Nikiwa na watalii mbalimbali karibu na mto wa ajabu, baada ya kuzunguka kutwa nzima eneo la Ngorongoro Crater, watalii huja mahali hapa penye idadikubwa ya viboko.
Imekuwa ni ziara ya kipekee kati ya ziara nilizowahi kuzifanya. Kwani nimejionea moja ya maajabu ya dunia, Ngorongoro Crater. Pia nimeweza kuibua vipaji vya watoto pamoja na kurekodi nyimbo kadhaa.Ngorongoro ("Ngorongoro Conservation Area") ni umbali wa takribani kilomita 180 kutoka Arusha na pia hifadhi ya taifa inayojulikana kote duniani. Eneo hili ni sehemu ya Serengeti.
Kuna
jumla la wanyamapori
wakubwa takriban 25,000, wakiwa pamoja na vifaru, viboko, nyumbu, pundamilia, nyati, simba,
fisi
na chui .
Ngorongoro
imepokelewa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO.
Je unajua kitu kuhusu Ngorongoro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? |
Pia, kuna
Ziwa Magadi ndani ya bonde refu na kubwa maarufu kwa jina la ‘Ngorongoro Crater’
lililosababishwa na milipuko ya volcano zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
Mahali
hapo si pengine popote, ni Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (Ngorongoro
Conservation Area Authority – NCAA) iliyoanzishwa mwaka 1959 na kukabidhiwa
majukumu makuu yafuatayo:
Kuhifadhi
maliasili (wanyamapori, ndege na mazingira) zilizopo, kuendeleza binadamu
wenyeji (Wamaasai) na utalii katika hifadhi hiyo.
Ina eneo
lenye ukubwa wa kilomita za mraba 8,292, inapakana na Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti (SENAPA) upande wa Kaskazini Magharibi na miji ya Arusha, Moshi na
Mlima Kilimanjaro upande wa Mashariki. Maelfu ya watalii kila mwaka kutoka pembe nne za dunia hutembelea Ngorongoro.
Nikiwa na watoto wa Shalom Orphanage center baada ya kukaribishwa kula chakula katika hotel ya Sarena
John Shabani, watoto wa Shalom na rafiki zetu wengine
Nikiwa na kundi kubwa la watoto baada yakupata chakula katika hotel ya Serena
0 comments:
Post a Comment