FAIDA ZA KUIMBA
Kuna aina mbili kuu za faida:
1.
Faida
za kuimba ambazo zinamsaidia mtu kiafya.
2.
Faida za kuimba
kwenye jamii
Kwanza kabisa naomba nikueleze maana ya kuimba.
KUIMBA ni kutoa sauti yenye ulinganifu, sauti hiyo
inatakiwa kufuata mapigo ya ki muziki na ni zaidi ya kughani. Zamani mababu
zetu walikuwa wanaimba kwenye kazi mbalimbali ili kurahisisha kazi yenyewe
iliyokuwa ikifanyika, mpaka sasa watu wengi huimba ili kuburudisha, kufundisha,
kukosoa au kuelimisha kikundi fulani cha watu.
Kuimba ni faida kwa mwimbaji kwani kuna faida
nyingi saana ambazo mwimbaji anazipata kama vile kuburudika, kuburudisha,
kuinjilisha, kuhamasisha, kufariji, kufurahisha n.k
Leo nitakueleza faida za kuimba ambazo
zinamsaidia mwimbaji kiafya:
- Kuimba
ni mazoezi. Unapoimba unafanya
mazoezi ambayo pia ni kinga kwa magonjwa mbalimbali yanayoweza kumuathiri
mtu ambaye hafanyi mazoezi. Mazoezi ambayo nayasemea hapa ni Kupanua
kiwambo (diaphragm), mwanakwaya anatumia nguvu nyingi sana wakati anaimba
ili kupanua mapafu na kiwambo. Hii itamsaidia mwimbaji ku zuia magonjwa
yanayoweza kuathiri mapafu kama vile kikohozi, mafua.
- Inasaidia kuboresha
mfumo wa upumuaji mwilini kwani msukumo wa damu utakuwa mkubwa
ambapo ndani ya chembe za damu huwa kuna hewa safi ya Oxygen ambayo
husambazwa mwilini pote na chembe za damu katika mzunguko.
- Inasaidia kupunguza
mawazo. Hili liko wazi kabisa kwa mwanakwaya au mwimbaji
yeyote yule, ukiimba unapunguza mawazo. Mtu mwenye mawazo anaweza kuugua
hata magonjwa ya akili na kisaikolojia.
- Husaidia kusimama
vizuri. Mwimbaji huwa ana staili yake ya jusimama ambapo kifua
chake anakiweka mbele, mabega yanakuwa yameinuka kidogo ili kumsaidia
kutoa sauti, mgongo pia unakuwa umenyooka vizuri. Hii inamsaidia kuufanya
uti wa mgongo usijikunje. Kwa hiyo mwanakwaya anapoimba kwa muda mrefu
huwa na tabia ya kusimama kama anataka kuimba na hivyo kumsaidia yeye
kutunza na kukinga uti wa mgongo.
- Huimarisha
mfumo wa kinga mwilini. (strengthen the immunity system) Kwenye
mwili wa binadamu kuna kinga (protini) ambayo ina jina la kitaalamu ambalo
ni Immunoglobulins, kwa hiyo mtu anapoimba anafanya mazoezi (kama
nilivyosema hapo juu) na unapofanya mazoezi ina maana kwamba unaongeza
kinga mwilini tofauti na mtu ambaye amekaa tu bila kufanya mazoezi
Kwa ufupi sasa kuimba kuna faida kiafya, faida
zingine nimezitaja hapa chini ambazo ni:
- Kuimba
nidawa ya asili ya mawazo (natural annti-depresant)
- Kuimba
kunapunguza mawazo kwa kiasi kikubwa sana (ni dawa kwa mtu mwenye mawazo)
- Kuimba
kunaongeza uwezo wa kufikiri na kuchukua maamuzi.
Faida za kuimba
kwenye jamii.
Kuimba humsaidia mtu kuongeza idadi ya marafiki.
Kuimba kunamwongezea mtu kujiamini katika kila kitu
anachokifanya kwa faida yake na jamii kwa ujumla.Kuimba kunapanua wigo wa
mawasiliano.
Lakini zaidi ya hapo kuimba ni ajira kubwa.
Naamini masomo haya yamefungua ufahamu kwako. Ukitaka kujifunza zaidi
tuwasiliane, ili nawewe uwe mmoja wa wanafunzi wangu katika darasa letu la
mafunzo ya sauti na uimbaji.
Whtspp/call
+255716560095
Facebook:
John Shabani (Mtoto wa Mfalme)
Instagram:
sjvocaltraining
E-mail: jshabani2011@gmail.com
No comments:
Post a Comment