31 March 2012
YVONNE CHAKA CHAKA AWASHIRIKISHA SOWETO GOSPEL CHOIR KWENYE ALBUM YAKE MPYA
10:39
No comments
Chaka chaka akiwa na mumewe Dr Mandlalele Mhinga.
Mwimbaji wa siku nyingi nchini Afrika ya kusini mwanamama Yvonne Chaka chaka yuko studio kwahivi sasa akijiandaa kutoa labum mpya ambayo kwa taarifa zilizopatikiana mpaka sasa katika album hiyo amewashirikisha waimbaji wengine kama Soweto gospel choir ambao juzi walikuwa studio(kwa kundi lililosalia afrika kusini wengine wako ziarani nchini Marekani) na mwimbaji huyo akiwa amewashirikisha katika nyimbo mbili,pamoja na mwanamuziki mwingine maarufu aitwaye Bono wa kundi la U2.
Chaka chaka ambaye amejizoelea mashabiki wengi barani Africa na duniani kutokana na muziki wake,itakumbukwa kwamba alipotembelea nchini Tanzania miaka ya karibuni alitangaza kwamba ameokoka na amekuwa ni mtu wa kanisani kumwabudu Mungu pamoja na kila kitu anachofanya anamtegemea Mungu,mpaka sasa haijajulikana ni nyimbo ngapi zitakazokuwemo kwenye album hiyo na ni nyimbo za aina gani, ingawa tayari amewashirikisha waimbaji kama Soweto gospel choir hata hivyo si kigezo album hiyo kuwa ya dini,ukweli utajulikana itakapotoka au yeye mwenyewe atakapotoa taarifa rasmi.
Chaka chaka ambaye mwishoni mwa mwezi January mwaka huu aliweza kuandika historia kwakuwa mwanamke wa kwanza kutoka Africa kupata tuzo ya World Economic Forum (WEF) iitwayo crystal award kutokana na juhudi zake katika kupambana na malaria pamoja na kazi nyingine za kijamii kwa ujumla,mwimbaji huyo ambaye enzi za utoto wake alikuwa mtoto wa kwanza mweusi kuonekana kwenye runinga ya taifa, south african television ambayo kwasasa inafahamika kama SABC,amekuwa na mafanikio mengi katika maisha yake ya muziki ambapo yeye na mumewe Dr Mandlalele Mhinga wanamiliki kampuni ya magari ya kifahari ya Limousine huko nchini kwao na shughuli nyingine.
26 March 2012
CALVARY GROUP BAND, BAND INAYOFANYA VIZURI AFRIKA MASHARIKI
10:46
No comments
Hawa si wengine, bali ni Calvary Group Band, kikundi chenye makao yake jijini Dar es salaam. Chini ya ulezi wa Askofu Moma wa kanisa la Calvary Tebernacle, band hii imekuwa ikifanya vizuri na kuwa kivutio kikubwa katika nchi kadhaa za Afrika. Siri kubwa ya waimbaji hawa kufanya vizuri ni kwa sababu pamoja na maombi, kusoma neno pia wamevunja mipaka ya ukabila, kwani ni kundi pekee lenye mchanganyiko wa watu kutoka nchi mbalimbali kama DRC kongo Tanzania n.k
Tutaendelea kukujuza zaidi kuhusu Kalvary G Band.
Tutaendelea kukujuza zaidi kuhusu Kalvary G Band.
24 March 2012
MWIMBAJI MAHIRI WA INJILI AZIDI KUNG’ARA HUKO INDIA
11:00
No comments
Mwana dada mwenye vipaji vingi azidi kufanya vizuri akiwa ugenini huko india. Huyu si mwingine bali ni Sarah shilla, mwimbaji mwenye sauti yenge mguso wa kipekee
Mwana dada huyo hivi kribuni, ametunukiwa tuzo ya heshima katika chuo kimoja maarufu huko india.
Akiongea na John shabani ambaye ndiye mmiliki wa blog hii, sra anasema na hapa nanukuu < ilikua tuzo nilipewa chuoni kwa kushiriki vitengo mbali mbali na vyuo vingine na kushinda ikiwemo debate, kuimba, maswala ya fashion shw,, so kutokana na kushiriki vitengo vyingi ndo nikapata hiyo tuzo>
Keep it up sister sara
22 March 2012
KADI ZA CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI ZAANZA KUTOLEWA KWA WANACHAMA
03:46
No comments
MEMBERSHIP CARD
KADI ZA UANACHAMA
Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (Chamuita) ni chama halali kilichosajiliwa na kutambulika na Srekali ya Tanzania. Namba ya usajili ni BST 4598
Tunapenda kuwatangazia kuwa, Kadi za chama cha muziki wa injili Tanzania zimeanza kutolewaa kwa wanachama wanaoendelea kujaza fomu za kujiunga na chama hicho. Ewe mwimbaji, mwanamuziki, mtengenezaji, msambazaji na mpenzi wa nyimbo za injili, hakikisha umejiunga na chama cha muziki wa injili Tanzania (Tanzania Gospel Music Association) ili upate kadi yako. Kadi hii itakusaidia sana. Chama hiki kimesajiliwa na kutambuliwa na serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, pia ni moja ya vyama vinavyounda shirikisho la muziki Tanzania, shirikisho ambalo ni mwanachama wa shirikisho la muziki Duniani.
MALENGO NA MADHUMINI
Chama kitaendeshwa kama chombo kisicho na malengo ya kupata faida na chenye malengo na madhumini yafuatayo;-
i) Kulinda utamaduni wa Tanzania na heshima ya muziki wa Injili, sawa na Neno la Mungu
ii) Kuhamasisha maendeleo ya muziki wa Injili na nyanja zake nyingine
iii) Kutoa ushauri katika mambo yote yahusuyo muziki wa Injili, na watumishi wa Mungu waimbaji pia.
iv) Kuwakilisha na kulinda maslahi ya wanachama kitaifa na kimataifa.
v) kuwa chombo cha kuwezesha mawasiliano kati ya watu na vikundi katika kupeana taarifa kuhusu muziki wa Injili hapa nchini, na pia kuwezesha mawasiliano ya kimataifa.
vi) Kuwa na rejista ya wanamuziki wa Injili na kazi zao. Ili kusaidia kulinda na kutangaza haki za wanachama.
vii) Kutafuta mapato kwa njia ya ada, michango, harambee, maonyesho, kukopa, ufadhili au zaidi katika kuendeleza malengo na madhumuni ya Chama.
viii) Kuwawezesha wanamuziki wa Injili kwa njia ya kuwaongezea elimu
ix) Kuinua hadhi ya muziki wa Injili nchini
x) Kutambuliwa rasmi na Serikali yetu na wadau wengine
xi) Kuwekeza katika miradi, na kujipatia kipato kwa njia ya kuwakomboa jamii ya wanamuziki wa injili.
kwa maawasiliano: Mob: 0754 818 767, 0716 560094.
E-mail: touchingvoice@yahoo.com
20 March 2012
DON MOEN NA WENZAKE KUPAMBA TAMASHA KUBWA LILILOANDALIWA NA UMOJA WA MAKANISA JIJINI DAR ES SALAAM.
03:35
No comments
Umoja wa makanisa ya Dar es salaaam ukishirikiana na shirika la kimataifa la LUISPALAU association,liko kwenye mikakati la kufanya tamasha kubwa la injili la upendo maeneo ya Jangwani kuanzia mwezi wa nane hadi mwezi wa 12 mwaka huu, na tamasha hili litafanyika jijini Dar es salaam kama sehemu ya mfululizo wa matamasha ya jinsi hiyo ambayo shirika hilo imekuwa ikiyaendesha katika miji mikuu kadhaa barani Africa.
Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo,iliyoundwa na makanisa mbalimbali jijini hapa,tamasha hilo litawaleta nchini wanamichezo mbalimbali wa kimataifa pamoja na waimbaji mashuhuri wa injili,akiwemo Don Moen,Nicole Mullen na wengine wengi,taarifa hiyo imebainisha kuwa wanamichezo wa kimataifa wanaoruka na pikipiki pamoja na baiskeli ya mashirika ya BMX na Fmx nao pia wataalikwa.
Nicole Mullen.
Kwamujibu wa taarifa ya mwenyekiti wa tamasha hilo Askofu Philemon Tibanenason ameongeza kuwa makanisa hayo yamepata fursa ya pekee ya kufanya kazi katika umoja kudhihirisha upendo wa Yesu ubadilishao maisha,tamasha hilo limewahi kufanyika katika miji kama Kigali Rwanda,Bujumbura Burundi,Kampala Uganda na Cairo Misri.
source---gazeti MSEMAKWELI/Gospel kitaa
source---gazeti MSEMAKWELI/Gospel kitaa
19 March 2012
FLORA MBASHA NA MUMEWE WAGUSA MIOYO YA WAMAREKANI
10:25
No comments
Mabango ya huduma ya flora mbasha yalivyozangaa mitaa ya marekani
Flora Mbasha na mumewe wakiimba kwa upako Jumapili katika kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministires huko Adelphi Md.
Mambo ya stejini
Haya bwana, mambo ya majuu hayo
Mbasha na wenyeji wake wakipata maakuli
17 March 2012
MWIMAJI MAARUFU WA BONGO FLEVA RENEE LAMIRA, AWA MTUMISHI WA BWANA
11:47
No comments
Bila shaka unamkumbuka mwanamuziki au mwimbaji Renee Lamira(pichani).Aliwahi kutamba vilivyo na albamu yake iliyoitwa Ngoma ya Kwetu.Lakini je unafahamu kwamba Renee siku hizi ameachana na nyimbo zinazoitwa za “kidunia” na badala yake anafanya nyimbo za injili Kama inavyojulikana kwa wengi Renee Lamira aliyekuwa kinara wa wa nyimbo za Bongo fleva na kupata heshima na umaarufu mkubwa dhidi ya mashabiki wake, Alitamba kwa album yake ya NGOMA YA KWETU pia alifanikiwa kutumbuiza Kora hukoo Afrika Kusini, Renee kwa sasa ameokoka, na zaidi ya hayo pia ni mchungaji katika huduma ya CHRIST EMBASY tawi la mbezi Dar ea salaam
Subscribe to:
Posts (Atom)