Pages

18 April 2019

TULIZA FM - MERU KENYA NA SJ STUDIO - TANZANIA WAKISHIRIKIANA NA UMOJA WA MAKANISA, WAANDAA KONGAMANO KUBWA LA KIROHO MERU KENYA


Tulizoea kualikwa, tulizoea kuandaliwa sasa tumevuka mipaka, tumekua,tunaanza kuandaa wenyewe na kualika.  SJ STUDIO, tumeandaa siku sita za mafundisho ya neno la Mungu, kuibua vipaji, kuwaona wenye shida then kurefresh. Ni huko Meru katikati ya Nchi ya Kenya. Wanenaji kutoka Tanzania, South Africa, kenya na waimbaji mbalimbali watakuwepo. Kongamano litarushwa live Tuliza FM. Menyeji wa kongamano hilo ni Askofu Dennis Mwenda wa Live Gospel Church


Ni wiki ya kudumu hekalu mwa Bwana, kuumega mkate, kusifu na kuabudu pamoja na kuanzisha kituo cha mafunzo ya sauti na kuibua vipaji. Lakini pia tutazungukia vivutio vya utalii pia kujifunza maisha ya watu vijijini. Ni kuanzia tarehe 23 mwezi huu wa nne. Njoo tumtumikie Mungu, njoo tujipe raha wenyewe😀😀 Twenzetu kenya

SJ STUDIO MKOMBOZI WA WANAMUZI NA WAIMBAJI

 SJ STUDIO : Kituo kinachoandaa wenye ndoto za kuimba kuwa waimbaji bora! Studio iliojipanga kurekodi kwa ubara na kutengeneza video bora.
 Pia mafunzo maalum ya muziki na sauté yanatolewa hapa


JIANDAE KWA UJIO MPYA WA VERONICA FRANK


Mtangazaji mahiri kutoka Praise Power Radio, mama wa simulizi, Veronica Frank ndani ya SJ Studio.  JIANDAE kwa nyimbo mpya zenye viwango zilizosimamiwa na kurekodiwa Sj Studio.

NEW ROSE MUHANDO


WOOOOOOH!💪💪💃💃NIANGUKAPO MIIIIIIMIIIIIIIII,NITASIMAMA TEEEEEEEEEEEEEEEENAAAAAA! HONGERA SANA DA ROSE MUHANDO KWA UPONYAJI

DEBORA MKONYA KUWASHA MOTO WA SIFA KENYA

Star mpya wa injili Debora Mkonya anayetamba na video yake "KWA NGUVU ZA MUNGU", ndani ya SJ Studio, tayari kwa maandalizi ya safari ya huduma huko kwa Kenyata. Twenzetu Kenya.

UJIO MPYA WA KWAYA YA KINAMAMA KUTOKA MLIMA WA MOTO


Mama zangu kutoka Mlima wa moto kwa mama Dr. Gertrude Rwakatare wakiwa ndani ya SJ Studio. Chini ya mafunzo ya mwalim John Shabani, jiandae kubarikiwa na nyimbo za kinamama hawa.