Pages

30 October 2014

MKAKATI WA KUWASAIDIA WATOTO YATIMA



 Bi Warra Nnko akiwa amekumbatia kitoto kichanga kilicholetwa baada ya mama yake kufariki wakati wa kujifungua

 Baadhi ya watoto wakipata kifungua kinywa



 Muonekano wa jengo la Shalom Orphanage Center

 John shabani akitoa mafunzo kwa watoto




 Mwenyekiti wa Chama Cha Wajane Tanzania, akiwa katika hali ya huzuni baada ya kujionea hali mbaya ya baadhi ya watoto walioletwa katika kituo cha Shalom

Hawa ni watoto wanaolelewa katika kituo cha SHALOM! watoto hawa, waliookotwa vichakani hali zao zikiwa mbaya sana, kila mara baba yao mzazi ambaye ni mlevi wa kupindukia, aliwalawiti kwa zamu. Maisha yao yalikua ya kuokota vyakula vilivyotupwa jalalani, huku makazi yao yakiwa ni kulala vichakani baada ya nyumba yao ya majani kuanguka.

 Watoto wakisherekea sikukuu ya Christsmass

 Wageni mbalimbali hujitolea kufanya kazi za kijamii katika kituo


 Moja ya madarasa

Baada ya kuzunguka maeneo mbalimba, hii ni ziara nyingine ya kutembelea kituo cha watoto yatima
                              “SHALOM ORPHANAGE CENTER”!    
                                           Mimi na wewe tunaweza.

Jambo moja nililojifunza chini ya jua, ni kufanya Jambo sahihi, kwa mazingira sahihi, kwa watu sahihi, na kwa wakati sahihi. Jambo lako, wazo lako, uamuzi wako, mkakati wako vyaweza kuwa, sahihi lakini si kwa watu sahihi, labda si kwa mazingira sahihi, lakini pia labda si kwa wakati sahihi.
Inawezekana umekuwa ukifanya mambo mengi, lakini pia unataka uonekane na watu, upongezwe au uambiwe asante! Si vibaya, lakini wakati mwingine fanya jambo katika mazingira ambayo si ya kupongezwa wala kusifiwa bali kwako ni wajibu kama mwanadamu ambaye uhai wako hujaugharimia chochote.

Moja ya mambo nilioamua ni kuwaona watu wenye uhitaji haswa tena huko maeneo ya vijijini, hilo ni jukumu letu sote. Ndio maana baada ya kuzungukia vituo mbalimba vya watoto yatima Tanzania, ziara iliyoratibiwa na Chama cha Wajane Tanzania (Tanzania Widows Association), moja ya kituo kilichonigusa sana ni cha SHALOM ORPHANAGE CENTER, kilichopo huko karatu, kilomita 160 kutoka jiji la Arusha. 

Moja ya vitu nilivyoguswa navyo ni kumuona mama mjane Bi Warra Nnko, akiwa amegeuza nyumba yake kuwa kituo cha kulelea watoto. Vipo vyumba vya watoto wachanga haswa, wengine wameokotwa wakiwa wametupwa baada ya kuzaliwa na wengine wazazi kufariki wakati wa kujifungua. Pia wapo watoto ambao huletwa wakiwa katika hali mbaya, wangine wamebakwa na kulawitiwa. Nilitiwa moyo kuona hata serikali ya wilaya na hata mkoa huleta watoto katika kituo hicho. 

Vipo vyumba vya watoto wenye hali mbaya, wengine wanaulemavu wa aina mbalimbali, wengine wameathiki na ukimwi n.k. Shalom Orphanage center ni kama Hospital, Shule, na mji wa makimbilio. Pia nimeguswa kuona Bibi huyo ameanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ya ng’ombe wa maziwa, kuku wa mayai na mashamba ili watoto wapate lishe na afya bora. Ukifika shalom lazima ulie kidogo; lakini cha kushangaza watoto hao,kuanzia wachanga na wale wanaosomeshwa sekondari wote humwita Bibi Warra Mama!

Mimi kama mwalimu wa sauti na uimbaji, nikiwanimeambatana na mwenyekiti wa Chama Cha Wajane Tanzania na baadhi ya watu, pamoja na kila mtu kutoa kile alichokuwanacho, lakini pia niliamua kuanzisha mpango wa kuibua vipaji vya watoto.

Wito wangu kwako, ni kukuomba tuungane kwa pamoja safari hii tena, kwa chochote ulichonacho tukawaone watoto hao mwishoni mwa mwezi huu wa Novemba. Pia ikumbukwe kuwa karatu nisehemu nzuri ya utalii wa ndani, utajifunza mengi pale MTO WA MMBU, lakini pia kutembelea mbuga za SERENGETI, NGORONGORO, pamoja na kutembelea kwenye misitu na mapango ya mawe wanakoishi waadzabe. 

Unaweza ukaleta nguo, chakula, pesa yako na chochote ulichonacho kisha ukakabidhi katika ofisi za Chama cha Wajane Tanzania zilizopo maeneo ya kinyerezi.
Kwa mawasiliano zaidi tupigie: 0754 366 530, 0713778778

No comments:

Post a Comment