John Shabani akiwa na baadhi ya wanafunzi wenzake wa sauti
John Shabani akisimamia waimbaji katika kuandaa wimbo wa miaka 50 ya uhuru wa Tanzania
0716 560094
Haya ni masomo machache
sana niliyoyachagua kati ya mengi ili kukupa hamasa kujiunga na darasa la
uimbaji linaloendelea katika kituo chetu cha mafunzo, Kamara Dar es salaam chini ya mwalimu John
Shabani na timu yake
Karibu ujifunze.
Lakini pia kwa wale wanaotaka kurekodi nyimbo zenye ubora na kufanya video zenye ubora, nimefungua studio yenye vifaa vya kisasa, unaweza ukatazama baadhi ya video zangu kama;
- Mtoto wa mfalme by John shabani
- Futa machozi by John Shabani
- Nakupenda by John Shabani
Karibu sana.
Utangulizi:
Nianze kwa kusema kwamba , kwa
wale wanaofahamu maana ya bora ktika muziki, ni kwamba ni kosa kubwa sana na
hairuhusiwa kuingia kwenye music recording studio bila kupitia vocal studio.
Kwa wenzetu unapotaka kuingia studio lazima uwe na voice coacher, vikundi
mbalimbali vya uimbaji lazima view na voice coache.
Kazi kuu ya voice coacher ni;
-
Kufundisha ( training)
-
Kukushauri (councel)
-
Na kulea kipaji hadi mtu atoke (mental)
MALENGO/MAONO
1.
Kuvipata/kuviendeleza na kuviwezesha vipaji vya uimba
2.
Kuwa ni program ya uimbaji itakayoongoza kimafanikio Tanzania
MAWASILIANO
Mob: 0716560094, 0754818767
E-Mail: touchingvoice@yahoo.com
Mambo ya msingi yanayofunzishwa
katika program hii:
Ø
Historia
ya uimbaji
Ø
Tofauti
ya mwimbaji na mwanamuziki
Ø Kuwa
na sauti bora au afya ya sauti (vocal health)
Ø
Vyakula
na vinywaji vinavyofaa na visivyofaa
Ø
Sifa
na mbinu za kuwa mwimbaji bora au uimbaji kitaalam
Ø
Jinsi
ya kuitunza na kuiponya sauti yako
Ø
Amri
10 za mwimbaji (za sauti)
Ø
Matumizi
ya kipaza sauti (Microphone technique)
Ø
Utunzi
au uandishi wa nyimbo
Ø
Mazoezi
ya viungo yanayofaa kwa mwimbaji na faida zake
Ø
Ushauri
kwa wanaotaka kurekodi nyimbo
Kumbuka moja ya vitu vya msingi katika uimbaji ni nguvu (energy) “As
you sing higher, you must need more energy, as you sing lower, you must
useless”. Zipo nguvu za kiroho na za kimwili. Ili kuwa na nguvu za kimwili
unahitaji maji ya kutosha, chakula kizuri pamoja na mazoezi ya viungo.
KUIMBA
Kuimba
ni mpangilio wa maneno na sauti unaoleta ladha fulani inayopendeza kwenye sikio
la mwanadamu, ni kutamka maneno katika hali ya ki-muziki au pia twaweza kusema
ni kutamka maneno moja baada ya jingine kwa sauti yenye lahani (sauti ya ala ya
muziki, tuni) au ghani (Singing is the act of producing musical sounds with the voice)
Mwimbaji ni mtu yeyote mwenye uwezo wa kuimba au bila
vyombo vya muziki (be sung a cappella) au kwa kutumia vyombo. Mwimbaji huyo kwa
lugha ya ki-muziki anaitwa vocalist. Ikumbukwe kuwa pia katika vikundi vya
uimbaji wapo wale wanaoongoza wengine katika uimbaji (A lead singer) na wengine kazi yao ni kuitikia (backing singers)
N.B Mwanadamu yeyote mwenye uwezo wa kuongea,
anao uwezo wa kuimba pia.
Kama vile
tulivyo na ala za aina mbalimbali, mwimbaji naye pia anazo ala mbili muhimu:
Mdomo wenye uwezo wa kutoa sauti
ya uimbaji
Mwili
Kumbuka moja ya vitu vya
msingi katika uimbaji ni nguvu (energy)
Mckinney alisema: “As

useless; as you sing higher, you must
use more space; asa you sing lower, youmust need use less””. Inamaanisha
kadri unavyotumia sana sauti hasa kwa sauti ya juu sana, ndipo unapohitaji pia
nguvu kubwa, japo wapo watu kwasababu ya uzoefu wa kuimba kwa muda mrefu au
kupitia madarasa kama yale yanayofundishwa na mwalimu John Shabani, kwao kuimba
sauti ya juu au ya chini ni jambo la kawaida.
Zipo nguvu za kiroho na za kimwili. Ili kuwa
na nguvu za kimwili unahitaji maji ya kutosha, chakula kizuri, hewa pamoja
na mazoezi ya viungo maalum kwaajili ya uimbaji au ya pumzi.
Mwimbaji pia anahitaji
Pumzi ya kutosha (Breathing support), chakula kizuri na maji ya kutosha.
UIMBAJI KITAALUMA
Mwimbaji asiyejua kuimba hawezi kuwa huru kuhudumu ni muhimu afahamu uimbaji
ili aimbe kwa uhuru na kwa ufanisi. Ufanisi unahitaji muda wa mazoezi yakutosha
pamoja na mwalimu mwenye uwezo wakukuelekeza jinsi ya kuimba Muziki (uimbaji), mambo
hayo upo katika mafungu makuu mawili :
I. Vocal
II. Instrumentals
VOCAL: Ni sauti ya wanadamu. Sauti isiyochanganywa kitu chochote. Sauti asilia
ya mtu (Natural voice)
INSTRUMENTALS:
Ni sauti zitokanazo na vyombo. Sauti pasipokuchanganywa na kitu chochote yaani
ala za muziki. Sehemu hizi mbili zikichanganywa pamoja hufanya kitu kinachoitwa
muziki (uimbaji) na kukamilisha maana ya NENO MUZIKI.
SAUTI. Ni hisia inayonaswa na masikio na hutokana (hutengenezwa) na msuguano wa
hewa katika mzunguko, mgongano wa vitu au mkwaruzo kiasi cha kutoa mlio
(sauti).
SAUTI –MLIO (AUDIBLE, SOUND)
1. Kitaalamu Sauti ina misingi au kanuni .
Misingi hiyo ni Miwili. Ni kwa misingi ya sehemu hizo mbili kuu- Sauti
hujengwa/huumbika, tutaelewa misingi hiyo vizuri kwa kuziangalia tabia za sauti
(Characteristics of Musical Sound) Au tabia za milio.
Msingi wa
kwanza:
Sehemu
hii ya kwanza nazungumzia nadharia ya tabia za sauti, tabia hizi huwezi kuziona
wala kuzihisi, ila unaweza kuzifikiria katika mawazo.
a) Sauti ina tabia ya – Melody – Yaani kwa Kiswahili – Ghani
Melody – Ghani – (Mpangilio wa nota
na maneno kimuziki). Ni mistari ya sauti ya muziki inayotambulisha chanzo
(tone) cha wimbo ni sauti yenye kuelekeza ubora wa mtiririko wa ghani (melody)
unaokupa hisia ya mlio unaohusika au unaousikia.
b) Rhythm – Ni utaratibu au mfumo wa
aina ya mwendo wa sauti katika wakati au mfululizo wa sauti katika muda,
mwendo, pigo, mdundo au msisimko. Uwezo wa sauti wa kutembea katika wakati
usiobadilika.
c) Harmony – Mkusanyiko wa sauti unaopendeza, utaratibu au mfumo wa ulinganifu
wa sauti, usawa, muafaka, kusikilizana pasipokuachana kwa sauti au kuwa nje ya
tune hasa wakati kuna watu wengi wanaimba, katika ngazi tofauti yaani sauti ya
msitari wa 1, 2, 3 na 4 pamoja.
d) Unison—Ni sauti ya aina moja
inayoimbwa na watu wengi bila ya kutofautisha ngazi za sauti ya kwanza,
pili,tatu na nne. Na kwa kawaida sauti ya unison hutumia sauti ya kwanza.
e) Form – Ni mwonekano wa kipekee, utaratibu au mfumo wa kuweka uimbaji katika aina
ya mfumo unaojitambulisha katika mtindo wake wenyewe kama vile mtindo wa
kizungu, wa kiafrika, kigogo, kihaya nakadhalika.
f) Tone Color – Aina mbalimbali za
sauti kufuatana na chombo au mtu anayeimba – kwa mwanadamu sauti hutegemea
mapafu yake na mishipa ya fahamu ya kichwani. Yaani sauti kavu, sauti laini,
yenye mikwaruzo, yenye mawimbi nakadhalika, kusikika kwa sauti kipekee, kivyake
kwa kadri ya mtu anavyotoa sauti au chombo kinavyo toa sauti kwa namna ya mlio
wake.
3. Msingi wa Pili:
Sehemu ya kwanza Nimetaja nadharia ya tabia za sauti, tabia hizi huwezi kuziona
wala kuzihisi, ama kuzisikia, ila unaweza kuzifikiria katika mawazo. Kuimba sio
nadharia wala mawazo ni matendo halisi. Nadharia hiyo lazima itafsiriwa katika
vitendo tunavyoweza kuviona, kuhisi, kusikia tabia za sauti au milio hiyo. Haya
yanawezekana kwa kutumia nyenzo , njia za muziki za kiufundi zinazotuwesha
kutenda. (Musical Skills Performance Methods)
Katika msingi huu wa pili tunafika
katika kukamilisha muziki na ndiyo uimbaji. Muziki ni sayansi lakini kila mmoja
wetu anayo na anaweza kuitendea kazi kwa kujifunza na kujizoeza.
Nyenzo au njia hizo ni:
a) Kuimba – (Singing – Melody)
Unapoimba ndipo Ghani itajitokeza katika mpangilio wa sauti kwa njia
inayopendeza na kwa utaratibu, hapo Tone Color itasikika yaani kwa kuimba
wimbo, ghani na aina za sauti katika ubora wake utasikika.
b) Kupiga vyombo vya muziki – Accompanyments
– vikolezo. Melody ambayo ni Ghani itasikika – Tone color pia itasikika.
c) Form, Kutenda vitendo – (Moving –
Movement –Steps) Rhythm na Form itaonekana yaani kucheza kwa mwendo wa mapigo.
Yaani sauti na maneno unayoimba yataenda kwa kufuata mapigo na midundo ya wimbo
na kuwa na muonekano wa kipekee.
d) Harmony. Kusikiliza ndiko
kutakuwezesha kuleta ulinganifu katika mkusanyiko wa sauti za kupendeza na
kukuwezesha uimbe sawasawa na sauti nyingine bila kuhitilafiana wala kuachana
au kuwa nje ya ghani.
e) Kuunda au Ubunifu (Creation –
Form, Rhythm na melody) Wimbo utakamilishwa kwa kuunganisha nyenzo hizo nakuwa
halisi yaani wimbo halisi wenye kusikika vizuri.
SIFA ZAKUWA MWIMBAJI BORA
Mambo muhimu yatakayokufanya uwe muimbaji bora;
Haya ni mafunzo ya msingi na ya kwanza kwa mtu anayetaka kujifunza kuimba au
kuwa mwimbaji bora. Sisi tunaita mafunzo ya chekechea kwa mwimbaji.
1.
Breath au breathing (pumzi au kupumua).
Jambo la kuzingatia na la kuelewa ni kwamba; msingi wa uimbaji (the foundation
of singing) ni pumzi. pumzi huhitajika sana
wakati wa uimbaji muimbaji mzuri
ni yule anaye jua kutumia pumzi yake vizuri, muimbaji asipokuwa na uwezo wa
kutumia vizuri pumzi katika maeneo yasio
takiwa itasababisha sentensi ya wimbo kukatika katika .vile vile muimbaji usipokuwa na pumzi utashindwa kuimba noti za
juu na katika noti ambazo unatakiwa uimbe na uzivute kwa muda hautaweza na itakusababishia
uimbe na kutoifikia pitch kama hauna pumza anza sasa kufanya mazoezi ya pumzi. Hivyo katika eneo hili tunajifunza
mazoezi ya kujenga uwezo wako wa kupumua. Zipo mbinu nyingi (teknics), moja
wapo ni;
-
Hissing sound (z, s, v)
-
Ballon teknics (mbinu ya
pulizo)
-
Book method
-
Birthday cake
-
Three methode (mbinu ya mti).
Hii tunaita ni aina ya juu sana ya mafunzo ya sauti (a deep breathing method)
n.k.
2.
Pitch
–pitch (Ear training) – yaani kufundisha sikio lako kujisikia mwenyewe kama uko
sahihi au la au kuwasikia watu wengine. Pitch ni uwiano wa sauti yako mwimbaji pamoja
na vyombo au waimbaji wenzio kutegemea na (key) ufunguo unaoimbia au mnaoimba.
mwimbaji asipoimba katika pitch humpelekea muimbaji huyo kuimba nje ya ufunguo
(out of key) kwa sababu ule uwiano wa sauti yake na ya vyombo katika
(key) ufunguo unaoimba unakuwa haupo kama unatatizo katika eneo hili unahitajika sana kufanya mazoezi ya pitch
3.
Rhythm-ni
mapigo ya mziki kwenda katika mwendo
usio badilika na kuwa na idadi sawa ya
mapigo katika kipimo(measure), mwimbaji lazima awe na uwezo wa kuimba na
kufuata beat (mdundo),vile vile na uwezo
wa kuimba akifuata ridhimu ya wimbo.
4.
Voice
(sauti) – Tone -
Range (ukomo wa sauti kwenda juu na chini) mwimbaji ni vizuri uimbe
katika sauti yako ya asili lakini sauti yako inabidi iwe inatoka au kuimbwa kwa
kufuata misingi ya kimuziki unatakiwa kufanya mazoezi ya sauti(voice training)
ili kuiboresha sauti yako pia fanya mazoezi ya kuimba scale mbali mbali za
muziki kama moja scale chromatic scale arpeggios…
5.
Diction
(lafudhi au matamshi) kujifunza sauti peke yake haitoshi bado unatakiwa kujifunza
kuimba na kutamka maneno vizuri ili wasikilizaji waweze kukuelewa
unachokiimba hivyo kuumba matamshi ni kitu muhimu sana katika uimbaji.
Baadhi ya mafunzo ya matamshi ni kama;
-
Zima
switch, washa switch
-
Masachusets
-
Entusiasm
Zingatia pia: Kusimama
kwenye ufunguo (Key), mwonekano, (appearance), Uwezo wa kuitumia sauti na
kuitawala (Manage your vocal), kuua lafunzi ya asili kulingana na aina ya
uimbaji, mwanekano jukwaani(Stage presence), kuwa na sikio la muziki eitha
ukiwa peke yako au katikati ya wengine, kujiamini, kujitambua, lugha ya mwili
(body language) kujithamini (Self Cofidance), kuwa mbunifu na kujitengenezea
swaga zako binafsi huku zinazoendana na muonekano wako usoni na mwili mzima
(facial expression). Kujituma, kujiachia lakini usipitilize, mawasiliano na
watu wengine ikiwa ni pamoja na wapigaji na madhabau n.k.
HATUA 4 ZA KUREKODI AU KUWA
NA ALBAM BORA
(Mwimbaji kuwa bora, tungo au ujumbe bora, muziki bora, Studio bora)
NGUZO 4
ZA MUZIKI
Kusikiliza muziki/uimbaji (Listening), Kuhifadhi muziki/uimbaji
(Copying), Kuiga au kukariri (imitate), Kuzalisha muziki (producing)
Mazoezi kwa mwimbaji
Yapo mazoezi maalum
kwaajili ya kuboresha uimbaji na pia kumfanya mwimbaji awe na nguvu ya kutosha
na kuepukana na baadhi ya magonjwa. Kwa ushauri zaidi wasiliana na mwalimu John
Shabani.
Pamoja na faida nyingi za
mazoezi lakini pia mazoezi huchangamsha mwili, hulainisha koo, husaidia kuwa na
pumzi ya kutosha, hukuhepusha au kupunguza baadhi ya magonjwa kama kisukari,
presha n.k, hung’arisha ngozi, na kusaidia mfumo wa mzunguko wa damu, mazoezi husaidia katika mfumo wa
usagaji chakula kuwa mzuri , kukupa nguvu na kuweza kufanya kazi kwa nguvu zako
bila kujiskia umechoka na mwisho wa siku hupunguza mafuta mwilini, hupunguza uzito, kunyoosha na kuimarisha
misuli ya mwili, husaidia mapigo mazuri ya moyo kwa kuongeza kasi ya mapigo
yake wakati wa mazoezi, hupunguza mrundiko wa damu kwenye mishipa, hii ni
muhimu kwa sababu mgando wa damu husababisha magonjwa ya moyo pamoja na
kupoteza fahamu, mazoezi huimarisha mifupa ya mwili, huboresha usingizi ambao
unafaida sana kwa mwimbaji.
Fikiria mwenyewe kama mwanamichezo
au mtu wa fani fulani na jifunze kuwa mtu wa kula na kunywa kulingana na fani
yako: Aina ya chakula na kinywaji na muda
wa kutumia ni jambo la kuzingatia sana. Kula na kunywa ni muhimu lakini
Jiepushe na ulafi kwani huleta uchovu, mfumo wa kupumua kuathirika na wakati
mwingine kusababisha magonjwa.
Kuna misimu fulani kama msimu wa vumbi au baridi kali au alegi au matatizo
mengine kibao, wakati mwingine aina fulani ya dawa kwa ajili ya ugonjwa fulani,
Wakati mwingine husababisha mafua au kutokwa na kamasi mara kwa mara au
kukausha koo kabisa, hivyo husumbua sana na kuathiri mfumo wako wa kuimba.
Wakati mwingine mazingira ya shughuli au kazi tuzifanyazo au pia mazingira ya
makazi huweza kuathiri sauti zetu. Hivyo masomo ya utunzaji wa sauti ni ya
muhimu sana.
VYAKULA NA VINYWAJI KATIKA UIMBAJI
1.0 Utangulizi
Uimbaji ni taaluma kama zilivyo taaaluma zingine za sheria, elimu, uhandisi,
usimamizi wa fedha, biashara na kadhalika. Taaluma hizo na zingine
zinautaratibu uliowekwa ili kumfanya mtu asiyejua kujua na hatimaye kuitwa
mwanasheria, mwalimu/mwezeshaji, muhandisi au msimamizi wa fedha. Hivyo basi,
uimbaji nao una taratibu zake hata mtu akafikia kiwango cha kuthibitika kuwa ni
muimbaji ama kwa kupewa cheti au kuonesha uwezo wake mbele ya wengine;
kanisani, kwenye majukwaa ya matamasha ya uimbaji na kadhalika.
Kwahiyo, makala hii imelenga
kumsaidia muimbaji kumpa sheria na taratibu za uimbaji hususani katika suala
zima la chakula gani muimbaji ale au asile na vinywaji gani muimbaji anywe au
asinywe ili awe na uwezo wa kuimba vizuri mahali popote.
2.0 Nafasi ya Vyakula na Vinywaji katika uimbaji.
Katika suala la kula na kunywa muimbaji yeyote anaweza kufananishwa na
mkimbiaji. Mkimbiaji hawezi kujishindilia chakula kingi au kunywa maji mengi
wakati akijua anakwenda kwenye mazoezi au mashindano ya kukimbia umbali wa
maili fulani. Hii ni kwa sababu, atashindwa kukimbia vizuri. Hata muimbaji;
hawezi kula au kunywa kwa kupitiliza halafu asipate shida wakati wa zoezi la
kuimba. Hii ni kwa sababu, kushiba sana kunazuia zoezi la upumuaji wakati wa
uimbaji na kusababisha muimbaji kushindwa kutengeneza sauti nzuri za uimbaji.
Pia, mkimbiaji hatokuwa na nguvu za
kukimbia kama hatokula chakula cha kutosha au kunywa maji ya kutosha. Muimbaji
halikadhalika, anahitaji kula chakula na kunywa maji kwa kuwa uimbaji ni kazi
ngumu ambayo inahitaji virutubisho vya kutia nguvu mwili ambavyo vinapatikana
katika vyakula na vinywaji tunavyotumia katika maisha yetu ya kila siku. Hivyo,
kula na kunywa ni jambo la muhimu sana kwa muimbaji katika zoezi la uimbaji
lakini kwa tahadhali. Kama nilivyotangulia kusema, kuimba ni kama riadha,
inahitajika nguvu kwa ajili ya utendaji wako. Hata hivyo, ni muhimu pia kuepuka
kuimba tumbo likiwa limeshiba sana. Yapo madhara mengi yanayotokana na shibe.
Unaweza ukawasiliana na mwalimu wa sauti ili kujua madhara hayo
2.1 Tahadhari ya vyakula na vinywaji katika uimbaji (nini muimbaji
hapaswi kula au kunywa katika siku ya uimbaji na wakati wa uimbaji)
Muimbaji asishinde na njaa au kutokunywa maji kabisa siku ya uimbaji. Hii ni
kwa sababu, kutokula kutanyong’onyesha mwili wake hivyo atashindwa kuimba kwa
ufanisi. Zingatia: kama muimbaji amefunga; atumie maji (anywe kidogokidogo) ili
kulainisha na kulifanya koo lake lisiwe kavu. Pia, maji yatampa muimbaji nguvu
ya kusimama na kuwahudumia watu kwa muda uliopangwa.
Muimbaji asinywe kinywaji chochote chenye kafeni. Hii hujumuisha
vinywaji kama vile; kahawa, cola (soda), chai ya rangi nyeusi (black tea) na
vinywaji vyote ambavyo vina cafeni ndani yake. Vinywaji hivi ni kichochezi cha
mkojo na hufanya mwili wa muimbaji kushindwa kufyonza maji kunakosababisha
mwili kukauka au kuishiwa maji ambayo ni muhimu sana katika kumpa muimbaji
nguvu ya kuimba. Pia, vinywaji hivi husababisha; kuzalishwa kwa kitu kama
uteute (kamasi) kwenye kinywa na koo, ukavu na maumivu kwenye koo, huleta
kiungulia na kusababisha kucheua mara kwa mara wakati wa uimbaji.
Zingatia: Kama muimbaji anashindwa kuacha vinywaji hivyo,
inashauriwa kusukutua koo kwa maji mara baada ya kunywa kinywaji cha namna hiyo
kwa siku nzima ili kusafisha koo na kuepuka athali zisababishwazo na vinywaji
hivyo katika uimbaji. Pamoja na hilo, muimbaji anywe maji mengi; zaidi ya glasi
nane kwa siku. Au, Muimbaji atumie chai nyeusi (black tea) ambayo inaelezwa
kuwa na kiwango kidogo sana cha kafeni. Ila matumizi ya chai ya kienyeji ni
bora zaidi (mchaichai).
Muimbaji asile vyakula au kunywa vinywaji vinavyoongeza au kuacha uteute
kwenye kinywa na katika koromeo kabla na wakati wa uimbaji. Mfano wa
vyakula hivyo ni mayai, maziwa, ‘ice cream’ na bidhaa zingine za maziwa kama
pipi, ‘chocolate’, biskuti, keki, siagi, samri, koni na kadhalika. Uteute
unaosababishwa na vyakula na vinywaji hivyo huzuia utokaji mzuri wa sauti ya
uimbaji wakati wa kuimba. Ndio maana utakuta waimbaji wengine wanahama funguo
za muziki au kushindwa kuimba sauti za funguo za juu au kupata tatizo la
kushindwa kupanda na kushuka vema kwa sauti wakati wa uimbaji.
Muimbaji asitumie vyakula au vinywaji vinavyokausha koo. Mfano wa
vinywaji hivyo ni kama vile; pombe, matunda jamii ya ndimu kama chungwa, limao,
chenza, daransi, embe bichi, na kadhalika. Kukauka kwa koo kutasababisha sauti
ya muimbaji kutotoka vema kwasababu koo lake ni kavu.
Muimbaji asitumie soda na vinywaji vyovyote vinavyotoa povu wakati
vinapofunguliwa. Vinywaji hivi huweka gesi/hewa tumboni na kumfanya
muimbaji kubeu na/au kucheua hovyo na kusababisha muimbaji kupata shida wakati
wa kuimba na kutoa sauti mbaya.
Muimbaji asile vyakula ambavyo vitaacha vitu kama makapi kwenye koo
lake. Vyakula hivyo ni kama vile; bisi, mahindi, karanga, tambi kavu,
chama, na kadhalika. Ulaji wa vyakula hivi kabla na wakati wa kuimba
husababisha ugumu wa utoaji wa sauti za kuimbwa. Pia, makapi hayo wakati
mwingine hurukia katika koo la chakula na kusababisha muimbaji kupaliwa na
hatimae muimbaji kushindwa kupumua vema, kukohoa na kuimba vibaya.
Muimbaji asile vyakula vya mafuta sana;
kama vile nyama zilizonona na
kadhalika. Pia, sukari nyingi haifai kwa muimbaji.
Muimbaji asile vyakula au vinywaji vinavyoleta mwasho au kukera koo
(throat irritants), vinavyochangamsha, kusisimua au kulewesha (Overly spicy
foods) kama vile; kahawa na pilipili, vinywaji baridi sana, sukari
iliyosafishwa, chocolate na kadhalika.
Muimbaji asitumie Jamii ya vitu vyenye alkoholi, Sigara, tumbako,
bangi, ugoro na aina yoyote ya madawa ya kulevya kwakuwa vinaathali kubwa
kwenye koo na mapafu ambavyo ni viungo muhimu sana katika utengenezaji wa sauti
bora za uimbaji.
Muimbaji asitumie vyakula vyenye madhara kwa mwili wake (mzio;
allege). Kwa mfano, baadhi ya waimbaji hupata shida baada ya kula matunda jamii
ya machungwa, ngano, karanga, samakigamba, soya na kadhalika.
Muimbaji asitumie vyakula vyenye mafuta
mengi, na nyama nyekundu kama ya ng’ombe, mbuzi na kadhalika.
2.2 Vyakula na vinywaji vitakavyofanya muimbaji aimbe vizuri (vyakula
na vinywaji ambavyo muimbaji anashauriwa kuvitumia kabla na /au wakati wa
uimbaji)
Muimbaji ale chakula cha wastani
(kiwango cha kutosheka) masaa mawili kabla ya uimbaji. Hii itasaidia chakula
kumengenywa vema na kumpatia muimbaji nguvu wakati wa kuimba. Kushiba sana
(kuvimbiwa) husababisha tumbo kushindwa kumeng’enya chakula kwa haraka na hivyo
kutamfanya muimbaji ashindwe kutoa sauti vema. Hii ni kwa sababu, tumbo
litashindwa kusukuma hewa kutoka nje ili kutengeneza sauti nzuri za uimbaji.
Pia, muimbaji atakuwa anabeua na kucheua hovyo wakati wa kuimba hali ambayo
humfanya kutoa sauti mbaya au kushindwa kuimba kabisa.
Muimbaji anywe maji ya kawaida
(room temperature water) yaani yasiwe ya moto wala ya baridi au barafu. Maji
hayo yanywewe masaa mawili kabla ya uimbaji. Maji haya yatampa nguvu muimbaji,
yatafanya koo la muimbaji kuwa bichi (sio kavu) na mwili kutokuwa mkavu.
Muimbaji hanabudi kutambua kuwa matumizi ya maji ya moto hutanua na maji ya
baridi (au barafu) husinyaza/hubana koromeo hivyo kusababisha kiboksi cha sauti
kushindwa kutengeneza sauti za kuimba vizuri na muimbaji ataimba vibaya.
Zingatia: Unaweza kunywa maji ya moto au ya baridi baada ya uimbaji na sio
kabla au wakati wa uimbaji.
Muimbaji ale matunda yenye maji mengi kwa ajiri ya kuufanya mwili wake
kufyonza maji na kupata nguvu. Mfano wa matunda hayo ni pamoja na tikiti
maji, tango na kadhalika.
Muimbaji ale mboga za majani zenye
maji mengi kwa ajiri ya kuufanya mwili kupata maji, chumvichumvi na madini
ambavyo vyote ni virutubisho vitakavyompa muimbaji nguvu ya kuimba na kutoa
sauti yake vizuri wakati wa kuimba. Mfano wa mboga hizo ni pamoja na mchicha,
tembele, ‘spinach’, ‘chinise’, na kadhalika.
Muimbaji anaweza kutumia asali, na chumvi kidogo ni nzuri kwa koo la lake
katika siku ya uimbaji.
NB. Matumizi ya chai ya mitishamba
(mchaichai) ni bora zaidi kwa afya ya koo na tumbo lako ili kusaidia
utengenezaji wa sauti nzuri za uimbaji.
3.0 Hitimisho na mapendekezo.
Koo hupendezwa, hutulizwa, huburudishwa, hutengenezwa na aina fulani ya pipi,
asali, mvuke, chai ya mitishamba (mchaichai), kusafisha koo kwa maji chumvi,
baadhi ya dawa kwa ushauri wa daktari, unywaji wa maji, na kadhalika. Pia,
kinyume chake koo laweza kuharibiwa na matumizi ya vyakula au vinywaji kama
vile; pombe, kahawa, soda, maziwa, chokoleti, pipi, ubuyu, matunda jamii ya
ndimu, mayai, karanga, mahindi, bisi na kadhalika. Hivyo, muimbaji awe na
taadhali katika matumizi ya vyakula na vinywaji ili kufanya sauti yake kuwa
bora na kupendeza mbele za watu na Mungu tunayemtukuza kupitia sauti zetu.
Mathalani, mwanafunzi mzuri ni yule
anayetafuta zaidi maarifa mara baada ya kujifunza jambo fulani. Hivyo, ni
matumaini yangu kuwa mafunzo haya yatakuwa msingi bora kwa muimbaji kutafuta
zaidi kwa habari ya vyakula na vinywaji katika uimbaji. Haya yalioelezwa hapa ni
machache sana. Pamoja na hayo, mabadiliko chanya ya uimbaji yatategemea
uzingativu na utekelezaji kwa vitendo wa mambo hayo na sio kusikiliza tu. Pia,
mabadiliko hasi yatatokea kwa wasiozingatia na kutekeleza kwa vitendo mambo
hayo. Yuko mshairi anasema,
“Mshumaa tuliwasha, ili nuru kumulika, Giza kulitokomesha, na nuru kuenezeka,
Mshumaa unawaka, giza mbona linazidi?” Pia, mshairi mwingine anasema,
“Mnazi walioukwea, Shinani wameanzia, Si kama mejirukia, Kileleni taka tua,
Jikazie yako kwego, mnazi upate kwea.” Hivyo, huu ni mwanzo wa kujifunza
uimbaji; huna budi kuifuata nuru (mafunzo) unayoangaziwa (kupewa) ili ufanikiwe
katika uimbaji. Hii ni kwa sababu, wote waliofanikiwa katika aina yoyote ile ya
huduma, walianzia chini na kwa kuwa walisikiliza na kutekeleza waliyoelekezwa
na viongozi wao wakaweza kupanda na leo hii ni watu wakuu katia huduma.
Ili kuwa na afya nzuri katika mwili na katika uimbaji
wako zingatia :
1.
Punguza matumizi
mengi ya sukari, ongeza matumizi ya matunda
2.
Punguza kula nyama nyekundu, ongeza matumizi ya
mbogamboga
3.
Punguza matumizi ya soda, ongeza matumizi ya maji
4.
Punguza kuendesha, ongeza kutembea kwa miguu
5.
Punguza kupoteza muda wa kulala, Zingatia kulala kwa
wakati
6.
Punguza msongo wa mawazo, ongeza kupumzika
UMUHIMU
WA MAJI NA ASALI MWILINI
Maji
Tunaambiwa kuwa maji ni muhimu sana
ndani ya miili yetu. Maji yana faida nyingi sana na wengi tunazijua, lakini
tutajikumbusha baadhi.
1.
Moja
maji husaidia kupunguza calories mwilini, yaani badala ya kunywa vimiminika
vingine kama soda, bia na juisi ambavyo vina calories, maji hayana calories.
hivyo utakua umekunywa maji ambayo ni salama mbadala na vinywaji vingine
ambavyo vina calories.Kumbuka pia maji hayana sukari, mafuta na viungo vingine
vinavyotengeneza vimiminika vingine
2.
Unywaji wa maji mengi hutupunguzia uwezekano
wa kupata magonjwa kama ya moyo, hivyo inashauriwa kwa siku tunywe zaidi ya
bilauri mbili za maji na kuendelea.
3.
Maji huongeza nguvu mwilini kwani unapokua na
upungufu wa maji, unaanza na kusikia kiu ambayo huenda kupelekea kujisikia
uchovu, misuli kuchoka, kizunguzungu na ishara nyingine za kunyongonyeza mwili.
4.
Maji ni dawa ya maumivu ya kichwa. Mara kwa
mara tuumwapo kichwa pengine ni upungufu wa maji ndio uliopelekea maumivu haya,
lakini tunywapo maji basi maumivu huoondoka. Kuna sababu nyingine zinazopelekea
vichwa vyetu kuuma lakini, ukosefu wa maji mwilini ni sababu inayojulikana
zaidi.
5.
unywaji maji hupelekea kusafisha ngozi yako,
na mara kwa mara Rafiqs wengi wamejivunia kuwa na ngozi bora baada ya unywaji
wa maji wa kutosha. Haiwezi tokea mara moja ila baada ya wiki moja utaanza
kuona mabadiliko ya ngozi yako na itaanza kung’ara.
6.
mfumo wa kuchanganya chakula ndani ya miili
yetu (digestive system) unahitaji maji mengi ili kufanikisha kazi yake
kifasaha, hivyo yatupasa kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi yake vyema katika
muda sahihi kwa kunywa maji ya kutosha. Pia maji husaidia kuponesha maumivu ya
vichomi vya tumbo, na pia hutupa urahisi pale tuendapo haja kubwa, kwani
tunakua hatuna ukosefu wa maji mwilini. Maji husaidia pia kuondosha uchafu
ndani ya miili yetu na kuacha mwili ukiwa msafi.
7.
Kwa unywaji mwingi wakati wa mfumo wa kuchanganya
chakula unaendelea, imeonekana kuwa maji husaidia kupunguza uwezekani wa kupata
saratani ya colon kwa asilimia 45, asilimia 50 ya saratani ya kibofu cha mkojo
na pia hupunguza uwezakano wa kupata saratani ya matiti kwa kina mama.
8.
Kuwa na ukosefu wa maji mwilini husababisha
kukurudisha nyuma katika swala zima la mazoezi na kukufanya iwe ngumu kunyanyua
vyuma vya mazoezi, pamoja naa kufanya mazoezi mengine, hivyo basi inashauriwa
kunywa maji kabla, wakati na baada ya mazoezi ili uweze kuyafanya vyema na katika
hali salama.
Tunaweza anza jiuliza, kiasi
gani cha maji twatakikana kunywa?
Inashauriwa ni glass nane kwa siku,??? Labda inawezakana
sio sahihi sana…… kwasababu kiasi hicho kinahusisha maji safi ya kunywa
tunayoyanywa, pia maji yanayopatikana kwenye vyakula tunavyokula na vinywaji
vingine mbali na maji ya kunywa. Pia kiasi hicho hakikuangalia uzito wa miili
yetu kitu ambacho ni muhimu sana tunapoongelea kiasi cha maji cha kunywa, na
pia kiasi cha maji hutofautiana pale ambapo tunaumwa, au kwa wale tunaofanya
mazoezi kila siku.
Jambo lingine, unaposikia kiu,
kumbuka kwamba tayari una upungufu wa maji kwa hiyo kunywa pale hakutimizi zile glass nane za kunywa maji.
Cha kufanya basi, ni kujenga mazoea:
2.
Kunywa
glass moja ya maji pale uamkapo, glass moja kila baada ya mlo, glass moja
katikati ya milo yako ya siku, na kumbuka kunywa maji kabla, wakati wa na baada
ya mazoezi. Jaribu kuepuka kupata kiu ya maji.
3.
Beba chupa ya maji: Wengi wenye shughuli za
kutembea hapa na pale itawapasa kubeba chupa ya maji mkononi na kunywa mara kwa
mara, inapoisha ongeza nyingine. Na kwa wale wanaokaa maofisini, weka glass ya
maji pembeni yako na uwe unakunywa mara kwa mara na kuongeza pale inapokwisha.
Njia nyingine, ni kuegesha mlio kwenye saa ya mkononi au ya kwenye simu, au
kwenye Computer yako, iwe inalia kila lisaa kamili linapotimu, ili uweze
kukumbuka pale unaposikia kengele au alarm.
Iwapo unajisikia hamu ya kunywa soda au kimiminika chenye kilevi au cha aina
nyingine yeyote, badala ya kukifuata hicho, badili na fuata glass ya maji na
unywe. Jaribisha maji yenye ladha pale unapokua katika sherehe au makutanoni na
marafiki.
Anza mazoezi, kwani mazoezi hukufanya uwe na hamu ya kunywa maji maana si
utasikia kiu. Si lazima kunywa vinywaji vya kuongeza nguvu, ila kama unafanya
mazoezi zaidi ya lisaa limoja na kuendelea waweza kuvinywa. Kunywa maji mapema
iwapo wajua utaenda kufanya mazoezi, kwani itasaidia maji kufika kwenye system
ya mwili wako vyema pale unapoanza mazoezi, kunywa maji wakati wa mazoezi na
baada ya mazoezi.
Fuatilia mwenendo wako wa unywaji maji kwa kuandika pahala kwa ajili ya
kumbukumbu. Hii itakusaidia kukuonesha na kukukumbusha kwamba yakupasa kunywa
maji katika muda ule ule kila ufikapo na kiasi ambacho umejipangia. Andika muda
upande wa kwanza na wapili unaweka alama ya vema kila mara unywapo maji .
Asali
Nyuki
anauwezo wa kutembea mile elfu tatu akikusanya maua ya aina mbalimbali toka
miti mbalimbali milioni kumi na tano kwa ajili ya kutengeza asali kilo moja
ndani ya miezi mitatu. Kutokana na mchanganyiko huu unaotengenezwa na mdudu
nyuki ASALI ina uwezo wa kutibu magonjwa zaidi ya mia moja. Bado utaendelea
kutumia sukari yenye 'chemicals' zinazopunguza uwezo wa kuona na kuleta madhara
mengine!. Unashauriwa na wataalamu wa afya kwamba kila siku uamkapo ramba asali
ujazo wa kifuniko cha soda kimoja pia tumia asali kama kiungo cha chai,
uji,maziwa na kadharika. Pia asali inatumika kama mboga kwa kulia ugali
uliopoa. Ukila na ugali wa moto unaweza kupata maumivu
ya tumbo. Tumia asali kwa wingi kwani ni 'antibiotics' pia. Kumbuka asali
Mbichi ambayo haijachemshwa motoni ndiyo inayofaa. Hakikisha umejiridhisha kuw
asali uliyonunua ni mbichi.
Pia
mazoezi mengine rahisi kwa mwimbaji ni ku Harmony (Harmonize) =
“Huuuuu,
haaaa, hoooo”. Mwimbaji lazima uwe mjanja na personal swagga na lazima ziendane
na facial expression pamoja na kukaa kwenye ufunguo (key) na mapigo ya wimbo.
Pia add lips (kuchombeza) huleta ubora wa uimbaji.
NB. Inawezekana
lugha niliyoitumia hujaielewa sana, na wakati mwingine nimechanganya na
kingereza au lugha ya muziki. Ikumbukwe kuwa muziki una lugha yake, na pia
nimejaribu kutafsi kutoka kwenye notisi zangu ambazo mimi mwenyewe najifunza
kwa lugha ya kingereza. Lakini kwa ushauri zaidi tuwasiliane.
Kumbuka
muziki au uimbaji ni kama bahari, kila mtu anaogelea pale anaweza kufika, mimi
naweza nikakutoa hapa nikakupeleka pale, na mwingine akakutoa pale na
kukupeleka kwingine. Hakuna aliyefika kikomo cha kujua muziki au uimbaji, sote
ni wanafunzi, na pia katika kufundishana sote tunajifunza. Ikiwa unataka kuwa
mwimbaji bora, na unahisi bado unatatizo fulani tuwasiliane.
MAFUNZO BINAFSI YA KUWA
MUIMBAJI BORA
Yafuatayo ni
baadhi maelekezo muhimu yatakayo
kufanya kuwa muimbaji bora, kwako wewe mwenye uwezo wa kuimba au usiye jua
kabisa na umekuwa na ndoto ya kuja kuwa muimbaji lakini hujui namna ya
kujifunza.
1.Anza kufanya mazoezi ya uimbaji pamoja na waimbaji
katika CD’s, hakikisha unaendana na mianguko yote. Sauti za juu, sauti za chini
na kati kwa kiingereza hufamika
kama(pitch).vile utajifunza jinsi ya kuhama ufunguo(key)kutoka ufunguo
mmoja na kwenda ufunguo mwingine na
jinsi ya redio, zoezi hili litakuwezesha kufahamu mbinu nyingi wanazotumia
waimbaji wakati mwingine bila hata wewe
kujijua yaani automatic,mambo unayoweza kujifunza kutumia pumzi wakati wa uimbaji nk.
2. Jaribu kuanza kuimba mbele ya watu wa karibu na yako
mfano marafiki zako, familia yako, mpenzi wako
na kuwaomba wakusikilize
ikiwezekana wakukosoe au kukuponda. Hapa ukipata msikilizaji anayejua muziki, itakuwa
ni vizuri zaidi kwani anaweza kukurekebisha maeneo utakayo kuwa umekosea wakati
unapoimba,kama kuchanganya sauti, kutofuata mwendo wa mapigo wakati unapoimba,
kuimba nje ya ufunguo nk.
3.
Jirekodi na jisikilize mwenyewe kama unaona kuna dosari yoyote kinyume na
ulivyotarajia katika uimbaji wako rudia tena kuimba na kujirekodi,ukizingatia
kutorudia tena makosa uliyoyaona mwanzoni. Aidha kama unaona umefaulu kwa kiwango ulichokitaka, jaribu
kuwapa wengine wasikilize rekodi ya wimbo wako na kutoa maoni yao.
4. Nunua vitabu au
video vitakavyokupa maelekezo na
mbiu tofauti kuhusu uimbaji, hii ikiwa
ni pamoja na kufanya mazoezi ya sauti voice training, itakupa uwezo zaidi
katika kuimba nyimbo za aina tofauti
5.Jiunge na vikundi vya
uimbaji na kuanza kuimba nao ilikupata uzoefu zaidi kwani kuna utofauti mkubwa
kati ya kujiimbia mwenyewe na kuimba mbele za watu kenye umati.
Pamoja na kufahamu mambo hayo lakini kuna vidokezo muhimu vya
kwako wewe unaweza kujifunza kuimba navyo ni:
1.
Fanya mazoezi ya kuimba mara kwa mara
hata wakati unapokuwa peke yako.
2.
Jiamini
wewe binafasi na usijinganishe na
waimbaji wengine,wenye majina kwani kila mtu anauwezo na kipaji chake hata wewe
unaweza kuwa juu siku moja.
3.
Hakikisha una sauti
nzuri japo si lazima sana na unakipaji na kuipenda kwa dhati kazi ya
uimbaji ili hata utakapokabiliana na vikwazo haita kuwa tatizo kwako, bali
itakupa changamoto ya kujifunza zaidi na kujisahihisha maeneo yenye udhaifu..
4.
Inawezekana katika uimbaji wako kuna
eneo unaliwezea sana na linakuongezea wapenzi au mashabiki wengi (kucheza,
kutawala jukwaa, kutetemesha sauti n.k) basi boresha zaidi.
5.
Kuwa na ukaribu na mwalimu wa
muziki/uimbaji au mtu mzoefu,aliye mwaminifu ili aweze kukupa mawaidha kadhaa
uweze kufikia kiwango kinachoridhisha hata kwa wasikilizaji watakao kusikia.
6.
Ukifanikiwa katika mambo hayo anza sasa
kujifunza ala za muziki, kama guitar, kinanda pia unaweza kujifunza hata
kucheza hii itakusaidia kukupa uzoefu wa kuimba na vyombo live
performance’'katika matamasha ya wazi na kanisani.
Vile vile kitu kingine
muhimu ni kuomba msaada kutoka kwa mwalimu wa muziki/ uimbaji au mtu
yeyote mtaalam wa muziki uanze kufanya mazoezi ya kuimba
scale kama major scale,chromatic scale na scale nyinginezo labda nikupe mfano
wa major na chromatic scale na unaweza kumuomba mpiga kinanda akakipigia ili uzisikie jinsi zinavyosikika
na uzifanyie mazoezi ya kuimba mara kwa mara.
Mfano wa major scale
katika ufunguo wa C(key C).C,D,E,F,G,A,B,C
Mfano wa chromatic scale katika ufunguo wa
C(keyC)
C,C#,D,D#,E,F,F#,G,G#,A,A#
B,C
Endapo
utasoma nadharia ya muziki unaweza
kujifunza aina za scale.pia mwalimu akupe mazoezi ya kujenga uwezo wa sikio
lako kimuziki uwe na sikio la muziki itakusaidia kuimba bila kutoka nje ya key,
kuijua sauti yako na kujua kama ala za muziki hazijarekebishwa vizuri,mpigaji
ukiwa na sikio la muziki ni muhimu
pia utabaini vitu hivyo
kama muimbaji anaimba na kutoka nje ya
key pia utaweza kutyuni ala zako. Lakini kama sikio la muziki hauna si rahisi
kutyuni ala kama gitaa. Ni vizuri waimbaji na wapigaji kujifunza nadharia ya
muziki (music theory) itasaidia sana katika kukuza uelewa. Pamoja na hayo
vilevile jifunze kufanya mazoezi mbalimbali kama major,minor na zinavyosikika
na kuziimba.
N.B. Sio kila mwimbaji
mwenye jina anafaa kuwa mwalimu wa kukuelekeza au kukufundisha. Pia sio lazima
uweze kila kitu kwenye uimbaji au muziki ndipo uwe mwimbaji bora.
Sio waimbaji wote ni
wanamuziki na sio wana muziki wote ni waimbaji. Sio kila mwimbaji ni mtunzi,
lakini pia inawezekana mtu akawa mtunzi na asiwe mwimbaji.
Zingatia nguzo nne za
muziki pamoja na mazoezi ya pumzi yanayofaa kwa mwimbaji.
UBORA WA SAUTI
Nianze kwa kusema, nimekuwa mmoja kati ya waalimu wa sauti na uimbaji,
niliyewezesha watu wengi, vikundi vingi, na kwaya nyingi kuimba vizuri.
Lakini pia nashangaa wapo watu wengi wanaokimbilia studio, wanatengenezewa
studio lakini ukweli ni kwamba hawajawa waimbaji wazuri, ni waimbaji wa kuimbia
CD. Jamani kuimba vizuri kuna gharama zake.
Ikumbukwe kuwa, ili uimbaji wetu au muziki wetu uwe wa viwango vya
kimataifa yapo mambo yanayotakiwa kufanyika:
Kwanza
ni uandishi mzuri, ubunifu zaidi, studio bora
(quality of studio), kuandaa video yenye viwango (quality of video).
Nimekua
nikifundisha kwa kina kuhusu hatua nne za kuelekea kuwa na albam bora ya audio,
ikiwa ni pamoja na: mwimbaji kuwa bora, tungo bora, muziki bora na studio bora.
Nikualike tena kuhudhuria mafunzo yetu ya sauti yanayoendelea maeneo ya
Ukonga. Kwa kuchangia kidogo tu nitakufundisha mbinu za kuwa mwimbaji bora. Tuwasiliane.
Tuendelee na somo:
Unahitaji kufanya nini?
Unahitaji kuboresha sauti yako kwa kupumua vizuri na kutuliza misuli yako
badala ya kuiga mtu mwingine.
Kwa Nini Ni Muhimu?
Sauti nzuri hufanya wengine watulie na kufurahia kusikiliza. Sauti mbaya huaribu
mawasiliano, na inaweza kumfadhaisha mwimbaji/msemaji na wasikilizaji.
KWA KAWAIDA watu hawavutiwi tu na
mambo yanayosemwa, bali wanavutiwa pia na jinsi yanavyosemwa. Ikiwa mtu
anayezungumza nawe au anayeimba mbele yako ana sauti nzuri, changamfu, ya
kirafiki, na yenye fadhili, utafurahia kumsikiliza kuliko kama ana sauti kali
isiyo ya kirafiki, sivyo? Kukuza sifa hizo nzuri hakutegemei tu kuboresha
sauti. Kunaweza kuhusu utu wa mtu pia.
Nyakati nyingine sauti isiyofaa
inaweza kusababishwa na kasoro fulani ambayo mtu amezaliwa nayo au ugonjwa
uliodhuru zoloto. Huenda kasoro hizo zisiweze kurekebishwa katika mfumo huu wa
mambo. Lakini, unaweza kuboresha sauti yako ukijifunza kutumia vizuri viungo
vya usemi. Kwanza, tufahamu kwamba sauti za watu hutofautiana. Kwa hiyo,
usijaribu kuiga sauti ya mtu mwingine. Badala yake, boresha sauti yako mwenyewe
pamoja na hali zake. Unawezaje kufaulu?
Kuna mambo mawili makuu;
-
Pumua Vizuri.
Ili sauti yako iwe nzuri, unahitaji hewa ya kutosha na unahitaji kupumua
vizuri. Bila kufanya hivyo, sauti yako inaweza kuwa dhaifu mno na unaweza
kukata-kata maneno katika hotuba yako au uimbaji wako.
Sehemu kubwa za mapafu haziko juu
kifuani; sehemu hizo huonekana kubwa kwa sababu tu ya mifupa ya mabega. Lakini,
sehemu za mapafu zilizo pana zaidi ziko chini, juu tu ya kiwambo. Kiwambo
kinashikana na mbavu za chini na kinatenganisha kifua na tumbo.
Ukivuta pumzi na kujaza tu sehemu
za juu za mapafu, utakosa pumzi haraka. Sauti yako itakosa nguvu na utachoka
haraka. Ili uvute pumzi vizuri, unahitaji kuketi au kusimama vizuri na kurejesha
mabega nyuma. Jaribu sana usipanue sehemu ya juu pekee ya kifua unapovuta
pumzi. Kwanza vuta pumzi kabisa. Sehemu za chini za mapafu zikijaa hewa, mbavu
zako za chini zitapanuka. Kwa wakati huohuo, kiwambo kitasonga chini,
kikisukuma chini kwa utaratibu sehemu za tumbo hivi kwamba utasikia mkazo
kwenye mshipi wako au kwenye vazi katika eneo la tumbo. Lakini mapafu hayako
kwenye eneo la tumbo; yamefunikwa na mbavu. Unaweza kuthibitisha jambo hilo kwa
kuweka mkono mmoja kila upande wa mbavu za chini. Kisha vuta pumzi kabisa. Kama
unavuta pumzi vizuri, utaona kwamba huingizi hewa tumboni na kuinua mabega. La,
badala yake, utasikia mbavu zikisonga juu kidogo na kupanuka.
Kisha, jaribu kushusha pumzi.
Usishushe pumzi kwa ghafula. Ishushe polepole. Usijaribu kuzuia pumzi kwa
kukaza koo kwa sababu sauti itajikaza au itakuwa nyembamba sana. Mkazo wa
misuli ya tumbo na mkazo wa misuli iliyo kati ya mbavu huondosha pumzi, lakini
kiwambo hudhibiti mwendo wa pumzi hiyo.
Msemaji au mwimbaji anaweza
kudhibiti jinsi anavyopumua kwa kujizoeza kama vile tu mwanariadha anavyofanya
mazoezi ya mbio. Simama vizuri kama umerejesha nyuma mabega, vuta pumzi kabisa
ili sehemu za chini za mapafu zijae hewa, kisha shusha pumzi polepole na kwa
utaratibu ukihesabu kwa kadiri uwezavyo kabla ya kuvuta tena pumzi. Kisha
jizoeze kusoma kwa sauti ukipumua kwa njia hiyo.
-
Tuliza Mkazo wa
Misuli. Jambo jingine muhimu linalotokeza sauti nzuri ni utulivu! Unaweza
kuboresha sana sauti yako ukijifunza kutulia unapozungumza. Ni lazima akili na mwili
zitulie, kwa kuwa mkazo wa akili husababisha mkazo wa misuli.
Ifikirie misuli ya koo na kujaribu kuituliza. Kumbuka kwamba nyuzi
zako za sauti hutikisika zinapopitisha hewa. Sauti hubadilika misuli hiyo
ikikazika au ikitulia kama tu vile uzi wa gitaa hubadili sauti ukikazwa au
ukilegezwa. Sauti hurudi chini nyuzi za sauti zinapotulia. Kutuliza misuli ya
koo pia hufanya mianzi ya pua ibaki wazi, na hiyo huboresha sauti.
Tuliza mwili wako mzima—magoti,
mikono, mabega, na shingo. Ukifanya hivyo, utaweza kuvumisha sauti vizuri ili
isikike wazi. Sauti huvumishwa wakati mwili wote unapohusika kuitokeza, lakini
mkazo huizuia. Sauti hutokezwa kwenye zoloto nayo huvumishwa katika mianzi ya
pua, kwenye mifupa ya kifua, meno, na kaakaa ya mdomo na mianya iliyo katika
mifupa ya pua. Sehemu hizo zote zinaweza kuchangia ubora wa sauti. Ukiweka kitu
kwenye kibao cha gitaa cha kupaazia sauti, sauti itafifia; ni lazima kibao
hicho kisiwe na kitu ili kitikisike na kutoa sauti vizuri. Ndivyo ilivyo pia na
mifupa ya mwili wetu ambayo imeshikiliwa na misuli. Uvumishaji mzuri wa sauti
unakuwezesha kuwa na ubadilifu wa sauti na kuweza kuonyesha hisia mbalimbali
unapoimba au kuzungumza. Pia utaweza kuimbia au kuhutubia watu wengi zaidi bila
kukaza sauti.
JINSI YA KUFAULU
Fanya mazoezi ya kuvuta pumzi,
ukijaza sehemu za chini za mapafu kwa hewa.
Unapoimba au kuzungumza, tuliza
misuli yako ya koo, shingo, mabega, na mwili wote mzima.
MAZOEZI: (1) Kwa dakika chache kila
siku katika juma, fanya mazoezi ya kuvuta pumzi kabisa mpaka uzijaze sehemu za
chini za mapafu yako. (2) Jaribu kutuliza misuli ya koo unapoimba au
unapoongea, angalau mara moja kwa siku.
SAUTI HUTOKEZWAJE?
Sauti zote hutokezwa na hewa
inayotoka mapafuni. Mapafu hupiga hewa kama pampu kupitia koo na kuingia ndani
ya zoloto ambayo iko katikati ya koo. Ndani ya zoloto mna misuli miwili midogo
inayoitwa nyuzi za sauti, msuli mmoja uko upande mmoja na msuli mwingine upande
mwingine. Nyuzi hizo za sauti ndizo vitokezaji vikuu vya sauti. Misuli hiyo
hufungua na kufunga njia ya hewa katika zoloto ili kuingiza hewa na kuitoa na
vilevile kuzuia vitu visivyotakikana visiingie kwenye mapafu. Tunapopumua kwa
njia ya kawaida nyuzi za sauti hazitokezi sauti wakati hewa inapopita. Lakini
mtu akitaka kuimba au kuzungumza, misuli hufinya nyuzi za sauti, na nyuzi hizo
hutikisika wakati hewa inayotoka mapafuni inaposukumwa kuzipitia. Utaratibu huo
hutokeza sauti.
Kadiri nyuzi za sauti zinavyokazika,
ndivyo zinavyotikisika kwa kasi zaidi na ndivyo sauti inavyoinuka. Na kadiri
nyuzi hizo zinavyolegea, ndivyo sauti inavyopungua. Mawimbi ya sauti yanayotoka
kwenye zoloto huingia sehemu ya juu ya koo inayoitwa koromeo. Kisha mawimbi
hayo hupitia mdomo na pua. Hapo sauti nyinginezo huongezwa ili kurekebisha,
kukuza, na kuimarisha sauti ya awali. Kaakaa la mdomo, ulimi, meno, utaya, na
midomo huungana pamoja ili kutawanya mawimbi ya sauti, na kutokeza usemi
unaoeleweka.
Sauti ya mwanadamu ni ajabu sana,
na haina kifani ikilinganishwa na chombo chochote kile ambacho binadamu
ametengeneza. Ina uwezo wa kuonyesha hisia mbalimbali kama vile upendo na chuki
kali. Sauti ikikuzwa na kuzoezwa vizuri, inaweza kubadilikana sana na kutokeza
nyimbo tamutamu na semi zinazogusa mioyo.
KUSHINDA MATATIZO FULANI HUSUSA
Sauti dhaifu.
Sauti ndogo huenda isiwe dhaifu.
Ikiwa nzuri na yenye kuvutia, wengine wanaweza kufurahi kuisikiliza. Lakini ni
lazima sauti iwe yenye kiasi kinachofaa ili iweze kufaidi wengine.
Ili uboreshe ukubwa wa sauti yako,
unahitaji kuivumisha zaidi. Unahitaji kutuliza mwili wote mzima, kama
ilivyoonyeshwa katika somo hili. Pamoja na kutuliza mwili, fanya mazoezi ya
kuimba hali umefunga midomo. Midomo inapaswa kugusana kidogo, isishikane sana.
Unapoimba kwa njia hiyo, sikia mitikisiko ya wimbo huo akilini na kifuani.
Nyakati nyingine sauti husikika kuwa dhaifu au kukazika kwa sababu ya ugonjwa
au kukosa usingizi. Bila shaka, hali hiyo ikiboreka, sauti itaboreka.
Sauti inayoinuka juu sana.
Mkazo kwenye nyuzi za sauti hufanya
sauti iinuke. Sauti yenye mkazo hufanya wasikilizaji wawe na mkazo. Unaweza
kupunguza sauti nyembamba kwa kutuliza misuli ya koo ili kupunguza mkazo kwenye
nyuzi za sauti. Jaribu kufanya hivyo, ukifanya mazoezi kila siku unapozungumza.
Pia ni vizuri kuvuta pumzi kabisa.
Sauti ya kubana pua.
Nyakati nyingine pua iliyofungika
hutokeza tatizo hilo, lakini mara nyingi hali hiyo husababishwa na jambo
jingine. Nyakati nyingine kwa kukaza misuli ya koo na mdomo, mtu hufunga mianya
ya pua na kuzuia hewa isipite vizuri. Jambo hilo hutokeza sauti inayobana pua.
Unahitaji kutulia ili kuepuka jambo hilo.
Sauti nzito na kali.
Sauti kama hiyo haileti mazungumzo
ya kirafiki uimbaji wa kirafiki. Inaweza kutisha wengine.
Katika hali fulani, jambo muhimu ni
kuendelea kujitahidi kubadili utu wako. Ikiwa tayari umefanya hivyo, kujaribu
kutumia kanuni za kurekebisha sauti kunaweza kusaidia. Tuliza koo na taya.
Kufanya hivyo kutafanya sauti yako ipendeze zaidi na kufanya maneno mengine
yasitokee vibaya kwa kuyalazimisha kupitia meno.
VIUNGO VYA MATAMSHI
Kaakaa, Ulimi, Meno, Midomo, Taya,
pua…
Kumbuka kwamba kila mtu duniani ana
tone yake na hii hutokana na hivyo viungo nilivyotaja hapo juu. Maana rahisi ya
tone ni sauti ya mtu inapotoka au kusikika. Hivyo awe mwimbaji, muhubiri,
mwalimu, mtangazaji, public speakers… ana tone yake. Wapo wengi sana wametokea
kupendwa au kupata ajira nzuri kwasababu tu ya tone. Kumbuka haya yote
yanafanyika kupitia kitu kinaitwa DIAPHRAM; Mfano halisi ni kwamba, mwimbaji
anaimba kupitia diaphragm singing, muhubiri anatumia diaphragm speaking …
MKONDO WA HEWA MWILINI
Tundu la pua, Kinywa, Koo, Nyuzi za
sauti, Njia ya chakula, Mapafu, Kiwambo
Nyuzi za Sauti (zikitazamwa kutoka
juu)
Unapozungumza
Unapovuta pumzi
Unapovuta pumzi kabisa.
AFYA YA SAUTI (VOCAL HEALTH);
UNAPENDA KUIMBA VIZURI? BASI HII NI KWA AJILI YAKO
You are the instruments – Learn to sing like a pro!
Wewe ndie chombo halisi, jifunze
kuimba kama pro!
Ieleweke kwamba, Kuwa na utimamu wa
kimwili (fitness) sio kuwa bora
kuliko mtu flani, bali ni kuwa bora kuliko ulivyokua awali. Watu wengi sana
hutumia muda wao mwingi tu katika majumba ya mazoezi (Gym) wakifanya mazoezi mbalimbali ya kimwili
na wana nidhamu sana katika hili, ni jambo zuri sana kiukweli. Lakini tunasahau
kitu kimoja; Koo lako ni sehemu ya mwili wako pia! na kama ukitenga muda kwa
ajili ya mazoezi, na utunzaji mzuri wa Sauti yako, utawashsangaza wengi sana na
ubora wa sauti yako! Ungependa kuelewa nini cha kufanya??
AFYA YA SAUTI:
Sauti yako ndiye balozi wako kwa
ulimwengu, umewahi kuona mtu hata awe mpole kiasi gani, lakini kama akiwa na
sauti ya kutisha (hasahasa wazee) hata watoto humuogopa?? au hata ukifatwa na
mtu ambae humjui na ana sauti ya ajabu ajabu we mwenyewe lazima uogope!
Sauti unayoitumia kuongea ndiyo hiyo
hiyo unayoitumia kuimba, hivyo basi, ukiitumia sauti yako hovyo katika maongezi
utaathiri pia uimbaji wako! Zingatia hili; kama vile mwanamuziki kitendea kazi
chake ni kile chombo cha muziki, vilevile mwimbaji kifaa chake ni lake. Sasa
guitar likikatika nyuzi unaweza ukatafuta uzi mwingine, lakini koo halina
spare, litunze. Unyevu, Mazoezi ya misuli ya shingo na mapumziko, ndiyo viungo
muhimu katika kuipika afya ya sauti yako. Vinafanyaje kazi? ENDELEA…
UNYEVU;
Msingi wa sauti ni maji mengi
Tumia Maji ya Kunywa kwa wingi sana
ili kuzifanya Ala zako za Sauti (Vocal Chords)
ziwe na unyevu, zisikauke. Maji hulainisha na kuyaondoa makohozi katika koo na
kuyafanya yasigandamane kwenye ala za sauti.
Usitumie “spray” ya aina yoyote kunyevusha koo lako. Kumbuka kubadili
mazingira yenye hali za hewa tofauti tofauti huathiri ala za sauti. Cha
kufanya, kunywa maji ya kutosha na kula matunda yenye maji mengi kama matikiti
maji na matango, achana na matunda yenye tindikali nyingi kama “citrus fruits” mfano machungwa, malimao, na
ndimu kwani yatazisugua ala za sauti na kuziachia mikwaruzo.
MAZOEZI;
“Mazoezi
ya sauti yanachekesha, yafanye ukiwa peke yako, hasa bafuni unapooga”
Fanya mazoezi ya sauti na mwili kwa
ujumla na kwa bidii. Fanya mazoezi ya ulimi kama “tongue
trill” (yafanye ukiwa mwenyewe, hasa bafuni ili usije ukachekesha
watu) ili kuruhusu upitaji mzuri wa hewa kwenye koo, na upumuaji mzuri kwa
ujumla.
Jifanyie pia masaji maalum za ulimi
na maungio ya taya, fanya “humming“,
yaani tamka herufi ‘m‘ kwa
muendelezo, ukiwa umefumba mdomo, (kama sauti ya
nyuki wengi) ukiwa bafuni ili kuipasha sauti yako. Hakikisha
unafanya hivi kila siku kwa matokeo mazuri.
Fanya pia mazoezi ya misuli ya
shingo, koo taya na mabega, pia legeza misuli ya shingo na koo unapoimba noti
za juu sana au za chini sana, ukikakamaza shingo itakusababishia maumivu na
sauti itaharibika.
MAPUMZIKO;
Baada ya kuunguruma kwa muda mrefu, pumzika
Hakuna kitu kinachoweza kufanya kazi
bila kuchoka, hata iwe mashine ya Mjerumani. Kwahiyo, hakikisha unapata
mapumziko ya kuongea baada ya kutoka kwenye maongezi au uimbaji uliokufanya
utumie nguvu nyingi ili kuinusuru sauti yako.
Epuka tabia za kupiga kelele hovyo,
kubishana kwa sauti na nguvu nyingi, au kuimba kwa nguvu sana kusiko kua na
maana yeyote. Epuka sana uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kwani
kutakusababishia madhara kwenye sauti.
KWA KUMALIZIA…
- Acha sauti yako ing’ae, kuwa wewe na usiigize sauti ya
mtu
- Siku zote kunywa maji mengi yasiyochanganywa na kitu,
maji tu!
- Pata muda wa kutosha wa kupumzika, epuka kelele zisizo
za msingi
- Mwisho, Jifunze mbinu bora za uimbaji
(Kwa masomo zaidi yanayohusu mbinu za uimbaji, hudhuria
madarasa yetu)
John Shabani akiongoza sifa
Moja ya huduma za John Shabani
Mwalimu John akiongoza mazoezi yapumzi
Joyce John akijifunza kupiga kinanda
0716 560094
Haya ni masomo machache
sana niliyoyachagua kati ya mengi ili kukupa hamasa kujiunga na darasa la
uimbaji linaloendelea katika kituo chetu cha mafunzo, Kamara Dar es salaam chini ya mwalimu John
Shabani na timu yake
Karibu ujifunze.
Lakini pia kwa wale wanaotaka kurekodi nyimbo zenye ubora na kufanya video zenye ubora, nimefungua studio yenye vifaa vya kisasa, unaweza ukatazama baadhi ya video zangu kama;
- Mtoto wa mfalme by John shabani
- Futa machozi by John Shabani
- Nakupenda by John Shabani
Karibu sana.
Lakini pia kwa wale wanaotaka kurekodi nyimbo zenye ubora na kufanya video zenye ubora, nimefungua studio yenye vifaa vya kisasa, unaweza ukatazama baadhi ya video zangu kama;
- Mtoto wa mfalme by John shabani
- Futa machozi by John Shabani
- Nakupenda by John Shabani
Karibu sana.
Utangulizi:
Nianze kwa kusema kwamba , kwa
wale wanaofahamu maana ya bora ktika muziki, ni kwamba ni kosa kubwa sana na
hairuhusiwa kuingia kwenye music recording studio bila kupitia vocal studio.
Kwa wenzetu unapotaka kuingia studio lazima uwe na voice coacher, vikundi
mbalimbali vya uimbaji lazima view na voice coache.
Kazi kuu ya voice coacher ni;
-
Kufundisha ( training)
-
Kukushauri (councel)
-
Na kulea kipaji hadi mtu atoke (mental)
MALENGO/MAONO
1.
Kuvipata/kuviendeleza na kuviwezesha vipaji vya uimba
2.
Kuwa ni program ya uimbaji itakayoongoza kimafanikio Tanzania
MAWASILIANO
Mob: 0716560094, 0754818767
E-Mail: touchingvoice@yahoo.com
Mambo ya msingi yanayofunzishwa
katika program hii:
Ø
Historia
ya uimbaji
Ø
Tofauti
ya mwimbaji na mwanamuziki
Ø Kuwa
na sauti bora au afya ya sauti (vocal health)
Ø
Vyakula
na vinywaji vinavyofaa na visivyofaa
Ø
Sifa
na mbinu za kuwa mwimbaji bora au uimbaji kitaalam
Ø
Jinsi
ya kuitunza na kuiponya sauti yako
Ø
Amri
10 za mwimbaji (za sauti)
Ø
Matumizi
ya kipaza sauti (Microphone technique)
Ø
Utunzi
au uandishi wa nyimbo
Ø
Mazoezi
ya viungo yanayofaa kwa mwimbaji na faida zake
Ø
Ushauri
kwa wanaotaka kurekodi nyimbo
Kumbuka moja ya vitu vya msingi katika uimbaji ni nguvu (energy) “As
you sing higher, you must need more energy, as you sing lower, you must
useless”. Zipo nguvu za kiroho na za kimwili. Ili kuwa na nguvu za kimwili
unahitaji maji ya kutosha, chakula kizuri pamoja na mazoezi ya viungo.
KUIMBA
Kuimba
ni mpangilio wa maneno na sauti unaoleta ladha fulani inayopendeza kwenye sikio
la mwanadamu, ni kutamka maneno katika hali ya ki-muziki au pia twaweza kusema
ni kutamka maneno moja baada ya jingine kwa sauti yenye lahani (sauti ya ala ya
muziki, tuni) au ghani (Singing is the act of producing musical sounds with the voice)
Mwimbaji ni mtu yeyote mwenye uwezo wa kuimba au bila
vyombo vya muziki (be sung a cappella) au kwa kutumia vyombo. Mwimbaji huyo kwa
lugha ya ki-muziki anaitwa vocalist. Ikumbukwe kuwa pia katika vikundi vya
uimbaji wapo wale wanaoongoza wengine katika uimbaji (A lead singer) na wengine kazi yao ni kuitikia (backing singers)
N.B Mwanadamu yeyote mwenye uwezo wa kuongea,
anao uwezo wa kuimba pia.
Kama vile
tulivyo na ala za aina mbalimbali, mwimbaji naye pia anazo ala mbili muhimu:
Mdomo wenye uwezo wa kutoa sauti
ya uimbaji
Mwili
Kumbuka moja ya vitu vya
msingi katika uimbaji ni nguvu (energy)
Mckinney alisema: “As
you sing higher, you must need more energy, as you sing lower, you must
useless; as you sing higher, you must
use more space; asa you sing lower, youmust need use less””. Inamaanisha
kadri unavyotumia sana sauti hasa kwa sauti ya juu sana, ndipo unapohitaji pia
nguvu kubwa, japo wapo watu kwasababu ya uzoefu wa kuimba kwa muda mrefu au
kupitia madarasa kama yale yanayofundishwa na mwalimu John Shabani, kwao kuimba
sauti ya juu au ya chini ni jambo la kawaida.
Zipo nguvu za kiroho na za kimwili. Ili kuwa
na nguvu za kimwili unahitaji maji ya kutosha, chakula kizuri, hewa pamoja
na mazoezi ya viungo maalum kwaajili ya uimbaji au ya pumzi.
Mwimbaji pia anahitaji
Pumzi ya kutosha (Breathing support), chakula kizuri na maji ya kutosha.
UIMBAJI KITAALUMA
Mwimbaji asiyejua kuimba hawezi kuwa huru kuhudumu ni muhimu afahamu uimbaji ili aimbe kwa uhuru na kwa ufanisi. Ufanisi unahitaji muda wa mazoezi yakutosha pamoja na mwalimu mwenye uwezo wakukuelekeza jinsi ya kuimba Muziki (uimbaji), mambo hayo upo katika mafungu makuu mawili :

VOCAL: Ni sauti ya wanadamu. Sauti isiyochanganywa kitu chochote. Sauti asilia ya mtu (Natural voice)
INSTRUMENTALS:
Ni sauti zitokanazo na vyombo. Sauti pasipokuchanganywa na kitu chochote yaani ala za muziki. Sehemu hizi mbili zikichanganywa pamoja hufanya kitu kinachoitwa muziki (uimbaji) na kukamilisha maana ya NENO MUZIKI.
SAUTI. Ni hisia inayonaswa na masikio na hutokana (hutengenezwa) na msuguano wa hewa katika mzunguko, mgongano wa vitu au mkwaruzo kiasi cha kutoa mlio (sauti).
SAUTI –MLIO (AUDIBLE, SOUND)
1. Kitaalamu Sauti ina misingi au kanuni .
Misingi hiyo ni Miwili. Ni kwa misingi ya sehemu hizo mbili kuu- Sauti hujengwa/huumbika, tutaelewa misingi hiyo vizuri kwa kuziangalia tabia za sauti (Characteristics of Musical Sound) Au tabia za milio.
Msingi wa
kwanza:
Sehemu
hii ya kwanza nazungumzia nadharia ya tabia za sauti, tabia hizi huwezi kuziona
wala kuzihisi, ila unaweza kuzifikiria katika mawazo.
a) Sauti ina tabia ya – Melody – Yaani kwa Kiswahili – Ghani
Melody – Ghani – (Mpangilio wa nota na maneno kimuziki). Ni mistari ya sauti ya muziki inayotambulisha chanzo (tone) cha wimbo ni sauti yenye kuelekeza ubora wa mtiririko wa ghani (melody) unaokupa hisia ya mlio unaohusika au unaousikia.
b) Rhythm – Ni utaratibu au mfumo wa aina ya mwendo wa sauti katika wakati au mfululizo wa sauti katika muda, mwendo, pigo, mdundo au msisimko. Uwezo wa sauti wa kutembea katika wakati usiobadilika.
c) Harmony – Mkusanyiko wa sauti unaopendeza, utaratibu au mfumo wa ulinganifu wa sauti, usawa, muafaka, kusikilizana pasipokuachana kwa sauti au kuwa nje ya tune hasa wakati kuna watu wengi wanaimba, katika ngazi tofauti yaani sauti ya msitari wa 1, 2, 3 na 4 pamoja.
d) Unison—Ni sauti ya aina moja inayoimbwa na watu wengi bila ya kutofautisha ngazi za sauti ya kwanza, pili,tatu na nne. Na kwa kawaida sauti ya unison hutumia sauti ya kwanza.
e) Form – Ni mwonekano wa kipekee, utaratibu au mfumo wa kuweka uimbaji katika aina ya mfumo unaojitambulisha katika mtindo wake wenyewe kama vile mtindo wa kizungu, wa kiafrika, kigogo, kihaya nakadhalika.
f) Tone Color – Aina mbalimbali za sauti kufuatana na chombo au mtu anayeimba – kwa mwanadamu sauti hutegemea mapafu yake na mishipa ya fahamu ya kichwani. Yaani sauti kavu, sauti laini, yenye mikwaruzo, yenye mawimbi nakadhalika, kusikika kwa sauti kipekee, kivyake kwa kadri ya mtu anavyotoa sauti au chombo kinavyo toa sauti kwa namna ya mlio wake.

Sehemu ya kwanza Nimetaja nadharia ya tabia za sauti, tabia hizi huwezi kuziona wala kuzihisi, ama kuzisikia, ila unaweza kuzifikiria katika mawazo. Kuimba sio nadharia wala mawazo ni matendo halisi. Nadharia hiyo lazima itafsiriwa katika vitendo tunavyoweza kuviona, kuhisi, kusikia tabia za sauti au milio hiyo. Haya yanawezekana kwa kutumia nyenzo , njia za muziki za kiufundi zinazotuwesha kutenda. (Musical Skills Performance Methods)
Sehemu ya kwanza Nimetaja nadharia ya tabia za sauti, tabia hizi huwezi kuziona wala kuzihisi, ama kuzisikia, ila unaweza kuzifikiria katika mawazo. Kuimba sio nadharia wala mawazo ni matendo halisi. Nadharia hiyo lazima itafsiriwa katika vitendo tunavyoweza kuviona, kuhisi, kusikia tabia za sauti au milio hiyo. Haya yanawezekana kwa kutumia nyenzo , njia za muziki za kiufundi zinazotuwesha kutenda. (Musical Skills Performance Methods)
Katika msingi huu wa pili tunafika
katika kukamilisha muziki na ndiyo uimbaji. Muziki ni sayansi lakini kila mmoja
wetu anayo na anaweza kuitendea kazi kwa kujifunza na kujizoeza.
Nyenzo au njia hizo ni:
a) Kuimba – (Singing – Melody) Unapoimba ndipo Ghani itajitokeza katika mpangilio wa sauti kwa njia inayopendeza na kwa utaratibu, hapo Tone Color itasikika yaani kwa kuimba wimbo, ghani na aina za sauti katika ubora wake utasikika.
b) Kupiga vyombo vya muziki – Accompanyments – vikolezo. Melody ambayo ni Ghani itasikika – Tone color pia itasikika.
c) Form, Kutenda vitendo – (Moving – Movement –Steps) Rhythm na Form itaonekana yaani kucheza kwa mwendo wa mapigo. Yaani sauti na maneno unayoimba yataenda kwa kufuata mapigo na midundo ya wimbo na kuwa na muonekano wa kipekee.
d) Harmony. Kusikiliza ndiko kutakuwezesha kuleta ulinganifu katika mkusanyiko wa sauti za kupendeza na kukuwezesha uimbe sawasawa na sauti nyingine bila kuhitilafiana wala kuachana au kuwa nje ya ghani.
e) Kuunda au Ubunifu (Creation – Form, Rhythm na melody) Wimbo utakamilishwa kwa kuunganisha nyenzo hizo nakuwa halisi yaani wimbo halisi wenye kusikika vizuri.
HATUA 4 ZA KUREKODI AU KUWA NA ALBAM BORA
VYAKULA NA VINYWAJI KATIKA UIMBAJI
Muimbaji asitumie vyakula vyenye mafuta mengi, na nyama nyekundu kama ya ng’ombe, mbuzi na kadhalika.
Anza mazoezi, kwani mazoezi hukufanya uwe na hamu ya kunywa maji maana si utasikia kiu. Si lazima kunywa vinywaji vya kuongeza nguvu, ila kama unafanya mazoezi zaidi ya lisaa limoja na kuendelea waweza kuvinywa. Kunywa maji mapema iwapo wajua utaenda kufanya mazoezi, kwani itasaidia maji kufika kwenye system ya mwili wako vyema pale unapoanza mazoezi, kunywa maji wakati wa mazoezi na baada ya mazoezi.
Fuatilia mwenendo wako wa unywaji maji kwa kuandika pahala kwa ajili ya kumbukumbu. Hii itakusaidia kukuonesha na kukukumbusha kwamba yakupasa kunywa maji katika muda ule ule kila ufikapo na kiasi ambacho umejipangia. Andika muda upande wa kwanza na wapili unaweka alama ya vema kila mara unywapo maji .
UBORA WA SAUTI
Nianze kwa kusema, nimekuwa mmoja kati ya waalimu wa sauti na uimbaji, niliyewezesha watu wengi, vikundi vingi, na kwaya nyingi kuimba vizuri.
Lakini pia nashangaa wapo watu wengi wanaokimbilia studio, wanatengenezewa studio lakini ukweli ni kwamba hawajawa waimbaji wazuri, ni waimbaji wa kuimbia CD. Jamani kuimba vizuri kuna gharama zake.
Tuendelee na somo:
Unahitaji kufanya nini?
Unahitaji kuboresha sauti yako kwa kupumua vizuri na kutuliza misuli yako badala ya kuiga mtu mwingine.
Kwa Nini Ni Muhimu?
Sauti nzuri hufanya wengine watulie na kufurahia kusikiliza. Sauti mbaya huaribu mawasiliano, na inaweza kumfadhaisha mwimbaji/msemaji na wasikilizaji.
a) Kuimba – (Singing – Melody) Unapoimba ndipo Ghani itajitokeza katika mpangilio wa sauti kwa njia inayopendeza na kwa utaratibu, hapo Tone Color itasikika yaani kwa kuimba wimbo, ghani na aina za sauti katika ubora wake utasikika.
b) Kupiga vyombo vya muziki – Accompanyments – vikolezo. Melody ambayo ni Ghani itasikika – Tone color pia itasikika.
c) Form, Kutenda vitendo – (Moving – Movement –Steps) Rhythm na Form itaonekana yaani kucheza kwa mwendo wa mapigo. Yaani sauti na maneno unayoimba yataenda kwa kufuata mapigo na midundo ya wimbo na kuwa na muonekano wa kipekee.
d) Harmony. Kusikiliza ndiko kutakuwezesha kuleta ulinganifu katika mkusanyiko wa sauti za kupendeza na kukuwezesha uimbe sawasawa na sauti nyingine bila kuhitilafiana wala kuachana au kuwa nje ya ghani.
e) Kuunda au Ubunifu (Creation – Form, Rhythm na melody) Wimbo utakamilishwa kwa kuunganisha nyenzo hizo nakuwa halisi yaani wimbo halisi wenye kusikika vizuri.
SIFA ZAKUWA MWIMBAJI BORA
Mambo muhimu yatakayokufanya uwe muimbaji bora;
Haya ni mafunzo ya msingi na ya kwanza kwa mtu anayetaka kujifunza kuimba au
kuwa mwimbaji bora. Sisi tunaita mafunzo ya chekechea kwa mwimbaji.
1.
Breath au breathing (pumzi au kupumua).
Jambo la kuzingatia na la kuelewa ni kwamba; msingi wa uimbaji (the foundation
of singing) ni pumzi. pumzi huhitajika sana
wakati wa uimbaji muimbaji mzuri
ni yule anaye jua kutumia pumzi yake vizuri, muimbaji asipokuwa na uwezo wa
kutumia vizuri pumzi katika maeneo yasio
takiwa itasababisha sentensi ya wimbo kukatika katika .vile vile muimbaji usipokuwa na pumzi utashindwa kuimba noti za
juu na katika noti ambazo unatakiwa uimbe na uzivute kwa muda hautaweza na itakusababishia
uimbe na kutoifikia pitch kama hauna pumza anza sasa kufanya mazoezi ya pumzi. Hivyo katika eneo hili tunajifunza
mazoezi ya kujenga uwezo wako wa kupumua. Zipo mbinu nyingi (teknics), moja
wapo ni;
-
Hissing sound (z, s, v)
-
Ballon teknics (mbinu ya
pulizo)
-
Book method
-
Birthday cake
-
Three methode (mbinu ya mti).
Hii tunaita ni aina ya juu sana ya mafunzo ya sauti (a deep breathing method)
n.k.
2.
Pitch
–pitch (Ear training) – yaani kufundisha sikio lako kujisikia mwenyewe kama uko
sahihi au la au kuwasikia watu wengine. Pitch ni uwiano wa sauti yako mwimbaji pamoja
na vyombo au waimbaji wenzio kutegemea na (key) ufunguo unaoimbia au mnaoimba.
mwimbaji asipoimba katika pitch humpelekea muimbaji huyo kuimba nje ya ufunguo
(out of key) kwa sababu ule uwiano wa sauti yake na ya vyombo katika
(key) ufunguo unaoimba unakuwa haupo kama unatatizo katika eneo hili unahitajika sana kufanya mazoezi ya pitch
3.
Rhythm-ni
mapigo ya mziki kwenda katika mwendo
usio badilika na kuwa na idadi sawa ya
mapigo katika kipimo(measure), mwimbaji lazima awe na uwezo wa kuimba na
kufuata beat (mdundo),vile vile na uwezo
wa kuimba akifuata ridhimu ya wimbo.
4.
Voice
(sauti) – Tone -
Range (ukomo wa sauti kwenda juu na chini) mwimbaji ni vizuri uimbe
katika sauti yako ya asili lakini sauti yako inabidi iwe inatoka au kuimbwa kwa
kufuata misingi ya kimuziki unatakiwa kufanya mazoezi ya sauti(voice training)
ili kuiboresha sauti yako pia fanya mazoezi ya kuimba scale mbali mbali za
muziki kama moja scale chromatic scale arpeggios…
5.
Diction
(lafudhi au matamshi) kujifunza sauti peke yake haitoshi bado unatakiwa kujifunza
kuimba na kutamka maneno vizuri ili wasikilizaji waweze kukuelewa
unachokiimba hivyo kuumba matamshi ni kitu muhimu sana katika uimbaji.
Baadhi ya mafunzo ya matamshi ni kama;
-
Zima
switch, washa switch
-
Masachusets
-
Entusiasm
Zingatia pia: Kusimama
kwenye ufunguo (Key), mwonekano, (appearance), Uwezo wa kuitumia sauti na
kuitawala (Manage your vocal), kuua lafunzi ya asili kulingana na aina ya
uimbaji, mwanekano jukwaani(Stage presence), kuwa na sikio la muziki eitha
ukiwa peke yako au katikati ya wengine, kujiamini, kujitambua, lugha ya mwili
(body language) kujithamini (Self Cofidance), kuwa mbunifu na kujitengenezea
swaga zako binafsi huku zinazoendana na muonekano wako usoni na mwili mzima
(facial expression). Kujituma, kujiachia lakini usipitilize, mawasiliano na
watu wengine ikiwa ni pamoja na wapigaji na madhabau n.k.
HATUA 4 ZA KUREKODI AU KUWA NA ALBAM BORA
(Mwimbaji kuwa bora, tungo au ujumbe bora, muziki bora, Studio bora)
NGUZO 4
ZA MUZIKI
Kusikiliza muziki/uimbaji (Listening), Kuhifadhi muziki/uimbaji
(Copying), Kuiga au kukariri (imitate), Kuzalisha muziki (producing)
Mazoezi kwa mwimbaji
Yapo mazoezi maalum
kwaajili ya kuboresha uimbaji na pia kumfanya mwimbaji awe na nguvu ya kutosha
na kuepukana na baadhi ya magonjwa. Kwa ushauri zaidi wasiliana na mwalimu John
Shabani.
Pamoja na faida nyingi za
mazoezi lakini pia mazoezi huchangamsha mwili, hulainisha koo, husaidia kuwa na
pumzi ya kutosha, hukuhepusha au kupunguza baadhi ya magonjwa kama kisukari,
presha n.k, hung’arisha ngozi, na kusaidia mfumo wa mzunguko wa damu, mazoezi husaidia katika mfumo wa
usagaji chakula kuwa mzuri , kukupa nguvu na kuweza kufanya kazi kwa nguvu zako
bila kujiskia umechoka na mwisho wa siku hupunguza mafuta mwilini, hupunguza uzito, kunyoosha na kuimarisha
misuli ya mwili, husaidia mapigo mazuri ya moyo kwa kuongeza kasi ya mapigo
yake wakati wa mazoezi, hupunguza mrundiko wa damu kwenye mishipa, hii ni
muhimu kwa sababu mgando wa damu husababisha magonjwa ya moyo pamoja na
kupoteza fahamu, mazoezi huimarisha mifupa ya mwili, huboresha usingizi ambao
unafaida sana kwa mwimbaji.
Fikiria mwenyewe kama mwanamichezo
au mtu wa fani fulani na jifunze kuwa mtu wa kula na kunywa kulingana na fani
yako: Aina ya chakula na kinywaji na muda
wa kutumia ni jambo la kuzingatia sana. Kula na kunywa ni muhimu lakini
Jiepushe na ulafi kwani huleta uchovu, mfumo wa kupumua kuathirika na wakati
mwingine kusababisha magonjwa.
Kuna misimu fulani kama msimu wa vumbi au baridi kali au alegi au matatizo
mengine kibao, wakati mwingine aina fulani ya dawa kwa ajili ya ugonjwa fulani,
Wakati mwingine husababisha mafua au kutokwa na kamasi mara kwa mara au
kukausha koo kabisa, hivyo husumbua sana na kuathiri mfumo wako wa kuimba.
Wakati mwingine mazingira ya shughuli au kazi tuzifanyazo au pia mazingira ya
makazi huweza kuathiri sauti zetu. Hivyo masomo ya utunzaji wa sauti ni ya
muhimu sana.VYAKULA NA VINYWAJI KATIKA UIMBAJI
1.0 Utangulizi
Uimbaji ni taaluma kama zilivyo taaaluma zingine za sheria, elimu, uhandisi, usimamizi wa fedha, biashara na kadhalika. Taaluma hizo na zingine zinautaratibu uliowekwa ili kumfanya mtu asiyejua kujua na hatimaye kuitwa mwanasheria, mwalimu/mwezeshaji, muhandisi au msimamizi wa fedha. Hivyo basi, uimbaji nao una taratibu zake hata mtu akafikia kiwango cha kuthibitika kuwa ni muimbaji ama kwa kupewa cheti au kuonesha uwezo wake mbele ya wengine; kanisani, kwenye majukwaa ya matamasha ya uimbaji na kadhalika.
Uimbaji ni taaluma kama zilivyo taaaluma zingine za sheria, elimu, uhandisi, usimamizi wa fedha, biashara na kadhalika. Taaluma hizo na zingine zinautaratibu uliowekwa ili kumfanya mtu asiyejua kujua na hatimaye kuitwa mwanasheria, mwalimu/mwezeshaji, muhandisi au msimamizi wa fedha. Hivyo basi, uimbaji nao una taratibu zake hata mtu akafikia kiwango cha kuthibitika kuwa ni muimbaji ama kwa kupewa cheti au kuonesha uwezo wake mbele ya wengine; kanisani, kwenye majukwaa ya matamasha ya uimbaji na kadhalika.
Kwahiyo, makala hii imelenga
kumsaidia muimbaji kumpa sheria na taratibu za uimbaji hususani katika suala
zima la chakula gani muimbaji ale au asile na vinywaji gani muimbaji anywe au
asinywe ili awe na uwezo wa kuimba vizuri mahali popote.
2.0 Nafasi ya Vyakula na Vinywaji katika uimbaji.
Katika suala la kula na kunywa muimbaji yeyote anaweza kufananishwa na mkimbiaji. Mkimbiaji hawezi kujishindilia chakula kingi au kunywa maji mengi wakati akijua anakwenda kwenye mazoezi au mashindano ya kukimbia umbali wa maili fulani. Hii ni kwa sababu, atashindwa kukimbia vizuri. Hata muimbaji; hawezi kula au kunywa kwa kupitiliza halafu asipate shida wakati wa zoezi la kuimba. Hii ni kwa sababu, kushiba sana kunazuia zoezi la upumuaji wakati wa uimbaji na kusababisha muimbaji kushindwa kutengeneza sauti nzuri za uimbaji.
Katika suala la kula na kunywa muimbaji yeyote anaweza kufananishwa na mkimbiaji. Mkimbiaji hawezi kujishindilia chakula kingi au kunywa maji mengi wakati akijua anakwenda kwenye mazoezi au mashindano ya kukimbia umbali wa maili fulani. Hii ni kwa sababu, atashindwa kukimbia vizuri. Hata muimbaji; hawezi kula au kunywa kwa kupitiliza halafu asipate shida wakati wa zoezi la kuimba. Hii ni kwa sababu, kushiba sana kunazuia zoezi la upumuaji wakati wa uimbaji na kusababisha muimbaji kushindwa kutengeneza sauti nzuri za uimbaji.
Pia, mkimbiaji hatokuwa na nguvu za
kukimbia kama hatokula chakula cha kutosha au kunywa maji ya kutosha. Muimbaji
halikadhalika, anahitaji kula chakula na kunywa maji kwa kuwa uimbaji ni kazi
ngumu ambayo inahitaji virutubisho vya kutia nguvu mwili ambavyo vinapatikana
katika vyakula na vinywaji tunavyotumia katika maisha yetu ya kila siku. Hivyo,
kula na kunywa ni jambo la muhimu sana kwa muimbaji katika zoezi la uimbaji
lakini kwa tahadhali. Kama nilivyotangulia kusema, kuimba ni kama riadha,
inahitajika nguvu kwa ajili ya utendaji wako. Hata hivyo, ni muhimu pia kuepuka
kuimba tumbo likiwa limeshiba sana. Yapo madhara mengi yanayotokana na shibe.
Unaweza ukawasiliana na mwalimu wa sauti ili kujua madhara hayo
2.1 Tahadhari ya vyakula na vinywaji katika uimbaji (nini muimbaji
hapaswi kula au kunywa katika siku ya uimbaji na wakati wa uimbaji)
Muimbaji asishinde na njaa au kutokunywa maji kabisa siku ya uimbaji. Hii ni kwa sababu, kutokula kutanyong’onyesha mwili wake hivyo atashindwa kuimba kwa ufanisi. Zingatia: kama muimbaji amefunga; atumie maji (anywe kidogokidogo) ili kulainisha na kulifanya koo lake lisiwe kavu. Pia, maji yatampa muimbaji nguvu ya kusimama na kuwahudumia watu kwa muda uliopangwa.
Muimbaji asishinde na njaa au kutokunywa maji kabisa siku ya uimbaji. Hii ni kwa sababu, kutokula kutanyong’onyesha mwili wake hivyo atashindwa kuimba kwa ufanisi. Zingatia: kama muimbaji amefunga; atumie maji (anywe kidogokidogo) ili kulainisha na kulifanya koo lake lisiwe kavu. Pia, maji yatampa muimbaji nguvu ya kusimama na kuwahudumia watu kwa muda uliopangwa.
Muimbaji asinywe kinywaji chochote chenye kafeni. Hii hujumuisha
vinywaji kama vile; kahawa, cola (soda), chai ya rangi nyeusi (black tea) na
vinywaji vyote ambavyo vina cafeni ndani yake. Vinywaji hivi ni kichochezi cha
mkojo na hufanya mwili wa muimbaji kushindwa kufyonza maji kunakosababisha
mwili kukauka au kuishiwa maji ambayo ni muhimu sana katika kumpa muimbaji
nguvu ya kuimba. Pia, vinywaji hivi husababisha; kuzalishwa kwa kitu kama
uteute (kamasi) kwenye kinywa na koo, ukavu na maumivu kwenye koo, huleta
kiungulia na kusababisha kucheua mara kwa mara wakati wa uimbaji.
Zingatia: Kama muimbaji anashindwa kuacha vinywaji hivyo,
inashauriwa kusukutua koo kwa maji mara baada ya kunywa kinywaji cha namna hiyo
kwa siku nzima ili kusafisha koo na kuepuka athali zisababishwazo na vinywaji
hivyo katika uimbaji. Pamoja na hilo, muimbaji anywe maji mengi; zaidi ya glasi
nane kwa siku. Au, Muimbaji atumie chai nyeusi (black tea) ambayo inaelezwa
kuwa na kiwango kidogo sana cha kafeni. Ila matumizi ya chai ya kienyeji ni
bora zaidi (mchaichai).
Muimbaji asile vyakula au kunywa vinywaji vinavyoongeza au kuacha uteute
kwenye kinywa na katika koromeo kabla na wakati wa uimbaji. Mfano wa
vyakula hivyo ni mayai, maziwa, ‘ice cream’ na bidhaa zingine za maziwa kama
pipi, ‘chocolate’, biskuti, keki, siagi, samri, koni na kadhalika. Uteute
unaosababishwa na vyakula na vinywaji hivyo huzuia utokaji mzuri wa sauti ya
uimbaji wakati wa kuimba. Ndio maana utakuta waimbaji wengine wanahama funguo
za muziki au kushindwa kuimba sauti za funguo za juu au kupata tatizo la
kushindwa kupanda na kushuka vema kwa sauti wakati wa uimbaji.
Muimbaji asitumie vyakula au vinywaji vinavyokausha koo. Mfano wa
vinywaji hivyo ni kama vile; pombe, matunda jamii ya ndimu kama chungwa, limao,
chenza, daransi, embe bichi, na kadhalika. Kukauka kwa koo kutasababisha sauti
ya muimbaji kutotoka vema kwasababu koo lake ni kavu.
Muimbaji asitumie soda na vinywaji vyovyote vinavyotoa povu wakati
vinapofunguliwa. Vinywaji hivi huweka gesi/hewa tumboni na kumfanya
muimbaji kubeu na/au kucheua hovyo na kusababisha muimbaji kupata shida wakati
wa kuimba na kutoa sauti mbaya.
Muimbaji asile vyakula ambavyo vitaacha vitu kama makapi kwenye koo
lake. Vyakula hivyo ni kama vile; bisi, mahindi, karanga, tambi kavu,
chama, na kadhalika. Ulaji wa vyakula hivi kabla na wakati wa kuimba
husababisha ugumu wa utoaji wa sauti za kuimbwa. Pia, makapi hayo wakati
mwingine hurukia katika koo la chakula na kusababisha muimbaji kupaliwa na
hatimae muimbaji kushindwa kupumua vema, kukohoa na kuimba vibaya.
Muimbaji asile vyakula vya mafuta sana;
kama vile nyama zilizonona na
kadhalika. Pia, sukari nyingi haifai kwa muimbaji.
Muimbaji asile vyakula au vinywaji vinavyoleta mwasho au kukera koo
(throat irritants), vinavyochangamsha, kusisimua au kulewesha (Overly spicy
foods) kama vile; kahawa na pilipili, vinywaji baridi sana, sukari
iliyosafishwa, chocolate na kadhalika.
Muimbaji asitumie Jamii ya vitu vyenye alkoholi, Sigara, tumbako,
bangi, ugoro na aina yoyote ya madawa ya kulevya kwakuwa vinaathali kubwa
kwenye koo na mapafu ambavyo ni viungo muhimu sana katika utengenezaji wa sauti
bora za uimbaji.
Muimbaji asitumie vyakula vyenye madhara kwa mwili wake (mzio;
allege). Kwa mfano, baadhi ya waimbaji hupata shida baada ya kula matunda jamii
ya machungwa, ngano, karanga, samakigamba, soya na kadhalika.
Muimbaji asitumie vyakula vyenye mafuta mengi, na nyama nyekundu kama ya ng’ombe, mbuzi na kadhalika.
2.2 Vyakula na vinywaji vitakavyofanya muimbaji aimbe vizuri (vyakula
na vinywaji ambavyo muimbaji anashauriwa kuvitumia kabla na /au wakati wa
uimbaji)
Muimbaji ale chakula cha wastani (kiwango cha kutosheka) masaa mawili kabla ya uimbaji. Hii itasaidia chakula kumengenywa vema na kumpatia muimbaji nguvu wakati wa kuimba. Kushiba sana (kuvimbiwa) husababisha tumbo kushindwa kumeng’enya chakula kwa haraka na hivyo kutamfanya muimbaji ashindwe kutoa sauti vema. Hii ni kwa sababu, tumbo litashindwa kusukuma hewa kutoka nje ili kutengeneza sauti nzuri za uimbaji. Pia, muimbaji atakuwa anabeua na kucheua hovyo wakati wa kuimba hali ambayo humfanya kutoa sauti mbaya au kushindwa kuimba kabisa.
Muimbaji anywe maji ya kawaida
(room temperature water) yaani yasiwe ya moto wala ya baridi au barafu. Maji
hayo yanywewe masaa mawili kabla ya uimbaji. Maji haya yatampa nguvu muimbaji,
yatafanya koo la muimbaji kuwa bichi (sio kavu) na mwili kutokuwa mkavu.
Muimbaji hanabudi kutambua kuwa matumizi ya maji ya moto hutanua na maji ya
baridi (au barafu) husinyaza/hubana koromeo hivyo kusababisha kiboksi cha sauti
kushindwa kutengeneza sauti za kuimba vizuri na muimbaji ataimba vibaya.
Zingatia: Unaweza kunywa maji ya moto au ya baridi baada ya uimbaji na sio
kabla au wakati wa uimbaji. Muimbaji ale chakula cha wastani (kiwango cha kutosheka) masaa mawili kabla ya uimbaji. Hii itasaidia chakula kumengenywa vema na kumpatia muimbaji nguvu wakati wa kuimba. Kushiba sana (kuvimbiwa) husababisha tumbo kushindwa kumeng’enya chakula kwa haraka na hivyo kutamfanya muimbaji ashindwe kutoa sauti vema. Hii ni kwa sababu, tumbo litashindwa kusukuma hewa kutoka nje ili kutengeneza sauti nzuri za uimbaji. Pia, muimbaji atakuwa anabeua na kucheua hovyo wakati wa kuimba hali ambayo humfanya kutoa sauti mbaya au kushindwa kuimba kabisa.
Muimbaji ale matunda yenye maji mengi kwa ajiri ya kuufanya mwili wake
kufyonza maji na kupata nguvu. Mfano wa matunda hayo ni pamoja na tikiti
maji, tango na kadhalika.
Muimbaji ale mboga za majani zenye
maji mengi kwa ajiri ya kuufanya mwili kupata maji, chumvichumvi na madini
ambavyo vyote ni virutubisho vitakavyompa muimbaji nguvu ya kuimba na kutoa
sauti yake vizuri wakati wa kuimba. Mfano wa mboga hizo ni pamoja na mchicha,
tembele, ‘spinach’, ‘chinise’, na kadhalika.
Muimbaji anaweza kutumia asali, na chumvi kidogo ni nzuri kwa koo la lake katika siku ya uimbaji.
Muimbaji anaweza kutumia asali, na chumvi kidogo ni nzuri kwa koo la lake katika siku ya uimbaji.
NB. Matumizi ya chai ya mitishamba
(mchaichai) ni bora zaidi kwa afya ya koo na tumbo lako ili kusaidia
utengenezaji wa sauti nzuri za uimbaji.
3.0 Hitimisho na mapendekezo.
Koo hupendezwa, hutulizwa, huburudishwa, hutengenezwa na aina fulani ya pipi, asali, mvuke, chai ya mitishamba (mchaichai), kusafisha koo kwa maji chumvi, baadhi ya dawa kwa ushauri wa daktari, unywaji wa maji, na kadhalika. Pia, kinyume chake koo laweza kuharibiwa na matumizi ya vyakula au vinywaji kama vile; pombe, kahawa, soda, maziwa, chokoleti, pipi, ubuyu, matunda jamii ya ndimu, mayai, karanga, mahindi, bisi na kadhalika. Hivyo, muimbaji awe na taadhali katika matumizi ya vyakula na vinywaji ili kufanya sauti yake kuwa bora na kupendeza mbele za watu na Mungu tunayemtukuza kupitia sauti zetu.
Koo hupendezwa, hutulizwa, huburudishwa, hutengenezwa na aina fulani ya pipi, asali, mvuke, chai ya mitishamba (mchaichai), kusafisha koo kwa maji chumvi, baadhi ya dawa kwa ushauri wa daktari, unywaji wa maji, na kadhalika. Pia, kinyume chake koo laweza kuharibiwa na matumizi ya vyakula au vinywaji kama vile; pombe, kahawa, soda, maziwa, chokoleti, pipi, ubuyu, matunda jamii ya ndimu, mayai, karanga, mahindi, bisi na kadhalika. Hivyo, muimbaji awe na taadhali katika matumizi ya vyakula na vinywaji ili kufanya sauti yake kuwa bora na kupendeza mbele za watu na Mungu tunayemtukuza kupitia sauti zetu.
Mathalani, mwanafunzi mzuri ni yule
anayetafuta zaidi maarifa mara baada ya kujifunza jambo fulani. Hivyo, ni
matumaini yangu kuwa mafunzo haya yatakuwa msingi bora kwa muimbaji kutafuta
zaidi kwa habari ya vyakula na vinywaji katika uimbaji. Haya yalioelezwa hapa ni
machache sana. Pamoja na hayo, mabadiliko chanya ya uimbaji yatategemea
uzingativu na utekelezaji kwa vitendo wa mambo hayo na sio kusikiliza tu. Pia,
mabadiliko hasi yatatokea kwa wasiozingatia na kutekeleza kwa vitendo mambo
hayo. Yuko mshairi anasema,
“Mshumaa tuliwasha, ili nuru kumulika, Giza kulitokomesha, na nuru kuenezeka,
Mshumaa unawaka, giza mbona linazidi?” Pia, mshairi mwingine anasema,
“Mnazi walioukwea, Shinani wameanzia, Si kama mejirukia, Kileleni taka tua, Jikazie yako kwego, mnazi upate kwea.” Hivyo, huu ni mwanzo wa kujifunza uimbaji; huna budi kuifuata nuru (mafunzo) unayoangaziwa (kupewa) ili ufanikiwe katika uimbaji. Hii ni kwa sababu, wote waliofanikiwa katika aina yoyote ile ya huduma, walianzia chini na kwa kuwa walisikiliza na kutekeleza waliyoelekezwa na viongozi wao wakaweza kupanda na leo hii ni watu wakuu katia huduma.
“Mshumaa tuliwasha, ili nuru kumulika, Giza kulitokomesha, na nuru kuenezeka,
Mshumaa unawaka, giza mbona linazidi?” Pia, mshairi mwingine anasema,
“Mnazi walioukwea, Shinani wameanzia, Si kama mejirukia, Kileleni taka tua, Jikazie yako kwego, mnazi upate kwea.” Hivyo, huu ni mwanzo wa kujifunza uimbaji; huna budi kuifuata nuru (mafunzo) unayoangaziwa (kupewa) ili ufanikiwe katika uimbaji. Hii ni kwa sababu, wote waliofanikiwa katika aina yoyote ile ya huduma, walianzia chini na kwa kuwa walisikiliza na kutekeleza waliyoelekezwa na viongozi wao wakaweza kupanda na leo hii ni watu wakuu katia huduma.
Ili kuwa na afya nzuri katika mwili na katika uimbaji
wako zingatia :
1.
Punguza matumizi
mengi ya sukari, ongeza matumizi ya matunda
2.
Punguza kula nyama nyekundu, ongeza matumizi ya
mbogamboga
3.
Punguza matumizi ya soda, ongeza matumizi ya maji
4.
Punguza kuendesha, ongeza kutembea kwa miguu
5.
Punguza kupoteza muda wa kulala, Zingatia kulala kwa
wakati
6.
Punguza msongo wa mawazo, ongeza kupumzika
UMUHIMU
WA MAJI NA ASALI MWILINI
Maji
Tunaambiwa kuwa maji ni muhimu sana
ndani ya miili yetu. Maji yana faida nyingi sana na wengi tunazijua, lakini
tutajikumbusha baadhi.
1.
Moja
maji husaidia kupunguza calories mwilini, yaani badala ya kunywa vimiminika
vingine kama soda, bia na juisi ambavyo vina calories, maji hayana calories.
hivyo utakua umekunywa maji ambayo ni salama mbadala na vinywaji vingine
ambavyo vina calories.Kumbuka pia maji hayana sukari, mafuta na viungo vingine
vinavyotengeneza vimiminika vingine
2.
Unywaji wa maji mengi hutupunguzia uwezekano
wa kupata magonjwa kama ya moyo, hivyo inashauriwa kwa siku tunywe zaidi ya
bilauri mbili za maji na kuendelea.
3.
Maji huongeza nguvu mwilini kwani unapokua na
upungufu wa maji, unaanza na kusikia kiu ambayo huenda kupelekea kujisikia
uchovu, misuli kuchoka, kizunguzungu na ishara nyingine za kunyongonyeza mwili.
4.
Maji ni dawa ya maumivu ya kichwa. Mara kwa
mara tuumwapo kichwa pengine ni upungufu wa maji ndio uliopelekea maumivu haya,
lakini tunywapo maji basi maumivu huoondoka. Kuna sababu nyingine zinazopelekea
vichwa vyetu kuuma lakini, ukosefu wa maji mwilini ni sababu inayojulikana
zaidi.
5.
unywaji maji hupelekea kusafisha ngozi yako,
na mara kwa mara Rafiqs wengi wamejivunia kuwa na ngozi bora baada ya unywaji
wa maji wa kutosha. Haiwezi tokea mara moja ila baada ya wiki moja utaanza
kuona mabadiliko ya ngozi yako na itaanza kung’ara.
6.
mfumo wa kuchanganya chakula ndani ya miili
yetu (digestive system) unahitaji maji mengi ili kufanikisha kazi yake
kifasaha, hivyo yatupasa kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi yake vyema katika
muda sahihi kwa kunywa maji ya kutosha. Pia maji husaidia kuponesha maumivu ya
vichomi vya tumbo, na pia hutupa urahisi pale tuendapo haja kubwa, kwani
tunakua hatuna ukosefu wa maji mwilini. Maji husaidia pia kuondosha uchafu
ndani ya miili yetu na kuacha mwili ukiwa msafi.
7.
Kwa unywaji mwingi wakati wa mfumo wa kuchanganya
chakula unaendelea, imeonekana kuwa maji husaidia kupunguza uwezekani wa kupata
saratani ya colon kwa asilimia 45, asilimia 50 ya saratani ya kibofu cha mkojo
na pia hupunguza uwezakano wa kupata saratani ya matiti kwa kina mama.
8.
Kuwa na ukosefu wa maji mwilini husababisha
kukurudisha nyuma katika swala zima la mazoezi na kukufanya iwe ngumu kunyanyua
vyuma vya mazoezi, pamoja naa kufanya mazoezi mengine, hivyo basi inashauriwa
kunywa maji kabla, wakati na baada ya mazoezi ili uweze kuyafanya vyema na katika
hali salama.
Tunaweza anza jiuliza, kiasi
gani cha maji twatakikana kunywa?
Inashauriwa ni glass nane kwa siku,??? Labda inawezakana
sio sahihi sana…… kwasababu kiasi hicho kinahusisha maji safi ya kunywa
tunayoyanywa, pia maji yanayopatikana kwenye vyakula tunavyokula na vinywaji
vingine mbali na maji ya kunywa. Pia kiasi hicho hakikuangalia uzito wa miili
yetu kitu ambacho ni muhimu sana tunapoongelea kiasi cha maji cha kunywa, na
pia kiasi cha maji hutofautiana pale ambapo tunaumwa, au kwa wale tunaofanya
mazoezi kila siku.
Jambo lingine, unaposikia kiu,
kumbuka kwamba tayari una upungufu wa maji kwa hiyo kunywa pale hakutimizi zile glass nane za kunywa maji.
Cha kufanya basi, ni kujenga mazoea:
2.
Kunywa
glass moja ya maji pale uamkapo, glass moja kila baada ya mlo, glass moja
katikati ya milo yako ya siku, na kumbuka kunywa maji kabla, wakati wa na baada
ya mazoezi. Jaribu kuepuka kupata kiu ya maji.
3.
Beba chupa ya maji: Wengi wenye shughuli za
kutembea hapa na pale itawapasa kubeba chupa ya maji mkononi na kunywa mara kwa
mara, inapoisha ongeza nyingine. Na kwa wale wanaokaa maofisini, weka glass ya
maji pembeni yako na uwe unakunywa mara kwa mara na kuongeza pale inapokwisha.
Njia nyingine, ni kuegesha mlio kwenye saa ya mkononi au ya kwenye simu, au
kwenye Computer yako, iwe inalia kila lisaa kamili linapotimu, ili uweze
kukumbuka pale unaposikia kengele au alarm.
Iwapo unajisikia hamu ya kunywa soda au kimiminika chenye kilevi au cha aina nyingine yeyote, badala ya kukifuata hicho, badili na fuata glass ya maji na unywe. Jaribisha maji yenye ladha pale unapokua katika sherehe au makutanoni na marafiki.
Iwapo unajisikia hamu ya kunywa soda au kimiminika chenye kilevi au cha aina nyingine yeyote, badala ya kukifuata hicho, badili na fuata glass ya maji na unywe. Jaribisha maji yenye ladha pale unapokua katika sherehe au makutanoni na marafiki.
Anza mazoezi, kwani mazoezi hukufanya uwe na hamu ya kunywa maji maana si utasikia kiu. Si lazima kunywa vinywaji vya kuongeza nguvu, ila kama unafanya mazoezi zaidi ya lisaa limoja na kuendelea waweza kuvinywa. Kunywa maji mapema iwapo wajua utaenda kufanya mazoezi, kwani itasaidia maji kufika kwenye system ya mwili wako vyema pale unapoanza mazoezi, kunywa maji wakati wa mazoezi na baada ya mazoezi.
Fuatilia mwenendo wako wa unywaji maji kwa kuandika pahala kwa ajili ya kumbukumbu. Hii itakusaidia kukuonesha na kukukumbusha kwamba yakupasa kunywa maji katika muda ule ule kila ufikapo na kiasi ambacho umejipangia. Andika muda upande wa kwanza na wapili unaweka alama ya vema kila mara unywapo maji .
Asali
Nyuki anauwezo wa kutembea mile elfu tatu akikusanya maua ya aina mbalimbali toka miti mbalimbali milioni kumi na tano kwa ajili ya kutengeza asali kilo moja ndani ya miezi mitatu. Kutokana na mchanganyiko huu unaotengenezwa na mdudu nyuki ASALI ina uwezo wa kutibu magonjwa zaidi ya mia moja. Bado utaendelea kutumia sukari yenye 'chemicals' zinazopunguza uwezo wa kuona na kuleta madhara mengine!. Unashauriwa na wataalamu wa afya kwamba kila siku uamkapo ramba asali ujazo wa kifuniko cha soda kimoja pia tumia asali kama kiungo cha chai, uji,maziwa na kadharika. Pia asali inatumika kama mboga kwa kulia ugali uliopoa. Ukila na ugali wa moto unaweza kupata maumivu ya tumbo. Tumia asali kwa wingi kwani ni 'antibiotics' pia. Kumbuka asali Mbichi ambayo haijachemshwa motoni ndiyo inayofaa. Hakikisha umejiridhisha kuw asali uliyonunua ni mbichi.
Nyuki anauwezo wa kutembea mile elfu tatu akikusanya maua ya aina mbalimbali toka miti mbalimbali milioni kumi na tano kwa ajili ya kutengeza asali kilo moja ndani ya miezi mitatu. Kutokana na mchanganyiko huu unaotengenezwa na mdudu nyuki ASALI ina uwezo wa kutibu magonjwa zaidi ya mia moja. Bado utaendelea kutumia sukari yenye 'chemicals' zinazopunguza uwezo wa kuona na kuleta madhara mengine!. Unashauriwa na wataalamu wa afya kwamba kila siku uamkapo ramba asali ujazo wa kifuniko cha soda kimoja pia tumia asali kama kiungo cha chai, uji,maziwa na kadharika. Pia asali inatumika kama mboga kwa kulia ugali uliopoa. Ukila na ugali wa moto unaweza kupata maumivu ya tumbo. Tumia asali kwa wingi kwani ni 'antibiotics' pia. Kumbuka asali Mbichi ambayo haijachemshwa motoni ndiyo inayofaa. Hakikisha umejiridhisha kuw asali uliyonunua ni mbichi.
Pia
mazoezi mengine rahisi kwa mwimbaji ni ku Harmony (Harmonize) =
“Huuuuu,
haaaa, hoooo”. Mwimbaji lazima uwe mjanja na personal swagga na lazima ziendane
na facial expression pamoja na kukaa kwenye ufunguo (key) na mapigo ya wimbo.
Pia add lips (kuchombeza) huleta ubora wa uimbaji.
NB. Inawezekana
lugha niliyoitumia hujaielewa sana, na wakati mwingine nimechanganya na
kingereza au lugha ya muziki. Ikumbukwe kuwa muziki una lugha yake, na pia
nimejaribu kutafsi kutoka kwenye notisi zangu ambazo mimi mwenyewe najifunza
kwa lugha ya kingereza. Lakini kwa ushauri zaidi tuwasiliane.
Kumbuka
muziki au uimbaji ni kama bahari, kila mtu anaogelea pale anaweza kufika, mimi
naweza nikakutoa hapa nikakupeleka pale, na mwingine akakutoa pale na
kukupeleka kwingine. Hakuna aliyefika kikomo cha kujua muziki au uimbaji, sote
ni wanafunzi, na pia katika kufundishana sote tunajifunza. Ikiwa unataka kuwa
mwimbaji bora, na unahisi bado unatatizo fulani tuwasiliane.
MAFUNZO BINAFSI YA KUWA
MUIMBAJI BORA
Yafuatayo ni
baadhi maelekezo muhimu yatakayo
kufanya kuwa muimbaji bora, kwako wewe mwenye uwezo wa kuimba au usiye jua
kabisa na umekuwa na ndoto ya kuja kuwa muimbaji lakini hujui namna ya
kujifunza.
1.Anza kufanya mazoezi ya uimbaji pamoja na waimbaji
katika CD’s, hakikisha unaendana na mianguko yote. Sauti za juu, sauti za chini
na kati kwa kiingereza hufamika
kama(pitch).vile utajifunza jinsi ya kuhama ufunguo(key)kutoka ufunguo
mmoja na kwenda ufunguo mwingine na
jinsi ya redio, zoezi hili litakuwezesha kufahamu mbinu nyingi wanazotumia
waimbaji wakati mwingine bila hata wewe
kujijua yaani automatic,mambo unayoweza kujifunza kutumia pumzi wakati wa uimbaji nk.
2. Jaribu kuanza kuimba mbele ya watu wa karibu na yako
mfano marafiki zako, familia yako, mpenzi wako
na kuwaomba wakusikilize
ikiwezekana wakukosoe au kukuponda. Hapa ukipata msikilizaji anayejua muziki, itakuwa
ni vizuri zaidi kwani anaweza kukurekebisha maeneo utakayo kuwa umekosea wakati
unapoimba,kama kuchanganya sauti, kutofuata mwendo wa mapigo wakati unapoimba,
kuimba nje ya ufunguo nk.
3.
Jirekodi na jisikilize mwenyewe kama unaona kuna dosari yoyote kinyume na
ulivyotarajia katika uimbaji wako rudia tena kuimba na kujirekodi,ukizingatia
kutorudia tena makosa uliyoyaona mwanzoni. Aidha kama unaona umefaulu kwa kiwango ulichokitaka, jaribu
kuwapa wengine wasikilize rekodi ya wimbo wako na kutoa maoni yao.
4. Nunua vitabu au
video vitakavyokupa maelekezo na
mbiu tofauti kuhusu uimbaji, hii ikiwa
ni pamoja na kufanya mazoezi ya sauti voice training, itakupa uwezo zaidi
katika kuimba nyimbo za aina tofauti
5.Jiunge na vikundi vya
uimbaji na kuanza kuimba nao ilikupata uzoefu zaidi kwani kuna utofauti mkubwa
kati ya kujiimbia mwenyewe na kuimba mbele za watu kenye umati.
Pamoja na kufahamu mambo hayo lakini kuna vidokezo muhimu vya
kwako wewe unaweza kujifunza kuimba navyo ni:
1.
Fanya mazoezi ya kuimba mara kwa mara
hata wakati unapokuwa peke yako.
2.
Jiamini
wewe binafasi na usijinganishe na
waimbaji wengine,wenye majina kwani kila mtu anauwezo na kipaji chake hata wewe
unaweza kuwa juu siku moja.
3.
Hakikisha una sauti
nzuri japo si lazima sana na unakipaji na kuipenda kwa dhati kazi ya
uimbaji ili hata utakapokabiliana na vikwazo haita kuwa tatizo kwako, bali
itakupa changamoto ya kujifunza zaidi na kujisahihisha maeneo yenye udhaifu..
4.
Inawezekana katika uimbaji wako kuna
eneo unaliwezea sana na linakuongezea wapenzi au mashabiki wengi (kucheza,
kutawala jukwaa, kutetemesha sauti n.k) basi boresha zaidi.
5.
Kuwa na ukaribu na mwalimu wa
muziki/uimbaji au mtu mzoefu,aliye mwaminifu ili aweze kukupa mawaidha kadhaa
uweze kufikia kiwango kinachoridhisha hata kwa wasikilizaji watakao kusikia.
6.
Ukifanikiwa katika mambo hayo anza sasa
kujifunza ala za muziki, kama guitar, kinanda pia unaweza kujifunza hata
kucheza hii itakusaidia kukupa uzoefu wa kuimba na vyombo live
performance’'katika matamasha ya wazi na kanisani.
Vile vile kitu kingine
muhimu ni kuomba msaada kutoka kwa mwalimu wa muziki/ uimbaji au mtu
yeyote mtaalam wa muziki uanze kufanya mazoezi ya kuimba
scale kama major scale,chromatic scale na scale nyinginezo labda nikupe mfano
wa major na chromatic scale na unaweza kumuomba mpiga kinanda akakipigia ili uzisikie jinsi zinavyosikika
na uzifanyie mazoezi ya kuimba mara kwa mara.
Mfano wa major scale
katika ufunguo wa C(key C).C,D,E,F,G,A,B,C
Mfano wa chromatic scale katika ufunguo wa
C(keyC)
C,C#,D,D#,E,F,F#,G,G#,A,A#
B,C
Endapo
utasoma nadharia ya muziki unaweza
kujifunza aina za scale.pia mwalimu akupe mazoezi ya kujenga uwezo wa sikio
lako kimuziki uwe na sikio la muziki itakusaidia kuimba bila kutoka nje ya key,
kuijua sauti yako na kujua kama ala za muziki hazijarekebishwa vizuri,mpigaji
ukiwa na sikio la muziki ni muhimu
pia utabaini vitu hivyo
kama muimbaji anaimba na kutoka nje ya
key pia utaweza kutyuni ala zako. Lakini kama sikio la muziki hauna si rahisi
kutyuni ala kama gitaa. Ni vizuri waimbaji na wapigaji kujifunza nadharia ya
muziki (music theory) itasaidia sana katika kukuza uelewa. Pamoja na hayo
vilevile jifunze kufanya mazoezi mbalimbali kama major,minor na zinavyosikika
na kuziimba.
N.B. Sio kila mwimbaji
mwenye jina anafaa kuwa mwalimu wa kukuelekeza au kukufundisha. Pia sio lazima
uweze kila kitu kwenye uimbaji au muziki ndipo uwe mwimbaji bora.
Sio waimbaji wote ni
wanamuziki na sio wana muziki wote ni waimbaji. Sio kila mwimbaji ni mtunzi,
lakini pia inawezekana mtu akawa mtunzi na asiwe mwimbaji.
Zingatia nguzo nne za
muziki pamoja na mazoezi ya pumzi yanayofaa kwa mwimbaji.
Nianze kwa kusema, nimekuwa mmoja kati ya waalimu wa sauti na uimbaji, niliyewezesha watu wengi, vikundi vingi, na kwaya nyingi kuimba vizuri.
Lakini pia nashangaa wapo watu wengi wanaokimbilia studio, wanatengenezewa studio lakini ukweli ni kwamba hawajawa waimbaji wazuri, ni waimbaji wa kuimbia CD. Jamani kuimba vizuri kuna gharama zake.
Ikumbukwe kuwa, ili uimbaji wetu au muziki wetu uwe wa viwango vya
kimataifa yapo mambo yanayotakiwa kufanyika:
Kwanza
ni uandishi mzuri, ubunifu zaidi, studio bora
(quality of studio), kuandaa video yenye viwango (quality of video).
Nimekua
nikifundisha kwa kina kuhusu hatua nne za kuelekea kuwa na albam bora ya audio,
ikiwa ni pamoja na: mwimbaji kuwa bora, tungo bora, muziki bora na studio bora.
Nikualike tena kuhudhuria mafunzo yetu ya sauti yanayoendelea maeneo ya
Ukonga. Kwa kuchangia kidogo tu nitakufundisha mbinu za kuwa mwimbaji bora. Tuwasiliane.Tuendelee na somo:
Unahitaji kufanya nini?
Unahitaji kuboresha sauti yako kwa kupumua vizuri na kutuliza misuli yako badala ya kuiga mtu mwingine.
Kwa Nini Ni Muhimu?
Sauti nzuri hufanya wengine watulie na kufurahia kusikiliza. Sauti mbaya huaribu mawasiliano, na inaweza kumfadhaisha mwimbaji/msemaji na wasikilizaji.
KWA KAWAIDA watu hawavutiwi tu na
mambo yanayosemwa, bali wanavutiwa pia na jinsi yanavyosemwa. Ikiwa mtu
anayezungumza nawe au anayeimba mbele yako ana sauti nzuri, changamfu, ya
kirafiki, na yenye fadhili, utafurahia kumsikiliza kuliko kama ana sauti kali
isiyo ya kirafiki, sivyo? Kukuza sifa hizo nzuri hakutegemei tu kuboresha
sauti. Kunaweza kuhusu utu wa mtu pia.
Nyakati nyingine sauti isiyofaa
inaweza kusababishwa na kasoro fulani ambayo mtu amezaliwa nayo au ugonjwa
uliodhuru zoloto. Huenda kasoro hizo zisiweze kurekebishwa katika mfumo huu wa
mambo. Lakini, unaweza kuboresha sauti yako ukijifunza kutumia vizuri viungo
vya usemi. Kwanza, tufahamu kwamba sauti za watu hutofautiana. Kwa hiyo,
usijaribu kuiga sauti ya mtu mwingine. Badala yake, boresha sauti yako mwenyewe
pamoja na hali zake. Unawezaje kufaulu?
Kuna mambo mawili makuu;
-
Pumua Vizuri.
Ili sauti yako iwe nzuri, unahitaji hewa ya kutosha na unahitaji kupumua
vizuri. Bila kufanya hivyo, sauti yako inaweza kuwa dhaifu mno na unaweza
kukata-kata maneno katika hotuba yako au uimbaji wako.
Sehemu kubwa za mapafu haziko juu
kifuani; sehemu hizo huonekana kubwa kwa sababu tu ya mifupa ya mabega. Lakini,
sehemu za mapafu zilizo pana zaidi ziko chini, juu tu ya kiwambo. Kiwambo
kinashikana na mbavu za chini na kinatenganisha kifua na tumbo.
Ukivuta pumzi na kujaza tu sehemu
za juu za mapafu, utakosa pumzi haraka. Sauti yako itakosa nguvu na utachoka
haraka. Ili uvute pumzi vizuri, unahitaji kuketi au kusimama vizuri na kurejesha
mabega nyuma. Jaribu sana usipanue sehemu ya juu pekee ya kifua unapovuta
pumzi. Kwanza vuta pumzi kabisa. Sehemu za chini za mapafu zikijaa hewa, mbavu
zako za chini zitapanuka. Kwa wakati huohuo, kiwambo kitasonga chini,
kikisukuma chini kwa utaratibu sehemu za tumbo hivi kwamba utasikia mkazo
kwenye mshipi wako au kwenye vazi katika eneo la tumbo. Lakini mapafu hayako
kwenye eneo la tumbo; yamefunikwa na mbavu. Unaweza kuthibitisha jambo hilo kwa
kuweka mkono mmoja kila upande wa mbavu za chini. Kisha vuta pumzi kabisa. Kama
unavuta pumzi vizuri, utaona kwamba huingizi hewa tumboni na kuinua mabega. La,
badala yake, utasikia mbavu zikisonga juu kidogo na kupanuka.
Kisha, jaribu kushusha pumzi.
Usishushe pumzi kwa ghafula. Ishushe polepole. Usijaribu kuzuia pumzi kwa
kukaza koo kwa sababu sauti itajikaza au itakuwa nyembamba sana. Mkazo wa
misuli ya tumbo na mkazo wa misuli iliyo kati ya mbavu huondosha pumzi, lakini
kiwambo hudhibiti mwendo wa pumzi hiyo.
Msemaji au mwimbaji anaweza
kudhibiti jinsi anavyopumua kwa kujizoeza kama vile tu mwanariadha anavyofanya
mazoezi ya mbio. Simama vizuri kama umerejesha nyuma mabega, vuta pumzi kabisa
ili sehemu za chini za mapafu zijae hewa, kisha shusha pumzi polepole na kwa
utaratibu ukihesabu kwa kadiri uwezavyo kabla ya kuvuta tena pumzi. Kisha
jizoeze kusoma kwa sauti ukipumua kwa njia hiyo.
-
Tuliza Mkazo wa
Misuli. Jambo jingine muhimu linalotokeza sauti nzuri ni utulivu! Unaweza
kuboresha sana sauti yako ukijifunza kutulia unapozungumza. Ni lazima akili na mwili
zitulie, kwa kuwa mkazo wa akili husababisha mkazo wa misuli.
Ifikirie misuli ya koo na kujaribu kuituliza. Kumbuka kwamba nyuzi
zako za sauti hutikisika zinapopitisha hewa. Sauti hubadilika misuli hiyo
ikikazika au ikitulia kama tu vile uzi wa gitaa hubadili sauti ukikazwa au
ukilegezwa. Sauti hurudi chini nyuzi za sauti zinapotulia. Kutuliza misuli ya
koo pia hufanya mianzi ya pua ibaki wazi, na hiyo huboresha sauti.
Tuliza mwili wako mzima—magoti,
mikono, mabega, na shingo. Ukifanya hivyo, utaweza kuvumisha sauti vizuri ili
isikike wazi. Sauti huvumishwa wakati mwili wote unapohusika kuitokeza, lakini
mkazo huizuia. Sauti hutokezwa kwenye zoloto nayo huvumishwa katika mianzi ya
pua, kwenye mifupa ya kifua, meno, na kaakaa ya mdomo na mianya iliyo katika
mifupa ya pua. Sehemu hizo zote zinaweza kuchangia ubora wa sauti. Ukiweka kitu
kwenye kibao cha gitaa cha kupaazia sauti, sauti itafifia; ni lazima kibao
hicho kisiwe na kitu ili kitikisike na kutoa sauti vizuri. Ndivyo ilivyo pia na
mifupa ya mwili wetu ambayo imeshikiliwa na misuli. Uvumishaji mzuri wa sauti
unakuwezesha kuwa na ubadilifu wa sauti na kuweza kuonyesha hisia mbalimbali
unapoimba au kuzungumza. Pia utaweza kuimbia au kuhutubia watu wengi zaidi bila
kukaza sauti.
JINSI YA KUFAULU
Fanya mazoezi ya kuvuta pumzi,
ukijaza sehemu za chini za mapafu kwa hewa.
Unapoimba au kuzungumza, tuliza
misuli yako ya koo, shingo, mabega, na mwili wote mzima.
MAZOEZI: (1) Kwa dakika chache kila
siku katika juma, fanya mazoezi ya kuvuta pumzi kabisa mpaka uzijaze sehemu za
chini za mapafu yako. (2) Jaribu kutuliza misuli ya koo unapoimba au
unapoongea, angalau mara moja kwa siku.
SAUTI HUTOKEZWAJE?
Sauti zote hutokezwa na hewa
inayotoka mapafuni. Mapafu hupiga hewa kama pampu kupitia koo na kuingia ndani
ya zoloto ambayo iko katikati ya koo. Ndani ya zoloto mna misuli miwili midogo
inayoitwa nyuzi za sauti, msuli mmoja uko upande mmoja na msuli mwingine upande
mwingine. Nyuzi hizo za sauti ndizo vitokezaji vikuu vya sauti. Misuli hiyo
hufungua na kufunga njia ya hewa katika zoloto ili kuingiza hewa na kuitoa na
vilevile kuzuia vitu visivyotakikana visiingie kwenye mapafu. Tunapopumua kwa
njia ya kawaida nyuzi za sauti hazitokezi sauti wakati hewa inapopita. Lakini
mtu akitaka kuimba au kuzungumza, misuli hufinya nyuzi za sauti, na nyuzi hizo
hutikisika wakati hewa inayotoka mapafuni inaposukumwa kuzipitia. Utaratibu huo
hutokeza sauti.
Kadiri nyuzi za sauti zinavyokazika,
ndivyo zinavyotikisika kwa kasi zaidi na ndivyo sauti inavyoinuka. Na kadiri
nyuzi hizo zinavyolegea, ndivyo sauti inavyopungua. Mawimbi ya sauti yanayotoka
kwenye zoloto huingia sehemu ya juu ya koo inayoitwa koromeo. Kisha mawimbi
hayo hupitia mdomo na pua. Hapo sauti nyinginezo huongezwa ili kurekebisha,
kukuza, na kuimarisha sauti ya awali. Kaakaa la mdomo, ulimi, meno, utaya, na
midomo huungana pamoja ili kutawanya mawimbi ya sauti, na kutokeza usemi
unaoeleweka.
Sauti ya mwanadamu ni ajabu sana,
na haina kifani ikilinganishwa na chombo chochote kile ambacho binadamu
ametengeneza. Ina uwezo wa kuonyesha hisia mbalimbali kama vile upendo na chuki
kali. Sauti ikikuzwa na kuzoezwa vizuri, inaweza kubadilikana sana na kutokeza
nyimbo tamutamu na semi zinazogusa mioyo.
KUSHINDA MATATIZO FULANI HUSUSA
Sauti dhaifu.
Sauti ndogo huenda isiwe dhaifu.
Ikiwa nzuri na yenye kuvutia, wengine wanaweza kufurahi kuisikiliza. Lakini ni
lazima sauti iwe yenye kiasi kinachofaa ili iweze kufaidi wengine.
Ili uboreshe ukubwa wa sauti yako,
unahitaji kuivumisha zaidi. Unahitaji kutuliza mwili wote mzima, kama
ilivyoonyeshwa katika somo hili. Pamoja na kutuliza mwili, fanya mazoezi ya
kuimba hali umefunga midomo. Midomo inapaswa kugusana kidogo, isishikane sana.
Unapoimba kwa njia hiyo, sikia mitikisiko ya wimbo huo akilini na kifuani.
Nyakati nyingine sauti husikika kuwa dhaifu au kukazika kwa sababu ya ugonjwa
au kukosa usingizi. Bila shaka, hali hiyo ikiboreka, sauti itaboreka.
Sauti inayoinuka juu sana.
Mkazo kwenye nyuzi za sauti hufanya
sauti iinuke. Sauti yenye mkazo hufanya wasikilizaji wawe na mkazo. Unaweza
kupunguza sauti nyembamba kwa kutuliza misuli ya koo ili kupunguza mkazo kwenye
nyuzi za sauti. Jaribu kufanya hivyo, ukifanya mazoezi kila siku unapozungumza.
Pia ni vizuri kuvuta pumzi kabisa.
Sauti ya kubana pua.
Nyakati nyingine pua iliyofungika
hutokeza tatizo hilo, lakini mara nyingi hali hiyo husababishwa na jambo
jingine. Nyakati nyingine kwa kukaza misuli ya koo na mdomo, mtu hufunga mianya
ya pua na kuzuia hewa isipite vizuri. Jambo hilo hutokeza sauti inayobana pua.
Unahitaji kutulia ili kuepuka jambo hilo.
Sauti nzito na kali.
Sauti kama hiyo haileti mazungumzo
ya kirafiki uimbaji wa kirafiki. Inaweza kutisha wengine.
Katika hali fulani, jambo muhimu ni
kuendelea kujitahidi kubadili utu wako. Ikiwa tayari umefanya hivyo, kujaribu
kutumia kanuni za kurekebisha sauti kunaweza kusaidia. Tuliza koo na taya.
Kufanya hivyo kutafanya sauti yako ipendeze zaidi na kufanya maneno mengine
yasitokee vibaya kwa kuyalazimisha kupitia meno.
VIUNGO VYA MATAMSHI
Kaakaa, Ulimi, Meno, Midomo, Taya,
pua…
Kumbuka kwamba kila mtu duniani ana
tone yake na hii hutokana na hivyo viungo nilivyotaja hapo juu. Maana rahisi ya
tone ni sauti ya mtu inapotoka au kusikika. Hivyo awe mwimbaji, muhubiri,
mwalimu, mtangazaji, public speakers… ana tone yake. Wapo wengi sana wametokea
kupendwa au kupata ajira nzuri kwasababu tu ya tone. Kumbuka haya yote
yanafanyika kupitia kitu kinaitwa DIAPHRAM; Mfano halisi ni kwamba, mwimbaji
anaimba kupitia diaphragm singing, muhubiri anatumia diaphragm speaking …
MKONDO WA HEWA MWILINI
Tundu la pua, Kinywa, Koo, Nyuzi za
sauti, Njia ya chakula, Mapafu, Kiwambo
Nyuzi za Sauti (zikitazamwa kutoka
juu)
Unapozungumza
Unapovuta pumzi
Unapovuta pumzi kabisa.
AFYA YA SAUTI (VOCAL HEALTH);
UNAPENDA KUIMBA VIZURI? BASI HII NI KWA AJILI YAKO
You are the instruments – Learn to sing like a pro!
Wewe ndie chombo halisi, jifunze
kuimba kama pro!
Ieleweke kwamba, Kuwa na utimamu wa
kimwili (fitness) sio kuwa bora
kuliko mtu flani, bali ni kuwa bora kuliko ulivyokua awali. Watu wengi sana
hutumia muda wao mwingi tu katika majumba ya mazoezi (Gym) wakifanya mazoezi mbalimbali ya kimwili
na wana nidhamu sana katika hili, ni jambo zuri sana kiukweli. Lakini tunasahau
kitu kimoja; Koo lako ni sehemu ya mwili wako pia! na kama ukitenga muda kwa
ajili ya mazoezi, na utunzaji mzuri wa Sauti yako, utawashsangaza wengi sana na
ubora wa sauti yako! Ungependa kuelewa nini cha kufanya??
AFYA YA SAUTI:
Sauti yako ndiye balozi wako kwa
ulimwengu, umewahi kuona mtu hata awe mpole kiasi gani, lakini kama akiwa na
sauti ya kutisha (hasahasa wazee) hata watoto humuogopa?? au hata ukifatwa na
mtu ambae humjui na ana sauti ya ajabu ajabu we mwenyewe lazima uogope!
Sauti unayoitumia kuongea ndiyo hiyo
hiyo unayoitumia kuimba, hivyo basi, ukiitumia sauti yako hovyo katika maongezi
utaathiri pia uimbaji wako! Zingatia hili; kama vile mwanamuziki kitendea kazi
chake ni kile chombo cha muziki, vilevile mwimbaji kifaa chake ni lake. Sasa
guitar likikatika nyuzi unaweza ukatafuta uzi mwingine, lakini koo halina
spare, litunze. Unyevu, Mazoezi ya misuli ya shingo na mapumziko, ndiyo viungo
muhimu katika kuipika afya ya sauti yako. Vinafanyaje kazi? ENDELEA…
UNYEVU;
Msingi wa sauti ni maji mengi
Tumia Maji ya Kunywa kwa wingi sana
ili kuzifanya Ala zako za Sauti (Vocal Chords)
ziwe na unyevu, zisikauke. Maji hulainisha na kuyaondoa makohozi katika koo na
kuyafanya yasigandamane kwenye ala za sauti.
Usitumie “spray” ya aina yoyote kunyevusha koo lako. Kumbuka kubadili
mazingira yenye hali za hewa tofauti tofauti huathiri ala za sauti. Cha
kufanya, kunywa maji ya kutosha na kula matunda yenye maji mengi kama matikiti
maji na matango, achana na matunda yenye tindikali nyingi kama “citrus fruits” mfano machungwa, malimao, na
ndimu kwani yatazisugua ala za sauti na kuziachia mikwaruzo.
MAZOEZI;
“Mazoezi
ya sauti yanachekesha, yafanye ukiwa peke yako, hasa bafuni unapooga”
Fanya mazoezi ya sauti na mwili kwa
ujumla na kwa bidii. Fanya mazoezi ya ulimi kama “tongue
trill” (yafanye ukiwa mwenyewe, hasa bafuni ili usije ukachekesha
watu) ili kuruhusu upitaji mzuri wa hewa kwenye koo, na upumuaji mzuri kwa
ujumla.
Jifanyie pia masaji maalum za ulimi
na maungio ya taya, fanya “humming“,
yaani tamka herufi ‘m‘ kwa
muendelezo, ukiwa umefumba mdomo, (kama sauti ya
nyuki wengi) ukiwa bafuni ili kuipasha sauti yako. Hakikisha
unafanya hivi kila siku kwa matokeo mazuri.
Fanya pia mazoezi ya misuli ya
shingo, koo taya na mabega, pia legeza misuli ya shingo na koo unapoimba noti
za juu sana au za chini sana, ukikakamaza shingo itakusababishia maumivu na
sauti itaharibika.
MAPUMZIKO;
Baada ya kuunguruma kwa muda mrefu, pumzika
Hakuna kitu kinachoweza kufanya kazi
bila kuchoka, hata iwe mashine ya Mjerumani. Kwahiyo, hakikisha unapata
mapumziko ya kuongea baada ya kutoka kwenye maongezi au uimbaji uliokufanya
utumie nguvu nyingi ili kuinusuru sauti yako.
Epuka tabia za kupiga kelele hovyo,
kubishana kwa sauti na nguvu nyingi, au kuimba kwa nguvu sana kusiko kua na
maana yeyote. Epuka sana uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kwani
kutakusababishia madhara kwenye sauti.
KWA KUMALIZIA…
- Acha sauti yako ing’ae, kuwa wewe na usiigize sauti ya mtu
- Siku zote kunywa maji mengi yasiyochanganywa na kitu, maji tu!
- Pata muda wa kutosha wa kupumzika, epuka kelele zisizo za msingi
- Mwisho, Jifunze mbinu bora za uimbaji
(Kwa masomo zaidi yanayohusu mbinu za uimbaji, hudhuria
madarasa yetu)
John Shabani akiongoza sifa
Moja ya huduma za John Shabani
Mwalimu John akiongoza mazoezi yapumzi
Joyce John akijifunza kupiga kinanda
MAFUNZO YA SAUTI
VOCAL TRAINING
By John Shabani
Mobile: 0716560094, 0754818767
Facebook: John Shabani
MAZOEZI NA FAIDA ZAKE