Kwa masomo zaidi tembelea kurasa
zangu za facebook:
-
JOHN SHABANI & SINGING MINISTRY
-
Dar es salaam Singing Lessons & Music
Academy
Nyimbo ni aina ya sanaa katika
fasihi ambayo hutumia lugha teule, sauti na kiimbo maalum.
Aghalabu nyimbo hutumia ala za mziki
kama vile ngoma. Nyimbo zinaweza kuimbwa na mtu mmoja au zaidi. Wimbo
hugawanywa katika beti na mishororo. Nyimbo nyingi huwa na kiitikio au
mstari ambao hurudiwa rudiwa.
Sifa
za Nyimbo
- Hutumia kiimbo au sauti maalum
- Huweza kuendamana na ala za muziki
- Huimbwa na mtu mmoja au watu wengi; wakati mwingine nyimbo huimbwa kwa kupokezanwa.
- Hutumia lugha ya mkato
- Hurudiarudia (kukariri) maneno ili kusisitiza ujumbe katika wimbo
Umuhimu
wa Nyimbo katika Fasihi Simulizi
- Kuburudisha
- Kuelimisha, kufunza, kuonya, kuelekeza
- Kuliwaza
- Kusifia kitu au mtu katika jamii
- Kuunganisha jamii
- Kudumisha/kuhifadhi tamaduni za jamii
- Kukuza talanta na sanaa katika jamii
- Hutumika katika mbinu nyingine za fasihi kama vile hadithi
Vipera/Aina
za Nyimbo
Kulingana
na Muundo:
Kulingana
na Ujumbe/Maudhui:
Nyimbo
za Ndoa
Nyimbo za harusi huimbiwa bwana na
bibi harusi kuwapongeza na kuwapa heko kwa kufunga ndoa yao. Aidha nyimbo hizi
huwapa wawili hao mawaidha ya kutunza familia na watoto wao ili waishi pamoja.
Nyimbo
za Jandoni/Tohara
huimbwa na vijana wanapopashwa
tohara. Nyimbo hizi huonyesha ushujaa, na kuashiria kutoka kwamba anayetahiriwa
amekuwa mtu mzima sasa.
Hodiya/Wawe
Hizi ni nyimbo ambazo huimbwa na
watu wanapofanya kazi ili kuwatia bidii wafanye kazi bila kuhisi machofu.
Kimai
Nyimbo za Mabaharia - Hizi ni nyimbo
za wanabahari wanaposafiri baharini.
Nyimbo
za Mazishi/Huzuni/Simanzi
Hizi ni nyimbo za kuliwaza na kuwapa
pole walioachwa na marehemu. Nyimbo hizi huwapa matumaini waombolezaji.
Nyimbo
za Kidini
Hizi ni nyimbo ambazo huimbwa
kumsifia Mungu, kuomba au kutoa mafunzo ya kidini.
Nyimbo
za Kisiasa
Hizi ni nyimbo za kuwasifia viongozi
wa kisiasa
Nyimbo
za Kizalendo
Nyimbo za huonyesha uzalendo kwa
kusifia taifa/nchi
Nyimbo
za Mapenzi
Katika nyimbo za mapenzi, mwimbaji
huimba kwa kumsifia mpenzi wake hasa kwa urembo na tabia zake
JOHN SHABANI & SINGING MINISTRY
Dar es salaam Singing Lessons & Music Academy
No comments:
Post a Comment