Pages

18 May 2019

VIJUE VYAKULA NA VINYWAJI MUHIMU VINAVYOFAA NA VISIVYOFAA KWA SAUTI YAKO KAMA MUIMBAJI''

Kama mwalimu wa sauti leo nimelazimika kuleta somo hili kutokana na maombi ya watu wengi mno!!(waimbaji na watoa hotuba)kutia ndani walimu na wahubiri .
Yawezekana umekuwa ukijiuliza,tunapozungumzia dhana nzima ya kukauka au kupotea kwa sauti,hivi huwa ina enda wapi???sijui kama ume wahi jiuliza swali hili mpenzi msomaji,leo na kuendelea utapata majibu mengi ya maswali yako kupitia mtiririko wa vipindi hivi. 
UIMBAJI ni kazi ngumu inayohitaji virutubisho vya kutia nguvu mwili ambavyo vinapatikana kwenye vyakula pamoja na baadhi ya vinywaji vinavyotumika katika maisha ya kila siku.
Asilimia kubwa ya waimbaji wameshindwa kuimba katika ubora unaopaswa kutokana na kutozingatia kanuni na taratibu za uimbaji.
Kwa hali ya kawaida kuna vinywaji na baadhi ya vyakula vinashauliwa kutumiwa kwa ajili ya afya, lakini vinaweza kukatazwa kwa wasanii ambao wanataka kupaza sauti zao.
Kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalamu, imegundulika kwamba kuna baadhi ya vyakula na vinywaji havipaswi kutumiwa na wasanii wa muziki ambavyo ni:
Vinywaji vyenye kafeni
Mwimbaji hapaswi kutumia vinywaji vyenye kafeni kama vile kahawa, soda jamii ya cola, chai nyeusi, wakati anataka kurekodi wimbo na hata wakati wa kuimba.
Vinywaji hivyo vinakatazwa kwa wasanii kwa kuwa vinachochea mkojo wa mara kwa mara, hivyo mwili wa binadamu unapunguza kiasi kikubwa cha maji kwa muda mfupi, hata hivyo hali hiyo inapoteza umakini wa kufanya jambo kwa wakati.
Vinywaji na vyakula vyenye gesi
Baadhi ya vinywaji vyenye gesi vinasababisha tumbo kujaa, hivyo msanii akiwa anataka kurekodi au kuimba anaweza kupata tatizo la kubeua.
Baadhi ya vyakula vinavyoweza kusababisha gesi tumboni ni pamoja na maharage, vitunguu, kabichi, kunde na vingine, wakati huo vinywaji ni pamoja na soda na pombe zote zenye gesi, kwa kuwa
husababisha gesi au hewa tumboni, hivyo kusumbua wakati wa kuimba.
Vyakula vyenye kuacha makapi kooni
Kwa hali ya kawaida koo ya mwimbaji inatakiwa kuwa safi kila wakati hasa pale anapotaka kuimba, hivyo akiwa amekula chakula ambacho kinaweza kubakia kooni, kinaweza kusababisha sauti kuwa na mikwaruzo.
Hata hivyo, wakati wa kuimba unaweza kupata tatizo la chembechembe kurukia kwenye koo la hewa na kusababisha mwimbaji kushindwa kupumua vizuri.
Baadhi ya vyakula ambavyo havipaswi kutumiwa na mwimbaji ni pamoja na bisi, tambi kavu, chama, mahindi, karanga na vinginevyo.
Hata hivyo, mwimbaji hatakiwi kula vyakula ambavyo vinaweza kumsababishia kooni kuacha uteute.
Baadhi ya vyakula hivyo ni pamoja na Ice cream na bidhaa zingine zenye maziwa kama vile pipi, keki, siagi, koni, biskuti ambavyo hupelekea utokaji mbaya wa sauti wakati wa kuimba na kuna uwezekano mkubwa wa kushindwa kupanda na kushuka wakati wa kuimba.
Mwimbaji pia hapaswi kutumia sigara, tumbako, bangi, ugoro na aina yoyote ya madawa ya kulevya, kwani vinaathiri koo na mapafu, ikiwa ni sehemu muhimu sana katika utengenezaji wa sauti bora za uimbaji.
Ukitaka jifunza zaidi jiunge na darasa letu kimara Dar. Pia karibu wewe na rafiki yako katika group letu la whatsapp kwakutuma jina, namba na picha kwa namba +255716560094

No comments:

Post a Comment