pili ni mwili.
Bila kuwa na afya bora ya mwili wako, ni ngumu sana kutekeleza majukumu mengine kwenye maisha yako. Kama mwili wako unasumbua hata mafanikio yako huwezi kabisa kuyafurahia.
Bila kuwa na afya bora ya mwili wako, ni ngumu sana kutekeleza majukumu mengine kwenye maisha yako. Kama mwili wako unasumbua hata mafanikio yako huwezi kabisa kuyafurahia.
Ni lazima utunze sana mwili wako.
Hakikisha unakula chakula bora na kufanya mazoezi ili kuujenga mwili wako. Pata
muda wa kutosha wa kupumzika pia. Usingangane kutafuta mafanikio kwa kujitesa
sana mwili wako. Hakuna maana ya kupata mafanikio, alafu mwisho wa siku unakuwa
mgonjwa na unashindwa kufurahia mafanikio yako. Wekeza kwa kutunza mwili wako.
- Eneo la tatu ni akili.
Ili uwe na ufanisi mkubwa, unahitaji kutunza afya yako ya akili. Afya yako ya akili inatunzwa kwa kuongeza maarifa kila siku. Soma vitabu, kati ya vitabu vizuri vya kuvisoma ni pamoja na kile nilichokiandika mimi mwenyewe, kitafute au toa oda nitakutumia. Kinaitwa "MARUFUKU KUKATA TAMAA". sikiliza kanda za sauti kukuhamsisha na kukufundisha, hudhuria semina na kuna muda inabidi urudi darasani kusoma. Kuandika pia ni njia nzuri ya kuwekeza kwenye akili yako, kuwa na sehemu ya kuandika kila siku. Kuandika kunaifanya akili yako ifikiri vizuri.

Je Unailisha Nafsi Yako Kama
Unavyoulisha Mwili Wako?
Watu wengi tunakula mara tatu kwa
siku yaani kifungua kinywa, chakula cha mchana na chakula cha usiku. Ukweli
tunahitaji chakula bora ili mili yetu iweze kufanya kazi. Mili yetu inapokuwa
na njaa, ni sharti kuipa chakula.
Kwenye kuipa mili yetu chakula uwa
hatuko nje ya muda. Tumekuwa ni wazuri sana kufata ratiba yetu ya kula,
inapofika muda fulani tunajua kabisa tunatakiwa kula, kwa hiyo tunatafuta
chakula tunakula.
Mili yetu tunaijali sana, lakini
nataka nikuulize swali moja; je unailisha nafsi yako kama unavyoulisha mwili
wako? Ukweli watu wengi hatuzilishi nafsi zetu chakula. Rafiki kama unakula
mara tatu kwa siku, je ni mara ngapi kwa siku unailisha akili yako?
Inawezekana unatumia zaidi ya elfu
kumi kwa siku kwa ajili ya chakula cha mwili. Je unatumia shilingi ngapi kwa
siku kwa ajili ya chakula cha nafsi yako?
Rafiki, naamini ulishawai kusikia
mtu anasema kuliko kupoteza shilingi elfu tano kwa ajili ya kitabu ni bora hiyo
pesa niende nikale chakula. Hili limenitokea mara nyingi ninapohamasisha watu
kununua kitabu changu. Watu wengine kununua kitabu kwa ajili ya nafsi yake ni
kupoteza pesa, anaona kama anaibiwa vile. Naamini sio wewe rafiki.
Watu wengi waliofanikiwa uwa tunaona
kama ni wenye bahati tu. Lakini ukifatilia unakuja kujua watu hawa
hawajafanikiwa kwa bahati tu. Moja ya kitu ambacho wanakifanya kila siku na
kinawafanya wazidi kufanikiwa ni kuzilisha nafsi zao. Yaani kila siku lazima
aingize kitu kipya kwenye nafsi yake.
Punguza muda mwingi unaoperuzi
kwenye mitandao ya kijamii, kusikiliza redio na kuangalaia Tv. Na tumia muda
huo kuwekeza kwenye akili yako. Usipokuwa makini na mambo unayoingiza kwenye
akili yako, dunia itakuendesha.
- Eneo la mwisho ni hisia na mahusiano.
Hapa unahitaji kuhakikisha mahusino yako na hisia zako zinaenda sawa. Unapojenga mahusiano bora, yanajenga hisia bora pia. Hakikisha unaboresha mahusiano yako na watu wako wa karibu na watu wengine wanaokuzunguka. Hakuna maana ya kubanana na mafanikio, ukakosa muda wa kutosha wa kuwa na familia yako na watu wako wa karibu. Hakikisha unapata muda wa kutosha wa kuwa na watu wako karibu. Hii itajenga hisia zako.

Mambo Mawili (2) Yanayojenga
Mahusiano Bora:
Kwa sababu mahusiano yetu yana
mchango mkubwa sana kwenye mafanikio yetu, leo naomba tujifunze/ tujikumbushe
mambo mawili ambayo yatatusaidia kujenga mahusiano bora kati yetu na watu
wengine. Haya hapa ni mambo mawili yanayojenga mahusiano yetu:
Upendo
Bila upendo mahusiano yetu lazima
yatapoa. Bila upendo mahusiano yetu na wengine yanapoteza thamani. Ni wajibu
wako rafiki yangu kuwapenda wengine kama unavyojipenda wewe. Ipende familia
yako, mpende bosi wako, wapende wafanyakazi wenzako, wapende wateja wako,
wapende wafanyabiashara wenzako.
Kama binadamu kila mtu ana mapungufu
yake. Kama binadamu kuna kipindi tunakosea. Upendo unapokuwepo ni rahisi sana
kwa watu kusameheana pale wapokoseana. Upendo unapokuwepo unaficha madhaifu
yetu pia na kutufanya tuishi kwa furaha na amani na watu wengine.
Upendo unawafanya watu wawe karibu
zaidi. Kinyume cha upendo ni chuki. Chuki inabomoa, upendo unajenga. Chuki
inaleta kugombona, upendo unapatanisha. Ili tufanikiwe tunahitaji kupendana
bila kuangalia dini zetu, kabila zetu, hata rangi zetu. Tumeumbwa na Mungu kwa
kutegemeana ni jukumu letu kupendana na sio kubaguana.
Kuheshimiana
Tunapaswa kuwaheshimu wengine. Mme
muheshimu mke na mke muheshimu mme. Watoto wawaheshimu wazazi na wazazi
wawaheshimu wanao. Kila mtu anapenda kuheshimiwa, kila mtu anapenda kuona
anapewa heshima kwa vile alivyo na kwa mchango anaotoa.
Hayo ndio maeneo manne makubwa
unayohitaji kuwekeza. Huu ni uwekezaji unaolipa kuliko uwekeza mwingine wowote.
Ukiwekeza vizuri, matunda yake sio haba na hii itajenga sana ufanisi wako.
Tafakari njema rafiki yangu. Tuko
pamoja.
No comments:
Post a Comment