24 March 2014
KADI ZA ZA CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI ZIMEBORESHWA ZAIDI, SASA ZINAPATIKANA
22:15
No comments
Ewe mwimbaji binafsi, mwana kwaya, mwana band, mwana muziki na mdau wa nyimbo za muziki, jiunge sasa na chama chako cha muziki wa Injili Tanzania, jipatie kadi yako ya uanachama.
15 March 2014
LIGHTNES BAYO, MAMA ALIYEJITOLEA KUWAKOMBOA MABINTI WANAOZALISHWA KATIKA UMRI MDOGO NA KUTELEKEZWA
05:16
No comments
Kwa wakaaji wa karatu na
vitongoji vyake, jina la Lightness Bayo si ngeni masikioni mwao, kwani ni mwana
mama alieamua kuyatumia maisha yake katika kuwasaidia mabinti waliozalishwa na
kutelekezwa, mabinti hao ni wale hasa wenye umri mdogo. Pamoja na mabinti pia
mama huyo amekuwa akiwasaidia watu wenye uhitaji mbalimbali wakiwemo wajane na
yatima. Ili kuweza kuwasaidia watu hao Bi Lightness akisaidiana na wafadhili
mbalimbali, amejenga kituo cha ufundi “Lake Eyasi Girls Vocation
Training Center”,katika kijiji cha Mang,ola wilaya ya karatu.
Kituo hicho kimeweza kuinua
kipata cha mabinti waliokuwa hawajiwezi na wengine kutaka kujiua. Moja ya mambo
yanayofanyika katika kituo hocho ni kujifunza ushonaji na ufumaji. Pia mama
huyo ameweza kuwasaidia jamii ya wamang’ati kwa kuwaanzishia mrati wa kufuga
mbuzi na nyuki wa asali. Pamoja na kituo hicho, pia anacho kituo cha kulea
watoto yatima.
Hata hivyo shule anayoiongoza yeye na mume wake katika mji wa karatu Tumaini Junior School, ni miongoni mwa shule zinazofanya vizuri nchini.
Inawezekana wewe ni Binti,
umezalishwa na kutelekezwa, au unaye binti wa aina hiyo, au ungependa kuwa
rafiki wa maono haya ya Bi Lightness, kwa kumuombea, kumtia moyo au kuchangia
chochote, basi usisite kuwasiliana naye kwa simu namba 0754317394
John Shabani katika kijiji cha Mang'ola huko karatu
John akiimba na kikundi cha wamang'ati
11 March 2014
JOHN SHABANI’S TOUR-TO VISIT HADZABE TRIBE (BUSHMAN)
14:48
No comments
Small groups of Hadzabe bushmen live around Lake Eyasi.
Their language resembles the click languages of other bushmen further south in
the Kalahari. Their small population was seriously threatened, in particular
during the period when Julius Nyere tried to introduce his Ujuma policy. The
tribe resisted the forcible settlement policies of Julius Nyere and nowadays
most of their children have never seen a doctor or school - the bush provides
for all their needs and is a class room for their offspring.
They are often willing for visitors to come and see their
simple bush homes where the tree canopy alone or a cave provides them with
shelter. They live entirely off the bush and from hunting, generally small
antelopes and baboons, although in rainy seasons gazelles and antelopes come
down from the Ngorongoro or Serengeti to their then lush bush lands offering
them richer pickings. In the recent past their hunting activities were resented
by trophy hunters who tried to stop their "illegal" hunting.
The string on their lethal bows is made from giraffe tendons and the arrows are coated with a strong poison made from another tree. The commiphora tree povides excellent firewood which they kindle by rubbing wood, a green commiphora provides a mosquito-repelling sap, juice squeezed out of the sansaveria provides a cure for snake bites while aloe is used to heal cuts. Roots provide a wide range of medicines and the mighty baobab fruits as a source of drink. A few hours spent with the bushmen makes the apparently unhospitable bush country come to life and to watch them hunt a unique experience as they stealthily spot then creep up on their prey skillfully killing it.
They Need your help!
3 March 2014
ALINE VYUKA, MWANA DADA MWENYE NDOTO ZA KUFIKA MBALI, AENDELEA KUFANYA VIZURI HUKO USA
15:27
No comments
Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Burundi na muigizaji wa filamu anayeishi huko Marekani, DUKUDE VYUKUSENGE aka ALINE VYUKA aendelea kujizolea sifa kwa kuvitumia vipaji alivyopewa na mwenyezi Mungu.
Akiongea na mwalimu John Shabani (Katibu mkuu wa chama cha muziki wa injili Tanzania), Aline amesema kuwa, anajua kule Mungu aliko mtoa, hivyo ana maono ya kwenda mbali zaidi ki huduma, kielimu na kijamii.
Akiongea na mwalimu John Shabani (Katibu mkuu wa chama cha muziki wa injili Tanzania), Aline amesema kuwa, anajua kule Mungu aliko mtoa, hivyo ana maono ya kwenda mbali zaidi ki huduma, kielimu na kijamii.
Aline Vyuka ambae alianza kuimba kwenye
kwaya akiwa na umri wa miaka 7, miwili
iliyopita aliweka hewani album yake 'Vyukusenge Vol 1' na baada ya hapo aliweka akaja na album yake ya pili 'Dukunde
Vol2' Nyimbo ambazo zimempa chati sana. Lakini hata hivyo Aline hajaridhika na
kiwango chake cha uimbaji, anatamani kufanya vizuri zaidi, hivyo basi katika
kuboresha huduma yake ya uimbaji, mwanadada huyo amekuwa akifanya kila awezalo
ili kuwa mwimbaji bora. Moja ya waalimu wa nyimbo za injili walioamua kusimama
na Aline ni mwalimu John Shabani . Mungu akipenda mwaka huu mwana dada huyo
anatarajia kutembelea nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Tanzania na kurekodi nyimbo
zake mpya.
Pia Mwana dada huyo anajiusisha na mpango mzima wakuigiza filamu. Mwaka 2010 filamu yake
'Family issues' iliwekwa hewani na ikamletea sifa kemu kemu kwa upande wawapenzi
wa filamu. Mwaka wa 2013 ali iweka wakfu filamu yake ya pili 'ORPHANS'. Ukizingatia
kuwa dada huyo ana mpango kabambe wa kuwasaidia watoto yatima na mabinti
waliozalishwa majumbani.Pamoja na ugumu kidogo wa kipato lakini kwa maombi yako na ushauri wako na hata pia mchango wako, vitamsaidia kufika mbali. Aline analo kundi linalo igiza filamu zake na yeye ndio
kiongozi wahilo kundi,linajulikana kama 'BAHOWOOD' akitambulika ka Director na
Muandishi (Story writer) kwenye filamu zote ambazo zilishatoka.
Mwsho Aline ametujulisha kuwa :" Ninaandaa
filamu itakayojulikana kama INTERPRET "
Endelea kumwombea!
Akirekodi mkanda wa video
Akiwa na rafiki yake baada ya ibada huko mareakani
Ndani ya studio
Subscribe to:
Posts (Atom)