WOKOVU SIYO KUWA "ANTI SOCIAL" (KUTO KUJICHANGANYA NA WATU)
Mara nyingi, mahusiano yanayopelekea uchumba hadi ndoa, huanzia katika hutua ya URAFIKI. urafiki hujengwa kwa watu kuwa pamoja, kubadilishana mawazo, kula pamoja, kucheza na kufanya mambo mengi pamoja.
WARAKA WA PILI WA ZAKAYO KWA
"BACHELORETTES" (Wanawake/Wasichana ambao hawajaingia kwenye ndoa na
walio katika mchakato wa kupata wenzi wa maisha).
Utafiti unaonyesha kwamba wadada wengi “WAPENDWA” wanashindwa katika
kipengele cha URAFIKI. Wapo wanaodhania kuwa KIROHO ni kuwa full-time kwenye
maombi; yani hakuna muda wa kucheka na kufurahi, hakuna michezo, wala kuzoeana
na WANAUME. Huu ni msimamo potofu. Yani unakuta MDADA yeye full-time anongelea
maombi, mkesha, ushuhudiaji, na ibada. Hana muda wa kuzungumza mambo ya kawaida
yanayohusu maisha na mahusiano hata na vijana wa kanisani.
Ni kweli ni vizuri kuwa KIROHO; lakini kuwa kiroho isiwe sababu ya
kuto-jichanganya na watu na kujenga mahusiano. Kuna baadhi WADADA WAPENDWA
wanawaona WANAUME wote ni watenda dhambi. Yani mtu akitaka kuanza nae mahusiano
ya kujuana/urafiki, yeye tayari anakuwa kwenye ALARM ya DANGER… yani
anachokiona kwa kijana ni kwamba lazima atakuwa ana nia mbaya.
Ushauri wangu kwa WADADA ni kwamba ni muhimu tujenge mahusiano ya kirafiki
na vijana makanisani mwetu. Urafiki ni hatua muhimu ya kufanya maamuzi
yanayopelekea uchumba hadi ndoa. Tusivae SURA YA MAOMBI kila saa….!!
Kwa upande mwingine, VIONGOZI WA MAKANISA, tusiwawekee vijana wetu
(KIKE/KIUME) vikwazo vingi ambavyo vinasababisha wasiweze kujenga mahusiano. Ni
kweli lazima TUSISITIZIE UTAKATIFU lakini tusifanye WOKOVU UGEUKE GEREZA.
Tusiporuhusu wajenge mahusiano, je, wataoanaje?? Tuwafundishe vijana wetu wawe
na nidhamu ya kuweza kujisimamia na kujua MIPAKA ya urafiki na mahusiano kati
yao. Vijana wetu wakibanwa sana wataanza mahusiano kwa siri ambayo mara nyingi
huishia vibaya; pia wanaweza kutafuta marafiki nje ya kanisa ambayo pia matokeo
yake siyo mazuri sana.
MITHALI 17:17 (BHN); "Rafiki wa kweli ni rafiki siku zote, ndugu
huzaliwa asaidie wakati wa taabu."