Wajane wakiwa wametulia nje ya ofisi za chama, huku wakimsikila mwenyekiti
Mwenyekiti akisaidia kubeba viti
Wajane wakigonganisha vinywaji vyao na mwenyekiti kwa kutakiana afya njema
Ni mkutano mwingine wa wajane, wakijadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja
na kuimarisha umoja huo.
Akionekana mwenye uso wa furaha, mwenyekiti wa chama hicho ambaye kabla ya
kikao kuanza alijitolea kubeba viti na kuvipanga, amewapongeza wajane kwa
kuendelea kujitokeza kwa wingi kujiunga na chama. Pia kwa juhudi zake
mbalimbali, zipo shule pamoja na
wafadhili mbalimbali wamekubali kuwasomesha watoto wa wajane. Wito wa
Mwenyekiti ni kuziomba shule mbalimbli kukukubali kuwasomesha watoto wa wajane.
Katika mkutano huo uliofanyika nje ya ofisi za Chama cha Wajane Tanzania ,
maeneo ya kinyerezi Dar es salaam, wajane pia wamenufaika na misaada kutoka kwa
wadhili mbalimbali ikiwa ni pamoja na mavazi, chakula, sukari, mchele pamoja na
sabuni.
Mkakati mkubwa sasa ni kuhakikisha kila mjane anasaidiwa kupata mtaji ili
kuwa na shughuli binafsi ya kumwingizia kipato, ili kujikimu kimaisha. Maana
lengo kuu la chama ni
kurejesha matumaini ya wajane.
Wito ni kwa wajane wote Tanzania kujitokeza kujiunga na chama hicho
kilichosajiliwa kihalali. Pia mlango uko wazi kwa wafadhili wa ndani na nje,
taasisi mbalimbali, matajiri na wakereketwa kujitokeza kusimama na wajane na
kuwasaidia kwa hali na mali.
Mkakati sasa ni kukieneza chama nchi nzima.