HEALTH TIPS - AFYA





DONDO ZA KI-AFYA

MABO 7 MUHIMU KUFANYA UWE NA AFYA BORA
Yafuatayo ni baadhi ya mambo unayoweza kuyafanya ili kuwa na afya bora katika mwaka huu wa 2013.  kabla sijaendelea mbele sana, naomba niweke wazi kwamba afya bora haihusu kula vizuri na mazoezi peke yake bali pia fikra chanya(positive attitude). Kuna umuhimu wa kuhakikisha kwamba siku zote unakuwa na mawazo chanya na pia kuwa karibu zaidi na watu wenye mawazo chanya.
  1. Kunywa Maji kwa wingi-
    Bila shaka unakumbuka msemo “Maji ni Uhai”.Hiyo ni kweli kabisa maji ni uhai sio tu kwa mazingira yetu na dunia kwa ujumla bali pia kwa afya au miili yetu. Maji ni kitu muhimu sana kwa afya zetu. Asilimia 60% ya miili yetu imetengenezwa au imesheheni maji. Maji yanahitajika kwa ajili ya kuondoa takataka au vitu visivyofaa kutoka mwilini, maji ndio hubeba virutubisho na oxygen.
Kiasi cha maji anachohitaji mtu kinategemea na mambo kadhaa kama vile unyevu(humidity) wa mahali ulipo, shughuli zinazohusisha mwili anazozifanya mtu na pia uzito wa mwili. Pamoja na hayo,kwa wastani miili yetu inahitaji lita 2 na nusu mpaka 3 za maji.Vyakula tunavyokula huchangia kama asimilia 20% za maji katika miili yetu. Kwa hiyo tunahitaji kunywa maji kiasi cha lita 2 mpaka lita 2.4 au glasi 8-9 za maji kwa siku.
Njia rahisi ya kujua kama mwili wako una maji ya kutosha ni katika kuangalia mkojo. Mkojo wako unatakiwa kutokuwa na rangi(colorless) au kuwa wa njano kidoogo. Kinyume cha hapo ni ishara kwamba hauna maji ya kutosha mwilini. Njia nyingine kutambua ni pamoja na kukaukwa na midomo(lips) na hata ulimi na pia kupata kiasi kiduchu cha mkojo.
  1. Pata Usingizi wa Kutosha:
    Unakumbuka tulipokuwa wadogo wazazi wetu walisisitiza sana kwamba twende tukalale mapema ili tukue? Bila shaka walikuwa wanajua kwamba usingizi ni sehemu muhimu sana katika afya. Ukiachilia mbali faida za usingizi kwa ajili ya afya za akili/ubongo wetu,usingizi au mapumziko ya kutosha ni muhimu kwa miili.Afya njema huenda sambamba na mapumziko.Ni wakati wa kuupa mwili nafasi ya kujijenga,kujiongezea nguvu na muhimu zaidi kuhakikisha kwamba tunakuwa na akili timamu. Pia ukosefu wa usingizi ni chanzo cha kuzeeka mapema.
  1. Fanya Mazoezi-
    Hili linaweza kupita bila maelezo ya ziada. Mazoezi ni muhimu sana kwa afya bora. Fanya mazoezi angalau mara tatu katika wiki. Jipatie muda wa kutembea japo kwa dakika 30. Kama inawezekana nenda Gym, badala ya kupanda lifti pale kazini kwako au mitaani, tumia ngazi za kawaida.Egesha gari lako mbali kidogo na unapokwenda ili upate nafasi ya kutembea nk. Muhimu zaidi ni kuchagua aina ya mazoezi unayoipendelea. Mazoezi hayatakiwi kuwa adhabu.
Faida za mazoezi ni pamoja na kujiepusha na magonjwa mbalimbali, kupunguza unene(bila shaka unajua kwamba unene kupindukia sio afya bali ni ugonjwa na sababu kubwa ya maradhi mengine)
.
  1. Kula Matunda Kwa Wingi-
    Matunda ni chanzo kizuri sana cha madini na vitamins ambazo miili yetu inahitaji sana kwa ajili ya afya bora. Unajua kwamba machungwa,kwa mfano, yana faida kubwa zaidi kiafya kuliko vidonge vya Vitamin C unavyobugia kila leo? Aina mbalimbali za matunda ambayo yana virutubishi vingi zaidi kiafya ni Parachichi(Avocado), apple, matikiti maji(cantaloupe),Zabibu(Grapefruit), Kiwi,Guava,mapapai, machungwa, strawberries nk.
  1. Kula mboga za majani-
    Kama ilivyo kwa matunda,mboga za majani(vegetables) ni muhimu sana kwa afya zetu. Wataalamu wa afya wanashauri kwamba tule aina 5 mpaka 9 za mboga za majani na matunda.Jitahidi kupata angalau zaidi ya aina 5 za mboga za majani na matunda.

  1. Punguza Kula Vyakula vya Makopo-

    Kutokana na jinsi dunia inavyozidi kwenda mbio,watu wengi huwa tunakosa muda wa kupika.Matokeo yake tunakimbilia kwenye vyakula vya kwenye makopo ambavyo ndivyo vimejaa katika maduka na ma-supermarket. Jitahidi kuviepuka vyakula hivyo kwa kadri unavyoweza.Mara nyingi vyakula vya makopo huwa na ingredients ambazo hazifai kwa afya zetu.Kwa mfano,vingi miongoni mwa vyakula hivyo huwa na chumvi nyingi kitu ambacho ni chanzo cha High Blood Pressure na maradhi ya moyo. Unaposhindwa kabisa kujizuia kununua vyakula hivyo vya makopo jaribu kuangalia ambavyo havina sukari au chumvi.
  1. Jipende- Kama nilivyodokeza hapo mwanzo,afya bora huenda sambamba na afya ya akili/ubongo.Njia mojawapo ya kupata afya hiyo ni pamoja na kujipenda.Pengine unajiuliza,kuna mtu ambaye hajipendi? Ukweli ni kwamba pengine ni kweli kwamba hakuna mtu ambaye hajipendi.Tofauti inakuja pale mtu anapofanya vitu ambavyo ni kinyume kabisa na mapenzi ya mwili.
Mfano, uvutaji sigara, unywaji pombe kupindukia, kutojisafisha mwili wako kwa mfano kuoga, kupiga mswaki na pia kupumzika nk.Hizo zote ni tabia ambazo zinaweza kuonyesha jinsi ambavyo hujipendi au huupendi mwili wako.

FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI KATIKA MAISHA YAKO
JE UNAJUA KILA MARA UFANYAPO MAZOEZI UNAFAIDIKA VYEMA NA AFYA YAKO

ZIFUATAZO NI SIRI ZA MAFANIKIO YA MAZOEZI

1.MAZOEZI HUSAIDIA KATIKA MFUMO WA USAGAJI CHAKULA KUWA MZURI NA UHAKIKA NA KUPELEKA SEHEMU INYOHUSIKA KWA MUDA MUAFAKA.

2.MAZOEZI HUKUFANYA KUJISIKIA NA AFYA NJEMA KUKUPA NGUVU NA KUWEZA KUFANYA KAZI KWA NGUVU ZAKO BILA KUJISKIA UMECHOKA NA MWISHO WA SIKU HUPUNGUZA MAFUTA MWILINI.

3.MAZOEZI HUPUNGUZA UZITO, KUNYOOSHA NA KUIMARISHA MISULI YA MWILI.

4.KUPUNGUZA PRESHA.

5.HUSAIDIA KUPUNGUZA MAFUTA

6. HUONGEZA HDL VIZURI.

7. HUSAIDIA MAPIGO MAZURI YA MOYO KWA KUONGEZA KASI YA MAPIGO YAKE WAKATI WA MAZOEZI.

8. HUONGEZA CHEMBE CHEMBE YEKUNDU KWENYE MZUNGUKO WA DAMU AMBAZO ZINABEBA OKSIJEN KWENYE MAPAFU NA PELEKA SEHEMU NYINGINE ZA MWILI.

9.UNGUZA MRUNDIKO WA DAMU KWENYE MISHIPA, HII NI MUHIMU KWA SABABU MGANDO WA DAMU HUSABABISHA MAGONJWA YA MOYO PAMOJA NA KUPOTEZA FAHAMU.

10.MAZOEZI HUIMARISHA MIFUPA YA MWILI

11.HUSAIDIA KUPANUA MISHIPA YA DAMU INAYOPELEKA KWENYE MOYO

12HUSAIDIA KUFANYA MISULI YA MOYO KUWA MADHUBUTI.

13.HUPUNGUZA KIASI CHA MAFUTA YALIKO KWENYE DAMU.

14.MAZOEZI HUSAIDIA KUPUNGUZA UGONJWA WA KISUKARI.

15.HUBORESHA USINGIZI.

16.HUSAIDIA MMOMONYOKO WA CHAKULA AMBAO HUSAIDIA KUPUNGUZA MAGONJWA YA KANSA.

17.MAZOEZI HUSAIDIA KUIMARISHA SEHEMU ZA VIUNGO VYA MWILI.

18.MAZOEZI HUSAIDIA MAAMBUKIZO YA INDOMETRIOSIS KWA ASILIMIA 50% KWA WANAWAKE.

19.MAZOEZI HUONGEZA KIASI CHA DAMU AMBACHO HUSAMBAA NA KUIFANYA NGOZI KUONEKANA YENYE AFYA ZAIDI

20.MAZOEZI HUKUFAYA UJISIKIE MCHANGAMFU NA AFYA.

MAZOEZI NI DAWA

Katika ripoti kuhusu faida za mazoezi, mtandao wa ''exercise is medicine''(mazoezi ni dawa) ulioanzia nchini marekani, umetoa ushahidi wa kitafiti kwamba, mazoezi yakifanyika mara kwa mara na katika kiwango kinachotakiwa:

1. Hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo kwa asilimia 40
2. Huzuia kupata kiharusi(stroke) kwa asilimia 27
3. Huzuia kupata kisukari kwa zaidi ya asilimia 50
4. Huzuia kupata shinikizo la damu(hypertension) kwa asilimia 50
5. Huweza kuzuia kufa kutokana na saratani, au kuzuia kujirudia kwa saratani ya matiti kwa asilimia 50
6. Hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya utumbo mpana(colob cancer) kwa zaidi ya asilimia 60.
7. Hupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa kusahau kwa asilimia 33.
8. Hutibu msongo wa mawazo(depression) kwa kiwango sawa na dawa za kutibu ugonjwa huu.

Mazoezi Kabla Kifungua Kinywa Hupunguza Mafuta Mwilini

Written by  KHAMIS
 Daktari mmoja aitwaye Mackod, alipitia makala nyingi za afya ili kuweza  kutambua visababishi vya vifo ambayo havitokani na umri au nasaba ya kiasili (genetic), na akagundua mambo tisa ambayo yanasabisha vifo ambavyo vingeweza kuzuilika. Mambo hayo tisa ni; uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe, ukosefu wa mazoezi, lishe duni, wadudu kama bakteria na virusi, ajali, tabia za ngono za kupita kiasi bila kinga,  vita na madawa ya kulevya.
Katika makala hii ningependa kuzungumzia juu ya ufanyaji wa wazoezi na hasa wakati bora wa kufanya mazoezi. Mazoezi ni muhimu sana kwa ajili ya kupunguza mafuta ya ziada mwilini, tafiti zinaonesha kuwa asiyefanya mazoezi, madhara anayopata ni sawa na mtu anayevuta tumbaku.
Utafiti uliofanywa na Dr. Jason na Nor Farah (2004) wa Chuo kikuu cha Glasgow, umeonesha kuwa unapofanya mazoezi kabla ya kifungua kinywa, wakati tumbo likiwa tupu, ni bora zaidi kuliko unapoweza kufanya mazoezi baada ya mlo wowote. Kufanya mazoezi ni jambo la maana kwa afya kuliko kutokufanya mazoezi ya mwili, lakini unaweza kupata  faida zaidi kama unaweza kufanya kabla hujala chochote.
Mazoezi kwa ujumla wake yana umuhimu mkubwa kwa afya ya binadamu, hasa kama yakiambatana na lishe bora. Mazoezi huweza kuzuia magonjwa sugu kama kisukari, magonjwa ya moyo, kansa na shinikizo la damu, pia kwa kufanya mazoezi unaweza kuongeza kipato kwa kuwa unaweza kufanya kazi muda mrefu kuliko asiye fanya mazoezi. Familia ambazo hufanya mazoezi huwa na afya bora na kipato kikubwa kwa kuwa fedha kidogo wanazopata hutumika kwenye maendeleo ambapo familia wasiofanya mazoezi, hujikuta wakitumia kipato hicho kidogo kwa ajili ya magonjwa ambayo yangeepukika kwa kufanya mazoezi.
Pia kwa kufanya mazoezi kila mara na hasa kabla ya mlo kuna faida nyingi ambazo haziwezi kuonekana kwa haraka, kama vile kuimarisha hali ya kiakili, ambayo matokeo yake ni kuwa na furaha. Hii inatokana na kuzalishwa kwa wingi kwa kemikali aina ya endorphins wakati wa kufanya mazoezi. Kemikali hii ya  endorphins  ni muhimu kwenye mapambano ya sonono (depression) na hivyo kumfanya mfanya mazoezi kuwa na furaha zaidi. Tafiti zinaonesha kuwa mwili huzalisha kemikali hii ya endorphins baada ya mtu kufanya mazoezi ya kawaida kwa dakika 12. Kama wanafamilia wanaweza kufanya mazoezi kwa muda hata wa saa moja, au nusu saa, wanaweza kuwa na furaha na kuzuia kusambaratika kwa ndoa zao.
Pia kuna kemikali nyingine muhimu ambayo tafiti zinaonesha kuwa huzalishwa baada ya kufanya mazoezi. Kemikali hii itwayo “serotonin” huongezeka kwenye mfumo wa neva baada ya kufanya mazoezi, ambayo hufanya mfanya mazoezi ajisikie vizuri kiafya na kupunguza sonono (depression). Tafiti pia zinaonesha kuwa kemikali hii, ni muhimu sana katika mwili, kwani hufanya mfanya mazoezi alale usingizi mnono.
Ufanyaji wa mazoezi mara kwa mara husaidia pia mfanya mazoezi ajithamini, na kuondoa uchovu na unyonge. Unapojithamini, pia inaleta tokeo ya kujiona bora na kuwa mwenye ustawi. Mazoezi pia hufanya tendo la ndoa kuwa bora na hivyo kuleta mahusiano bora ya kinyumba na mpwendwa wako.
Nimejaribu kuanisha umuhimu na faida za maozezi  na hasa wakati  yanapokuwa na tija ili kuleta hamasa ya kufanya mazoezi kwa kila msomaji wa makala hii. Unaweza kufanya mazoezi wewe na familia yako au na wenzako, au pekee yako, chukua muda kidogo katika masaa 24 na ufanye mazoezi, maana utajisikia vizuri na kuwa mwenye afya, lakini kumbuka utapata faida zaidi ukifanya mazoezi wakati tumbo likiwa tupu, yaani kabla ya mlo, baada ya kula chakula tembea taratibu ili kukifanya kitulie vema tumboni.
 Usisahau, kabla ya kifungua kinywa asubuhi jitahidi ufanye mazoezi angalau kwa muda wa robo saa.

 Na: ZAWADI ALLY NKULIKWA,
NI MTAFITI NA MWANASOSHOLOJIA WA AFYA NA MAGONJWA
CHUO KIKUU CHA ST. JOHN’S CHA TANZANIA, DODOMA

AINA MBILI YA VYAKULA HUTAKIWI KUVILA BAADA YA MAZOEZI

KAMA wewe ni miongoni mwa watu wenye utaratibu wa kufanya mazoezi ya mwili kila siku au mara kwa mara unahitaji kusoma makala haya kwa makini, kwani yanahusu suala muhimu ambalo pengine hukuwahi kulijua kabla.
Inaeleweka na kukubalika na tafiti zote kuwa mazoezi ya mwili ni miongoni mwa vitu muhimu kiafya kufanywa na mtu baada ya kuzingatia lishe. Imeelezwa pia kwamba mazoezi yanachukua asilimia 20 ya ustawi wa afya ya mtu, hii ina maana kwamba hata kama utakula vyakula sahihi, kama hufanyi mazoezi, ubora wa afya yako utakuwa haujakamilika kwa asilimia 20.
Aidha, unajua kwamba chakula chochote unachokula mara baada ya kufanya mazoezi ndani ya muda wa masaa 2, una athari kubwa katika faida unazoweza kuzipata kutokana na mazoezi unayoyafanya? Elewa kwamba unachokula muda huo kinaweza kuijenga au kuibomoa afya yako, licha ya mazoezi unayoyafanya.

SUKARI
Kuna aina mbili ya vyakula au vitu ambavyo hutakiwi kuvila mara baada ya kumaliza kufanya mazoezi, moja ya vyakula hivyo ni sukari tunayoitumia kwenye matumizi yetu ya kila siku katika vinywaji na vyakula tunavyokula majumbani.
Imeeleezwa kuwa utumiaji wa sukari ndani ya muda wa masaa mawili mara baada ya kumaliza kufanya mazoezi, huvuruga mfumo wa homoni za ukuaji wa mwili na mfumo wa urekebishaji wa kiwango cha sukari mwilini, ambacho kinaweza kusababisha ugonjwa wa kisukari.
Utafiti wa hivi karibuni wa jarida la Applied Physiology la nchini Marekani umegundua kwamba badala ya kula sukari au vyakula na vinywaji vyenye sukari, inashauriwa kula vyakula vyenye kiwango kidogo cha wanga ambavyo huepusha magonjwa ya kisukari (Type2) na magonjwa mengine ya moyo. Vyakula hivyo ni pamoja na viazi, mkate, muhogo, karanga au korosho n.k.
http://i.telegraph.co.uk/multimedia/archive/01807/bread_1807973b.jpg





FRUCTOSE
‘Fructose’ ni jamii ya sukari ambayo hutumika zaidi kwenye vinywaji kama juisi na vinywaji vingine vya baridi, zikiwemo soda. Aina zote za vinywaji vyenye sukari aina hii vinapotumiwa muda mfupi baada ya mazoezi, navyo huharibu mfumo wa homoni za ukuaji wa mwili na husababisha ugonjwa wa kisukari.
Mbali ya kupata athari hizo kama zilivyotajwa hapo juu, vilevile utakosa faida za mazoezi za kupunguza mafuta mwilini, badala yake utajikuta unafanya mazoezi ya mwili, badala ya kupungua ukajikuta unaongezeka uzito au unabaki na uzito huohuo kila siku.
Suala la kujiepusha na unywaji wa vinywaji vyenye sukari nyingi ni muhimu sana iwapo unafanya mazoezi kwa minajili ya kupunguza mafuta mwilini na kupunguza uzito. Vinywaji hivyo ni pamoja na vile vinavyojulikana kwa majina ya ‘Energy Drink’ ambavyo mara nyingi huwa na sukari nyingi.
Mwisho, jitahidi kunywa maji ya kutosha mara baada ya kupumzika, hasa kama mazoezi unayoyafanya yanasababisha kutokwa na jasho jingi ambalo hutoka ili kuondoa sumu lakini hupunguza maji mwilini.


DIET NYINGINE RAHISI YA KUPUNGUZA MWILI NA TUMBO LA CHINI KWA WANAWAKE....Inaenda kwa mwezi mmoja" Ukipenda kufuatilia tuanze wote leo"
Kuna njia nyingi sana ambazo watu huwa wanajaribu ili kupunguza mwili na tumbo lakini either zinakuwa ngumu sana au zinakuwa haziendani na mazingira wanamoishi hivyo kupelekea kushindwa njiani.

Zipo njia za kutumia madawa kama kahawa na vinginevyo ambazo huwa si za kudumu.
Kwakuwa kahawa huwezi kutumia zaidi ya round 3 kwa maana hiyo ukinenepa tena inabidi utafute njia nyingine.

Lakini njia hii ifuatayo unaweza kuifanya ikawa ni maisha yako ya kila siku ikazoeleka na ukawa unaishi hivyo hivyo bila kuongezeka mwili.
Mara nyingi vyakula tunavyokula na vinywaji tunavyokunywa ndio vinatuponza

Sasa, je! Unaweza kujaribu kuishi hivi bila ku cheat hii process???

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi8dMyd0PuXde0MhyphenhyphenrzelhaRWIrOqugNbYlZOV1sOugh3KKfI9_Fuor5UzClH5IoNQaOJCyMjUUydplmqKA7ej6gbUf40lVlEQewAeUdnejpk2E6-BAIuXxzZV4xdjW6qZRDQG7c4kC7eo/s400/walking+exersice.jpgSiku ya kwanza, ukiamka tu kitandani ukapata nguvu kabla ya kufanya chochote jivalie raba zako na nguo za mazoezi. Jaribu kutembea dakika 15 toka nyumba unayoishi na dakika 15 kurudi nyumba unayoishi hapo jumla utakuwa umetembea kwa miguu kwa dakika 30.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjm7iavwaK6tvAY-kGVubHq8m_RC2bM_78oqzrGMEspD_sjjiU1x8EntfNSJvdA6-q_osir1r4OilYkIIGbhyphenhyphenGM4fSnvYCycJ4FdoJt13agSjcPqOz2cXwAZndUNpyrpVDjjfUItsgNZiE/s400/Sit+up+bench.gif
Na kama mkakati wako ni kupunguza Tumbo pia, Ukirudi fanya sit-ups 15 -20 kwa siku ya kwanza. Ukiona ni ngumu unaweza kujaribu kuanza hata na 10. Utaongeza kadri siku zinavyoenda na kadri utakavyokuwa unazoea maumivu ya nyama za mbavu.

Unaweza kutumia Bench au unaweza kulala sakafuni
Kwa wanaoishi Dar es Salaama ma bench ya Sit ups yanapatikana Shopperz Plaza kwenye duka la vifaa vya michezo

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiIEv84GF0J0O6HjXRJnJH25YtwGmdA9Y7UZ6zFQkGwSy01L6Sp36h6RdIjDOG1JKO6clcmO7oKHnoCnZQ-r3GVI5JVqcAxl02zG8xhx4YXnoBQi9dQ3BZYD3G-DPn9L1H_nBNYp_23dts/s400/Glass+of+Water.jpgUkimaliza kutembea na kufanya sit-ups kunywa maji ya uvuguvugu glass 4
Sio lazima uyanywe yote kwa wakati mmoja
Unaweza kuwa unakunywa huku unaendelea na mambo mengine mpaka glass 4 ziishe
Ili kuongezea ladha unaweza kukamulia ndimu au limao katika maji hayo ya uvuguvugu

Limao na ndimu sio tu huongeza ladha bali pia vinasaidia kupunguza mafuta mwilini

Baada ya hapo unaruhusiwa kwenda kuoga, na kujiweka sawa ila usipige mswaki
Nitakwambia kwa nini!!
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiQxkeTpFMgiSdML_KVuMjS3sxFTC7n8yWJYBmVXue55iuTxFcErE2fwIsrWtTDJ0npw2nXiVPGVsWSRFvlS0SiKuHCfDAwaWc8UnGuQDRqdRmdNtHBN7xuEa1OvN7ROE57XuV5_yzXxtI/s400/coffee+cup.jpgKunywa breakfast yako:
Unaruhusiwa kunywa kikombe 1 cha kahawa au Chai lakini usiweke zaidi ya kijiko 1 cha sukari
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgLPaGNfJRawsG2Tak15FGQ5820QenIrFvlD9wUUUDg-AiAVNPBWviPh1ghnmt4Xu4H6fmqmZqd5KWyV0X-Ndh-nZeioMU4EAQcnmS1vOcuXsDxYJlUABr8v8H3ZDvTWlr_ft6Q0xvAJcU/s400/boiled+eggs.jpgUnaruhusiwa kula yai 1 tu la kuchemsha
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgapNW2DDwOnmm1QDPcjMdG6ZWzCACMfZztxVhsJCN7yr1NG4d9J0LNtHaQBTWHRZ2Ob-1b1Pffep87FH9dw3k4UTZ9khHCuT2ajwngyQrjSwvryR7WruodEmmd9NYI_f283UHD91N_T9E/s400/brown-bread.jpgMikate hii ya brown mimi siipendi na wala haina ladha nzuri lakini utafanyaje maadam unataka lako la kuepuka unene yabidi ule tu.

Slice 1 tu ya brown bread tena iwe toasted, usithubutu kuweka Siagi wala vinavyofanana na hivyo
Matunda jimiminie kadri uwezavyo, epukana na ndizi tamu
Baada ya hapo unaweza kupiga mswaki sasa na kuendelea na shughuli zako
Ila kabla ya kuendelea na shughuli zako ni lazima utaenda haja kubwa
Ndio lengo hasa la kutopiga mswaki kabla ya breakfast

Lunch:
Kula upande wa kuku Robo, 1/4 my friend kama ni upande wa paja ndio uliochagua
Kuku unaetakiwa kula ni lazima awe wa kuchoma au kuchemsha na si vinginevyo

Ukitaka upande wa kipapatio ndio utakao kuwa umeuchagua pia.
Unaruhusiwa kusindikizia na kachumbari/ au hata Salady zenu za kizungu za mahotelini
Kama ukiona hujashiba kunywa maji.
Bold
Kumbuka lengo sio kushiba bali kupunguza mwili.
Baada ya hapo ni lazima unywe tena maji ya uvugu vugu glass 4

Epukana kabisa na maswala ya juice zenye sukari nyingi
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiGjkGP1u9SD8yo0mbu8-HVhuyxNgh4I4wZPXoQNs8IWPwd6SsWhkGFTIvJWG6M30af4bhPvG_UHf7xwqEz_ar1uEeQe0TPMZnYsZYEfCR39MkQcMTQY-Fmr8nVNQP1QCILXVGpXdFjuAg/s400/Sit-ups+2.gifMida ya jioni jua likishazama baada ya kazi ukirudi nyumbani, au kama utakuwa umebeba nguo za mazoezi kwenda nazo kazini. Unaweza ukatembea tena kwa nusu saa
Halafu ukamalizia na sit ups ukingoja Dinner

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj-2Xafod0Iv8zfPt0xb6Gg1kV17tD-N2mfAO0vOmMpIlC7EiSoDUGMlU8Y1JuyQda2uRSryqHIs95w0jhyphenhyphenwG49_cEN6rppbaIOlv3JabBXVKVbhI4xatzO6cPUei3ws-16oYm8Mo2GhXs/s400/Red+snapper+soup.jpgUkishaoga jioni.
Huu ndio uwe mlo wako wa kufunga siku "Supu ya Samaki"
Samaki wa aina yoyote tu ile weka bakuli kubwa la kutosha.
Ila pia, hakikisha supu hiyo ni chuku chuku na haina mafuta wala viazi hata kidogo

Njia 5 za kupunguza tumbo kirahisi


WADADA au WAMAWAKE wengi wanatamani kuwa na matumbo madogo, lakini wengi hushindwa kufikia ndoto hiyo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za uzazi na kupenda chakula. Makala hii inaangalia njia rahisi ya kupunguza tumbo.

1. Uangalifu katika kula
Epuka chakula chenye wanga, mafuta mengi na sukari. Badala yake unaweza kula matunda na mboga za majani. Vile vile samaki wa baharini si wabaya kwani hawana mafuta mengi.

2. Namna ya kula
Usiache kula kwani jambo hilo litakunyima nguvu, unatakiwa kula milo mitatu mpaka minne lakini kwa kiasi kidogo. Unatakiwa kukaa zaidi ya saa tatu kabla ya kula mlo mwingine.

3. Mazoezi ya kawaida
Si lazima ufanye mazoezi makali kwa ajili ya kupunguza tumbo. Unaweza kufanya zoezi la kutembea badala ya kupanda basi, kama hufiki mbali sana. Kama unaweza kuogelea, unaweza kufanya hivyo mara kwa mara, hiyo pia itakusaidia.

4. Zoezi maalum
Kama unaweza kufanya zoezi la kulala chali na kukaa, 'abs exercise' unaweza kufanya kwa dakika chache kila siku. Hiyo itasaidia kukomaza misuli ya tumbo hivyo tumbo kutokulegea.

5. Kunywa maji
Maji yanasaidia mmeng'enyo wa chakula, hilo husaidia mtu kuwa na afya njema. Kwa kuwa mtu akiwa katika hatua za awali za kupunguza tumbo husikia njaa mara kwa mara, ni bora anywe maji badala ya kula.
AINA YA MAZOEZI YA KUONDOA TUMBO (KITAMBI)
Mara nyingi sana katika maisha watu wengi hupata tatizo la kuwa na tumbo kubwa na baadae humletea madhara. Ili kuepuka tatizo hili ni kuamua kufanya mazoezi  kupunguza  ya mafuta katika chakula na kufanya mazoezi ya tumbo hii ndio njia pekee hakuna njia mbadala.

                                                           
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhmUgyD1pxGmawy16HUKA66yv1ZIfNdnNmiJO2W6g953RRHJz3VbS58NKWGJUHSL521riq-CFUJofDMWnRviQnRWmdWzp5Cx0pzy108XQp0lKyzWwoJOegPm9ZSVHPOjoQhr2Mqxx-ZWiw/s320/Copy+of+IMG_0539.jpg
                                        Zoezi hili ni kufanya kwa kutumia mashine(abs board)




https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjpO6qoQvZr0eq0KpDlcV5kJP5Fb-8hyvkJmZ43UI0rxdWp-f_Wz6X1iN5hw17owgR0wZsU9kQEgc9TTw_-PUVXYsRIPwFi0eOQnoE6yOvR2oqHZAyJZdMy5QQ4dsiFScesfLfPSJWyygc/s320/DSCN0504.jpg
Hapo ni zoezi ambalo utumia mpira maalum. uanzapo;

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiTjm8qCp0fMxjxn6dX3LuM4TOvMsfx-Vx8IB24PPAdz-bBXURaAPLO5EjJv4YjLBg2VGMnbwovfCrn0rUy1hMgKq_z1ndzztNq8j3xDrMDrSErSPqLjW3MtRb41LwEp0jAiajf1UiMo9g/s320/DSCN0505.jpg
                                            Zoezi  la mpira maalum umaliziapo kwa kunyaua juu.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj0MkjQlFTFmFDpYFFsfNWamNjhuJHczI1oKJ-3tpT-euC5FduQPgIA2EEYc2xUKD9OWxHKqE_Gf1nM8XYVH2ZsSRbwE_XF-_mNBfodcEN3Ddcsp-oSv_77pnt8D9xtJcK6umnn295NRvo/s320/DSCN0500.jpg
                                         Hapa ni mazoezi ya tumbo kwa kutumia mpira maalum

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg6wfK23O8lzBOLbzbvMHt1zj_DB24CN7aXMaxZcjIGVUabKhYJkyjOPpLycHLd5QPDPk6secIk-5fIayCUGOTUjp-MaKOm0c7nnhYm5Uz1CaehlzP1vAdPg41rGVN8ogQ_4mrQqME8e6U/s320/IMG_0545.jpg
                                          Kwa kutumia bench la zoezi la tumbo unavyoanza
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi0Uufm4o-9mG1sIZbwXi4O09EsEUJj0i3hVUiebnYJszSafAKdHMwYf2Xeit3fWxRY5lfQysPM4DoOK604recM_bLbWYnM-rWcu7BCbU91R3SVIIPEAodwVd4BzpB5v9aTZv-gYaKuqTY/s320/IMG_0544.jpg
                                          Namna unvyomalizia  zoezi kwa kunyanyuka.



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh8xl8xJaFkSJmoSGmYpZrjcoVVnM4OUbX6mguNaW-mLRJVYt5Kqx4smLEvphsrZgraXJyQrLioQqqkCZVAl4_kIsYwmHA09Owl35MKbeUwdmvmZjHpYYupRSt6ghG5MotTOLLzIZD75cM/s320/IMG_0548.jpg
                                          Zoezi la tumbo kwa kutumia hypic chair unavyoanza.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEitXn6SGieLROZXlyN09uaogi_0I7Fed60HHqzMy911kczY4og9mR7RVqqGp83IV8Upxw5kWQntWBLVUnUHU0rq9sptpsvjAlSr8aNM4aJCJHPrhpAS6Mijg0TzQSDdPDJPTLlszt9YhZM/s320/IMG_0549.jpg
                                         Zoezi la tumbo unavyomalizia kwa kutumia hypic chair


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg7jW9zvR_cO0xybl-VX8PfFF-lWTIZtByziVksFClhHs4q5nEZFrsIgLPc5pGhtBlgR78N4p6MY3r8EVo1jx24GHyiPhVWgDSsAYlTzm7oRwe32myw9zzBy-dsqo9Ouf1gdstbAACkN78/s320/DSCN0502.jpg
                                         Zoezi la aina nyingine kwa kutumia mpira wa zoezi hilo

Health Benefits of Watermelon

# Watermelons are an excellent source of several vitamins: vitamin A, which helps maintain eye health and is an antioxidant. vitamin C, which helps strengthen immunity, heal wounds, prevent cell damage, promote healthy teeth and gums and vitamin B6, which helps brain function and helps convert protein to energy.

# Watermelon has the highest concentrations of lycopene of any fresh fruit or vegetable. lycopene a powerful antioxidant that helps fight heart disease and several types of cancer — prostate cancer in particular.

# A great source of potassium, which helps muscle and nerve function, helps maintain the body’s proper electrolyte and acid-base balance, and helps lower the risk of high blood pressure.

BANANA -A very interesting FACTS

This is interesting. After reading this, you'll never look at a banana in the same way again.

Bananas contain three natural sugars - sucrose, fructose and glucose combined with fiber. A banana gives an instant, sustained and substantial boost of energy.

Research has proven that just two bananas provide enough energy for a strenuous 90-minute workout. No wonder the banana is the number one fruit with the world's leading athletes.

But energy isn't the only way a banana can help us keep fit. It can also help overcome or prevent a substantial number of illnesses and conditions, making it a must to add to our daily diet.

DEPRESSION:
According to a recent survey undertaken by MIND amongst people suffering from depression, many felt much better after eating a banana. This is because bananas contain tryptophan, a type of protein that the body converts into serotonin, known to make you relax, improve your mood and generally make you feel happier.

PMS:
Forget the pills - eat a banana. The vitamin B6 it contains regulates blood glucose levels, which can affect your mood.

ANEMIA:
High in iron, bananas can stimulate the production of hemoglobin in the blood and so helps in cases of anemia.

BLOOD PRESSURE:
This unique tropical fruit is extremely high in potassium yet low in salt, making it perfect to beat blood pressure So much so, the US Food and Drug Administration has just allowed the banana industry to make official claims for the fruit's ability to reduce the risk of blood pressure and stroke.

BRAIN POWER:
200 students at a Twickenham (Middlesex) school ( England ) were helped through their exams this year by eating bananas at breakfast, break, and lunch in a bid to boost their brain power. Research has shown that the potassium-packed fruit can assist learning by making pupils more alert.

CONSTIPATION:
High in fiber, including bananas in the diet can help restore normal bowel action, helping to overcome the problem without resorting to laxatives.

HANGOVERS:
One of the quickest ways of curing a hangover is to make a banana milkshake, sweetened with honey. The banana calms the stomach and, with the help of the honey, builds up depleted blood sugar levels, while the milk soothes and re-hydrates your system.

HEARTBURN:
Bananas have a natural antacid effect in the body, so if you suffer from heartburn, try eating a banana for soothing relief.

MORNING SICKNESS:
Snacking on bananas between meals helps to keep blood sugar levels up and avoid morning sickness.

MOSQUITO BITES:
Before reaching for the insect bite cream, try rubbing the affected area with the inside of a banana skin. Many people find it amazingly successful at reducing swelling and irritation.

NERVES:
Bananas are high in B vitamins that help calm the nervous system..

Overweight and at work? Studies at the Institute of Psychology in Austria found pressure at work leads to gorging on comfort food like chocolate and chips. Looking at 5,000 hospital patients, researchers found the most obese were more likely to be in high-pressure jobs. The report concluded that, to avoid panic-induced food cravings, we need to control our blood sugar levels by snacking on high carbohydrate foods every two hours to keep levels steady.

ULCERS:
The banana is used as the dietary food against intestinal disorders because of its soft texture and smoothness. It is the only raw fruit that can be eaten without distress in over-chronicler cases. It also neutralizes over-acidity and reduces irritation by coating the lining of the stomach.

TEMPERATURE CONTROL:
Many other cultures see bananas as a 'cooling' fruit that can lower both the physical and emotional temperature of expectant mothers. In Thailand , for example, pregnant women eat bananas to ensure their baby is born with a cool temperature.

So, a banana really is a natural remedy for many ills. When you compare it to an apple, it has FOUR TIMES the protein, TWICE the carbohydrate, THREE TIMES the phosphorus, five times the vitamin A and iron, and twice the other vitamins and minerals.. It is also rich in potassium and is one of the best value foods around So maybe its time to change that well-known phrase so that we say, 'A BANANA a day keeps the doctor away!'

PS: Bananas must be the reason monkeys are so happy all the time!


WANAWAKE WANAVYO-SHAMBULIWA NA U.T.I




U.T.I kirefu chake ni Urinary Tract Infection ni maambukizi ya bakteria mbalimbali wanaoshambulia  mfumo wa mkojo, yaani kwenye figo (kidney), kibofu cha mkojo na mifereji inayotoa mkojo (urethra)
Mifereji inayotoa mkojo kwenye figo (ureter) na mfereji unaotoa mkojo nje, mara nyingi bakteria hushambulia sehemu za chini za mfumo wa mkojo yaani urinary bladder na kitaalamu kuitwa bladder infection.
Bakteria hao baada ya kumuingia binadamu hupona mara moja  pindi mgonjwa anapoanza dozi lakini kama wadudu hawa hawatatibiwa vizuri wanaweza kupanda na kushambulia figo na mshipa unaounga sehemu hiyo uitwao renal pelvis na kuleta madhara makubwa, hivyo kusababisha ugonjwa wa figo.

Kuna wadudu wanaotoka kwenye utumbo mkubwa wa binadamu ambao kila binadamu anaishi nao, hawa husaidia kulinda mwili na kitaalamu hujulikana kama  normal flora na huwa ni askari wa mwili.
Vijidudu hivyo hushuka hadi kwenye mlango wa  haja kubwa na kuenea mpaka sehemu za siri. Kama wataingia kwenye mfumo wa mkojo hushambulia sehemu hizo kwani wadudu  hao wanakuwa hawajazoea mazingira ya sehemu za mkojo.
WANAWAKE WANAVYOSHAMBULIWA NA UTI
Mara nyingi wanawake  ndiyo wanaoshambuliwa kirahisi na bakteria wa UTI  kutokana na maumbile yao ya sehemu za siri.
Sababu kubwa ya kushambuliwa kirahisi ni kwa kuwa wanakuwa na mfereji mfupi wa kutoa nje mkojo (shot urethra).
Sababu nyingine inayosababisha UTI ni kutokumywa maji kwa wingi, hivyo kushindwa kwenda haja ndogo mara kwa mara, ikumbukwe kwenda haja ndogo mara kwa mara husaidia wadudu kutokustahimili kukaa kwenye mfereji
Kama mtu ana ugonjwa wa mawe kwenye figo (kidney stone) pia kwa wanaume  wenye ugonjwa wa kuvimba tezi la manii (enlarged prostate), wana uwezekano wa kukumbwa na maradhi haya.

 

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP