THE OFFICIAL JOHN SHABANI AND GOSPEL IN AFRICA BLOG

Welcome to the official blog of the the gospel singer, songwriter and teacher John Shabani. If you are one of the fans among the millions, feel free to get connected with John Shabani and stay updated on this blog.To learn more about John Shaban and his Ministry, please click the about button above.

GET THE LATEST FROM JOHN SHABAN AND THE GOSPEL NEWS COMMUNITY

You will be able to read and review the latest news on John Shabani's tour and other specials. You will also come across the best articles of news on Gospel from all across Africa and the International Community.Please do feel free to review our categories of news and events.

FEEL FREE TO LEARN MORE ABOUT JOHN SHABANI AND HIS MINISTRY

If you wish to learn more about John Shabani and his ministry, please feel free to connect with John Shabani on the social networks. You can keep up with John Shabani and the Gospel in Africa community on both twitter, facebook, google plus and many other more.

STAY UPDATED WITH INTERNATIONAL AND LOCAL GOSPEL NEWS

Gospel in Africa Blog is a comprehensive gathering place for African Gospel music fans. Offering the latest news and information about Local and International Gospel music and news, Gospel in Africa Blog also shares the spotlight with other genres of Christian music that more than ever, seemingly overlap musical genre lines, such as Bluegrass Gospel, Christian Country and others. Singing News, the leading African Gospel and International music Blog, features African and international Gospel lyrics, radio, news, Christian concerts, songs, artists, and more.

GET IN TOUCH AND STAY CONNECTED WITH JOHN SHABANI

If you are interested in contacting and staying in touch with John Shabani then here are the contacts. E- mail: touchingvoice@yahoo.com or , princejohntz@yahoo.com, Mob: +255 754 818 767 or +255 716 560 094, www.facebook.com/john.shabani.

22 March 2012

KADI ZA CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI ZAANZA KUTOLEWA KWA WANACHAMA


MEMBERSHIP CARD
 KADI ZA UANACHAMA

Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (Chamuita) ni chama halali kilichosajiliwa na kutambulika na Srekali ya Tanzania. Namba ya usajili ni  BST 4598
Tunapenda kuwatangazia kuwa, Kadi za chama cha muziki wa injili Tanzania zimeanza kutolewaa kwa wanachama wanaoendelea kujaza fomu za kujiunga na chama hicho. Ewe mwimbaji, mwanamuziki, mtengenezaji, msambazaji na mpenzi wa nyimbo za injili, hakikisha umejiunga na chama cha muziki wa injili Tanzania  (Tanzania Gospel Music Association) ili upate kadi yako. Kadi hii itakusaidia sana. Chama hiki kimesajiliwa na kutambuliwa na serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, pia ni moja ya vyama vinavyounda shirikisho la muziki Tanzania, shirikisho ambalo ni mwanachama wa shirikisho la muziki Duniani.

MALENGO NA MADHUMINI
Chama kitaendeshwa kama chombo kisicho na malengo ya kupata faida na chenye malengo na madhumini yafuatayo;-
i)             Kulinda utamaduni wa Tanzania na heshima ya muziki wa Injili, sawa na   Neno la Mungu
ii)            Kuhamasisha maendeleo ya muziki wa Injili na nyanja zake nyingine
iii)           Kutoa ushauri katika mambo yote yahusuyo muziki wa Injili, na watumishi wa Mungu waimbaji pia.
iv)           Kuwakilisha na kulinda maslahi ya wanachama kitaifa na kimataifa.
v)            kuwa chombo cha kuwezesha mawasiliano kati ya watu na vikundi katika kupeana taarifa kuhusu muziki wa Injili hapa nchini, na pia kuwezesha mawasiliano ya kimataifa.
vi)           Kuwa na rejista ya wanamuziki wa Injili na kazi zao. Ili kusaidia kulinda na kutangaza haki za wanachama.
vii)          Kutafuta mapato kwa njia ya ada, michango, harambee, maonyesho, kukopa, ufadhili au zaidi katika kuendeleza malengo na madhumuni ya Chama.        
viii)         Kuwawezesha wanamuziki wa Injili kwa njia ya kuwaongezea elimu
ix)           Kuinua hadhi ya muziki wa Injili nchini
x)            Kutambuliwa rasmi na Serikali yetu na wadau wengine
xi)           Kuwekeza katika miradi, na kujipatia kipato kwa njia ya kuwakomboa jamii ya wanamuziki wa injili.
 kwa maawasiliano: Mob: 0754 818 767, 0716 560094.
                              E-mail: touchingvoice@yahoo.com

20 March 2012

DON MOEN NA WENZAKE KUPAMBA TAMASHA KUBWA LILILOANDALIWA NA UMOJA WA MAKANISA JIJINI DAR ES SALAAM.



Umoja wa makanisa ya Dar es salaaam ukishirikiana na shirika la kimataifa la LUISPALAU association,liko kwenye mikakati la kufanya tamasha kubwa la injili la upendo maeneo ya Jangwani kuanzia mwezi wa nane hadi mwezi wa 12 mwaka huu, na tamasha hili litafanyika jijini Dar es salaam kama sehemu ya mfululizo wa matamasha ya jinsi hiyo ambayo shirika hilo imekuwa ikiyaendesha katika miji mikuu kadhaa barani Africa.

Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo,iliyoundwa na makanisa mbalimbali jijini hapa,tamasha hilo litawaleta nchini wanamichezo mbalimbali wa kimataifa pamoja na waimbaji mashuhuri wa injili,akiwemo Don Moen,Nicole Mullen na wengine wengi,taarifa hiyo imebainisha kuwa wanamichezo wa kimataifa wanaoruka na pikipiki pamoja na baiskeli ya mashirika ya BMX na Fmx nao pia wataalikwa.

Nicole Mullen.
Kwamujibu wa taarifa ya mwenyekiti wa tamasha hilo Askofu Philemon Tibanenason ameongeza kuwa makanisa hayo yamepata fursa ya pekee ya kufanya kazi katika umoja kudhihirisha upendo wa Yesu ubadilishao maisha,tamasha hilo limewahi kufanyika katika miji kama Kigali Rwanda,Bujumbura Burundi,Kampala Uganda na Cairo Misri.

source---gazeti MSEMAKWELI/Gospel kitaa

19 March 2012

FLORA MBASHA NA MUMEWE WAGUSA MIOYO YA WAMAREKANI

 Mabango ya huduma ya flora mbasha yalivyozangaa mitaa ya marekani

Flora Mbasha na mumewe wakiimba kwa upako Jumapili katika kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministires huko Adelphi Md.

 Tangazo la mkutano uliohudumiwa na Mch. Deo lubala, huku mwimbaji wa kimataifa Flora mbasha na mumewe wakiwa ndio waimbaji wakuu.

 Mambo ya stejini
Haya bwana, mambo ya majuu hayo
Mbasha na wenyeji wake wakipata maakuli

17 March 2012

MWIMAJI MAARUFU WA BONGO FLEVA RENEE LAMIRA, AWA MTUMISHI WA BWANA


Bila shaka unamkumbuka mwanamuziki au mwimbaji Renee Lamira(pichani).Aliwahi kutamba vilivyo na albamu yake iliyoitwa Ngoma ya Kwetu.Lakini je unafahamu kwamba Renee siku hizi ameachana na nyimbo zinazoitwa za “kidunia” na badala yake anafanya nyimbo za injili Kama inavyojulikana kwa wengi Renee Lamira aliyekuwa kinara wa wa nyimbo za Bongo fleva na kupata heshima na umaarufu mkubwa dhidi ya mashabiki wake, Alitamba kwa album yake ya NGOMA YA KWETU pia alifanikiwa kutumbuiza Kora hukoo Afrika Kusini, Renee kwa sasa ameokoka, na zaidi ya hayo pia ni mchungaji katika huduma ya CHRIST EMBASY tawi la mbezi Dar ea salaam

REBECCA MALOPE KUFANYA KWELI KATIKA TAMASHA LA PASAKA



Tamasha la Pasaka ambalo hufanyika kila mwaka Tanzania baada ya kuwa na uzoefu wa kualika waimbaji wa Gospel kutoka nchi jirani kama Zambia, Kenya, Rwanda na Uganda, mwaka huu limevuka boda mpaka kwa mzee Mandela na kumpa mwaliko malkia wa GOSPEL AFRIKA Rebecca Malope ambae ameukubali.

Malope atakua mmoja kati wanamuzili wa injili watakiaoimba siku hiyo ya april 8, akiwemo Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Epraim Sekeleti (Zambia), Anastazia Mukabwa na wakali wengine ambapo Mgeni rasmi ni Waziri wa mambo ya nje Benard Membe na time hii kwa mara ya kwanza tamasha hilo litafanyika kwenye uwanja wa Taifa.

14 March 2012

FLORA MBASHA APAA MAJUU

FLORA MBASHA (MWIMBAJI WA NYINBO ZA INJILI-TANZANIA) AKIWA BOSTON MAREKANI AKIFANYA KAZI YA BWANA
Flora Mbasha soars during rehearsal for the concert on Sunday
Flora Mbasha and Deus Cosmos


Ukimtumikia Mungu utafika mbali na utakaa na wakuu wa nchi.
Flora Mbasha na mumwe wanashukuru sana wote waliowaombea katika safari yao ya Marekani...Mungu na wabariki.

Mbali na kuwa Marekani pia anapenda kuwajulisha kuwa studio yake ya FLAME inazidi kufanya mambo makubwa maeneo ya Tabata..Karibu Sana.

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP