Kila mtu anaweza kuitumia sauti yake, lakini si kila mtu anajua jinsi ya kuitunza au kuiponya inapopatwa na tatizo. afya yake, au nini cha kufanya. Makala hii itasaidia kila mtu kujifunza jinsi ya kuponya sauti na pia kutoa ushauri wa jinsi ya kuitunza na kuifanya kuwa na afya na nguvu kwa ajili ya siku zijazo. Masomo haya yanawafaa walimu, wainjilisti, wanasiasa, wazazi, wanasheria, madaktari, na waimbaji, na kila mtu ambaye shughuli zake hulazimu kakuongea sana.
Yawezekana umekuwa ukijiuliza,tunapozungumzia dhana nzima ya kukauka au kupotea kwa sauti, hivi huwa ina enda wapi? Sijui kama ume wahi jiuliza swali hili mpenzi msomaji, leo na kuendelea utapata majibu mengi ya maswali yako kupitia mtiririko wa vipindi hivi ndio maana pia tume lazimika tumia kiswahili ili kuwafikia watu wengi zaidi.MWANADAMU anasehemu laini sana kama ute wa viji ngozi viwili ndani ya boksi la sauti kooni(voice box/larynx)vinavyo itwa vocal cords au vocal folds, kwa lugha ya kigeni. hapa ndipo maala muhimu ni sisitize tena muhimu mno maana ndipo naweza sema ni kama kiwanda cha sauti. Mitetemo ya sauti ni matokeo ya kani msukumo wa hewa itokayo mapafuni kupitia kwenye kijisanduku cha sauti(voice box/larynx)mtetemo wa hivyo vijinyama viwili(vocal cords) ndani ya kijisanduku cha sauti(voice box) ndipo hupelekea huo mlindimo wa sauti uisikiayo. Hakika Mungu wa ajabu. Sasa Sikila unacho kula hugusa au kufikia mahala hapa itokapo sauti, isipo kuwa vinavyofika mahala hapa ni vile vitu unavyo weza vuta mfano: mvuke na moshi kama vile moshi wa sigara ambao ni hatari sana. Sasa nikujibu sauti hupotelea wapi/hukauka kweli??. Kiukweli sauti haikauki ila inakoma kuzalishwa kwa muda, hii nipale ambapo Vijinyama laini hivyo viwili(vocal cords) vinapo vimba hali hii hufanya vishindwe tetemeka na kutoa sauti, hapo watu husema sauti ime potea au ime kauka. SASA NI NINI hupelekea uvimbe huu? Yafuatayo ni majibu: Uvutaji wa sigara, matumizi ya juu mno ya sauti kama kupayuka na kupiga yowe, kikohozi cha mara kwa mara na pia maambukizi katika koo la sauti, mfano virus wa mafua (flu viruses).
Niruhusu nikupe darasa kidogo kuhusu sauti;
Nidhahiri umewahi sikia au kuona mwalimu akiwaambia kwa ukali waimbaji mwanzo kabisa mwa zoezi kuwa;"jamani mbona leo siwaelewi namna mnavyo imba/TOENI Sauti/Mnaimba kama hamtaki/Naomba kwanza wote msimame n.k... Niliwahi kufundisha juu ya tabia ya sehemu ya ndani ya kijisanduku cha sauti(VOICE BOX/LARYXN):
NDANI ya kiji sanduku hiki kuna kijisehemu laini sana kiitwacho (VOCAL FORD/VOCAL CORD). Sehemu hii ina tabia ya kusinyaa na kubadilika hali yake kutokana na mazingira au hali ya hewa, mfano, ubadilipo mazingira yenye joto au baridi huchukua muda kujishape na yale mazingira, kadharika ukiwa unaongea hutenda tofauti kabisa na pale uimbapo. Lakini pia mazingira ya mfumo wa maisha ya kila siku; malazi, makazi, vyakula, vinywaji, msongo wa mawazo, matumizi ya sauti, kupumzika n.k.
Kama walivyo wanariadha na wacheza soka kabla hawajaingia ulingoni lazima wawe na maandalizi ya mazoezi ili kuweka misuli yao sawa. Hivyohivyo misuli yetu ya koo vocal fold), lazima uiwarm up kabla hujaitumia. HIVYO si sahihi kuingia kwenye uimbaji moja kwa moja pasi kuandaa koo kwa mazoezi andalio (VOCAL WARM UP). Hapa naomba unielewe mpendwa hapa namaanisha vocal warm up na si VOCAL EXERCISES), tutajifunza tofauti ya haya mambo mawili taratibu. Kuna kipindi serikali ili tangaza kwamba kansa inayoongoza nchini ni kansa ya kizazi na kansa ya koo. Sasa huyu mwimbaji au muhubiri hanywi maji vizuri at least glass nane kwa siku (maana hatunywi maji kwasababu tuna kiu, tunakunywa kwasababu makoo yetu yanatakiwa kuwa na unyevunyevu kila wakati), ni mtumiaji mzuri wa vitu vya baridi kisa ana friji (jamani friji haipo kwa ajili ya kutumaliza, eti friji yangu inagandisha kweli! Kiasi kwamba umekubali ikugandishe nawewe haaah! Hatutakiwi kula barafu, friji inakusaidia kutunza kitu, unapokihitaji, utoa, kinapoa kisha unatumia. Wewe mwimbaji, muhubiri, umeshinda kutwa nzima ukiitumia sauti, maji hujanywa, huna maandalizi ya misuli ya koo then jioni unaagiza maji ya baridi sana, au soda (kemikali), unachotafuta hapo ni majanga kwenye koo.
Au unaagiza majuice yenye kemikai au energy drink eti upate nguvu, ukifahamu fika kinywaji hicho kina cafein, unadiriki kuingiza cafein kujerui koo, hatari saaaana! Jambo linguine microphone inayotumika imekaa miaka miwili, haijasafishwa, imetumika na kila kiumbe na wengine midomo yao utadhani ina kisima cha mate tena yenye madhara, alafu hiyo mic inakutu, alafu mtu anaitumia tu, mwisho wa siku jamani tumwmbee mwimbaji wetu, mchungaji wetu kuna pepo limevamia sauti yake halitaki watu wapone, waokolewe, hapana pepo ni yeye mwenyewe. Ni kukosa maarifa, na ukikosa maarifa lazima uangamie.
SASA ili uweze imba kwa uhuru na sauti bora yenye ujazo ni lazima mishipa ya koo lako iwe huru kwa msawazo(RELAXATION). Moja ya mishipa inayoweza mpelekea muimbaji kuimba/kuto imba kwa muda mrefu ni mishipa ya kichwa iliyopo nyuma ya shingo karibu na kisogo, ndio maana usikia watu kulalamika naumivu ya kichwa(STRAINING IN BACK MUSCLES) baada ya kuimba kwa muda mrefu.Waweza jaribu hapo ulipo kufungua kinywa chako mpaka mwisho wako kisha ona ni wapi mishipa ya kichwa, vuta utagundua ni nyuma ya shingo. ZOEZI HILI LA KITAALAMU BAADA YA TAFITI ZA KISAYANSI ndio suruhisho la matatizo hayo mawili (Tone~vocal fatigue na Straining in back muscles).
Hapa unaosha mikono kwa sabuni(ant bacterial soap)kwa maji safi kisha jikaushe kwa taulo safi.
*Ukiwa ume kaa au simama wima weka vidole vitatu kwa kinywa kisha imba herefi hizi; "A E I O U"kwa sekunde15- 35-60,.Baada ya hapo toa vidole kwa mdomo na jaribu ongea au kuimba utaona pumzi na wepesi/uzuri wa sauti. #ZOEZI MBADALA NI HILI
*Pasi vidole fungua kinywa kadri uwezavyo na imba kwa ulimi maneno haya LAGA LAGA LAGA LAGA LAA LAA×2,Kwa sekunde 15-45-60Bila kuruhusu taya na kidevu kucheza.mazoezi hayo yote hufanya kazi moja.
Vifuatavyo ni vitu muhimu kwa ajili ya afya ya sauti yako
Kuna vitu vitatu cha kwanza KUNYWA MAJI, cha pili KUNYWA MAJI na cha
tatu KUNYWA MAJI. Maji ni muhimu sana kwa sauti yako. Hakikisha
unakunywa maji ya kutosha.
Pumua kama muimbaji wakati wote hata ukiwa unazungumza na simu.
Hakikisha unakaa katika mkao mzuri kama ilivyoshauri katika sura ya pili.
Unaweza kutumia sauti yako yote pale unapotaka kusikika lakini hakikisha
hupigi mayowe ni hatari kwa sauti yako.
Hakikisha unapata muda wa kutosha wa kulala. Hakikisha una masaa 6 – 8
ya kulala
TANGAWIZI. Hii ni tiba nyingine nzuri ya sauti. Kiukweli huu ni mmea pekee na wa ajabu unao weza rejesha sauti ndani ya masaa machache mno,kuku toa kutoka hali ya kuto ongea kabisa mpaka kuimba kwa kishindo cha ajabu mimi nimeshuhudia hili kama muimbaji na mwalimu wa sauti.TANGAWIZI inatabia ya upasha joto pekee tu ilivyo,hali hii hupelekea hali kama ya muwasho(irritation)inayo pelekea ongezeko la kasi la mzunguko wa damu pale popote igusapo katika mwili.pia Tangawizi ni suruhisho la vimbe kutokana na hiyo sifa tajwa hapo juu.JINSI YA KUANDAA.osha mzizi wa hiyo tangawizi na maji safi bila kumenya(usiondoe ganda) kata vipande nyembamba mno vijae kijiko cha mezani kisha viweke kwenye maji(vikombe viwili vichemkavyo).kwa dakika kumi,ukiwa umefunika chombo unacho chemshia kisha chuja acha ipoe kidogo kwa joto unalo tumiaga kwa chai ya kawaida, usiweke sukari, badala yake waweza tumia kijiko cha asali kuongeza radha na asali ni tiba kubwa pia,hapo waweza tumia.ni vyema utumie unapoenda lala.Ifikapo asubuhi uta shuhudia haya maajabu ya mmea huu. Katika mafunzo haya ASALI ni somo lingine tutakalo jifunza pia.
Kama sauti yako imejeruhiwa vibaya, basi jambo muhimu zaidi la kufanya sasa hivi ni kuacha kutumia hiyo Sauti, ipumzishe. Punguza pia kuzungumza kwa muda mrefu na hasa kwa kupaza sauti kubwa au kupayuka na kutumia muda kidogo zaidi katika ukimya.
- Jambo jingine kubwa ambayo husaidia sauti iliyojeruhiwa ni chai ya moto (Kama vile coat tea). Au maji moto ukichanganya na asali na limau. Unaweza kupata pia dawa za mitishamba zilizohifadhiwa kitaalam katika maduka ya dawa, lakini ikiwa dini yako au tamaduni yako haina shida katika hili. Chai nzuri ni ile iliyo shauriwa ki afya na si kila chai ni bora. Unaweza kupata na dawa za mitishamba katika duka la dawa, ambazo ni maalumu kwa ajili ya sauti, Kunywa angalau kikombe asubuhi na kikombe wakati wa usiku.
kama kuna kitu ambacho kinaweza kusaidia kuponya sauti yako na pia inaweza kutumika kulinda kwa haraka ni unywaji wa maji ya kila siku. Maji husaidia na sauti yako kuwa hidrati, kuwa hidrati husaidia kuweka mwili wako katika afya nzuri na sauti yako tayari kufanya kazi. Pia asali mbichi husaidia. Maji ya mvuke ikiwezekana yachanganye na aina ya vics husaidia pia. Unaweza ukaogea au kujifunika na nguo nzito.
Naomba uzingatie kwamba sauti inataka matunzo. Na jinsi rahisi sana kuhifadhi sauti yako ili ifanye kazi vizuri na idumu kwa muda mrefu ni kama ifuatavyo.
- Mazoezi ya sauti mara kwa mara kama nilivoelekeza humu.
- Usinywe vinywaji baridi sana au barafu.
- Usivute sigara.
- Usivute bangi.
- Usitumie madawa ya kulevya.
- Chunga sana kwenye swala la pombe, aidha usitumie kabisa au tumia kidogo sana.
- Usiwe na tabia ya kukohowa kwa kasi ili kuondoa kitu kooni. Nadhani mnanielewa. Hii tabia hukwangua koo.
Virutubisho Vya Kutumia
- Vitamin C 1000mg wakati unahisi mafua au sauti imechoka. Yeyusha tembe moja kila siku ndani ya glasi ya maji unywe. Zinapatikana pharmacy.
- Kunywa maji mara kwa mara, yanasaidia kulainisha koo. Mwili wa binaadamu asilimia kubwa ni maji.
- Tumia Multivitamins
- Tumia Antioxidants
Hizi mbili za mwisho zina gharama kidogo, kwahivyo angalia tu uwezo wako.
3.0 Hitimisho na mapendekezo.
Koo hupendezwa, hutulizwa, huburudishwa, hutengenezwa pia na aina fulani ya pipi, asali, mvuke, chai ya mitishamba (mchaichai), kusafisha koo kwa maji, baadhi ya dawa kwa ushauri wa daktari, unywaji wa maji, na kadhalika. Pia, kinyume chake koo laweza kuharibiwa na matumizi ya vyakula au vinywaji kama vile; pombe, kahawa, soda, maziwa, chokoleti, pipi, ubuyu, matunda jamii ya ndimu, mayai, karanga, mahindi, bisi na kadhalika. Hivyo, muimbaji awe na taadhali katika matumizi ya vyakula na vinywaji ili kufanya sauti yake kuwa bora na kupendeza mbele za watu na Mungu tunayemtukuza kupitia sauti zetu.
Koo hupendezwa, hutulizwa, huburudishwa, hutengenezwa pia na aina fulani ya pipi, asali, mvuke, chai ya mitishamba (mchaichai), kusafisha koo kwa maji, baadhi ya dawa kwa ushauri wa daktari, unywaji wa maji, na kadhalika. Pia, kinyume chake koo laweza kuharibiwa na matumizi ya vyakula au vinywaji kama vile; pombe, kahawa, soda, maziwa, chokoleti, pipi, ubuyu, matunda jamii ya ndimu, mayai, karanga, mahindi, bisi na kadhalika. Hivyo, muimbaji awe na taadhali katika matumizi ya vyakula na vinywaji ili kufanya sauti yake kuwa bora na kupendeza mbele za watu na Mungu tunayemtukuza kupitia sauti zetu.
Niseme kwamba, mwanafunzi mzuri ni yule anayetafuta zaidi maarifa mara baada ya kujifunza jambo fulani. Hivyo, ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya yatakuwa msingi bora kwa muimbaji kutafuta zaidi kwa habari ya vyakula na vinywaji katika uimbaji. Haya yalioelezwa hapa ni machache sana. Pamoja na hayo, mabadiliko chanya ya uimbaji yatategemea uzingativu na utekelezaji kwa vitendo wa mambo hayo na sio kusikiliza tu. Pia, mabadiliko hasi yatatokea kwa wasiozingatia na kutekeleza kwa vitendo mambo hayo. Yuko mshairi anasema,
“Mshumaa tuliwasha, ili nuru kumulika, Giza kulitokomesha, na nuru kuenezeka,
Mshumaa unawaka, giza mbona linazidi?” Hivyo, huu ni mwanzo wa kujifunza uimbaji; huna budi kuifuata nuru (mafunzo) unayoangaziwa (kupewa) ili ufanikiwe katika uimbaji. Hii ni kwa sababu, wote waliofanikiwa katika aina yoyote ile ya huduma, walianzia chini na kwa kuwa walisikiliza na kutekeleza waliyoelekezwa na viongozi wao wakaweza kupanda na leo hii ni watu wakuu katia huduma.
“Mshumaa tuliwasha, ili nuru kumulika, Giza kulitokomesha, na nuru kuenezeka,
Mshumaa unawaka, giza mbona linazidi?” Hivyo, huu ni mwanzo wa kujifunza uimbaji; huna budi kuifuata nuru (mafunzo) unayoangaziwa (kupewa) ili ufanikiwe katika uimbaji. Hii ni kwa sababu, wote waliofanikiwa katika aina yoyote ile ya huduma, walianzia chini na kwa kuwa walisikiliza na kutekeleza waliyoelekezwa na viongozi wao wakaweza kupanda na leo hii ni watu wakuu katia huduma.
Ili kuwa na afya nzuri katika mwili na katika uimbaji wako zingatia :
- Punguza matumizi mengi ya sukari, ongeza matumizi ya matunda
- Punguza kula nyama nyekundu, ongeza matumizi ya mbogamboga
- Punguza matumizi ya soda, ongeza matumizi ya maji
- Punguza kuendesha, ongeza kutembea kwa miguu
- Punguza kupoteza muda wa kulala, Zingatia kulala kwa wakati
- Punguza msongo wa mawazo, ongeza kupumzika
Zingatia :
Maji ya moto au aina ya chai mitishamba (herbal tea) ni bora, Mwimbaji mzuri hutumia class 8 za maji kwa siku, wapo ambao hutumia hadi lita 4 pia yapo maji ya ziada kutoka katika vyakula.
Kupasha sauti kwa kukohowa kohowa sio njia ya kukusaidia kuimba vizuri, badala yake hukata sauti
Pamoja na umuhimu wa maji, lakini acha matumizi ya maji mengi saa moja au mbili kabla ya kuanza uimbaji badala yake asali ni bora zaidi. Lakini pia sauti ikipatwa na tatito unaruhusiwa kupata maji ya moto pamoja na asali
Angalizo kuhusu mazoezi: Mazoezi huwa yana ugumu wake hasa pale unapokuwa unaanza, usikate tamaa wala usikubali uvivu au maumivu yakakurudisha nyuma. Jitengee muda maalum kwa ajili ya kufanya mazoezi na usianze kwa kufanya mazoezi magumu bali anza na mepesi mepesi ili kuupa mwili nafasi ya ku-adopt mabadiliko
Kwa mafunzo zaidi jiunge na darasa letu pele SJ STUDIO Dar es salaam
Lakini pia unaweza kujiunga na group lets la WhatsApp Kama utakidhi vigezo
kwa mawasiliano zaidi; +255716560094
0 comments:
Post a Comment