Zoezi lingine la warm up ni TONGUETRILL, au kuchezesha ulimi. Mfano wake ni kama kupiga kigelegele nk. Ni zoezi lenye matokea makubwa katika uimbaji, linatengeneza sana mishipa ya nyuma na mbele na kusaidia kujenga stamina ya uimbaji hasa kwa wale wanaoimba kwa muda mrefu. Suala la kichwa kuuma au shingo au uchovu havitakuwepo. Linasaidia kuimba sauti yenye punch na yenye ubora
Zoezi lingine ni la kuweka vidole vitaux au vinne mdomoni (4 fingers in your mouth) kwa kuvisimamisha sio kulaza huku ukiwa umefungua kinywa chako hadi kiwango cha mwisho ukitoa sauti. Ni zoezi linalofanya mishipa ya nyuma kukaza hivyo kukujengea uwezo mkubwa kiuimbaji.
Ili kujifunza zaidi hudhuria program zetu za mafunzo pale SJ Studio Kimara Korogwe Dar es salaam. Kwa walio mikoani, endelea kutega sikio kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kocha John Shabani na timu ya waalimu wa sauti wana ziara mikoa mbalimbali pamoja na nchi kadhaa za Afrika Mashariki. Lakini pia unaweza ukajifunza kwa njia ya mitandao kupitia skype, whatsapp video call kwa njia ya simu n.k
Tuwasiliane kwa kutupigia au kwa whatsapp
+255716560094
+255716560094
No comments:
Post a Comment