(Rafiki mzuri atakufanya uwe na furaha, tabasamu na kicheko)
Nilipokua nikijifunza somo la saikolojia hasa kwa habari za mahusiano, somo hili lilinisaidia sana kujihepusha na marafiki wasikua na tija katika maisha yangu. Acha nikusaidie pia;
UTANGULIZI
Katika lugha ya kingereza kuna Mithali moja inasema “A Friend in need is a friend indeed” kwa maana ya“Rafiki anayakutafuta ndiye rafiki wa kweli.Ni dhahiri kwamba hapa duniani kuna marafiki wa aina tofauti tofauti wakiwemo wenye nia njema na wenye nia mbaya.
Huyu anayezungumzwa hapo juu ni aina mojawapo ya rafiki mwenye upendo wa dhati na anayejali,kuthamini na kumpa furaha na amani mtu yule anayemtafuta.Mwandishi wa mashairi mmoja aliandika kwamba “Niambie nani rafiki yako nami nitakuambia wewe ni mtu wa aina gani.”Kwa mantiki kwamba rafiki wa mtu ana uwezo mkubwa sana wa kumusaidia mtu husika au kumpotosha kabisa katika njia isiyo salama.
Katika maisha ya kawaida ,ni muhimu sana kutambua na kuelewa kwa kina marafiki uliyonao kwa sababu wanaweza kuyajenga au kuyaathiri maisha yako kwa kiwango kikubwa sana.Hivyo basi ni vema ukagundua vigezo vinavyoashiria aina tofauti tofauti za marafiki ili uweze kubaini marafiki watakaoweza kukusaidia maishani na wale watakaoweza kukuharibia maisha yako .
Kwa kukosa kuyafahamu haya ,watu wengi wameumizwa na kujutia maisha yao baada ya kutendwa na wale waliodhania kuwa ni watu wao wa karibu kumbe walikuwa siyo watu wazuri
Kuna aina nne za Marafiki kama ifuatavyo:
1. Rafiki wa Kweli (Intimate Friend,Real Friend)
2. Rafiki Mnafiki (Hypocritic Friend)
3. Rafiki Mnyonyaji (Absorbant Friend)
4. Rafiki Mpoteza muda (Time loser Friend)

Ebu nikudadavulie rafiki mmoja baada ya mwingine :
1. RAFIKI WA KWELI: (INTIMATE FRIEND)
Ni Yule :
• Anayekujali kwa kila hali,
• Anayekujulia hali muda mwingi,
• Anakuthamini ,
• Anakuonyesha upendo wa dhati kwa vitendo si kwa maneno tu,
• Anakutafuta kwa hiari yake mwenyewe bila kushinikizwa na mtu
• Anakushirikisha mambo yake
• Ni mkweli na mwaminifu kwako
• Anatafuta mbinu za kukufanya ufurahi,utabasamu,ucheke na uwe na amani.
• Ndiye mfariji na mdhamini wako wa kwanza unapopatwa na magumu.
• Anakuamini katika mengi unayomwambia
• Muda mwingi anapenda kuwa na wewe,kutembea na wewe,kula na wewe nk..
• Mnapokuwa pamoja anaona fahari ya kuwa na wewe na hata anasahau ratiba zake zingine alizo nazo
• Anakuheshimu na kuheshimu mawazo ,maoni na mapendekezo yako.
• Hana maswali ya kimtego-mtego wala ya kijinga maana anahofia kukupoteza .Daima maswali yake yana msingi wa kujenga mahusiano yenu.
• Hataki kukuona ukinuna wala ukikwazika,
• Hawezi kukusema vibaya na Hataki kusikia ukisemwa na watu vibaya hata kidogo badala yake anakutetea
• Ni mwaminifu katika mambo yote
• Furaha yake ni kukuona:
Umechangamka
Una amani,
Umefanikiwa
Umestawi
Umekua na afya njema
Umefaulu
Mambo yako yanakwenda vizuri
Umefarijika
Umeinuka
• Ni mstarabu ,mpole,muelewa na mtii kwako pia anaelewa hali ya mambo ilivyo pindi unapomuelekeza
• Siku zote anatafuta maslahi ya ninyi wote (wewe na yeye) ,
• Akiwa nacho anakukumbuka,asipokuwa nacho anakupa taarifa
• Ni mwepesi wa kukuomba msamaha,
• Anakuomba ushauri,
• Mara zote anakupa nafasi ya kutoa mapendekezo,mawazo na maoni yako kuhusu jambo lolote linalowahusu.
• Mnapopishana kwa jambo lolote anajitahidi kutafuta suluhu haraka iwezekanavyo ili myamalize.

2. RAFIKI MNAFIKI (HYPOCRYTIC FRIEND):
Ni Yule:
Anayejidai kukupenda anapokuona lakini mnapoachana anakusahau kabisa
Usipombipu,kumtumia meseji au kumpigia simu,hawezi kukujulia hali.
Anakupigia simu pindi anapokuwa na shida na wewe au anapohitaji faraja kutoka kwako.
Anakuinjoyi mara nyingi na kujidai kukupenda kwa dhati pasipo kuwa na ukweli wowote.
Ana maneno mengi ya udanganyifu
Ni mtoa ahadi nyingi asizotekeleza
Hana upendo wa dhati na wewe hata kidogo
Anakusengenya ,kukushusha hadhi na kukubeza anapokuwa na watu wengine
Anatangaza habari na taarifa zako nzuri na mbaya kwa wengine kwa lengo la kukuharibia sifa.
Anakudadisi sana na kujiweka karibu na wewe ili apate maneno ya kukuchafulia jina.
Hapendi mafanikio yako
Siyo mwaminifu hata kidogo
Hataki uwe na kitu chochote kinachomzidi yeye .
Anatafuta visingizo kutafuta namna ya kukuacha.

3. RAFIKI MNYONYAJI (ABSORBANT FRIEND):
Ni Yule:
Anatafuta faida kutoka kwako,anahitaji kunufaika kupitia wewe kwa namna moja ama nyingine .
Ana agenda ya siri kuhusu wewe siri ya kukunyonya.
Anakuweka karibu sana ili umpe kile anachohitaji:
o Mfano: PESA, MWILI WAKO, KUJIPATIA AJIRA kupitia wewe , MALI ya aina FULANI,….. akishafanikiwa kupata kile alichokuwa anawinda kwako basi anakupiga chini,anakusahau kabisa wala hataki kukuona na anabadili hata namba za simu .
Si mwepesi kukuomba msamaha anapokukosea baada ya kupata kile alichokuwa anahitaji.
Hakubembelezi hata kidogo baada ya kupata alicholenga kwako.Hata anakuwa mkali kwako.
o Msimamo wake siku zote ni “POTELEA MBALI”
Mara zote anakuwekea masharti yatakayomfanya afanikiwe kupata anachokitafuta kwako.
Anapotaka kukuacha anatafuta sababu isiyo ya msingi yaani kisingizio
Anapenda sana kuchunguza mambo yako .
Haoni aibu kukuomba vitu mbalimbali kama vile Pesa , Mali, Mwili wako nk…

4. RAFIKI MPOTEZA MUDA (TIMELOSER FRIEND ):
Ni Yule:
o Anatoa ahadi kibao kwa asilimia kubwa sana lakini hatekelezi
o Anakukatisha tamaa unapotaka kufanya jambo linaloleta maendeleo
o Hakutii moyo hata siku moja.
o Anakuthibitishia kwamba huwezi kabisa kufanya kama wengine wanavyofanya.
o Anakucheleweshea mipango na ratiba zako
o Kwenye mahusiano anakuahidi kuwa mko pamoja sana lakini anakupotezea muda tena kwa makusudi
o Ana wivu wa kijinga jinga usiyokuwa na sababu za msingi
o Anakuvurugia mipango na ratiba zako
o Anakuwekea masharti mengi katika ushirikiano wenu
o Anajali maslahi yake binafsi ,haangalii maslahi yako.
o Amejaa maeneno ya uwongo na udanganyifu
o Ana mizaha mingi sana ,hana hekima wala busara.
o Haoni fursa,hajishughulishi kwa mambo yanayowahusu.
o Hana maono wala mipango inayohusu maendeleo yenu na hatima yenu baadaye.
o Anakuongezea msongo wa mawazo siku hadi siku kwa maneno yasiyokuwa ya kukujenga.
o Katika mahusiano haongei mambo ya msingi hana pointi zenye misingi.
o Anapenda mpoteze muda mwingi kwenye vitu visivyokuwa na tija kama vile starehe, michezo na burudani nk….

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana namimi kwenye simu yangu au ukatembelea kituo chetu.
Nakupenda.
0 comments:
Post a Comment