Hapa ni mwalimu John Shabani sambamba na Masanja mkandamizaji pamoja na Emmanuel Mabisa wakimtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji
Huu ni muendelezo wa masomo yanayofundishwa na John shabani, ili kukufanya unayetaka kujifunza kuimba, uwe mwanafunzi mzuri na yule mwimbaji awe bora zaidi.
Tahadhari:
Usilazimishe kutumia nguvu ili uweze kuimba vizuri, kinyume chake jizoeshe
kutumia nguvu kidogo lakini utaalam mwingi (Vocal Technique). Shida ni pale
tunapodhani kwamba nguvu hizi ni kama za wanariadha au wacheza mieleka!
Inawezekana nguvu hizi zisionekane kwa macho ya nyama lakini zinadhihirishwa na
uimbaji wetu. Tunapoimba tunatakiwa kuwa na uhuru (freedom in singing), na sio
kama mtu aliyelazimishwa. Lakini ikumbukwe pia nguvu hizi asili yake inatoka
pia na mfumo wetu wa maisha ya kila siku iki pia ni pamoja na mazoezi ya
viungo, vyakula na vinyaji tunavyotumia, makazi na malazi safi n.k.
Mazoezi mengi
yanayofanyika kwenye vikundi mbalimbali, ni ya kupayuka na kutumia nguvu
nyingi, matokeo yake watu wengi wamekaa kwenye zoezi hilo kwa muda mrefu bila
kuwa na mabadiliko yoyote huku miili yao ikizoofika au kuishia kuwa mtu wa
kupiga kelele na sio kujfunza kuimba vizuri. Haya sio mazoezi ya kumpata
mshindi wa dansi mia mia, ni mazoezi ya kuimba. Imefika mahali sasa masikio
hayawezi kujisikia vile tunavyoimba kwasababu ni kelele na kujichosha.
Ikumbukwe kuwa sauti
hutunzwa kama yai; wengi wetu hufanyishwa mazoezi magumu yasiyolingana na umri
wao na hali yao ya mfumo wa miili yao pamoja na kuzingatia afya zao, matokeo
yake nimeshuhudia watu wakipata matatizo katika koo zao na hata bathi ya miili
yao.
Inashangaza kuona mtu ambaye hajawahi kukimbia maili moja unataka
kumkimbiza maili kumi, matokeo yake ni kudondoka kama sio kupoteza fahamu
kabisa. Yapo mazoezi ya kawaida ya jumla lakini mazoezi mengine ya uimbaji
lazima yazingatie umri wa mtu, hali ya mtu huyo sambamba na afya yake.
Nasikitika kusema kuwa wapo waliofundishwa kwamba akiweza kuimba noti za juu
ndio amekuwa mwimbaji mzuri, matokeo yake mtu anatumia nguvu nyingi, kukaza
misuli ya uso huku usoni akijaribu kuvimba na kutoa macho kama mjusi aliyebanwa
na mlango ili tu awezekufika huko!...
Najua wapo waalimu
wengi katika masomo haya ya uimbaji, na wengine inategemea amejifunza wapi,
lakini bado mwisho wa siku ukweli unabaki kuwa ukweli. Mimi ningeshauri hata kama
wewe ni mwalimu mzuri, mwimbaji mzuri, sote tubaki kuwa wanafunzi.
Kwa ushauri zaidi tupigie
0716560094, au niandikie: touchingvoice@yahoo.com
Pia unaweza ukahudhuria masomo
tunayofundisha sehemu mbalimbali.
No comments:
Post a Comment