Baada ya kulitumikia kanisa la TAG kwa miaka mingi kama mchungaji msaidizi na baadaye kuanzisha huduma ya injili vijijini - VHM, hatimaye Mwalimu na Mchungaji Peter Mitimingi aanzisha kanisa lijulikano kwa jina la Ghala la chakula au kwa kimombo; Warehouse Christian Centre - WCC
Mchungaji Peter Mitimingi akiwa katika picha ya pamoja na wahudumu siku ya uzinduzi wa kanisa.
Maelfu ya watu waliohudhuria siku hiyo
Na John Shabani - Dar es salaam
Baada ya kutumika katika kanisa la Tanzania Asseblies of God (TAG ) zaidi ya miaka ishirini Mchungaji na mwalimu Dr Peter Mitimingi azindua kanisa lake rasmi Kebbys Hotel Jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika uzinduzi wa kanisa hilo uliohudhuriwa na zaidi ya watu elfu tatu Dr Mitimingi amesema kuwa yapo malengo matatu ambayo yamepelekea yeye kuanzisha WCC ikiwa ni pamoja watu kukua kiroho ,wawe na Ufahamu,waijue kweli ambao utamsafirisha kupata majibu ya changamoto mbalimbali pamoja na Uhuru
Amesema kuwa wengi waneokoka na wapo makanisani miaka mingi lakini hawajakua kiroho,amesema kuwa mtu akilifahamu tatizo ni jibu sahihi kuliko kutokujua tatizo.
"Kwakutolifahamu tatizo unaweza ukatibu ugonjwa ambao siyo kabisa ila ukilifahamu tatizo utajua uanzie wapi kulitatua,kwani ratizonlinaanzia kwenye kulijua tatizo lenyewe " alisema Mitimingi
Ameeleza kuwa katika malengo hayo endapo angeendelea kuwa katika kanisa la TAG malengo hayo yasingekamilika kutokana na taratibu za Kanisa hilo.
"Sijatoka kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG )kwa ugomvi kama watu wanavyozusha bali nilikwenda kwa viongozi wa juu wa Kanisa wakanisa nilianza na nyumbani Mwenge TAG
ambapo nilikuwa mchungaji msaidizi, nikaenda kwa mchungaji wa wilaya , nikaenda kwa Makamu wa Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Dkt. Magnus Mhiche ,wote hawa walinikubali ,wakaniombea na kuniwekea mikono tayari kwa kutumika." Alisema Mitimingi.
Mungu akubariki Mtumishi kwa maono haya makubwa.
No comments:
Post a Comment