29 January 2013
NAMSHUKURU MUNGU KWA KUMALIZA MASOMO YANGU KATIKA CHUO CHA KIMATAIFA CHA HUDUMA (INTERNATINAL SCHOOL OF MINISTRY)
12:54
No comments
Baadhi ya waalimu wa chuo cha ISOM
Baadhi ya wanafunzi huko Singapore
Baadhi ya wanafunzi huko Marekani
Kwa neema ya Mungu nimemaliza masomo
yangu kwa ngazi ya diploma katika chuo cha kimataifa cha huduma, Graduation ni
mwezi tatu mwishoni, nitakapo kualika usisite kuhudhuria. Endelea pia kuniombea
kwa ajili ya kuendelea na degree yangu.
Nawewe unayetaka kujiunga na chuo
hiki, tayari wamefungua tawi hapa Dar es salaam, bado hujachelewa. Kwa habari
kuhusu ISOM (International School of Ministry) tembelea
24 January 2013
14 January 2013
MTANGAZAJI MAHIRI WA TOP RADIO MOROGORO BI LEVINA STEVEN KUJA KIVINGINE KATIKA MUZIKI WA INJILI, AMSHIRIKISHA MWL JOHN SHABANI
12:52
No comments
John Shabani akiwa na Bi Levina Steven
Mwana dada Levina Steven anayetangaza Top Radio, amekua
gumzo kwa watanzania baada ya kuachia ngoma kadhaa za nyimbo za injili. Chini ya usimamizi wa Mwl John Shabani,
Nyimbo zake zinaonekana kufanya vizuri sana. Kabla ya kuhamia morogoro,
mtangazaji huyo machachari alikuwa akifanya kazi katika kituo cha Praise Power
radio cha jijini Dar es salaam.
Endelea kumuombea.
Endelea kumuombea.
13 January 2013
MIRACLES WITH BISHOP MABOYA
10:20
No comments
Sunday 13 jan the lady with bishop
maboya crying was healed in the sunday service from a n operation done in
september and had alot of pain and purse was coming out was healed instantly
and started crying with joy"
12 January 2013
UJUMBE WA January 2013 na John Shabani
11:55
No comments
Mfumo wa maisha ya mwanadamu huwa kama unavyoziona picha
hizi;
Kuna wakati wa kuonekana umefifia(upo kama haupo),
wakati wa mchoro wako wa kimaisha kuanza kuonekana kwa mbali, wakati wa
kuonekana katika rangi nyingine, wakati wa rangi yako ya ki uchumi au kiroho
n.k kuanza kuonekana kwa mbali, wakati
wa wewe kung’aa katika rangi yako na baadaye kuchanua.
Picha hizo zinaashiria changamoto mbalimbaliza kimaisha,
yawe ya kiroho, kia-afya na ki-uchumi. Katika kila changamoto, usiogope,
usikiate tamaa bali zione changamoto kama daraja la kuvukia upande wa pili wa
mafanikio yako. Kuna wakati wa kudharauliwa, kuchekwa, kushushwa chini na kuachwa/kutengwa.
Lakini wakati wa kung’aa kwako na baadaye kuchanua utafika tu!
MARUFUKU KUKATA TAMAA
Subscribe to:
Posts (Atom)