14 June 2019

MAFUNZO MAALUM YA UIMBAJI AU SAUTI NA KOCHA JOHN SHABANI

YALIYOMO KATIKA MAFUNZO HAYA
  • PUMZI
  • UTULIVU
  • MKAO WA MWIMBAJI
  • SAUTI
  • AFYA YA SAUTI
  • MAZOEZI
 MWALIMU WA SAUTI 
Naitw John Shabani. Mwimbaji, Mtunzi wa nyimbo na Mwalimu wa sauti.
Nimefanya uchunguzi au utafiti kwa zaidi ya miaka kumi juu ya SautiAfya ya Sauti na
Mazoezi ya sauti. Uchunguzi wangu umenipatia taarifa zilizothibitishwa na madaktari
wa sauti na walimu wa sauti ulimwenguni.

Nimeandaa mafunzo haya kwa lugha ya kiswahili J Vocal Course katika misingi ya taarifa nilizo kusanya, uzoefu wangu katika tasnia hii ya Uimbaji na mafunzo niliopata. Ni imani yangu kuwa kozi hii itakusaidia mwimbaji unayeanza kuimba kwa mara ya kwanza lakini pia kwa wewe uliyekuwa ukiimba kwa muda mrefu.

Kozi hii ingekugharimu zaidi ya laki tano au zaidi kama ungeenda kusoma katika
vyuo au shule za Muziki. Lakini nimeiandaa na kuletea kama mchango wangu ili kukiboresha kipaji chako. Unachokihitaji ni muda wako na juhudi zako pekee. Lakini ukiguswa kuchangia maono au mkakati huu basi usisite kufanya hivyo. Vilevile unaweza kupitia masomo haya kwenye blogu yangu www.johnshabani.blogspot.com, au ukajiunga na group letu la whatsapp lakini pia unaweza kuhudhuria masomo yanayoendelea Dar es salaam kwa waliopo Tanzania.

Kwa maswali zaidi au mchango wowote usisite kunitumia barua pepe
Jshabani2011@gmail.com au Whatsapp: +255716560094.
Ahsante na Karibu.
JINSI YA KUTUMIA
Maelezo na maelekezo yote ya kozi hii yanapatikana katika Makala hii, kwenye blog yangu blogu, darasa langu la mafunzo ya sauti, kwenye page zangu za facebook  na kwenye group langu la whatsapp
inayofahamika kama Swahili Vocal Course 
Vilevile Videos za mazoezi pamoja Audio za ala za muziki kwa ajili ya mazoezi
(Workouts) zinapatikana katika.
Ili upate mafanikio kutoka kwenye kozi hii, Usiwe na haraka ya kumaliza. Kozi hii
italeta mafanikio makubwa endapo kama utakuwa mvulivu na usie kimbilia matokeo
ya haraka. Fuata mfuatilio huu kwa ajili ya mafanikio makubwa;

UTANGULIZI
Kuimba ni nini?
Kuimba ni kitendo cha kutumia sauti kutengeneza ala za muziki kwa maneno. Mfano
mzuri ni kile tunachojifunza darasa awamu ya kwanza yaani Ala za muziki, tunaweza kuzitumia ala za muziki kwa maneno (do-re-mi-fa-so-la-ti-do) na hiyo ndio maana ya Uimbaji. 
Kuimbapia ni kitendo cha kufikisha ujumbe kwenye jamii kwa kutumia maneno na ala za
muziki. Uimbaji ni njia yenye nguvu sana kuleta matokeo katika jamii. Na hii ndio
maana waimbaji hutumia sauti zao kuzungumza kwa niaba ya wanyonge kuleta
mabadiliko katika siasa, dini na kadhalika.

Je naweza kuimba?
Umewahi au unajiuliza swali hili? Jibu ni kwamba mtu yeyote anaeweza kutamka
maneno, na kusikia ala za muziki anaweza kuimba. Kinachohitajika ni mafunzo na
mwongozo sahihi. Ni kweli kwamba kuna waliozaliwa na kipaji cha uimbaji, lakini
kuna waimbaji wengi waliojifunza kuimba na sasa wana mafanikio makubwa katika
tasnia hii. Hivyo haijalishi ni kundi lipi upo, na wewe pia utafanikiwa ukiamua.

Faida za Uimbaji
Zipo faida nyingi sana za kuimba, inategemea na malengo yako ni nini. Kuimba ni
starehe, kufikisha ujumbe kwa jamii, chanzo cha kipato, kupata marafiki lakini pia
Uimbaji huweza kutumika kwa ajili Ibada.

Jitayarishe Kuimba
Jambo la kwanza na la msingi ni Kujenga Mtazamo Mpya. Inawezekana umekatiliwa
kuimba mara nyingi na wengine wamekukatisha tamaa kuwa huwezi kuimba.
Imefikia hatua ukaanza kukiri kwamba huwezi kuimba. Ili ufanikiwe katika kozi hii ni
lazima kwanza ubadilishe mtazamo wako na ujiamini kuwa unaweza kuimba. Iambie
nafsi yako kuwa “NAWEZA KUIMBA”. Mafanikio ya kitu chochote huanza kwenye
fikra na saikolojia zetu. Ni muhimu sana ukaanza na saikolojia yako.


PUMZI KWA AJILI YA WAIMBAJI
Kama ilivyo Injini kwa gari, ndivyo Pumzi kwa uimbaji. Pumzi ya kutosha itawezesha
mwimbaji kuimba mstari mzima pasipo kukwama. Inawezekana umewahi
kuimba na ukashindwa kumaliza mstari katika wimbo kwa sababu ya ufinyu wa
Pumzi. Katika sura hii utajifunza mazoezi ya jinsi ya kupumua wakati wa kuimba na
kujiongeza pumzi ya kutosha. Kabla ya kujifunza sura nyingine ni muhimu sana
kufahamu kuhusiana na pumzi; Msingi wa Uimbaji.

MAZOEZI YA SEHEMU YA KWANZA
Katika kipengele hiki utajifunza jinsi ya kupumua wakati wa kuimba. Waimbaji na
walimu wa sauti wanaposema “Imbia kutoka Tumboni”? Wanachokimaanisha ni
pumzi yako katika uimbaji ianzie tumboni Na hiki ndio kitu cha kwanza
tutakachojifunza katika sura hii

Zoezi 1
Fuata Maelekezo yafuatayo ili kukusaidia kukufahamu jinsi ya kupumua ipasavyo;
 Weka mikono juu yako ya tumbo lako.
 Kisha toa hewa kwa kutumia mdomo wako ukisema (shiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii)-kama vile
unanyamazisha kelele. Unavyotoa hewa, ndivyo ambavyo tumbo linavyoingia
ndani. Hakikisha unatoa hewa yote pasipo ya kukata.
 Kisha ingiza hewa taratibu kwa kutumia pua. Tumbo litajazwa na hewa, hivyo
litaonekana kuwa kubwa.
Ulipokuwa ukifanya hili zoezi umeona unapotoa hewa nje, tumbo linaingia ndani. Na
unapoingiza hewa ndani, tumbo linatoka nje. Rudia Zoezi 1 mara 10.

Zoezi 2
Katika zoezi hili utajifunza jinsi ya kupumua katika Uimbaji wakati wa hali mbalimbali.
Fuata maelekezo yafuatayo;
 Ingiza hewa kwa kutumia pua (mara tano pasipo kutoa hewa). Kisha toa hewa
ukiwa umefunga mdomo. Rudia mara nne.
 Ingiza hewa kwa kutumia pua (mara tano pasipo kutoa hewa). Kisha toa hewa
ukiwa umefungua mdomo. Rudia mara nne.
 Ingiza hewa kwa kutumia pua (mara tano pasipo kutoa hewa). Kisha toa hewa
kwa kuguna. Rudia mara nne.
 Ingiza hewa kwa kutumia pua (mara tano pasipo kutoa hewa). Kisha toa hewa
kwa kusema “Ahhhhhhhhhhhhh”. Rudia mara nne
Zoezi 3
Katika daraja la kwanza, hili ni zoezi la mwisho na katika zoezi hili utajifunza jinsi
kupumua wakati wa Uimbaji. Katika zoezi jitahidi uwe na saa au simu yako
ilikuhesabu sekunde unazotumia wakati ukitoa hewa. Fuata maelekezo yafuatayo;
 Ingiza hewa mpaka ambapo Tumbo litakapo kuwa limejaa hewa ya kutosha.
 Bofya “Anza” kwenye stop watch au simu yako, kisha toa hewa kwa kutumia
“ssssssssssssssssss” pasipo kukwama mpaka utakapofikia mwisho wako.
 Bofya “Simama” pale ambapo pumzi yako imekata.
 Tazama ni sekunde ngapi. Weka katika rekodi yako kwa ajili ya matumizi ya
baadae.
Kwa kawaida kwa mtu anaeanza kufanya zoezi hili kwa mara ya kwanza hufikisha
sekunde 15 – 20. Kama umefika hapo hongera sana, kama hujafanikiwa kufika hapo
pia usiwe na wasiwasi utakapoendelea kufanya mazoezi kwa juhudi utafanikiwa.
Sekunde unazopaswa kufikia ni 40 – 45, Uvumilivu na juhudi vyote vinahitajika.

MAZOEZI YA PUMZI SEHEMU YA PILI
Katika sehemu hii tutakupatia mazoezi kwa ajili ya kujiongezea pumzi ya kutosha
kwa ajili ya Uimbaji. Naamini mpaka sasa utakuwa umepitia sehemu ya kwanza na
kufanya mazoezi yaliyotolewa katika sehemu ya kwanza. Kwa sababu mazoezi
katika sehemu ya kwanza ni msingi katika tunachoenda kujifunza sasa.
Fuata maelekezo yatakayotolewa 
Kumbuka: Kabla ya kufanya mazoezi yafuatayo , hakikisha kwanza
umepasha mwili wako tayari. Unaweza kuupasha mwili wako kwa kukimbia, kuruka
kamba au kuruka ruka. Kisha fanya mazoezi utayapatiwa katika ;
1. Fungua tumbo.
2. Fungua pande za tumbo.
3. Fungua nyuma.

UTULIVU
Be comfort when you are singing, ili kupata matokeo mazuri,  mwili wako, akili yako, hisia zako, mawazo yako vyote vielekezwe kwenye hicho unachokifanya. Jambo linguine tawala sauti unayoimbia (master the sound in singing). Usipende kuimba kikawaida kawaida, shawishi wanaokusikiliza wakukubali. Lakini pia epuka sana kupayuka hata kama unaimba in high. Badala ya kuimba in  head voice be smooth, lainisha sauti.


MKAO WAKATI WA KUIMBA
li kutoa sauti nzuri ni muhimu sana kufahamu jinsi ya kuweka mwili wakati wa
uimbaji. Mwili wako unapokuwa hauko katika mkao mzuri ni vigumu kupumua
ipasavyo na hii inaweza kupelekea sauti yako kupoteza nguvu na uhalisia wake.
Jinsi unavyoweka mwili wako wakati wa kuimba kunaweza kufanya sauti yako kuwa
bora au kupoteza ubora wa sauti. Mkao usio sahihi hufanya upumuaji kuwa mgumu,
sauti kuwa hafifu na minyifu. Kwa upande mwingine, Mkao usio sahihi wakati wa
uimbaji unaweza kukuletea maumivu katika mwili wako na matatizo mengine ya
kiafya.
Katika sura hii utajifunza mkao (posture) sahihi ya kutumia wakati wa uimbaji.
Ili kuwa na mkao sahihi hakikisha vitu vifuatavyo;
1. Usiinue shingo yako juu (Never sing with your Neck up). Wengi tumeambiwa ukitaka sauti yako itoke vizuri wakati wa uimbaji inua shingo. Hapana, kee your neck streit. Kuimba sio kujiumiza au kujilazimisha.
1. Hakikisha kichwa kimetazama mbele.
2. Uti wa mgongo umenyooka.
3. Usiinue Kifua juu sana.
4. Usiinue mabega.
Katika mchoro ufuatao hivyo ndivyo ambavyo mifupa hupangiliwa pale ambapo mtu
hutumia mkao sahihi.


Kama unataka kujiona unavyosimama wakati wa Uimbaji unaweza ukawa unafanya
mazoezi mbele ya kioo ili kujitazama na kufanya marekebisho pale unapotambua
hauko sawa. Hii itakusaidia kujitathmini na baada ya muda fulani kupita utajikuta sio
jambo la kufikiria tena bali unalifanya pasipo hata ya kujitazama.
Hivyo katika mazoezi yako kipaumbele chako kiweke katika kutengeneza
mkao ulio sahihi wakati wa Uimbaji.

SAUTI
Aina za sauti
Ni vizuri kufahamu aina ya sauti yako. Yapo makundi mengi sana ya sauti
ketegemeana na kigezo cha ugawanyishi kilichotumika. Katika kozi hii
tumegawanyisha sauti katika makundi manne ambayo ni Soprano, Mezzo, Tenor na
Bass.
Soprano, ni sauti nyembamba ya juu ya mwanamke. Mezzo ni sauti nzito ya chini ya
mwanamke. Tenor ni sauti ya juu ya Mwanaume na Bass ni sauti ya Chini ya
mwanaume. Uwezo wa kuimba funguo mbalimbali hutokana na aina za sauti
uliyonayo.

Rejista za sauti - vocal register (range of tones in human voice produced by a particular vibratory pattern of the vocal folds)
Zipo rejista tatu za sauti ambazo ni muhimu kufahamu kila moja kivyake vilevile jinsi
ya kuzitumia katika uimbaji. Rejista ya kwanza ni Sauti ya kifuani (Chest Voice),
Sauti ya Utosini (Head Voice) na Sauti Mchanganyiko (Mixed Voice).

Toni ya Sauti
Waimbaji wawili wanaoimba katika ufunguo mmoja wanasikika tofauti – Sababu ni
toni ya sauti. Unaposikiliza redio ni rahisi kufahamu nani ameimba wimbo fulani kwa
kusikiliza toni ya sauti. Toni ya sauti ni muhimu sana kwa sababu hiyo ndiyo
itakutofautisha na waimbaji wengine.
Jinsi ya kutengeneza Toni ya kipekee
Mwenyezi Mungu aliweka upekee katika sauti ya kila mtu. Tatizo ni kwamba wengi
wetu wanajikuta wakiiga sauti za waimbaji wengine na hatimaye kupoteza upekee
wao. Kama utaiga sauti ya mwimbaji mwingine basi utatunyima (mashabiki zako)
ladha ya sauti yako.
Jiamini una sauti ya kipekee, fuata maelekezo tutakayokupatia ili kufungua ule
upekee wa sauti yako katika kiwango cha juu.
Zoezi la toni ya sauti (#1) - Katika zoezi hili utafungua toni ya sauti yako na
baada ya muda utajikuta ukiimba kwa kutumia sauti yako. (Fuata maelekezo
yaliyopo kwa wale  )
Zoezi la toni ya sauti (#2) Resonance – Katika kipengele hiki utaifunza sauti
yako kujaa na kuwa na nguvu. Hata kama huimbi pasipo ya kipaza sauti,
utaweza kujaza chumba kwa sauti yako
AFYA YA SAUTI
atumizi mabaya ya sauti au vitu ambavyo huleta madhara kwenye sauti
inaweza kupoteza ubora wa sauti yako baada ya muda fulani. Kama unaimba
kanisani au kwenye sherehe na matamasha kuzingatia swala la afya ya sauti ni
jambo ambalo si la kukwepa.
Vipo vitu vingi ambavyo si sahihi na watu wanafanya kisha hawaoni madhara yake
kwa wakati huo lakini ndani ya kipindi fulani matokeo hutokea. Ni lazima uwe makini
kwenye vitu unavyofanya kwa maana vinaweza kupelekea kupotea kwa ubora wa
sauti yako katika kipindi kifupi au muda mrefu.
Vifuatavyo ni vitu hatari kwa ajili ya Afya ya sauti yako
Alkoholiki: Hupanua mishipa yako ya damu, hivyo sio nzuri kwenye kodi za
sauti yako.
Moshi wa sigara: Moshi wa sigara hupeleka madhara hasi kwenye koo. Hivyo
jizue kuvuta sigara au kuvuta moshi wa sigara kutoka kwa mtu anaevuta.
Dawa: Dawa nyingi kwa ajili ya kuponyesha magonjwa mbalimbali hukausha
koo. Hii hupelekea koo kuwa kavu jambo ambalo si jema katika uimbaji.
Muulize daktari wako kama kuna uwezekano wa kubadilisha mpangilio wa
unywaji dawa katika kipindi ambacho utakuwa unatumia sauti yako sana.
Kama umekunywa dawa na unahitajika kuimba hakikisha unakunywa maji
mengi ya kutosha.
Vyakula: Baadhi ya vyakula vina matokeo hasi kwenye sauti. Vyakula
vinavyotokana na maziwa (dairy products) sio vizuri kwenye sauti kwa sababu
vinatengeneza mucus kwenye koo lako nah ii itakufanya kusafisha koo lako
kila mara ambayo haishauriwi kwa mwimbaji kufany hivyo. Ni muhimu pia
ukafahamu ni vyakula gani ambavyo vinakuwa na madhara hasi kwenye sauti
yako ili usivitumie wakati unapokuwa na uimbaji wa muda mrefu.
Kusafisha koo: Kama ni tabia yako kusafisha koo lako kila mara, leo ni vyema
ukaacha hiyo tabia. Mara nyingi waimbaji hujikuta wakisafisha makoo yao
kwa sababu ya mucus ambayo imekaa kwenye koo wakijitayarisha kwa ajili
ya uimbaji.
Vifuatavyo ni vitu muhimu kwa ajili ya afya ya sauti yako
Kuna vitu vitatu cha kwanza KUNYWA MAJI, cha pili KUNYWA MAJI na cha
tatu KUNYWA MAJI. Maji ni muhimu sana kwa sauti yako. Hakikisha
unakunywa maji ya kutosha.
Pumua kama muimbaji wakati wote hata ukiwa unazungumza na simu.
Hakikisha unakaa katika mkao mzuri kama ilivyoshauri katika sura ya pili.
Unaweza kutumia sauti yako yote pale unapotaka kusikika lakini hakikisha
hupigi mayowe ni hatari kwa sauti yako.
Hakikisha unapata muda wa kutosha wa kulala. Hakikisha una masaa 6 – 8
ya kulala.

MAZOEZI 
Mwana riadha hukimbia, Wachezaji wa mpira hucheza mpira, na wewe
mwimbaji unachopaswa kufanya ni kimoja KUIMBA. Wachezaji imara na
wanariadha makini hufanya mazoezi yakutosha kila mara. Vilevile kama unataka
kuwa mwimbaji makini lazima ufanye mazoezi ya kutosha kila wakati. Katika sura hii
utajifunza jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya mazoezi, kuchagua mahali pa kufanyia
mazoezi na jinsi ya kufanya mazoezi.
Katika kozi hii tumekupatia mazoezi mbalimbali kama vile mazoezi ya pumzi,
mazoezi ya toni ya sauti na mazoezi ya matayarisho. Fanya mazoezi haya kila siku,
asubuhi, mchana au jioni wakati wowote ambao utafaa kwako.
Fuata maelekezo haya wakati wako wa mazoezi
Kama unataka kufahamu mpangilio mzuri wa mazoezi ambao unaweza kuutumia
wakati wako wa mazoezi, unaweza kutumia mpangilio huu ufuatao:
1. Pasha mwili wako tayari kwa ajili ya mazoezi (Body Warm Up). Ili kufanya
mwili wako tayari kwa ajili ya mazoezi ni muhimu ukaanza kukimbia au kuruka
kamba (kurukaruka).
2. Fanya mazoezi ya pumzi yaliyopendekezwa katika katika kipengele cha pumzi.
3. Fanya matayarisho ya sauti (Vocal Warmup). Unaweza kutumia mazoezi
kabla ya uimbaji au mazoezi ya sauti. (Tazama Video ya matayarisho ya sauti
kwa ajili ya Uimbaji ) – katika blogu ya Swahili Vocal Course.
4. Fanya zoezi la toni ya sauti ulilojifunza kutoka sura ya tatu.
5. Fanya zoezi la kuimarisha rejesta ya utosi na rejesta ya kifua ( kama
ulivyojifunza katika sura ya tatu)
Mazoezi hayo yanaweza kuchukua dakika 20-30 ndani ya siku. Kumbuka mazoezi
hayo ni kwa ajili ya kuimarisha sauti yako, mazoezi ya nyimbo bado ni muhimu sana
kwa ajili ya maandalizi ya uimbaji mbele za watu au kurekodi.
Vitu ambavyo si vya kufanya wakati wa mazoezi;
Usifanye zoezi ambalo hufahamu linasaidia nini katika sauti yako, Usifuate mkumbo.
Hakikisha unafanya zoezi ambalo unafahamu linakusaidia nini katika sauti yako.
Nimekutana na watu wengi wanaodhani mazoezi ya kuimba ni kupiga kelele pekee
ufukweni mwa bahari. HAPANA, ni zaidi na hayo. Usipohamu kwa nini unafanya
zoezi fulani itakuwia vigumu kufahamu maendeleo yako ya sauti.

MENGINEYO
  • Imbia kwenye key yako, utakuwa huru zaidi.
  • Nenda na mapigo ya muziki bila kutoka nje ya ufunguo(key)
  • Angalia mitetemo yako (kama ni wimbo unahusu mitetemo), iwe ya kiasi.
Ushauri
Pamoja na kwamba mazoezi ya kuimba si kupiga kelele pekee ila tunakushauri uwe
na mahali au muda ambao huwezi kusumbua mtu mwingine. Vitu ambavyo
vinaweza kukutoa katika hali ya mazoezi, vitu kama vile simu, TV, Internet na
chochote ambacho kinaweza kuondoa focus yako wakati wa mazoezi .


0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP