Ni maelezo mbalimbali kuhusu
maisha ya Akofu. Baada ya kuulizwa maswali mbalimbali kuhusu maisha yake
na huduma, hapa Askofu Zakaria anaendelea kumjibu mwandishi:
Naendelea kuwaletea maelezo kuhusu
maisha ya Askofu Kakobe baada ya kuokoka na kuanzisha kanisa.
Mwandishi: Kuna waliosema kuwa
ulianzisha kanisa nchini Marekani na ulikuwa na mpango wa kuhamia huko, je ni
kweli?
Askofu Kakobe:
Kuhama nchi siwezi lakini ni kweli baada ya maombi ya muda mrefu
Aprili 16, 2012 nilifungua kanisa Marekani, hii ni nia ileile ya kuokoa mataifa
na kuinua jina la Yesu.
Mwandishi: Tunaona watu wakifunga
ndoa
wanavaa pete
lakini katika kanisa lako hilo halipo, unazungumziaje hilo?
Askofu Kakobe: Pete kwenye ndoa
siyo agizo la Bwana na ndiyo maana tunaona Mungu mwenyewe
akichukizwa na watu waliovaa pete, vikuku na mapambo mengineyo. Soma maandiko
haya Isaya 3:21, 16-24; Hosea 2:13; Mwanzo35:1-5; Kutoka 33:4-6; Yeremia
4:30; 1Timotheo 2:9-10; 1Petro 3:3-5. Mapambo ni mavazi ya waabudu miungu,
yanahusishwa na ibada ya miungu (mashetani).
Mwandishi: Lakini wanaotumia pete
katika ndoa wanasema eti pete ni mfano wa upendo usio na mwanzo na mwisho,
unasemaje kuhusu madai hayo?
Askofu Kakobe: Hiyo siyo kweli,
mwanzo wa upendo ni pale walipokutana na wakapendana na mwisho wa upendo ni
pale mmoja anapofariki na kumfanya mwenzake kuwa huru kuolewa au kuoa.
Yesu alisema mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa.
Hutapewa mke wako au mume wako
uishi naye huko mbinguni. Yote hii ni janjajanja ya shetani anayekuja kwa mfano
wa malaika wa nuru ili kutufanya tuingize mapambo katika nyumba ya Mungu na
kujenga ngome za mashetani kwa visingizio kwamba mimi nimevaa pete sasa
ni mke wa mtu au mume wa mtu. Mbona nyumba za wageni (guest houses) zimejaa
watu wenye pete za ndoa? Kama pete hizo zingekuwa zinawafanya watu wasiwe
makahaba, tusingekuwa na matatizo tuliyonayo leo.
Habari
kutoka: www.kigoma24hours.blogspot.com
No comments:
Post a Comment