Hii ni ziara ya kihistoria
iliyoandaliwa na chama cha Muziki wa Injili Tanzania.
Mungu alipoumba Dunia,
aliifanya yenye kupendeza na kuvutia sana, lakini kwasababu ya matumizi mabaya
ya wanadamu, sasa maeneo mengi duniani yanaonekana kama jangwa, kwasababu ya matumizi
mabaya ya ardhi, kumekuwa na ukame uliokithiri, ardhi sasa haina rutba ya
asili, joto linasumbua duniani kote, majira ya upatikanaji mvua yamebadilika
sana; wanaoathirika ni viumbe hai akiwemo mwanadamu.
Kwakulitambua hilo,
waimbaji wa nyimbo za injili, tumeamua kujitolea kufanya kampeni nchi nzima ya
upandaji miti pamoja na miche ya maua na matunda ili kurejesha uoto wa asili
katika nchi yetu.
Pamoja na hayo pia ziara
hiyo inaandaa matamasha ya uimbaji ikiwa ni pamoja na kuwahubiri watu waache
uovu na kuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Jambo linguine la msingi ni pamoja
na kuwa na kuiombea nchi amani, utulivu,
umoja na mshikano wetu.
Baada ya ziara ya umisheni
mkoani singida, waimbaji walipata fursa ya kuhudhuria kikao cha bunge na
baadaye kupata picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda, Naibu Waziri wa Fedha Mh. Mwigulu
Nchemba, Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Razaro Nyarandu, Mbunge wa CCM Viti
Maalum – Singida Mh. Martha Mlata, Mbunge wa Viti Maalum CCM – Mbeya Mh. Marry
Mwanjelwa, Mh. Magreth Sitta na wengine wengi.
Ziara
ilihitimishwa kwa kupata chakula cha mchana kilichoandaliwa na Mh. Nyarando
ndani ya Dodoma Hotel. Mh. Nyarando aliweza kuwashukuru waimbaji kwa
ushiriakiano wao na jinsi walivyoweza kujitolea kufika vijijini kufanya kazi ya
Mungu.
Pia aliweza
kuwaahidi waimbaji kutembelea Ngorongoro Crater mapema iwezekanavyo, ili
kujifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja na kutangaza
vivutio vya utalii.
Kwa msaada wa Mungu
tunaweza!
waimbaji wakiwa wamejipanga tayari kuelekea kupanda miti
Msafara wa waimbaji wakishirikiana na wanakijiji wa tarafa ya Ndago mkoani Singida pamoja na viongozi wa dini, wakielekea kupanda miti
Mheshimiwa Martha Mlata akipanda mti
Stela Joell akipanda mti
Madam Ruti akishirikiana na mtangazaji wa Star Tv, bi Sauda kupanda mti
John shabani na Jane Misso, wakipanda mti
Edson Mwasabwite akipanda mti
Mch. Vaileth na Bupe kingu wakishirikiana na watumishi wengine kupanda mti
0 comments:
Post a Comment