30 December 2012
Naibu Waziri Wa Habari Akutana Viongozi na Wadau Wa Muziki na Filamu Nchini
11:22
No comments
Kwa mara
nyingine tena kimefanyika kikao kikubwa kati ya wadau na viongozi mbalimbali wa
muziki na filamu na Mheshimiwa Makala (Naibu waziri wa habari, vijana,
utamaduni na michezo)
Kikao hicho
kimefanyika katika ukumbi mdogo uliopo
gorofa ya tisa katika ofisi za wizara hiyo. Lengo la kikao hicho ni wasanii
kufahamishwa jinsi serikali ilivyojipanga kuwasaidia wasanii wa Tanzania, ili
wanufahike na kazi zao na kuwajengea heshima zaidi.
Katika kikao
hicho chama cha muziki wa Injili Kimewakilishwa na Addo November, John Shabani, Bahati Bukuku,
Upendo Kilahiro, Cosmas Chidumule, George Mpella na Stella Joel.
Mwimbaji
wa nyimbo za Injili Bahati Bukuku, akizungumza wakati wa Mkutano na Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makalla, jijini Dar es
Msanii JB
akizungumza wakati wa Mkutano huo leo jijini, Dar es Salaam
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amos Makalla akiwa na baadhi ya
wasanii
Naibu
Waziri, Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla akizungumza na
wasanii alipokutana nao katika Ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo
29 December 2012
VIONGOZI WA CHAMUITA WAMTEMBELEA MZEE MAKASY
06:37
No comments
Viongozi wa Chama
chamuziki wa injili Tanzania wakiongozwa na Mchungaji Cosmas
Chidumule, wamemtembelea mzee Makasy ili kumjulia hali pamoja na
kumkabidhi mchango kwa ajili ya matibabu. Mwimbaji huyo mkongwa na
mshauri wa chama cha muziki wa injili Chamuita
Tanzania, amekuwa akisumbuliwa na tatizo la macho. Viongozi
waliomtembelea Mzee makasy ni: Addo
November Mwasongwe, John shabani, Stella Joel pamoja na Mzee
cosmas Chidumule. Endapo utaguswa kumchangia chochote mzee makasy,
wasiliana na viongozi wa chama cha muzili wa injili. Mungu akubariki
27 December 2012
NEW YEAR MESSAGE TO MY FRIENDS
10:50
1 comment
Let
the next twelve months be the most amazing days that one can have, May you achieve all
your aspirations,
May this year shower
upon you the choicest blessings that you could ever hope for, May the New Year
dispel any clouds of gloom from your life. May you have a stress free, May you
have a year that is filled with love, laughter, brightness and hope, May the
New Year bring with it all things beautiful and lovely. Have a blessed New
Year.
26 December 2012
PADRI wa Kanisa Katoliki Mjini Zanzibar amepigwa risasi
22:58
No comments
PADRI Ambrose Mkenda wa
Kanisa Katoliki, Mjini Zanzibar amepigwa risasi na watu wasiojulikana nje ya
nyumba yake juzi saa 1:45 jioni wakati akitokea kanisani.
Hili ni tukio la kwanza
katika historia ya Zanzibar kwa kiongozi wa kanisa kushambuliwa wakati wa
Krismasi, lakini ni tukio la pili kwa kiongozi wa dini kushambuliwa mwaka huu.
Hivi karibuni, Katibu wa
Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga alimwagiwa tindikali iliyomjeruhi
vibaya usoni na kifuani na watu wasiojulikana. Shambulio hilo lilimlazimu
kiongozi huyo kwenda kutibiwa India ambako ameambiwa anapaswa kuripoti
hospitalini kila baada ya miezi sita.
Habari
zilizopatikana jana zimeeleza kuwa Mkenda ambaye ni Paroko wa Parokia ya
Mpendae, alipigwa risasi begani na shingoni na afya yake si nzuri.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Aziz Juma Mohammed alisema jana kuwa majeraha hayo yamemsababishia kutokwa na damu nyingi.
Alisema baada ya shambulio hilo, Padri Mkenda alipelekwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, Zanzibar. Hata hivyo, padri huyo alisafirishwa kwa ndege jana hadi Dar es Salaam ambako amelazwa katika chumba cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU), katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kamanda Aziz alisema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, lakini akabainisha kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa alipigwa risasi baada ya watu hao kumshuku kuwa alikuwa na fedha za sadaka.
“Father Mkenda kitaaluma ni mhasibu na amekuwa akishika makusanyo ya fedha pale kanisani. Sasa huenda wahalifu hao waliona amechukua fedha na ndipo walipomfuata na kumpiga. Lakini hata hivyo, huo bado ni uchunguzi wa awali tu,” alisema Kamanda Aziz na kuongeza:
“Waliofanya tukio hili wamelifanya kwa madhumuni gani, ni swali gumu kujua sasa. Inawezekana kuna mambo mengine zaidi ya watu hao kutafuta fedha. Uchunguzi ukimalizika tutajua cha kufanya.”
Kamanda Aziz alisema walipata taarifa za tukio hilo saa 2:00 usiku na polisi walikwenda katika eneo hilo la Francis Maria anakoishi Padri Mkenda.
“Tulipofika tukakuta maganda mawili ya risasi za bastola na upande wa kulia wa kioo cha gari yake (padri) kuna damu katika viti vyake,” alisema Kamanda Aziz.
Alisema baadaye padri huyo alipelekwa hospitalini kwa ajili matibabu ambako madaktari walifanikiwa kumtoa mabaki ya risasi mwilini kabla ya jana kupelekwa Muhimbili.
“Tumempokea padri huyo saa 4:20 asubuhi leo (jana). Tulianza kumchunguza afya yake, baadaye kumfanyia uchunguzi kisha kumchukua kipimo cha CT Scan ili kubaini ilipo risasi hiyo,” alisema, mkurugenzi wa zamu katika hospitali hiyo, Agnes Mtawa.
Source: Mwananchi

21 December 2012
HATMAYE ALBUM YA DEBORA SHABANI IKO TAYARI
05:22
No comments
Kwa wale wapenzi wa nyimbo za Debora Shabani, sasa album hiyo ijulikanoayo kwa jina la Amesikia kilio chako iko tayari kwa mfumo wa Audio huku tukiendelea na mchakato wa kutengeneza video. Unaweza ukaipata kwa bei ya jumla na rejareja. Mungu akubariki.
20 December 2012
KONGAMANO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI l LATIKISA DAR ES SALAAM, PIA CHAMUITA WAIOMBA SERIKALI KUWABANA MAHARAMIA WA KAZI ZA MUZIKI
11:20
No comments
Waimbaji mbalimbali na wadau wa muziki wa injili ndani ya ukumbi wa wanyama hotel sinza
Mchungaji Abel
Kongamano kubwa la waimbaji wa Muziki wa
Injili lililo andaliwa na chama cha Muziki wa Injili Tanzania "CHAMUITA" limefanyika likiwa na lengo la kutambulisha
viongozi wapya wa chama cha muziki wa Injili Tanzania pamoja na kutaja malengo
ya chama.
Katika kongamano hilo CHAMA cha
Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA), kimeiomba serikali kuhakikisha inasimamia
vema kazi zao ili zisihujumiwe, na wao waweze kupata faida kupitia kazi hizo za
Mungu.
Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa
semina ya kutoa elimu kwa wadau mbalimbali juu ya kazi zao jijini Dar es Salaam
jana, Rais wa chama hicho, Addo Mwasongwe Mwl John Shabani, Bahati bukuku
pamoja na waimbaji mbali mbali kwa nyakati tofauti, wametoa ombi hilo kutokana
na serikali kuwa na mamlaka makubwa hapa nchini ya kulisimamia suala hilo.
“Serikali ina uwezo mkubwa wa
kuhakikisha sisi wasanii tunanufaika na kazi zetu, kwa kuwa wao wakianza
kuwakamata ambao wanatuhujumu na kuwachukulia hatua, nina imani mambo haya
yataisha na sisi tutazidi kujivunia kazi zetu ambazo zinaleta ajira hapa
nchini,” alisema Mwasongwe.
Aidha, Mwasongwe alisema
wanachukizwa na kitendo cha Wakristo kufanya wizi wa kazi za Mungu, wakati kila
Jumapili huenda kwenye ibada na kumtukuza.
“Tunasikitishwa sana kwa kuwa
miongoni mwa wezi wa kazi zetu na Wakristo nao wamo, inauma sana, mtu anakwenda
kwa wale ‘wanaobani’ CD na kumuomba nichanganyie nyimbo ya Bukuku, Mkone na
wengine, wakati yeye kama Mkristo anatakiwa kuwa mstari wa mbele kuacha kufanya
hivyo. Hivyo basi tuna imani serikali itatusaidia,” aliongeza.
Katika hatua nyingine, CHAMUITA
kiliwatambulisha viongozi wapya ambao ni Addo Mwasongwe (Mwenyekiti), Mchungaji
Joseph Malumbu (Makamu Mwenyekiti), David Mwamsojo (Katibu), Stella Joel
(Katibu Msaidizi), John Shabani (Naibu Mwenezi), na Upendo Kilahiro (Mweka
Hazina), huku wajumbe wa Kamati Kuu wakiwa zaidi ya 60, wakiongozwa na Mbunge
Martha Mlata, Christina Shusho na Bahati Bukuku.pamoja
mh. Martha mlata (Mbunge wa singida viti maalum CCM na Mr Alex Msama ambao ni
walezi wa chama hicho.
Miongoni mwa madhumuni ya semina hiyo ni kulinda
utamaduni wa Tanzania na heshima ya muziki huo, kuhamasisha maendeleo ya muziki
huo na nyanja zake nyingine, kuwa na chombo cha kuwezesha mawasiliano kati ya
watu na vikundi katika kupeana taarifa mbalimbali na mengine mengi ambapo
iliudhuriwa na wanamuziki wengi wa injili hapa nchini.
Lulyalya
Sayi Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki akieleza umuhimu wa mfuko wa LAPF
Abubakari Ndwaka Meneja Mafao wa LAPF.
Katika kongamano hilo liliudhuriwa na viongozi wa mfuko wa pensheni wa LAPF ambao ndio waliokuwa wadhamini wakuu wa kungamano hilo. Mfuko huu ulizungumzia umuhimu kwa waimbaji wa muziki wa injili kujiunga nao kama sehemu mojawapo ya wao kuwekeza katika maisha ya baadae, pia kutoa fursa kwao kujipatia mikopo ya nyumba na kuwekeza katika akiba yao ya baadae.
Pia
kampuni ya Grace products ltd inayojihusisha na kutengeneza mafuta ya ngozi, shampoo,
sabuni na bidhaa mbalimbali zisizokuwa na kemikali, walikuwepo katika kongamano
hilo wakiwaelimisha waimbaji na watumishi wa Mungu kutumia bidhaa nzuri
kwaajili ya kulinda miili yao. Pia afisa kutoka TRA alifafanua jinsi serikali
ilivyojipanga kuwasaidia wasanii nchini. Kongamano hilo limehudhuriwa pia na
wachungaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi akiwemo Nabii Machibya kutoka
wingereza.
Subscribe to:
Posts (Atom)