Pages

15 June 2018

HACK MOYO WA MPENZI WAKO USIHACK SIMU YAKE - UJUMBE MUHIMU KWA WANANDOA NA WALIO KWENYE MAHUSIANO

    Huu ni ujumbe muhimu kwa wanandoa na walio 
kwenye muhusiano kutoka kwa
Winnie Nzobakenga

Nimewahi kusikia wanawake wengi wanaulizia jinsi ya kuhack simu za waume zao ili wawe wanasoma meseji za waume zao. Haya yapo pia hata kwa wachumba.  Mmh! hivi ninyi wamama au wan awake wenzangu, mnajipenda kweli? Sasa ukishahack simu yake then what?

Ukikuta msg za wanawake wengine then what,inakusaidia nini??ukishajua mmeo anamchepuko utachukua mapanga na visu na panga kwenda kupigana?utaweza kweli?ukishajua kuna mwanamke kazaa naye na amempangishia nyumba utapata nguvu za kwenda kumpiga huyo mwanamke?? Ukishajua utaongeza mapenzi kwa mme wako au ndio utaenda kuvunja ndoa na kubeba vilago na kuondoka?watoto utaawaacha au utaondoka nao,nani atawalea,nani atawapa matumizi??ninawambia kabisa ninyi ambao mnahangaika kujua namna ya kuhack simu ya mme wako kujua kinachoendelea.
NISIKIE NIKWAMBIE
Hapo tatizo sio simu,tatizo ni moyo ,unatakiwa udeal kuurudisha moyo wake.Ukihangaika na simu,simu haina shida wanaweza wakaacha kuwasiliana mme akahamia kabisa kwa mchepuko utamfanyaje?mbona simu ni kitu kidogo saaana.Wewe fanya juu chini huo moyo wake usikuponyoke,moyo ukishaponyoka hata uhack nini hamna kitu. Kuna mwingine anataka akishakuta msgs kwenye simu ya mme wake ndio aanze kufunga na kuomba,kuombea ndoa yake.Sikia tu nikupe siri sio rahisi kuomba ukishajua kuna anayekuzunguka utachemsha,utaishia tu kulia.Askari yeyote huwa hafanyi mazoezi siku ya vita,siku ya vita huwa anaenda kufanya alichofanyia mazoezi miaka au miezi kadhaa iliyopita ya maandalizi.
Huna haja ya kukamata msgs za mapenzi za mwenzi wako ndio uanze kuomba,anza kuomba sasa,wewe omba kabisa kwa nguvu zako zoote.Biblia inasema kuwa "Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.(1 Wathesalonike 5:3). Kumbe kati ya watu wanaotakiwa kuombea ndoa zao kwa mzigo mkubwa ni wale ambao saivi wanaona kuwa ndoa zao zina amani.Amani uliyonayo na furaha visikufanye ukajisahau na kulala omba omba hayo maombi yatatumika wakati wa vita.Wala haina haja ya kukuta msgs za mcheps ndo uanze kuomba .Yafanye maombi kuwa maisha yako,usiishi bila maombi,usiongeje maombi ya zima moto. Jambo jingine Biblia inasema kwamba Aogopacho mtu asiye haki ndicho kitakachomjilia; Na wenye haki watapewa matakwa yao.(Mithali 10:24)
Kuna wanawake wao masaa 24 wanawaza kuhusu michepuko,hawana imani kabisa na waume zao,kila wakati kila saa anawaza mme yuko na mtu mwingine,akichelewa tu kurudi nyumbani anawaza mme wangu yuko kwa mwanamke,simu ya mwanaume isipopatikana tu kidogo hewani mke anajua mme yuko kwa mchepuko,pesa asipoona matumizi yake anajua kapewa mchepuko. Yaani mwanamke anaishi hayo maisha ya wasiwasi wakati wote utafikiri kuku mtetea anayetafuta sehemu ya kutaga.Mara ashike simu ya mme atafute msgs na dialled calls na received calls,mara aende kwenye messenger ya facebook na whatsup,mara atafute jinsi ya kuhack number ya mmewe,mara anunue number mpya aanze kumtumia mmewe msgs na kujifanya mwanamke mwingine ili mradi tu afanye fujo.Mme akirudi ananuswa hadi nguo za ndani hadi mdomo utanuswa hahaha utafikiri mbwa wa usalama,kwa madai ya kuwa mke ni mlinzi.
Rafiki wala hatulindagi hivyo,ulinzi ni kufanya majukumu yako kama mke na kusugua goti.Hayo mengine mwachie Mungu ashugulike naye,ukisugua vizuri goti hakuna kitu ambacho kitafanyika kinyume Mungu asikujulishe.Lolote kabla halijatokea ktk ulimwengu wa mwili,Mungu atakuonyesha ktk ulimwengu wa roho na utakisambaratisha kabla hakijatokea juu kwa juu.Ndio maana nasema usighulike sana kwa namna ya mwili kuhack sijui simu na msg,shugulika magotini.Kuna mambo ukiyafanya kwa mmeo automatically utauhack moyo wa mwanaume na kikubwa ni #Unyenyekevu.,vingine nitakupa siku nyingine.Ila ukweli ni kwamba unaweza kuuteka moyo wa mmeo,kama Delila aliweza na wewe unaweza.Stop hacking your husbands phones,kwanza huo muda mnapata wapi??
Winnie Nzobakenga

No comments:

Post a Comment