YAH: KUOSHA/SAFISHA MICROPHONE YAKO
Salaam.
Nimeona niwaandikie barua hii fupi ambayo imetafsiriwa kwa lugha mbalimbali baada ya kuombwa na watu mbalimbali ambao kwa namna moja au nyingine siwezi kumjibu kila mmoja.
Nimeona niwaandikie barua hii fupi ambayo imetafsiriwa kwa lugha mbalimbali baada ya kuombwa na watu mbalimbali ambao kwa namna moja au nyingine siwezi kumjibu kila mmoja.
KINGA NI BORA KULIKO TIBA
Kila mhubiri/ muimbaji, au mtumiaji mzuri wa kipaza sauti (microphone) atakubaliana na mimi kwamba kuna wakati kipaza sauti hutoa harufu mbaya.
Kila mhubiri/ muimbaji, au mtumiaji mzuri wa kipaza sauti (microphone) atakubaliana na mimi kwamba kuna wakati kipaza sauti hutoa harufu mbaya.
Harufu hiyo inaweza kusababisha magonjwa kama kansa ya koo (throat cancer, kifua kikuu (tubaculoses), flu virus (virusi vya mafua), kuaribiwa sauti au kupoteza sauti na mengineyo.
Je! Umewahijiuliza kwa nini umekuwa na kawaida kikohozi wakati wote hasa baada ya shughuli ya uimbaji?
Watu wengi katika huduma hutumia kipaza sauti vibaya kwasababu ya kukosa nidhamu kisha kuhifadhi mate ndani na wakati mwingine harufu kali. Ukweli ni kwamba unatumia mic husika chochote alichokiacha humo ndani ikiwepo maambukizi fulani lazima yakuathiri.
Tafadhali jaribu kuosha kipaza sauti chako kila Jumamosi kama zinatumika kwa masuala ya ibada, au kila mara baada ya matumizi hasa kama wanaotumia ni watu tofauti. Yapo madhara mengine mengi ikiwepo pia kutu
Taadhari, kinachosafishwa ni kichwa cha kipaza sauti pamoja na sponji yake. Usije ukasema kocha kasema tudumbukize mic kwenye maji, sitaki kesi. Na hizi ni zile mic kwa ajili ya live performance maana zipo aina nyingi za mic na zingine kama za studio au kuigizia filamu zina ulizi wa kutosha lakini pia zipo zile za watangazaji na hata wahubiri na waimbaji walioendelee au wenye uwezo ambazo si rahisi kuathiriwa. Zipo ambazo huwezi kuziona kirahisi. Zingine huwekwa kwenye kola ya nguo, zingine kuzungushwa sikioni au kichwani...
Pia hakikisha umekausha vizuri kabla ya kurudishia
Narudia kusema, kamwe usije ukadumbukiza mic nzima kwenye maji. Mic huoshwa au kufutwa na kitambaa chenye unyevu wa sabuni maalum.
Kibongobongo unaweza ukatumia omo.
Kwa masomo zaidi ya uimbaji jiunge na Group letu la whatsapp kwa kutuma namba yako na jina lako kamili kwa namba 0716560094.
Kwa masomo zaidi ya uimbaji jiunge na Group letu la whatsapp kwa kutuma namba yako na jina lako kamili kwa namba 0716560094.
Lakni zaidi hudhuria masomo yanayoendelea pale SJ STUDIO Kimara Korogwe.
Njoo pia urekodi nasi kwa ubora na kwa gharama nafuu.
No comments:
Post a Comment