UANDISHI WA NYIMBO ZA INJILI UNAENDANA SANA NA
WITO WA HUDUMA YA MWANDISHI AU MTUNZI.
#Ushauri
kwa mtunzi au mwandishi wa nyimbo za Injili.
Usitumie nguvu kubwa kutaka
Kuandika Nyimbo zitakayozependwa au kukubaliwa
sana maarufu kama HIT SONGS.
Andika tu nyimbo kwa kadri ya msukumo utokao
ndani yako. Imba Uimbaji wako, Tumia sauti yenye upekee na si ya kuigilizia.
Fanya mziki wako ambao unaupenda kutoka moyoni.
Kuwa halisi na mkweli kwa Nafsi yako (hisia,
dhamira safi, shauku, ufahamu).
#Mashairi
au Lyrics huja kutokana na kiwango ufahamu wa Neno la Mungu, Kiwango cha Imani,
kiwango cha Ushuhuda na Uvuvio wa Roho.
#Injili
ikimgusa hata mtu mmoja ujue tayari imeshafanya kazi yake.
Nyimbo kukubaliwa au kupendwa sana si maamuzi
ya mtunzi au mwandishi hata kama yeye binafsi ameupenda au amefurahishwa sana
na wimbo huo bado sio tafsiri kwamba watu wataupenda kwa kiwango hicho hicho...
Kuna wakati watu wanaweza penda wimbo ambao
mtunzi hakuutiliana maanani sana au matarajio makubwa (hiyo nahitaga surprise).
Wimbo kuwa maarufu kuna maswala mengi
huchangia ikiwemo na promotion (kuutangaza sana).
Ila wimbo kuishi muda mrefu utatokana na kitu
ambacho huo wimbo umebeba. Kiasi gani watu wanaupokea na kuguswa mioyo au
kubarikiwa na wimbo husika. Ile Impact ambayo wimbo umesababisha ndio
husababisha nyimbo ziishi muda mrefu sana zikipendwa bila kuchuja.
Ujumbe wake na maudhui yake vina nafasi kubwa.
Kiuhalisia ni kwamba nyimbo za Injili
hazipaswi kuchuja au kupitwa na wakati kwa kuwa ni Injili Kamili na Ni Neno la
Mungu.
Hivyo nyimbo za Injili zinatakiwa zishibe Neno
la Mungu. Zimtukuze Mungu na Kumtangaza Yesu Kristo.
Usiache pia kufuatilia masomo wangu ya Sauti
na kuyazingtia. Kumbuka una kuimba kupitia kiapaji (talent), kwa kupata ujuzi
(skill) na kuimba kwa uptake au kupakwa (anointing). Sasa mwimbaji wa kipaji au
ujuzi anaweza akawafurahisha watu, akagusa watu lakini asiguse mbingu kwani
wengi wanachofanya ni kutoa burudani lakini maisha yao ni machafu. Usishanga
mtu katoka kujirusha guest house au kapigilia bia yake au kilevi chochote akita
na mzuka huo akapewa nafasi kwasababu ya kujulikana kwake akaimba au kutuongoza
katika uimbaji uliojaa uzinzi na ulevi.
Lakini uimbaji uliopakwa na Mungu mwenyewe
umejaa hofu, neema, uponyaji, kicho na Kibali cha mbingu.
Pamoja na upako bado nashauri waimbaji kupata ujuzi kwa watu
sahihi wenye uzoefu au waalimu wa sauti, ni muhimu sana
No comments:
Post a Comment