Yafuatayo ni
baadhi ya mambo unayoweza kuyafanya ili kuwa na afya bora katika mwaka huu wa
2013. kabla sijaendelea mbele sana, naomba niweke wazi
kwamba afya bora haihusu kula vizuri na mazoezi peke yake bali pia fikra
chanya(positive attitude). Kuna umuhimu wa kuhakikisha kwamba siku zote unakuwa
na mawazo chanya na pia kuwa karibu zaidi na watu wenye mawazo chanya.
Kunywa Maji kwa wingi- Bila shaka
unakumbuka msemo “Maji ni Uhai”.Hiyo ni kweli kabisa maji ni uhai sio tu kwa
mazingira yetu na dunia kwa ujumla bali pia kwa afya au miili yetu. Maji ni
kitu muhimu sana
kwa afya zetu. Asilimia 60% ya miili yetu imetengenezwa au imesheheni maji.
Maji yanahitajika kwa ajili ya kuondoa takataka au vitu visivyofaa kutoka mwilini,
maji ndio hubeba virutubisho na oxygen.
Kiasi
cha maji anachohitaji mtu kinategemea na mambo kadhaa kama
vile unyevu(humidity) wa mahali ulipo, shughuli zinazohusisha mwili
anazozifanya mtu na pia uzito wa mwili. Pamoja na hayo,kwa wastani miili yetu
inahitaji lita 2 na nusu mpaka 3 za maji.Vyakula tunavyokula huchangia kama asimilia 20% za maji katika miili yetu. Kwa hiyo
tunahitaji kunywa maji kiasi cha lita 2 mpaka lita 2.4 au glasi 8-9 za maji kwa
siku.
Njia
rahisi ya kujua kama mwili wako una maji ya
kutosha ni katika kuangalia mkojo. Mkojo wako unatakiwa kutokuwa na
rangi(colorless) au kuwa wa njano kidoogo. Kinyume cha hapo ni ishara kwamba
hauna maji ya kutosha mwilini. Njia nyingine kutambua ni pamoja na kukaukwa na
midomo(lips) na hata ulimi na pia kupata kiasi kiduchu cha mkojo.
Pata Usingizi wa Kutosha: Unakumbuka
tulipokuwa wadogo wazazi wetu walisisitiza sana kwamba twende tukalale mapema ili tukue?
Bila shaka walikuwa wanajua kwamba usingizi ni sehemu muhimu sana katika afya. Ukiachilia mbali faida za
usingizi kwa ajili ya afya za akili/ubongo wetu,usingizi au mapumziko ya
kutosha ni muhimu kwa miili.Afya njema huenda sambamba na mapumziko.Ni wakati
wa kuupa mwili nafasi ya kujijenga,kujiongezea nguvu na muhimu zaidi kuhakikisha
kwamba tunakuwa na akili timamu. Pia ukosefu wa usingizi ni chanzo cha kuzeeka
mapema.
Fanya Mazoezi- Hili
linaweza kupita bila maelezo ya ziada. Mazoezi ni muhimu sana kwa afya bora. Fanya mazoezi angalau
mara tatu katika wiki. Jipatie muda wa kutembea japo kwa dakika 30. Kama inawezekana nenda Gym, badala ya kupanda lifti pale
kazini kwako au mitaani, tumia ngazi za kawaida.Egesha gari lako mbali kidogo
na unapokwenda ili upate nafasi ya kutembea nk. Muhimu zaidi ni kuchagua aina
ya mazoezi unayoipendelea. Mazoezi hayatakiwi kuwa adhabu.
Faida
za mazoezi ni pamoja na kujiepusha na magonjwa mbalimbali, kupunguza unene(bila
shaka unajua kwamba unene kupindukia sio afya bali ni ugonjwa na sababu kubwa
ya maradhi mengine)
Kula Matunda Kwa Wingi-Matunda ni
chanzo kizuri sana cha madini na vitamins ambazo
miili yetu inahitaji sana
kwa ajili ya afya bora. Unajua kwamba machungwa,kwa mfano, yana faida kubwa
zaidi kiafya kuliko vidonge vya Vitamin C unavyobugia kila leo? Aina mbalimbali
za matunda ambayo yana virutubishi vingi zaidi kiafya ni Parachichi(Avocado),
apple, matikiti maji(cantaloupe),Zabibu(Grapefruit), Kiwi,Guava,mapapai, machungwa,
strawberries nk.
Kula mboga za majani- Kama
ilivyo kwa matunda,mboga za majani(vegetables) ni muhimu sana kwa afya zetu. Wataalamu wa afya wanashauri
kwamba tule aina 5 mpaka 9 za mboga za majani na matunda.Jitahidi kupata
angalau zaidi ya aina 5 za mboga za majani na matunda.
Punguza Kula Vyakula vya Makopo- Kutokana
na jinsi dunia inavyozidi kwenda mbio,watu wengi huwa tunakosa muda wa
kupika.Matokeo yake tunakimbilia kwenye vyakula vya kwenye makopo ambavyo
ndivyo vimejaa katika maduka na ma-supermarket. Jitahidi kuviepuka vyakula
hivyo kwa kadri unavyoweza.Mara nyingi vyakula vya makopo huwa na ingredients ambazo
hazifai kwa afya zetu.Kwa mfano,vingi miongoni mwa vyakula hivyo huwa na chumvi
nyingi kitu ambacho ni chanzo cha High Blood Pressure na maradhi ya moyo.
Unaposhindwa kabisa kujizuia kununua vyakula hivyo vya makopo jaribu kuangalia
ambavyo havina sukari au chumvi.
Jipende- Kama
nilivyodokeza hapo mwanzo,afya bora huenda sambamba na afya ya
akili/ubongo.Njia mojawapo ya kupata afya hiyo ni pamoja na kujipenda.Pengine
unajiuliza,kuna mtu ambaye hajipendi? Ukweli ni kwamba pengine ni kweli kwamba
hakuna mtu ambaye hajipendi.Tofauti inakuja pale mtu anapofanya vitu ambavyo ni
kinyume kabisa na mapenzi ya mwili.
Mfano,
uvutaji sigara, unywaji pombe kupindukia, kutojisafisha mwili wako kwa mfano
kuoga, kupiga mswaki na pia kupumzika nk.Hizo zote ni tabia ambazo zinaweza
kuonyesha jinsi ambavyo hujipendi au huupendi mwili wako.
0 comments:
Post a Comment