29 July 2013
MAZOEZI YA KUSIFU NA KUABUDU CHINI YA MWALIMU JOHN SHABANI NA WAALIMU WENGINE KWA AJILI YA MAANDALIZI YA MKUTANO WA MWINJILISTI BONNKE YAENDELEA VIZURI
10:47
No comments
Zaidi ya waimbaji 500 kutoka makanisa mbalimbali, wakimsikiliza mwalimu John shabani, alipokuwa akielekeza kuhusu sifa na mbinu za kuwa mwimbaji bora
Mratibu
wa mikutano ya Bonnke barani Afrika, Mwinjilisti Pascal Ado kutoka Togo,
akipongeza mazoezi pamoja na kuongea na waimbaji wanaoendelea kuhudhuria
mazoezi hayo
Je wewe ni mwimbaji, kwaya au kikundi, mnakaribishwa
kuungana waimbaji wengine kwa ajili ya maandalizi ya mkutano mkubwa wa injili
utakaohubiriwa na muhubiri wa kimataifa Dr. Rehinard Bonnke
Ni jumamosi hii, pale magomeni mikumi, katika kanisa la T.A.G.
Bado tuhitaji waimbaji, ili kukamilisha idadi ya watu 5000
22 July 2013
UZINDUZI WA KIKUNDI CHA KUSIFU NA KUABUDU KATIKA MKUTANO WA MWINJILISTI BONNKE WAFANYIKA DAR, KARIBU WAIMBAJI 500 WAJISAJILI.
22:00
No comments
Zaidi ya waimbaji 500 ktoka kwaya, vikundi na waimbaji binafsi wakiimba kwa pamoja katika uzinduzi wa kuandaa kikundi cha sifa, kitakachotumika kwenye mkutano wa mwinjilisti Bonnke
Mratibu wa mikutano ya Bonnke barani Afrika, Mwinjilisti Pascal Ado kutoka Togo, akiongea na waimbaji
Mwalimu John Shabani, akisimamia zoezi hilo
Akiongea na mamia ya
waimbaji na wanamuziki, mratibu wa mikutano ya Bonnke barani Afrika, Mwinjilisti Pascal Ado kutoka
Togo, amesifia sana uimbaji wa Tanzania na kuwaasa waimbaji kufanya huduma hiyo
kwa moyo wote. Amesema mkutano huo utatazamwa katika nchi mbalimbali duniani, hivyo unadhifu
na uchangamfu unahitajika sana. Pamoja na hayo, amependekeza aina ya nyimbo zinazohitajika na kujiandaa
kuwa na sare ya aina ya mavazi ya ki-Afrika
Mratibu wa mikutano ya Bonnke barani Afrika, Mwinjilisti Pascal Ado kutoka Togo, akiongea na waimbaji
Mwalimu John Shabani, akisimamia zoezi hilo
Waimbaji 5000
wanahitajika ili kukamilisha kikundi cha kusifu na kuabudu, kitakachoongoza
sifa katika mkutano wa Bonnke, unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 21 mwezi ujao.
JE WEWE NI MWIMBAJI BINAFSI, KWAYA AU KIKUNDI, UNAKARIBISHWA
KUUNGANA NA WAIMBAJI WENGINE KWA AJILI YA KUANDAA TIMU HIYO
Ni jumamosi hii, pale magomeni mikumi, katika kanisa la T.A.G.
Bado tuhitaji waimbaji.
18 July 2013
MCHUNGAJI DK. GETRUDE RWAKATARE AONGOZA MAOMBI YA KUWEKA WAKFU ALBAM YA MWIMBAJI EMMANUEL MGOGO
06:15
No comments
Ile album ijulikanayo kwa jina la “Msikilize Mungu” ya kwake
Emmanuel Mgogo, imewekwa wakfu katika
kanisa la Mikocheni B’ Assemblies of God. Album hiyo iliyorekodiwa katika
studio ya Eck Production, imekuwa gumzo
na hasa ule wimbo wa Msikilize Mungu.
Kabla mwimbaji huyo hajaanza kuimba jumapili hii,
aliweza kuzileta Cd kadhaa madhabahuni, ndipo Mchungaji kiongozi wa Mlima wa
moto pamoja na jopo la watumishi walipoziinua na kuziweka nyimbo hizo wakfu kwa
maombi, ili Mungu amtumie zaidi kijana huyo.
Endelea kunyenyekea, ili Mungu akuinue zaidi.
13 July 2013
NIMEGUSWA SANA NA HABARI HII YA WAIMBAJI WA INJILI AFRIKA YA KUSINI WALIPOKUSANYIKA NJE YA HOSPITALI ALIYOLAZWA MANDELA
05:41
No comments
Solly na
Deborah katikati wakiimba na wenzao nje ya hospitali kumtakia afya njema mzee
Mandela
Kundi la waimbaji muziki wa injili nchini Afrika ya kusini jumatano wiki hii walikusanyika nje ya hospitali ya Medi-clinic Heart alikolazwa baba wa taifa hilo mzee Nelson Mandela jijini Pretoria akipatiwa matibabu ya ugonjwa ambapo walikuwa wamebeba maua kumtakia afya njema.
Kundi hilo la wanamuziki wapatao 10 wakiongozwa na mchungaji Solly Mahlangu na mwanamama Debora Frazer na waimbaji wengineo walikaririwa wakisema kuwa, kama waimbaji muziki wa injili nchini humo walifika hospitalini hapo kuonyesha upendo wao na heshima kwa Rais huyo mstaafu ambaye wanasema bado wanamuhitaji, ambapo walitumia muda nje ya hospitali hiyo wakiimba pamoja na kufanya maombi kwa kiongozi huyo mstaafu.
Aidha mwimbaji anayeitwa Zanele Mbokazi amesema wao hawana fedha wala dhahabu lakini wanalo jina la Yesu ambalo ndio wanalolitoa kwa mzee Madiba na familia yake.Kwa upande wake Deborah amelitaka taifa hilo kuendelea na maombi juu ya mzee Madiba kwakuwa nchi hiyo na dunia kwa ujumla bado wanamuhitaji mzee Madiba "Ni baba wa kwetu sote, Mungu ampe maisha marefu zaidi duniani", amesema Deborah
Ni siku ya 35 tangu mzee Madiba kupelekwa hospitalini hapo kwa matibabu kutokana na maradhi ya mapafu yanayomfanya kushindwa kupumua vyema. Huku mzozo ambao ulikuwa umeigubika familia yake kuhusiana na masuala ya maziko yameonekana kumalizwa kama wajukuu wa mzee huyo walivyonukuliwa na vyombo vya habari wakijibu maswali ya watu waliokuwa wakiwauliza maswali kwenye mtandao wa twitter.
10 July 2013
MAELFU YA WATU WAENDELEA KUFUNGULIWA KATIKA SEMINA INAYOENDELEA KATIKA KANISA LA MIKOCHENI B’ ASSEMBLIES OF GOD - MLIMA WA MOTO
06:27
No comments
Mwimbaji wa kimataifa, Sarah K, akimtukuza Mungu akitika siku ya ufunguzi wa semina
Mchungaji Getrude Rwakatare akiombea watu
Mnenaji wa semina, Askofu Mrisa
Sehemu ya umati wa watu wanaoendelea kuhudhuria smina hiyo
Mchungaji Msaidizi, Noah Lukumai akifungua kwa maombi
Papag Mphella akiweka mambo sawa
Mwinjilisti Stanley akimtukuza Bwana
Ni siku nane za kukupeleka kwenye hatma yako. Haijawahi kutokea, moto wa Roho Mtakatifu, unateketeza kila roho chafu, kila mikosi na balaa na kila kifungo. Mnenaji katika semina hiyo ni Muhubiri wa kimataifa, Askofu Mrisa akishirikiana na mwenyeji wake Dk Getrudw Rwakatare
Ni siku nane za kukupeleka kwenye hatma yako. Haijawahi kutokea, moto wa Roho Mtakatifu, unateketeza kila roho chafu, kila mikosi na balaa na kila kifungo. Mnenaji katika semina hiyo ni Muhubiri wa kimataifa, Askofu Mrisa akishirikiana na mwenyeji wake Dk Getrudw Rwakatare
Panga kuhudhuria semina hiyo.
Kwa mawasiliano zaidi:
0715524441
Subscribe to:
Posts (Atom)