30 July 2014
HATIMAYE ALINE VYUKA ATUA DAR
14:25
No comments
Hapa ni shilo studio, sehemu ya kupata kifungua kinywa na msosi
Hapa kazi imeanza ndani ya shilo studio
Ashukuriwe Mungu wetu kwa kumfikisha Aline
Vyuka salama hapa Bongo. Najivunia kuwa na mwanafunzi mwenye bidii kama
huyu. Tumekuwa tukifanya masomo ya uimbaji (Singing lessons) kwa njia ya
mtandao na sasa nimempokea rasmi Dar es salaam baada ya safari ndefu
kutoka huko kwao kwa Mr. Obama. Tayari kazi rasmi ya kuandaa nyimbo kwa mfumo wa audio na video imeanza.
28 July 2014
HONGERA FURAHA ISAYA
21:42
No comments
Furaha isaya akiimba kwa hisia katika tamasha aliloliandaa mwenyewe, ndani ya ukumbi wa Urafiki Social Hall - Dar es salaam
Furaha Isaya sambamba na mwalimu John Shabani wakishusha uwepo
Hii ni timu nzima iliyomsaidia furaha kuimba live.
Hongera Furaha Isaya kwa kuthubutu kufanya tamasha la live, pia kunishirikisha mimi kama mwalimu wako kikamilifu. Najua zipo changamoto nyingi pamoja na gharama, jambo ambalo hata waimbaji wengi, na wengine wenye uwezo kidogo, hawajawahi hata kuthubutu.
Katika Dunia ya sasa, suala la kutumia mtindo wa mshindo nyuma (play back) sio kabisa!... Nivizuri hata kujifunza kwa watu wengine. Wewe umejitaidi, na ninaamini utafika mbali usipozimia moyo. Songa mbele mwanafunzi wangu ninayejivunia. Gharama uliotumia ni mbegu kwa ajili ya mafanikio yako makubwa.
Hongera Furaha Isaya kwa kuthubutu kufanya tamasha la live, pia kunishirikisha mimi kama mwalimu wako kikamilifu. Najua zipo changamoto nyingi pamoja na gharama, jambo ambalo hata waimbaji wengi, na wengine wenye uwezo kidogo, hawajawahi hata kuthubutu.
Katika Dunia ya sasa, suala la kutumia mtindo wa mshindo nyuma (play back) sio kabisa!... Nivizuri hata kujifunza kwa watu wengine. Wewe umejitaidi, na ninaamini utafika mbali usipozimia moyo. Songa mbele mwanafunzi wangu ninayejivunia. Gharama uliotumia ni mbegu kwa ajili ya mafanikio yako makubwa.
26 July 2014
CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI CHASABABISHA DAR ES SALAAM- JANUARY MAKAMBA AONGOZA MKUTANO WA WANAMUZI WA MUZIKI WA INJILI NA WASAMBAZAJI NA TAASISI MBALIMBALI ZINAZOHUSIKA NA MUZIKI TANZANIA
15:55
No comments
Katika kikao hicho Mh. Januari Makamba aliweza kutoa hutuba ndefu yenye ufasaha kwa wanamuziki wa Injili Tanzania. Hotuba yake ilikuwa na matumaini kwa wanamuziki na iliweza kuwafurahisha sana wanamuziki hawa hasa pale alipoweza kutoa ahadi zake za kukisaidia Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania ikiwemo kuwaahidi kuchangia katika kufanikisha zoezi la kuwa na Channel ya TV ya waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, kuwa na studio ya kisasa itakayomilikiwa na chama cha muziki Tanzania, kufikia suala la kupata eneo la kuendeshea shughuli zao n.k. Aliomba sana wanamuziki kuwa na nguvu za bidii za kuweza kufanikisha yale yote yanayowazunguka na wasibweteke wakisubiria, na pia wanamuziki wa injili wanategemewa kuwa kioo na mfano wa kuigwa, hivyo wawe na nidhamu na uchaji wa Mungu na kujiepusha na skendo, maana nyimbo za injili zinapendwa na kila mtu hata wapagani na wale wa dini zingine. Pia ameahidi kutekeleza ahadi zake haraka iwezekanavyo
Wadau wa muziki wa Injili wakiwa kwenye mkutano huo.
Katibu wa Shirikisho la Muziki wa Injili John Shaban
akiendesha mkutano.
Kiongozi wa mtandao wa wanamuziki Tanzania, mzee John Kitime
George Mpella akiwakilisha vyombo vya habari vya kiristo
Kutoka TRA
Ofisa Mtendaji Mkuu wa COSOTA, Doreen Sinare (kulia), akitoa
ufafanuzi wa masuala mbalimba kwa wadau wa muziki wa Injili. Wa pli kulia ni
Muimbaji wa nyimbo za Injili, Christina Shusho.
Watu mbali mbali wakiuliza maswali
Rais wa Shirikisho la Muziki wa Injili Tanzania (TAF), Ado
Novemba (kushoto), akizungumza na wadau wa Muziki wa Injili Tanzania
Hoteli ya Wanyama Sinza Dar es Salaam kabla ya kumakribisha mgeni rasmi wa
mkutanmo huo, Mhe. January Makamba.
Balozi mstaafu, Profesa Coster Mahalu akizungumza na wadau
wa muziki wa nyimbo za Injili. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Kinondoni Revival
Choir, Dk. Jotham Mackenzie
Wadau wa muziki wakiwa kwenye mkutano huo wakifuatiliamambo
mbalimbali.
Wadau wa muziki wakiwa kwenye mkutano huo.
Wawakilishi wa ATN (Agape Television Network)
Kiongozi CHAMUITA kutoka Morogoro akikabidhi MIC
baada ya kujitambulisha
Muwakilishi kutoka ATN akijitambulisha
John Shabani akihakikisha kila kitu kinakaa sawa
Wadau wa eneo la usambazaji wa kazi za wanamuziki
wakiwa kwenye mkutano huo
Mwanahabari wa Kituo cha TV 1, Gervas Mwaitebela naye
alikuwepo kupata taarifa za mkutano huo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Mhe.
January Makamba (kulia), akizungumza na wadau wa Muziki wa Injili Tanaznia
Hoteli ya Wanyama Sinza Dar es Salaam leo.
22 July 2014
PAMOJA NA KEBEI NA KUZOMEWA MCHUNGAJI STELLA AENDELEA KUHUBIRI INJILI
23:17
No comments
Mchungaji Stella Mahiga akiendelea kuchapa injili maeneo ya k/koo
Huku akiendelea kuhubiri, huku akizomewa na kundi la watu
Mhubiri wa Injili ambaye ni mama
aliyejitambulisha kwa jina la Stella Mahiga amejikuta akipata wakati mgumu
alipokuwa anahubiri majira ya jioni katika kituo cha kupandia daladala
kilichopo Kariakoo jijini Dares salaam.
Aidha, mhubiri huyo aliyekuwa anahubiri kuhusu wokovu amejikuta akizomewa na watu aliokuwa akiwahubiria injili katika eneo hilo. Asilimia kubwa ya watu walikuwa katika hilo walikuwa ni wa dini nyingine.
Mpaka mwandishi wetu anaondoka katika eneo hilo aliacha wananchi wakiwa wanamzomea mhubiri huyo kwa maneno ya kejeli. Kwa ujumla hajapata ushirikiano hata kidogo kutoka eneo hilo, lakini Neno litaendelea kuhubiriwa.
Aidha, mhubiri huyo aliyekuwa anahubiri kuhusu wokovu amejikuta akizomewa na watu aliokuwa akiwahubiria injili katika eneo hilo. Asilimia kubwa ya watu walikuwa katika hilo walikuwa ni wa dini nyingine.
Mpaka mwandishi wetu anaondoka katika eneo hilo aliacha wananchi wakiwa wanamzomea mhubiri huyo kwa maneno ya kejeli. Kwa ujumla hajapata ushirikiano hata kidogo kutoka eneo hilo, lakini Neno litaendelea kuhubiriwa.
18 July 2014
VIONGOZI WA CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI TANZANIA KANDA YA KASKAZINI WAFANYA VIKAO KWA MAENDELEO YA CHAMA
11:07
No comments
CHAMUITA ni Chama cha Muziki wa Injili Tanzania ambacho kinasimamia haki za
mwanamuziki wa Injili Tanzania nzima. Chama hiki chenye malengo mazuri ya
kuhakikisha mwanamuziki hatokwi na machozi kwa kuonewa kupata kile
alichotarajia kukipata kutokana na jasho lake la kumtumikia Mungu kwa njia ya
muziki.
Mwanachama wa chama hiki ni yule tu aliyejiunga na chama hiki cha CHAMUITA na kupata kitambulisho halali kutoka kwa viongozi wa Chamuita.
CHAMUITA Imegawanyika katika kanda mbalimbali kama vile Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Mashariki na Pwana, Kanda ya kusini. Na kila kanda kuna uongozi ulioteuliwa na viongozi kutoka makao makuu ambayo yako jijini Dar es Salaam. Wanachama kutoka kanda hizo wana haki ya kujadilki yale yanowahusu wakishirikiana na uongozi wa juu kutoka makao makuu ya CHAMUITA.
Leo hii tunataka kukuletea baadhi ya picha za viongozi wa kanda ya kaskazini wa CHAMUITA waliofaya vikao vyao vya kanda kwa lengo la kulinda haki za mwanamuziki na mambo mengi yanayowahusu katika kanda yao.
Kikao hiki kilifanyika katika ukumbi wa Kimalia kikiwa na lengo la kuwafikia wanamuziki wa kada mbalimbali katika mikoa minne ya kanda ya kaskazini yaani Tanga, Arusha na Manyara, kupanga siku ya kukutana na kuweka wakfu Chama Cha Muziki wa Injili Kanda ya Kaskazini mwezi wa 10, 2014 katika uwanja wa Obedi. Na sasa wapo mbioni kuongea na mgeni rasmi kutoka serikalini na Baba wa Kiroho kanda ya Kaskazini.
16 July 2014
APOSTLE ALOIS RUTIVI INVITES YOU TO THE GO YE FORTH CONFERENCE – NAIROBI
13:55
No comments
“Celebrating the 25 years of effective Ministry”
The "Go Ye Forth Conference" starts tomorrow at 5.00pm ... 17th
– 20th, 2014 at Nairobi Gospel Assembly Church Ruaraka complex
Garden estate.
You are all welcome
14 July 2014
Welcome to Dorcus Christian Ministries “Embassy of God on Earth”
22:34
No comments
Dorcus Christian Ministries - Hand of help others
Dorcus Christian Ministries - Burundi branch
Patron Boniface Muhegi praying for people
Bishop Jane Muhegi with orphans
Our prayer for you is that the God of all grace anoints
you with fresh oil and His precious Spirit illuminates the Word as you read.
May He empower you to effectively communicate to others the vibrant hope that
He has given you to persevere the struggles that you have overcome and continue
to overcome.
Furthermore, my Husband and I pray that your home be a
reflection of the joy and peace that God has promised to all of His children
who follow Him. We bless your children, the fruit of your body. We speak life
into your marriage, your ministry and your mission.
As you lie down at night we pray for more than sleep. We
pray for rest. Rest in Him and arise refreshed for we need you. Your prayers,
your support and your love are important to us. So we pray you will take care
of yourself.
-Bishop Jane Muhegi
We have pleasure to introduce Dorcus Christian Ministries to
you. First and foremost is a christian oriented organization which was born
through great travail in prayer to God. It actually existed in the heart of the
founder as a normal spoken vision before its birth.
The founder had done tremendous task on voluntary basis to
affirm her vision and the white side of God truth to the orphans, widow,
disables and other member of the communiy by supporting them both spiritually
and physically as God supplies by promote and provide social service and activities
within the communities.
Through this ministries we have seen the glory of God his
unconditional love as it overflows to all his people. His love is what has made
us what we are today as the body of Christ as we become stronger in faith, hope
and love.
Kindly note that this organization is a purely non
organization and doesn't have any absolute connection with political affairs of
other than to pray for the development of the country.
The Ministry was founded by Pastor Jane Muhegi in the year
2003 after prompting to register the Umoja wa kuendeleza Vijana yatima Ubungo
(UKUVYU) in the year 2000.
The Dorcus Christian Ministries handles issue that pertain
to spiritual while UKUVYU specializes in matters relating social and economic
aspects of the community.
Both Ngo’s are open to serve all people without any
boundaries, religious backgrounds, color and tribal backgrounds.etc.
For any
help or request, please feel free to contact us by calling, mailing or coming
to us directly.
Postal Address: 13504
Kunduchi Beach - Near Jordan Sec. School
Bahari Beach Road.
Dar es Salaam – Tanzania
+255-22-2650378
dorcuschristianministries@yahoo.com
info@dorcuschristianministries.org
Kunduchi Beach - Near Jordan Sec. School
Bahari Beach Road.
Dar es Salaam – Tanzania
+255-22-2650378
dorcuschristianministries@yahoo.com
info@dorcuschristianministries.org
Subscribe to:
Posts (Atom)