Pages

25 November 2019

WIMBO NI NINI?

Wimbo ni aina ya sanaa katika Fasihi ambayo hutumia lugha teule,sauti na kiimbo maalum. Nyimbo nyingi hugawanywa katika beti(verse) na kiitikio(chorus),pia zipo zenye kuwa na daraja/kiunganishi(bridge) na kiopoo/ndoano(hook). Pia nyimbo hutumia Ala za muziki kama vile ngoma,filimbi, gitaa na kinanda.
Ikumbukwe kuwa nyimbo zinaweza kuimbwa na mtu mmoja au zaidi.
SIFA ZA NYIMBO
1. Hutumia kiimbo au sauti maalum.
2. Huweza kuendana na Ala za muziki.
3. Huimbwa na mtu au watu kwa pamoja au kwa kupokezana.
4. Hutumia lugha ya mkato.
5. Hurudiarudia maneno ili kusisitiza ujumbe katika wimbo.
UMUHIMU WA NYIMBO
1. KUBURUDISHA.
2. KUELIMISHA, KUFUNZA, KUONYA NA KUELEKEZA, KULIWAZA, KUSIFIA KITU AU MTU KATIKA JAMII, KUUNGANISHA JAMII AU WATU TOFAUTI, KUDUMISHA/KUHIFADHI TAMADUNI ZA JAMII, KUKUZA TALANTA NA SANAA KATIKA JAMII, HUTUMIKA KATIKA MBINU ZINGINE ZA FASIHI KAMA VILE HADITHI MWISHO NYIMBO HUTUMIKA ILI KUMTUKUZA MUNGU MUUMBAJI.
Kabla sijaanza kutoa dondoo na maelezo ya namna au jinsi ya kuandika wimbo/uandishi,ni bora ukapata kujua baadhi ya mambo kuhusu nyimbo zenyewe na muziki kwa ujumla.

SONG STRUCTURE/MUUNDO WA WIMBO.
Ifahamike kwamba miundo ya nyimbo ipo mingi ikitegemea matakwa ya msanii au waandaaji wa wimbo husika.
MUUNDO WA NYIMBO ni mpangilio wa viunda wimbo katika mfutatano wa kujirudia. Hapa naongelea
1. ITRODUCTION/ITRO/MWANZO/UTAMBULISHO/UINGIAJI
2. KIITIKIO/CHORUS
3.VERSES/BETI
4.UTOKAJI/OUTRO/UMALIZIAJI/ENDING.
Viunda wimbo hivi hupangiliwa kulingana msanii anataka wimbo wake upangiliwe vipi. Ifuatayo ni mipangilio miwili pendwa na bora kutumiwa,ambayo ni;
1. Intro-chorus-verse-chorus-verse- chorus-outro.
2. Intro-verse-chorus-verse-chorus-verse-chorus-outro.
INTRO NA OUTRO.
Intro ni mwanzo wa wimbo, ni sehemu fupi ya mwanzo wa wimbo ambayo mara nyingi huwa na mistari minne tu. Mara nyingi hakuna vionjo Vingi vya midundo ni sehemu iliyo poa. Hapa ni sehemu utaaamua wimbo wako uanze vipi.
Outro ni sehemu ya mwisho ya wimbo au mwisho ambapo pia utaamua wimbo wako uishie vipi,mara nyingi ni baada ya kiitikio/chorus kurudiwa kwa mara ya mwisho au baada tu ya ubeti/verse ya mwisho inategemea na maamuzi yako msanii.
VERSES/BETI
Hiki ni kifungu kimoja cha shairi ambacho kina uzani sawa kutokana mpangilio wa vina vyako. Unaweza kuwa na verse yenye mashairi ya kimapokeo/yanayofata sheria za uandishi au verse yenye mashairi huru/ya kisasa/yasiyofuata sheria ili mradi yalete maana.
Hii ni sehemu ambayo stori yote ya wimbo huelezewa ni hapa ambapo unatakiwa kudadavua kinagaubaga ujumbe wako ukiendana na chorus/kiitikio chako pamoja na jina la wimbo wako maana ndio hubeba taswira ya beti/verse zako.
Mistari 16(sixteen bars) hutengeneza verse moja katika nyimbo mbalimbali ila sana za HIPHOP. Unaweza kuwa na verse ya misatari 8(8/eight bars), 12 adi 32,48,40/fourty bars.
Nakushauri andika mistari 16. Na mistari 8 unapoona inatosheleza mahitaji yako.
Wakati ujao tukijaaliwa nitafundisha jinsi ya kuhesabu mistari kulingana na midundo/beats,vina(vya mwanzo,vya kati,vya mwisho),pamoja na chorus/kiitikio.
By Vocal Coacher John Shabani


Anaehitaji huduma hii ya kuandikiwa nyimbo,
mawasiliano yapo apo juu.

No comments:

Post a Comment