14 February 2017
JIAMBATANISHE NA WATU WATAKAO KUFANYA UWE BORA ZAIDI
02:34
No comments
Kuna watu wanaweza kuwa sababu ya
mafanikio yako au kushindwa kwako, kuinuka kwako au kushuka kwako, kufanya
vizuri au kufanya vibaya, kwenda mbali au kubaki hapo hapo!
Chunguza kwa makini watu unao ambatana
nao na ikiwezekana, achana na wale wasiokufaa. Sijasema uwadharau, nimesema
ujitenge nao. Wengine ni nyoka kwako wanatema sumu, wengine ni kinyonga,
wanabadilika badilika, wengine ni konokono, wengine ni Mbweha, kazi yao
kuharibu mizabibu, wengine ni Kuku, maisha yao ni ya chini, hivyo wewe kama Tai
unahitaji kwenda juu…
Lakini pia zingatia haya;
KUWA NA HESHIMA KWA WATU WENYE
MAMLAKA YA KIROHO.
Kuna maeneo 3 yenye mamlaka ya
kiroho. Serikali [Taifa], Kanisa na Familia.
Heshimu maeneo haya. Kuna watu
wanajikosesha baraka kwa kukosana na maeneo haya 3. Yule ambaye unadhani ni
adui ktk maeneo haya matatu mpendwa wangu yamkini ndo amebeba muujiza wa
kuinuliwa kwako. Daudi hakumdharau Sauli pamoja na kwamba Mungu alikuwa tayari
ameshamkataa. Yusufu hakumdharau Farao au Potifa. Daniel hakuudharau uongozi wa
Babeli. Maadui zako ndio waliobeba baraka zako na miujiza yako. Kwenye maeneo
haya matatu usigombane nao kama wanakuchukia. Waombee na kuwatakia baraka siku
zote nawe utashangaa namna utakavyokuwa ukitembea ktk kibali na neema ya Mungu.
Nakuhakikishia hebu chukua nafasi
ya kuombea viongozi wako eneo lako la kazi kila siku uone mabadiliko ktk ofisi
yako. Chukua nafasi ya kuombea viongozi wako wa kanisa hata kama wanakuchukia.
Chukua nafasi kuwaombea wazazi wako na mwenzi wako hata kama hajaokoka na hata
kama anakuchukia. Hao ndio waliobeba ushuhuda na muujiza na baraka zako mwana
wa Mungu. Usiwachukie. Maandiko yanasema ‘Wala haikanushiki kabisa kwamba mdogo
hubarikiwa na mkubwa’ #WAEBRANIA 7:7. Wakubwa
wako hawa wamebeba muujiza wako. Waombee sasa.
Nasema asante kwa Bishop Kitonga, Mtume Fernandos, Dr.
Livingstone Banjagala, Dr. Lakhan wa UK, Rose Sarwatt (Mwenyekiti wa TAWIA),
Dr. Getrude Rwakatare, Askofu Jangalason, Dr. Migiro (balozi wa Tanzania
Wingereza), Mh. Jakaya, Rev. Alex (Mkufunzi wangu pale ISOM na Christian
Leadership University), Rev. Wilson Waidhaka (Rafiki yangu sana hapo Nairobi),
Rev. Benjamin Bukuku na wengine kibao.
Hekima yenu, ushauri wenu, mafundisho yenu na maisha yenu yamefanyika msaada
kwangu na kwa watu wengi.
Subscribe to:
Posts (Atom)