Waumini wa dini ya Kihindu wakienda kuoga ili kujitakasa na dhambi
walizotenda
Kutokana na wingi wa watu, treni kama unavyoona zinakuwa zimepakia hadi dereva hapati pa kuangalizia. Kila penye upenyo panakaa mtu isipokuwa tu kwenye magurudumu
Baada ya kuoga wateule hubeba maji kwenye vyungu vya vhuma kupeleka
mahekaluni
Tofauti na imani ya Kikristo, ALLAHABAD,
India, Mamilioni ya wai wa dini ya Hindu kila mwaka hufanya hija yao ya kuoga katika makutano ya mito
mitatu ya Ganges, Yamuna na Saraswati inapokutana. Kwa mujibu wa Imani ya
Kihindu, binadamu anakuwa ametenda dhambi nyingi katika mzunguko wa mwaka na
hivyo anahitaji kutakaswa na dhambi zake. Waumini wanaume wanajipaka majivu
kuanzia utosini hadi unyayo na mara nyingi wanakuwa uchi wa mnyama ingawa
sikuhizi wengine wanapendelea kuvaa pajama, wanaingia kwenye mto huo na kuoga
nakuamini kuwa wameondolewa dhambi zao zote na nuksi nyingine zote. Hii ni sherehe kubwa na inayodumu
muda mrefu kuliko zote duniani kwani inadumu kwa kipindi cha siku 55.
Mratibu mkuu wa sherehe hizo Mani
Prasad Mishra alisema, mwaka huu karibu watu milioni zaidi ya milioni 110 walikadiriwa kuoga kwenye eneo
hilo liitwalo SANGAM. Hili ni eneo ambapo makutano ya mito ya GANGES, YAMUNA
NASARASWATI . Sikukuu hii inatelemea mwonekano wa nyota zinazolandana angani.
Baada ya nyota hizo kukaa katika mkao fulani basi wahindu wanaenda kuoga ili
kujitakasa na madhambi yao na kuopuka kufo na kuzaliwa upya katika hali ya
adhabu.
0 comments:
Post a Comment