Pages
▼
28 December 2011
21 December 2011
BELLA KOMBO AMRUDIA BWANA
Christabella Kombo kwa jina maaarufu Bella Kombo, hivi karibuni ameamua kuachana na muziki wa dunia na kuanza kumwimbia Bwana. Mwanadada huyo aliyeonekana kuvutia sana kwenye mashindano ya Bongo Star Seach BSS ya 2010 na 2011, hivi sasa amerekodi album yake ya nyimbo za injili. Kabla hajajiunga na Bss, Bella alikua mwimbaji mzuri kanisani na pia sauti ya Bella imesikika sana ktika baadhi ya nyimbo mbalimbali za mwalimu John Shabani.
Akiongea na mwandishi wa blog hii, bella amekiri kumrudia Bwana maana yeye siku zote alikua ni mwimbaji kanisani. Kilichotokea ni kwamba, baada ya watu na wadau mbalimbali kugundua kipaji chake, walimshauri na kumshawishi ajiunge na Bss kwamba huko kipaji chake kitajulikana zaidi pamoja na kujitangaza kwasababu kazi ya Bss ni kuinua vipaji haijalishi unaimba maadhi gani ya muziki. Baada ya kipaji chake kujulikana zaidi, alishawishiwa kujiunga na kundi la Machozi Band, hata hivyo moyo wake umekuwa ni wa kumwimbia mwenyezi Mungu. Baada ya kushauriwa na watu pamoja na watumishi mbalimbali hasa zaidi mwalimu wake bwana John Shabani ambaye hapo awali amekuwa akiimba pamoja na bella, ndipo alipoamua kurudi kundini na kuanza tena kumwimbia Bwana.
Hivi sasa Bella anategemea kujiunga na kundi la Glorious Celebration la jijini Dar es salaam.
19 December 2011
JOHN SHABANI, FARAJA NTABOBA, UPENDO KILAHIRO NA CHIDUMULE NDANI YA VIDEO MOJA
John Shabani na Upendo kilahiro baada ya kuimba wimbo maalum wa miaka 50 ya huru wa Tanzania kwenye uwnja wa uhuru.
John Na Faraja Ntaboba wakirekodi mkanda wa video
John Na Faraja Ntaboba wakirekodi mkanda wa video
Wapenzi wa nyimbo za injili wakae mkao wa kula, Album mpya ya John shabani alioshirikisha waimbaji nyota wa nyimbo za injili wa Tanzania, DRC kongo na Uganda sasa kukamilika mwanzoni mwa January katika mfumo wa audio na video. Hii ni albam ya kipekee na ni kwamara ya kwanza kuwepo na albam ya mwimbaji ilioshirikisha waimbaji mbalimbali nyota. Hii ni ktokana na moyo wakipekee alionao Mwalimu John shabani, kwani amekua akijitolea kuinua vipaji mbalimbali vya waimbaji bila kubagua. Baadhi ya waimbaji katika albam hiyo ni: Faraja Ntaboba (Mwimbaji maarufu anaye tikisa Afrika kutoka kule kongo Drc, Cosmas Chidumule, Upendo kilahiro, Askofu John komanya(Aliyetamba na kibao cha zawadi gani nitamtolea Bwana), Jane miso (Mama wa Omayo), Christina Matai(Mwang'onda), Tina Marego, X-tano Family group (Kampala Uganda) na wengine kabao.
Albam hiyo inasimamiwa na kusambazwa na kampuni ya Msama Promotions.
15 December 2011
• COSMAS CHIDUMULE NA JOHN SHABANI WAKONGA MIOYO YA MAELFU YA WATU
Mkongwe wa muziki wa injili Afrika Mzee Cosmas Chidumule pamoja na mwalimu maarufu wa Muziki wa injili afrika mashariki bwana John Shabani,Wamegusa mioyo ya maelfu ya waumini walioshiriki ibada katika kanisa la mlima wa moto (Mountain of fire) la mikocheni b assemblies of God linaongozwa na Dr, Rv. Getrude Rwakatare. Kibao cha Kwa Yesu kuna raha chake john Shabani alichomshirikisha Chidumule ndicho kilicho tifua maelfu ya waumini hao. Wimbo huo umo ndani ya album mpya yakwake John shabani alioshirikisha waimbaji nyota wa nyimbo za injili Tanzania, Congo na Uganada. Album hiyo inatarajia kukamilika mwishoni mwa mwaka huu kwa mfumo Audio na video na inasimamiwa na kusambazwa na Kampuni ya Msama Promotions
13 December 2011
WIMBO ULIOIMBWA NA TANZANIA GOSPEL ALL STARS WAPATA HESHIMA YA KUWA WIMBO MAALUM KATKA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA
Umati wa maelfu ya watu
Upendo kilahiro akiwa na mwalimu John Shabani
G stars wakiimba mbele ya marais na waheshimiwa mbalimbali
Mwalimu maarufu wa nyimbo za injili Afrika mashariki
(John shabani), akiimba kwa hisia kali mbele ya rais
Mzee makasy (Mwimbaji mkongwe), Akiimba mbele ya rais
Mheshimiwa martha mlata akiimba kwa hisia
Mtoto wa miaka 6 Gloria kilahiro akiimba kwa hisia kali mbele ya waheshimiwa

Wimbo wa kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania ulioimbwa na Tanzania Gospel All stars (Waimbaji nyota wa muziki wa injili Tanzania), umepata hadhi na heshima ya kuwa wimbo maalumu katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara.
Chini ya mwalimu John shabani na usimamizi wa chama cha muziki wa injili Tanzania(Chamuita), Waimbaji hao walipewa nafasi maalum ya kuimba wimbo huo mbele ya Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Mrisho Kikwete na mbele ya marais wa nchi mbalimbali, mawaziri, wabunge, mabalozi, pomoja na maelfu ya watu waliohudhuria katika maadhimisho hayo. Viongozi na watu mbalimbali wamewapongeza waimbaji hao wa injili kwa umoja na mshikamano wao, pia wameupongeza wimbo huo, hivyo kuwaomba kuusambaza wimbo huo kwa watanzania ili kila mtu abarikiwe na wimbo huo
Hii ni mara ya kwanza kwa waimbaji wa injili kuungana pamoja na kurekodi wimbo wa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili ya uhuru wa Tanzania.
Video ya wimbo huo inategemea kusambazwa kwa watanzania kwa gharama ndogo.
Waimbaji walioshiriki kurekodi wimbo huo ni:
1. Gloria kilahiro 18. Mzee Makassy
2. Amon Kilahiro 19. Mzungu Four
3. Masanja Mkandamizaji 20 Jane Misso
4. Upendo kilahiro 21 Addo November
5. Stella Joel 22. Mheshimiwa Martha Mlata
6. Nely Nyamanga 23. Ambwene mwasongwe
7. Joyce Ombeni
8. Bony Mwaitege 24. Douglas Pius
9. John Shabani 25. Mchumu Maximillian
10. Rose Manoza 26. Charles Thobias Malya
11. Yona Abiud 27. Joshua makondeko
12. Miriam Lukindo Mauki 28. Daniel Safari
13. Robert Bukelebe 29. Naomy Mbwambo
14. Nicholaus Misuzi 30. Joseph kasigala
15. Christina Matai 31. Debora Said
16. Tina Marego 32. Stara Thomas
17. Martha Mwaipaja 33. Victor Ahron
Na wengine wengi.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania
8 December 2011
Tanzania gospel all stars kuimba kwenye maadimisho ya miaka 50 ya uhuru
Hatimaye waimbaji wa injili (Tanzania All Gospel Stars) walioshiriki kurekodi wimbo wa miaka 50 ya uhuru wa Tanzania chini ya uongozi wa Camuita(Chama cha muziki wa injili Tanzania), wameingizwa katika ratiba ya uimbaji katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru. Maadhimisho hayo yatafanyika kesho katika viwanja vya uhuru/kiwanja cha taifa. Waimbaji hoa wameombwa kuwahi mapema yaani saa moja kamili asubui, ili kupewa ratiba kamili pamoja na taratibu nyingine. Pia kila mshiriki avae sare ya maadhimisho. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
29 November 2011
Martha Mwaipaja avishwa pete ya uchumba
Habari zisizo na chenga zilizotua kwenye meza ya ya blog hii zilisema, Martha alivishwa pete ya uchumba na mchungaji huyo katika Kanisa la Victoria lililopo Ubungo External jijini Dar na baada ya zoezi hilo kulikuwa na sherehe ndogo kanisani hapo kwa ajili ya kumpongeza kwa kufikia hatua hiyo,”
Mwana dada huyo anayetamba na vibao kama vile Usikate tama, wewe ni baba n.k amekiri kuchumbiwa na mchungaji huyo na kuongeza shughuli ya kesho ilinogeshwa na waimbaji wenzake kama vile Bahati Bukuku, Sarah Mvungi, Ambwene Mwasongwe na Christina Matai.
Wengine ni David Robert, Debora John, Josephine Mwasulama, Ado November, Jennifer Mgendi, Lianga George, Stella Swai na wengineo.
11 November 2011
ZIARA YA KUENEZA CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI MIKOANI
bwana John Shabani akihojiwa na bi Revina Steven mtangazaji
wa Top radio kuhusu chama cha muziki wa injili Tanzania
Mkurugenzi wa Top radio bwana Steven Lukindo akiwa katika picha
na makatibu wenezi wa chamuita.
bwana Magida Timotheo amabaye ni mjumbe wa chamuita
anayewakilisha watu wenye ulemavu, akiwa ameshikilia katiba ya chama
kabla ya kukikabidhi kwenye uongozi wa morogoro
John Shabani akikabidhi fomu za kujiunga na chama
Wawakilishi wa kwaya, bendi na waimbaji binafsi wakionyesha nyuso za
furaha baada ya kuletewa chama cha muziki wa injili morogoro.
Viongozi wa chama wakiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa
Vatican Lodge bwana Thomas B. Butabile. Hapo ndipo walipofikia viongozi hao.
Maswali mbalimbali yakiulizwa
Chama cha Muziki wa Injili kupitia kamati ya uenezi chini ya makatibu wenezi bwana John Shabani na bi stella Joel, wameanza ziara ya kukieneza chama hicho mikoani, wakianzia na mkoa wa morogoro. Ziara hiyo imetokana na maagizo ya shirikisho la muziki Tanzania (Tanzania music federation) na braza la sanaa la taifa (BASATA), kwamba chama hai ni kile kilichoenea nchi nzima. Wakwa mkoani morogoro, viongozi hao wakiwa wameongozana na mwimbaji bwana Magida Timotheo ambaye ni mjumbe wa chama hicho anayewakilisha watu wenye ulemavu, wamepewa ushirikiano mkubwa na Top Radio chini ya uongozi wa bwana Steven Lukindo. Pia Dada Revina Steven na Dada Bupe kama watangazaji wa redio hiyo, wamefanya kazi kubwa ya kuhamasisha wakaaji wa morogoro na vitongoji vyake, waweze kujiunga na Chama hicho. mamia ya wakaaji wa morogoro wameonyesha kuitikia mwito wa kujiunga na chama hicho na kuomba ziara hiyo isiishie morogoro peke yake bali katika nchi nzima. Viongozi hao wa chama wamekabidhi katiba ya chama na fomu za kujiunga na baada ya muda si mrefu uongozi wa mkoa wa morogoro utaundwa chini ya usimamizi wa makao makuu

31 October 2011
MUME WA MAREHEMU ANJELA CHIBALONZA AJIPATIA UBAVU MPYA
Hatimaye aliyekuwa mume wa marehemu Angela Chibalonza, ajipatia ubavu mwingine. Mtumishi huyo wa Mungu ameoa hivi karibuni huko DRC kongo. Picha hizi ni baada ya wiki chache za ndoa alipohudumu ni mke wake mpya katika kanisa la Mikocheni B assemblies of God, linaloongozwa Na Mchungaji Getrude Rwakatare.
Kuhusu jina la mke wake na habari zote za harusi hiyo tutakujulisha hivi karibuni.
Mchungaji Muliri akiimba mke mpya hivi karibuni katika kanisa la mikocheni BMke wa Elisha muliri akiimba kwa hisia kali
24 October 2011
TANZANIA GOSPEL STARS WAKAMILISHA VIDEO YA WIMBO WA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA
Hatimaye waimbaji wa nyimbo za injili Tanzania wakiongozwa na mwalimu wa muziki wa injili afrika mashariki bwana John Shabani, chini ya usimamizi wa chama cha muziki wa injili Tanzania (Chamuita) wamekamilisha video ya wimbo ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania. Pamoja na waimbaji mbalimbali kushiriki katika wimbo huo pia yumo mheshimiwa Martha Mlata ambaye amechangia sana katika kufanikisha kurekodi wimbo huo. Baadhi yam abo aliyo yafanya ni pamoja na kufanikisha kupata sare na bendera kutoka serekalini pamoja na kutoa feha za kufanikisha kurekodi video. Pia studio ya Pro arts studio ya jijini Dar es salaam ilijitolea kurekodi sauti. Wazo la kuwakusanya waimbaji wa injili na kurekodi wimbo wa miaka 50 ya uhuru, lilianzishwa na bwana Tc Timothy Chelula na kumshirikisha mwalimu John Shabani, ndipo walipo kihusisha chama cha muziki wa injili na vyombo mbalimbali vya habari. Muda si mrefu wimbo huo utasambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Baadhi ya waimbaji walioshiriki kurekodi wimbo huo ni:
1. Gloria kilahiro 18. Mzee Makassy
2. Amon Kilahiro 19. Mzungu Four
3. Masanja Mkandamizaji 20 Jane Misso
4. Upendo kilahiro 21 Addo November
5. Stella Joel 22. Martha Mlata
6. Nely Nyamanga 23. Ambwene mwasongwe
7. Joyce Ombeni
8. Bony Mwaitege 24. Douglas Pius
9. John Shabani 25. Mchumu Maximillian
10. Rose Manoza 26. Charles Thobias Malya
11. Yona Abiud 27. Joshua makondeko
12. Miriam Lukindo Mauki 28. Daniel Safari
13. Robert Bukelebe 29. Naomy Mbwambo
14. Nicholaus Misuzi 30. Joseph kasigala
15. Christina Matai 31. Debora Said
16. Tina Marego 32. Stara Thomas
17. Martha Mwaipaja 33. Victor Ahron
Na wengine wengi.
Mheshimiwa Martha, Mr Masanja na Malimu John wakitabasamuKampuni ya Pro arts wakiwa kazini
Masanja mkandamizaji akifanya vitu vyake
Baadhi ya magari mbalimbali ya waimbaji nnje ya jengo la studio
Mwimbaji mkongwe mzee makasi katika pozi
Mwalimu John Shabani akiwaongoza waimbaji wa Injili
Pamoja na hayo, viongozi wa chama cha muziki wa injili Tanzania tunatoa wito wa kujiunga na chama hicho, kwani kuna faida nyingi za kujiunga na chama. Fomu sasa zinapatyikana. kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0754818767, 0716560094.