Pages

20 November 2014

CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI TANZANIA NA MKAKATI WA KUPANDA MITI NA MICHE YA MATUNDA NA MAUA NCHI NZIMA



Hii ni ziara ya kihistoria iliyoandaliwa na chama cha Muziki wa Injili Tanzania.

Mungu alipoumba Dunia, aliifanya yenye kupendeza na kuvutia sana, lakini kwasababu ya matumizi mabaya ya wanadamu, sasa maeneo mengi duniani yanaonekana kama jangwa, kwasababu ya matumizi mabaya ya ardhi, kumekuwa na ukame uliokithiri, ardhi sasa haina rutba ya asili, joto linasumbua duniani kote, majira ya upatikanaji mvua yamebadilika sana; wanaoathirika ni viumbe hai akiwemo mwanadamu.
Kwakulitambua hilo, waimbaji wa nyimbo za injili, tumeamua kujitolea kufanya kampeni nchi nzima ya upandaji miti pamoja na miche ya maua na matunda ili kurejesha uoto wa asili katika nchi yetu.
Pamoja na hayo pia ziara hiyo inaandaa matamasha ya uimbaji ikiwa ni pamoja na kuwahubiri watu waache uovu na kuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Jambo linguine la msingi ni pamoja na kuwa na kuiombea nchi  amani, utulivu, umoja na mshikano wetu.
Baada ya ziara ya umisheni mkoani singida, waimbaji walipata fursa ya kuhudhuria kikao cha bunge na baadaye kupata picha ya pamoja na  Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda, Naibu Waziri wa Fedha Mh. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Razaro Nyarandu, Mbunge wa CCM Viti Maalum – Singida Mh. Martha Mlata, Mbunge wa Viti Maalum CCM – Mbeya Mh. Marry Mwanjelwa, Mh. Magreth Sitta na wengine wengi.
Ziara ilihitimishwa kwa kupata chakula cha mchana kilichoandaliwa na Mh. Nyarando ndani ya Dodoma Hotel. Mh. Nyarando aliweza kuwashukuru waimbaji kwa ushiriakiano wao na jinsi walivyoweza kujitolea kufika vijijini kufanya kazi ya Mungu.
Pia aliweza kuwaahidi waimbaji kutembelea Ngorongoro Crater mapema iwezekanavyo, ili kujifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja na kutangaza vivutio vya utalii.

Kwa msaada wa Mungu tunaweza!

 waimbaji wakiwa wamejipanga tayari kuelekea kupanda miti


 Msafara wa waimbaji wakishirikiana na wanakijiji wa tarafa ya Ndago mkoani Singida pamoja na viongozi wa dini, wakielekea kupanda miti
 Mheshimiwa Martha Mlata akipanda mti
  Stela Joell akipanda mti
  Madam Ruti akishirikiana na mtangazaji wa Star Tv, bi Sauda  kupanda mti
 John shabani na Jane Misso, wakipanda mti
 Edson Mwasabwite akipanda mti
Mch. Vaileth na Bupe kingu wakishirikiana na watumishi wengine kupanda mti

No comments:

Post a Comment