THE OFFICIAL JOHN SHABANI AND GOSPEL IN AFRICA BLOG

Welcome to the official blog of the the gospel singer, songwriter and teacher John Shabani. If you are one of the fans among the millions, feel free to get connected with John Shabani and stay updated on this blog.To learn more about John Shaban and his Ministry, please click the about button above.

GET THE LATEST FROM JOHN SHABAN AND THE GOSPEL NEWS COMMUNITY

You will be able to read and review the latest news on John Shabani's tour and other specials. You will also come across the best articles of news on Gospel from all across Africa and the International Community.Please do feel free to review our categories of news and events.

FEEL FREE TO LEARN MORE ABOUT JOHN SHABANI AND HIS MINISTRY

If you wish to learn more about John Shabani and his ministry, please feel free to connect with John Shabani on the social networks. You can keep up with John Shabani and the Gospel in Africa community on both twitter, facebook, google plus and many other more.

STAY UPDATED WITH INTERNATIONAL AND LOCAL GOSPEL NEWS

Gospel in Africa Blog is a comprehensive gathering place for African Gospel music fans. Offering the latest news and information about Local and International Gospel music and news, Gospel in Africa Blog also shares the spotlight with other genres of Christian music that more than ever, seemingly overlap musical genre lines, such as Bluegrass Gospel, Christian Country and others. Singing News, the leading African Gospel and International music Blog, features African and international Gospel lyrics, radio, news, Christian concerts, songs, artists, and more.

GET IN TOUCH AND STAY CONNECTED WITH JOHN SHABANI

If you are interested in contacting and staying in touch with John Shabani then here are the contacts. E- mail: touchingvoice@yahoo.com or , princejohntz@yahoo.com, Mob: +255 754 818 767 or +255 716 560 094, www.facebook.com/john.shabani.

22 June 2019

NAMNA YA KULINDA, KUTUNZA NA KUIPONYA SAUTI YAKO

Kila mtu anaweza kuitumia sauti yake, lakini si kila mtu anajua jinsi ya kuitunza au kuiponya inapopatwa na tatizo. afya yake, au nini cha kufanya. Makala hii itasaidia kila mtu kujifunza jinsi ya kuponya sauti  na pia kutoa ushauri wa jinsi ya kuitunza na kuifanya kuwa na afya na nguvu kwa ajili ya siku zijazo. Masomo haya yanawafaa walimu, wainjilisti, wanasiasa, wazazi, wanasheria, madaktari, na waimbaji, na kila mtu ambaye shughuli zake hulazimu kakuongea sana.

Yawezekana umekuwa ukijiuliza,tunapozungumzia dhana nzima ya kukauka au kupotea kwa sauti, hivi huwa ina enda wapi? Sijui kama ume wahi jiuliza swali hili mpenzi msomaji, leo na kuendelea utapata majibu mengi ya maswali yako kupitia mtiririko wa vipindi hivi ndio maana pia tume lazimika tumia kiswahili ili kuwafikia watu wengi zaidi.MWANADAMU anasehemu laini sana kama ute wa viji ngozi viwili ndani ya boksi la sauti kooni(voice box/larynx)vinavyo itwa vocal cords au vocal folds, kwa lugha ya kigeni. hapa ndipo maala muhimu ni sisitize tena muhimu mno maana ndipo naweza sema ni kama kiwanda cha sauti. Mitetemo ya sauti ni matokeo ya kani msukumo wa hewa itokayo mapafuni kupitia kwenye kijisanduku cha sauti(voice box/larynx)mtetemo wa hivyo vijinyama viwili(vocal cords) ndani ya kijisanduku cha sauti(voice box) ndipo hupelekea huo mlindimo wa sauti uisikiayo. Hakika Mungu wa ajabu. Sasa Sikila unacho kula hugusa au kufikia mahala hapa itokapo sauti, isipo kuwa vinavyofika mahala hapa ni vile vitu unavyo weza vuta mfano: mvuke na moshi kama vile moshi wa sigara ambao ni hatari sana. Sasa nikujibu sauti hupotelea wapi/hukauka kweli??. Kiukweli sauti haikauki ila inakoma kuzalishwa kwa muda, hii nipale ambapo Vijinyama laini hivyo viwili(vocal cords) vinapo vimba hali hii hufanya vishindwe tetemeka na kutoa sauti, hapo watu husema sauti ime potea au ime kauka. SASA NI NINI hupelekea uvimbe huu? Yafuatayo ni majibu: Uvutaji wa sigara, matumizi ya juu mno ya sauti kama kupayuka na kupiga yowe, kikohozi cha mara kwa mara na pia maambukizi katika koo la sauti, mfano virus wa mafua (flu viruses).

Niruhusu nikupe darasa kidogo kuhusu sauti;
Nidhahiri umewahi sikia au kuona mwalimu akiwaambia kwa ukali waimbaji mwanzo kabisa mwa zoezi kuwa;"jamani mbona leo siwaelewi namna mnavyo imba/TOENI Sauti/Mnaimba kama hamtaki/Naomba kwanza wote msimame n.k... Niliwahi kufundisha  juu ya tabia ya sehemu ya ndani ya kijisanduku cha sauti(VOICE BOX/LARYXN):
 NDANI ya kiji sanduku hiki kuna kijisehemu laini sana kiitwacho (VOCAL FORD/VOCAL CORD). Sehemu hii ina tabia ya kusinyaa na kubadilika hali yake kutokana na mazingira au hali ya hewa, mfano, ubadilipo mazingira yenye joto au baridi huchukua muda kujishape na yale mazingira, kadharika ukiwa unaongea hutenda tofauti kabisa na pale uimbapo. Lakini pia mazingira ya mfumo wa maisha ya kila siku; malazi, makazi, vyakula, vinywaji, msongo wa mawazo, matumizi ya sauti, kupumzika n.k.

Kama walivyo wanariadha na wacheza soka kabla hawajaingia ulingoni lazima wawe na maandalizi ya mazoezi ili kuweka misuli yao sawa. Hivyohivyo misuli yetu ya koo vocal fold), lazima uiwarm up kabla hujaitumia.   HIVYO si sahihi kuingia kwenye uimbaji moja kwa moja pasi kuandaa koo kwa mazoezi andalio (VOCAL WARM UP). Hapa naomba unielewe mpendwa hapa namaanisha vocal warm up na si VOCAL EXERCISES), tutajifunza tofauti ya haya mambo mawili taratibu. Kuna kipindi serikali ili tangaza kwamba kansa inayoongoza nchini ni kansa ya kizazi na kansa ya koo. Sasa huyu mwimbaji au muhubiri hanywi maji vizuri at least glass nane kwa siku (maana hatunywi maji kwasababu tuna kiu, tunakunywa kwasababu makoo yetu yanatakiwa kuwa na unyevunyevu kila wakati), ni mtumiaji mzuri wa vitu vya baridi kisa ana friji (jamani friji haipo kwa ajili ya kutumaliza, eti friji yangu inagandisha kweli! Kiasi kwamba umekubali ikugandishe nawewe haaah! Hatutakiwi kula barafu, friji inakusaidia kutunza kitu, unapokihitaji, utoa, kinapoa kisha unatumia. Wewe mwimbaji, muhubiri, umeshinda kutwa nzima ukiitumia sauti, maji hujanywa, huna maandalizi ya misuli ya koo then jioni unaagiza maji ya baridi sana, au soda (kemikali), unachotafuta hapo ni majanga kwenye koo. 

Au unaagiza majuice yenye kemikai au energy drink eti upate nguvu, ukifahamu fika kinywaji hicho kina cafein, unadiriki kuingiza cafein kujerui koo, hatari saaaana! Jambo linguine microphone inayotumika imekaa miaka miwili, haijasafishwa, imetumika na kila kiumbe na wengine midomo yao utadhani ina kisima cha mate tena yenye madhara, alafu hiyo mic inakutu, alafu mtu anaitumia tu, mwisho wa siku jamani tumwmbee mwimbaji wetu, mchungaji wetu kuna pepo limevamia sauti yake halitaki watu wapone, waokolewe, hapana pepo ni yeye mwenyewe. Ni kukosa maarifa, na ukikosa maarifa lazima uangamie.

SASA ili uweze imba kwa uhuru na sauti bora yenye ujazo ni lazima mishipa ya koo lako iwe huru kwa msawazo(RELAXATION). Moja ya mishipa inayoweza mpelekea muimbaji kuimba/kuto imba kwa muda mrefu ni mishipa ya kichwa iliyopo nyuma ya shingo karibu na kisogo, ndio maana usikia watu kulalamika naumivu ya kichwa(STRAINING IN BACK MUSCLES) baada ya kuimba kwa muda mrefu.Waweza jaribu hapo ulipo kufungua kinywa chako mpaka mwisho wako kisha ona ni wapi mishipa ya kichwa, vuta utagundua ni nyuma ya shingo. ZOEZI HILI LA KITAALAMU BAADA YA TAFITI ZA KISAYANSI ndio suruhisho la matatizo hayo mawili (Tone~vocal fatigue na Straining in back muscles).
Hapa unaosha mikono kwa sabuni(ant bacterial soap)kwa maji safi kisha jikaushe kwa taulo safi.
*Ukiwa ume kaa au simama wima weka vidole vitatu kwa kinywa kisha imba herefi hizi; "A E I O U"kwa sekunde15- 35-60,.Baada ya hapo toa vidole kwa mdomo na jaribu ongea au kuimba utaona pumzi na wepesi/uzuri wa sauti. #ZOEZI MBADALA NI HILI
*Pasi vidole fungua kinywa kadri uwezavyo na imba kwa ulimi maneno haya LAGA LAGA LAGA LAGA LAA LAA×2,Kwa sekunde 15-45-60Bila kuruhusu taya na kidevu kucheza.mazoezi hayo yote hufanya kazi moja.


Vifuatavyo ni vitu muhimu kwa ajili ya afya ya sauti yako
Kuna vitu vitatu cha kwanza KUNYWA MAJI, cha pili KUNYWA MAJI na cha
tatu KUNYWA MAJI. Maji ni muhimu sana kwa sauti yako. Hakikisha
unakunywa maji ya kutosha.
Pumua kama muimbaji wakati wote hata ukiwa unazungumza na simu.
Hakikisha unakaa katika mkao mzuri kama ilivyoshauri katika sura ya pili.
Unaweza kutumia sauti yako yote pale unapotaka kusikika lakini hakikisha
hupigi mayowe ni hatari kwa sauti yako.
Hakikisha unapata muda wa kutosha wa kulala. Hakikisha una masaa 6 – 8
ya kulala

TANGAWIZI. Hii ni tiba nyingine nzuri ya sauti. Kiukweli huu ni mmea pekee na wa ajabu unao weza rejesha sauti ndani ya masaa machache mno,kuku toa kutoka hali ya kuto ongea kabisa mpaka kuimba kwa kishindo cha ajabu mimi nimeshuhudia hili kama muimbaji na mwalimu wa sauti.TANGAWIZI inatabia ya upasha joto pekee tu ilivyo,hali hii hupelekea hali kama ya muwasho(irritation)inayo pelekea ongezeko la kasi la mzunguko wa damu pale popote igusapo katika mwili.pia Tangawizi ni suruhisho la vimbe kutokana na hiyo sifa tajwa hapo juu.JINSI YA KUANDAA.osha mzizi wa hiyo tangawizi na maji safi bila kumenya(usiondoe ganda) kata vipande nyembamba mno vijae kijiko cha mezani kisha viweke kwenye maji(vikombe viwili vichemkavyo).kwa dakika kumi,ukiwa umefunika chombo unacho chemshia kisha chuja acha ipoe kidogo kwa joto unalo tumiaga kwa chai ya kawaida, usiweke sukari, badala yake waweza tumia kijiko cha asali kuongeza radha na asali ni tiba kubwa pia,hapo waweza tumia.ni vyema utumie unapoenda lala.Ifikapo asubuhi uta shuhudia haya maajabu ya mmea huu. Katika mafunzo haya ASALI ni somo lingine tutakalo jifunza pia.

         Kama sauti yako  imejeruhiwa vibaya, basi jambo muhimu zaidi la kufanya sasa hivi ni kuacha kutumia hiyo Sauti,  ipumzishe. Punguza pia kuzungumza kwa muda mrefu na hasa kwa kupaza sauti kubwa au kupayuka na kutumia muda kidogo zaidi katika ukimya. 

  • Jambo jingine kubwa ambayo husaidia sauti iliyojeruhiwa ni chai ya moto (Kama vile coat tea). Au maji moto ukichanganya na asali na limau. Unaweza kupata pia  dawa za mitishamba zilizohifadhiwa kitaalam katika maduka ya dawa, lakini ikiwa dini yako au tamaduni yako haina shida katika hili. Chai nzuri ni ile iliyo shauriwa ki afya na si kila chai ni bora. Unaweza kupata na dawa za mitishamba katika duka la dawa,  ambazo ni maalumu kwa ajili ya sauti, Kunywa angalau kikombe asubuhi na kikombe wakati wa usiku. 

         kama kuna kitu ambacho kinaweza kusaidia kuponya sauti yako na pia inaweza kutumika kulinda kwa haraka  ni unywaji wa maji ya kila siku. Maji husaidia na sauti yako kuwa hidrati, kuwa hidrati husaidia kuweka mwili wako katika afya nzuri na sauti yako tayari kufanya kazi. Pia asali mbichi husaidia. Maji ya mvuke ikiwezekana yachanganye na aina ya vics husaidia pia. Unaweza ukaogea au kujifunika na nguo nzito.

Naomba uzingatie kwamba sauti inataka matunzo. Na jinsi rahisi sana kuhifadhi sauti yako ili ifanye kazi vizuri na idumu kwa muda mrefu ni kama ifuatavyo.
  • Mazoezi ya sauti mara kwa mara kama nilivoelekeza humu.
  • Usinywe vinywaji baridi sana au barafu.
  • Usivute sigara.
  • Usivute bangi.
  • Usitumie madawa ya kulevya.
  • Chunga sana kwenye swala la pombe, aidha usitumie kabisa au tumia kidogo sana.
  • Usiwe na tabia ya kukohowa kwa kasi ili kuondoa kitu kooni. Nadhani mnanielewa. Hii tabia hukwangua koo.

Virutubisho Vya Kutumia
  • Vitamin C 1000mg wakati unahisi mafua au sauti imechoka. Yeyusha tembe moja kila siku ndani ya  glasi ya maji unywe. Zinapatikana pharmacy.
  • Kunywa maji mara kwa mara, yanasaidia kulainisha koo. Mwili wa binaadamu asilimia kubwa ni maji.
  • Tumia Multivitamins 
  • Tumia Antioxidants
Hizi mbili za mwisho zina gharama kidogo, kwahivyo angalia tu uwezo wako. 

3.0 Hitimisho na mapendekezo.
Koo hupendezwa, hutulizwa, huburudishwa, hutengenezwa pia na aina fulani ya pipi, asali, mvuke, chai ya mitishamba (mchaichai), kusafisha koo kwa maji, baadhi ya dawa kwa ushauri wa daktari, unywaji wa maji, na kadhalika. Pia, kinyume chake koo laweza kuharibiwa na matumizi ya vyakula au vinywaji kama vile; pombe, kahawa, soda, maziwa, chokoleti, pipi, ubuyu, matunda jamii ya ndimu, mayai, karanga, mahindi, bisi na kadhalika. Hivyo, muimbaji awe na taadhali katika matumizi ya vyakula na vinywaji ili kufanya sauti yake kuwa bora na kupendeza mbele za watu na Mungu tunayemtukuza kupitia sauti zetu.

Niseme kwamba,  mwanafunzi mzuri ni yule anayetafuta zaidi maarifa mara baada ya kujifunza jambo fulani. Hivyo, ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya yatakuwa msingi bora kwa muimbaji kutafuta zaidi kwa habari ya vyakula na vinywaji katika uimbaji. Haya yalioelezwa hapa ni machache sana. Pamoja na hayo, mabadiliko chanya ya uimbaji yatategemea uzingativu na utekelezaji kwa vitendo wa mambo hayo na sio kusikiliza tu. Pia, mabadiliko hasi yatatokea kwa wasiozingatia na kutekeleza kwa vitendo mambo hayo. Yuko mshairi anasema,
“Mshumaa tuliwasha, ili nuru kumulika, Giza kulitokomesha, na nuru kuenezeka,
Mshumaa unawaka, giza mbona linazidi?” Hivyo, huu ni mwanzo wa kujifunza uimbaji; huna budi kuifuata nuru (mafunzo) unayoangaziwa (kupewa) ili ufanikiwe katika uimbaji. Hii ni kwa sababu, wote waliofanikiwa katika aina yoyote ile ya huduma, walianzia chini na kwa kuwa walisikiliza na kutekeleza waliyoelekezwa na viongozi wao wakaweza kupanda na leo hii ni watu wakuu katia huduma.

Ili kuwa na afya nzuri katika mwili na katika uimbaji wako zingatia :
  • Punguza  matumizi mengi ya sukari, ongeza matumizi ya matunda
  • Punguza kula nyama nyekundu, ongeza matumizi ya mbogamboga
  • Punguza matumizi ya soda, ongeza matumizi ya maji
  • Punguza kuendesha, ongeza kutembea kwa miguu
  • Punguza kupoteza muda wa kulala, Zingatia kulala kwa wakati
  • Punguza msongo wa mawazo, ongeza kupumzika

Zingatia :
         Maji ya moto au aina ya chai mitishamba (herbal tea) ni bora, Mwimbaji mzuri hutumia class 8 za maji kwa siku, wapo ambao hutumia hadi lita 4 pia yapo maji ya ziada kutoka katika vyakula.
         Kupasha sauti kwa kukohowa kohowa sio njia ya kukusaidia kuimba vizuri, badala yake hukata sauti
         Pamoja na umuhimu wa maji, lakini acha matumizi ya maji mengi saa moja au mbili kabla ya kuanza uimbaji badala yake asali ni bora zaidi. Lakini pia sauti ikipatwa na tatito unaruhusiwa kupata maji ya moto pamoja na asali

         Angalizo kuhusu mazoezi: Mazoezi huwa yana ugumu wake hasa pale unapokuwa unaanza, usikate tamaa wala usikubali uvivu au maumivu yakakurudisha nyuma. Jitengee muda maalum kwa ajili ya kufanya mazoezi na usianze kwa kufanya mazoezi magumu bali anza na mepesi mepesi ili kuupa mwili nafasi ya ku-adopt mabadiliko

Kwa mafunzo zaidi jiunge na darasa letu pele SJ STUDIO Dar es salaam
Lakini pia unaweza kujiunga na group lets la WhatsApp Kama utakidhi vigezo
kwa mawasiliano zaidi; +255716560094

14 June 2019

FAHAMU MBINU KUU NNE ZA KUMUWEZESHA MUIMBAJI KUIMBA VIZURI (TONE NZURI)KWA MUDA MREFU PASI KUPATA MAUMIVU YA KICHWA AU KUCHOKA MAPEMA.




Tangazo: Ukitaka kujifunza zaidi Tuna kituo cha mafunzo Kimara Dar es salaam pia unaweza kujiunga na group letu la whatsapp kwakututumia jina lako na picha yako kwa namba +255716560094.
Sasa niendelee:

Imekuwa ni vita kubwa katika vikundi mbalimbali vya uimbaji hususani baina ya waalimu na wale wanaofundishwa(wana team/kwaya);hata kupelekea wengine kukimbia/kuacha uimbaji.Kukosekana kwa elimu sahihi ya Sauti,kutia ndani utunzaji mpaka matumizi sahihi ya sauti bila kusahau namna ya kuboresha sauti(tone),imepelekea wengi kuona uimbaji ni kama adhabu au ni kitu cha walio barikiwa wachache tu!!HAPANA!!LEO na kuendelea utakwenda pata maarifa ya juu zaidi katika hili.

LEO TUNA ANZA NA MBINU YA KWANZA;
(1)UFUNGUZI WA KOO NA ULAINISHAJI WA MISHIPA YA SHINGO NA YA NYUMA YA KICHWA(REMEDY FOR VOCAL FATIGUE).
Nidhahili umewahi sikia au kuona mwalimu akiwaambia kwa ukali waimbaji MWANZO kabisa mwa zoezi kuwa;"jamani mbona leo siwaelewi namna mnavyo imba/TOENI Sauti/Mnaimba kama hamtaki/Naomba kwanza wote msimame n.k...
SOMO lililo pita tulijifunza juu ya tabia ya sehemu ya ndani ya kijisanduku cha sauti(VOICE BOX/LARYXN):Waweza rejea katika ukurasa wetu huu.NDANI ya kiji sanduku hiki kuna kijisehemu laini sana kiitwacho (VOCAL FORD/VOCAL CORD).Sehemu hii ina tabia ya kusinyaa na kubadilika hali yake kutokana na mazingira au hali ya hewa,mfano,ubadilipo mazingira yenye joto au baridi huchukua muda kujishape na yale mazingira,kadharika ukiwa unaongea hutenda tofauti kabisa na pale uimbapo.HIVYO si sahihi kuingia kwenye uimbaji moja kwa moja pasi kuandaa koo kwa mazoezi andalio(VOCAL WARM UP)Hapa naomba umielewe mpendwa hapa na maanisha vocal warm up na si VOCAL EXERCISES)tutajifunza tofauti ya haya mambo mawili hapo mbele.
SASA ili uweze imba kwa uhuru na sauti bora yenye ujazo ni lazima mishipa ya koo lako iwe huru kwa msawazo(RELAXATION).Moja ya mishipa inayo weza mpelekea muimbaji kuimba/kuto imba kwa muda mrefu ni mishipa ya kichwa iliyopo nyuma ya shingo karibu na kisogo,ndio maana usikia watu kulalamika naumivu ya kichwa(STRAINING IN BACK MUSCLES) baada ya kuimba kwa muda mrefu.Waweza jaribu hapo ulipo kufungua kinywa chako mpaka mwisho wako kisha ona ni wapi mishipa ya vuta utagundua ni nyuma ya shingo.ZOEZI HILI LA KITAALAMU BAADA YA TAFITI ZA KISAYANSI ndio suruhisho la matatizo hayo mawili (Tone~vocal fatigue na Straining in back muscles).REJEA PICHA
#VIDOLE VITATU(3) KWA MDOMO.
Hapa unaosha mikono kwa sabuni(ant bacterial soap)kwa maji safi kisha jikaushe kwa taulo safi.
*Ukiwa ume kaa au simama wima weka vidole vitatu kwa kinywa kisha imba herefi hizi; "A E I O U"kwa sekunde15- 35-60,.Baada ya hapo toa vidole kwa mdomo na jaribu ongea au kuimba utaona pumzi na wepesi/uzuri wa sauti. #ZOEZI MBADALA NI HILI
*Pasi vidole fungua kinywa kadri uwezavyo na imba kwa ulimi maneno haya LAGA LAGA LAGA LAGA LAA LAA×2,Kwa sekunde 15-45-60Bila kuruhusu taya na kidevu kucheza.mazoezi hayo yote hufanya kazi moja.
(2) NAMNA YA KUBAJETI PUMZI NA KUIMBA KWA MSAADA WA MISULI YA TUMBO.
Mpendwa msomaji bila shaka umekuwa ukisikia juu ya umuhimu wa kuwa na pumzi kwa muimbaji na uwenda umewahi jiuliza huku kuimba kwa msaada wa MISULI YA TUMBO kukoje??na kuna tofauti gani na kule kuimba kwa kifuani.Wengi wametoa majina mengi mno juu ya namna ya uimbaji wengine hata kunyosheana vidole na kusema:sauti hiyo haitokei tumboni niya puani au kooni:FUATANA NAMI JUU YA UKWELI HUU!!.
kiuhalisia kuna aina nne za sauti japo tatu ndio maarufu sana na ndio zinazo fundishwa na wengi duniani kote nazo ni hizi;
(1)SAUTI YA ASILI (CHEST VOICE)
Aina hii ya sauti mitetemo yake hufanyikia kifuani.hutokea mtu akiwa kwenye msawazo (Relaxation)kama mazungumzo ya kawaida.
(2)SAUTI YA KICHWA (FALSETTO/HEAD VOICE).
Imeitwa jina hili kwa sababu hutokea kwa milindimo ya juu/(RESONANCE) na mvutano wa mishipa ndani(eneo) la kichwa.mlio wake ni kama mlio wa king'ora (POLICE ALARM)
(3)SAUTI MCHANGANYIKO (MIXED VOICE).
Sauti hii ni muunganiko wa sauti hizo mbili juu za awali (namba moja na namba mbili).Aina hii ya sauti humsaidia muimbaji kuimba sauti za mitetemo ya juu (HIGH PITCHED VOICE).Bila kutoka nje ya ufunguo(KEY).
(4)SAUTI KOROMEO (PHARYNGEAL VOICE).
Hii ni sauti ambayo mara nyingi huwa haifundishwi;mlio wake ni kama sauti ya kichwa (HEAD VOICE+...)iimbwayo na mtu aliye na mafua.
HIVYO sauti hizo tatu za juu ndio sauti kuu kwa muimbaji yeyote duniani.tutakuja jifunza kwa undani wakati na maeneo sahihi ya kuzitumia.LEO NITA ELEZA juu ya SAUTI ASILI (CHEST VOICE)ambayo kimsingi ina tegemezwa na misuli ya TUMBO.
MUIMBAJI ataweza imba kwa muda mrefu pasi kuchoka haraka,Sauti kukauka na hata kupata maumivu ya kichwa Akijua umuhimu wa kutumia sauti hii Asili naomba niite ya TUMBO japo si jina la kitaalamu.Uimbaji wa namana hii unatumiwa na waimbaji wengi wakubwa wenye mafanikio duniani hususani walio pitia madarasa ya muziki na sauti,ndio maana wanaweza imba LIVE kwa muda mrefu na Sauti zao kuto choka au kukauka.
UKWELI HALISI JUU YA PUMZI KWA MUIMBAJI NA NAMNA YA KUIBAJETI.
*UPUMUAJI sahihi wa mwanadamu ambao ndio unatakiwa utumike kwa muimbaji ni ule tuna uona kwa MTOTO MCHANGA au kwa mtu mzima akiwa na utulivu wa juu (PUMZIKO/AT CONFORT ZONE).Hapa TUMBO hutoka nje pindi avutapo pumzi na kurudi ndani atuapo nje pumzi.Huu ndio upumuaji sahihi anao takiwa pumua muimbaji pindi anapo imba kinyume na hapo tunasema muimbaji huyu hapumui/imba tokea tumboni bali hutoa KIFUANI AU KOONI.Na waimbaji wengi wasio fuata uimbaji huu huchoka mapema na kuto enda mwendo mrefu katika uimbaji na wengine SAUTI zao kupoteza kabisa mvuto.
MAZOEZI YA KUKUZA PUMZI KWA MUIMBAJI
●Mazoezi ni mengi kama kuruka kamba kwa namna ya kufunga na kuachia pumzi kwa njia ya pua tu,KUOGELEA,na KUKIMBIA uwanjani penye mzunguko safi wa hewa.
LEO tuna jifunza ZOEZI moja la kitaalamu duniani ambalo linapendekezwa kiafya kwa muimbaji na lina matokeo ya muda mfupi sana kwa kukuza pumzi na kukaza misuli ya tumbo ya muimbaji na kumuwezesha aimbe (DEEP VOICE)sauti yenye ujazo na mvuto sana.
●ZOEZI; (SHEE SOUND"UNDER BALANCED&RELAXED SHOULDERS).
※HATUA KUFUATA:
Simama wima mabega yakiwa katika hali ya msawazo.VUTA PUMZI ya kutosha hakikisha TUMBO lina toka NJE pindi uvutapo pumzi.
TOA PUMZI kwa mshindo mkuu (HIGH PRESSURE)kupitia mdomo(MENO yakiwa yame umana ya juu nabya chini kutoa mlio "SHIII" huku ukishusha mabega na kuruhusu tumbo kuingia ndani.
HESABU sekunde kwa saa kuanzia SEKUNDE 10~.....Rudia mara kwa mara utaona mabadiliko kwa muda mfupi.Kwaleo ni ishie hapa.SHALOM!!SHALOM!!Uwe na siku njema.

Wako John Shabani:VOCAl Coacher!!.
WASILIANA NASI
SIMU/WHATSAPP :+255716560094
EMAIL; jshabani2011@gmail.com 
"You are blessed"


 SEHEMU YA PILI:
MBINU KUU NNE ZA KUMUWEZESHA MUIMBAJI KUIMBA VIZURI (TONE NZURI) KWA MUDA MREFU PASI KUPATA MAUMIVU YA KICHWA AU KUCHOKA MAPEMA.
..Shalom!!mpendwa msomaji,

Sasa tuna endelea na sehemu ya nyinginei ya somo letu lenye kichwa tajwa hapo juu.Kumbuka tuli ishia kwa kuangalia njia namba moja;UFUNGUZI WA KOO NA ULAINISHAJI WA MISHIPA YA SHINGO NA YA NYUMA YA KICHWA (REMEDY FOR VOCAL FATIGUE).

Leo tuendelee mbele na kuangalia mbinu ya pili.
(2)KUJIFUNZA NAMNA YA KUBAJETI PUMZI NA KUIMBA KWA MSAADA WA MISULI YA TUMBO.
Mpendwa msomaji bila shaka umekuwa ukisikia juu ya umuhimu wa kuwa na pumzi kwa muimbaji na uwenda umewahi jiuliza huku kuimba kwa msaada wa MISULI YA TUMBO kukoje??na kuna tofauti gani na kule kuimba kwa kifuani.Wengi wametoa majina mengi mno juu ya namna ya uimbaji wengine hata kunyosheana vidole na kusema:sauti hiyo haitokei tumboni niya puani au kooni:FUATANA NAMI JUU YA UKWELI HUU!!.
kiuhalisia kuna aina nne za sauti japo tatu ndio maarufu sana na ndio zinazo fundishwa na wengi duniani kwote nazo ni hizi;
(1)SAUTI YA ASILI (CHEST VOICE)
Aina hii ya sauti mitetemo yake hufanyikia kifuani.hutokea mtu akiwa kwenye msawazo (Relaxation)kama mazungumzo ya kawaida.
(2)SAUTI YA KICHWA (FALSETTO/HEAD VOICE).
Imeitwa jina hili kwa sababu hutokea kwa milindimo ya juu/(RESONANCE) na mvutano wa mishipa ndani(eneo) la kichwa.mlio wake ni kama mlio wa king'ora (POLICE ALARM)
(3)SAUTI MCHANGANYIKO (MIXED VOICE).
Sauti hii ni muunganiko wa sauti hizo mbili juu za awali (namba moja na namba mbili).Aina hii ya sauti humsaidia muimbaji kuimba sauti za mitetemo ya juu (HIGH PITCHED VOICE).Bila kutoka nje ya ufunguo(KEY).
(4)SAUTI KOROMEO (PHARYNGEAL VOICE).
Hii ni sauti ambayo mara nyingi huwa haifundishwi;mlio wake ni kama sauti ya kichwa (HEAD VOICE+...)iimbwayo na mtu aliye na mafua.
HIVYO sauti hizo tatu za juu ndio sauti kuu kwa muimbaji yeyote duniani.tutakuja jifunza kwa undani wakati na maeneo sahihi ya kuzitumia.LEO NITA ELEZA juu ya SAUTI ASILI (CHEST VOICE)ambayo kimsingi ina tegemezwa na misuli ya TUMBO.
MUIMBAJI ataweza imba kwa muda mrefu pasi kuchoka haraka,Sauti kukauka na hata kupata maumivu ya kichwa Akijua umuhimu wa kutumia sauti hii Asili naomba niite ya TUMBO japo si jina la kitaalamu.Uimbaji wa namana hii unatumiwa na waimbaji wengi wakubwa wenye mafanikio duniani hususani walio pitia madarasa ya muziki na sauti,ndio maana wanaweza imba LIVE kwa muda mrefu na Sauti zao kuto choka au kukauka.
UKWELI HALISI JUU YA PUMZI KWA MUIMBAJI NA NAMNA YA KUIBAJETI.
*UPUMUAJI sahihi wa mwanadamu ambao ndio unatakiwa utumike kwa muimbaji ni ule tuna uona kwa MTOTO MCHANGA au kwa mtu mzima akiwa na utulivu wa juu (PUMZIKO/AT CONFORT ZONE).Hapa TUMBO hutoka nje pindi avutapo pumzi na kurudi ndani atuapo nje pumzi.Huu ndio upumuaji sahihi anao takiwa pumua muimbaji pindi anapo imba kinyume na hapo tunasema muimbaji huyu hapumui/imba tokea tumboni bali hutoa KIFUANI AU KOONI.Na waimbaji wengi wasio fuata uimbaji huu huchoka mapema na kuto enda mwendo mrefu katika uimbaji na wengine SAUTI zao kupoteza kabisa mvuto.
MAZOEZI YA KUKUZA PUMZI KWA MUIMBAJI
●Mazoezi ni mengi kama kuruka kamba kwa namna ya kufunga na kuachia pumzi kwa njia ya pua tu,KUOGELEA,na KUKIMBIA uwanjani penye mzunguko safi wa hewa.
LEO tuna jifunza ZOEZI moja la kitaalamu duniani ambalo linapendekezwa kiafya kwa muimbaji na lina matokeo ya muda mfupi sana kwa kukuza pumzi na kukaza misuli ya tumbo ya muimbaji na kumuwezesha aimbe (DEEP VOICE)sauti yenye ujazo na mvuto sana.
●ZOEZI; (SHEE SOUND"UNDER BALANCED&RELAXED SHOULDERS).
※HATUA KUFUATA:
Simama wima mabega yakiwa katika hali ya msawazo.VUTA PUMZI ya kutosha hakikisha TUMBO lina toka NJE pindi uvutapo pumzi.
TOA PUMZI kwa mshindo mkuu (HIGH PRESSURE)kupitia mdomo(MENO yakiwa yame umana ya juu nabya chini kutoa mlio "SHIII" huku ukishusha mabega na kuruhusu tumbo kuingia ndani.
HESABU sekunde kwa saa kuanzia SEKUNDE 10~.....Rudia mara kwa mara utaona mabadiliko kwa muda mfupi.Kwaleo ni ishie hapa.

Wako John Shabani:VOCAl Coacher!!.
WASILIANA NASI
SIMU/WHATSAPP :+255716560094
EMAIL; jshabani2011@gmail.com 

"You are blessed"

MAFUNZO MAALUM YA UIMBAJI AU SAUTI NA KOCHA JOHN SHABANI

YALIYOMO KATIKA MAFUNZO HAYA
  • PUMZI
  • UTULIVU
  • MKAO WA MWIMBAJI
  • SAUTI
  • AFYA YA SAUTI
  • MAZOEZI
 MWALIMU WA SAUTI 
Naitw John Shabani. Mwimbaji, Mtunzi wa nyimbo na Mwalimu wa sauti.
Nimefanya uchunguzi au utafiti kwa zaidi ya miaka kumi juu ya SautiAfya ya Sauti na
Mazoezi ya sauti. Uchunguzi wangu umenipatia taarifa zilizothibitishwa na madaktari
wa sauti na walimu wa sauti ulimwenguni.

Nimeandaa mafunzo haya kwa lugha ya kiswahili J Vocal Course katika misingi ya taarifa nilizo kusanya, uzoefu wangu katika tasnia hii ya Uimbaji na mafunzo niliopata. Ni imani yangu kuwa kozi hii itakusaidia mwimbaji unayeanza kuimba kwa mara ya kwanza lakini pia kwa wewe uliyekuwa ukiimba kwa muda mrefu.

Kozi hii ingekugharimu zaidi ya laki tano au zaidi kama ungeenda kusoma katika
vyuo au shule za Muziki. Lakini nimeiandaa na kuletea kama mchango wangu ili kukiboresha kipaji chako. Unachokihitaji ni muda wako na juhudi zako pekee. Lakini ukiguswa kuchangia maono au mkakati huu basi usisite kufanya hivyo. Vilevile unaweza kupitia masomo haya kwenye blogu yangu www.johnshabani.blogspot.com, au ukajiunga na group letu la whatsapp lakini pia unaweza kuhudhuria masomo yanayoendelea Dar es salaam kwa waliopo Tanzania.

Kwa maswali zaidi au mchango wowote usisite kunitumia barua pepe
Jshabani2011@gmail.com au Whatsapp: +255716560094.
Ahsante na Karibu.
JINSI YA KUTUMIA
Maelezo na maelekezo yote ya kozi hii yanapatikana katika Makala hii, kwenye blog yangu blogu, darasa langu la mafunzo ya sauti, kwenye page zangu za facebook  na kwenye group langu la whatsapp
inayofahamika kama Swahili Vocal Course 
Vilevile Videos za mazoezi pamoja Audio za ala za muziki kwa ajili ya mazoezi
(Workouts) zinapatikana katika.
Ili upate mafanikio kutoka kwenye kozi hii, Usiwe na haraka ya kumaliza. Kozi hii
italeta mafanikio makubwa endapo kama utakuwa mvulivu na usie kimbilia matokeo
ya haraka. Fuata mfuatilio huu kwa ajili ya mafanikio makubwa;

UTANGULIZI
Kuimba ni nini?
Kuimba ni kitendo cha kutumia sauti kutengeneza ala za muziki kwa maneno. Mfano
mzuri ni kile tunachojifunza darasa awamu ya kwanza yaani Ala za muziki, tunaweza kuzitumia ala za muziki kwa maneno (do-re-mi-fa-so-la-ti-do) na hiyo ndio maana ya Uimbaji. 
Kuimbapia ni kitendo cha kufikisha ujumbe kwenye jamii kwa kutumia maneno na ala za
muziki. Uimbaji ni njia yenye nguvu sana kuleta matokeo katika jamii. Na hii ndio
maana waimbaji hutumia sauti zao kuzungumza kwa niaba ya wanyonge kuleta
mabadiliko katika siasa, dini na kadhalika.

Je naweza kuimba?
Umewahi au unajiuliza swali hili? Jibu ni kwamba mtu yeyote anaeweza kutamka
maneno, na kusikia ala za muziki anaweza kuimba. Kinachohitajika ni mafunzo na
mwongozo sahihi. Ni kweli kwamba kuna waliozaliwa na kipaji cha uimbaji, lakini
kuna waimbaji wengi waliojifunza kuimba na sasa wana mafanikio makubwa katika
tasnia hii. Hivyo haijalishi ni kundi lipi upo, na wewe pia utafanikiwa ukiamua.

Faida za Uimbaji
Zipo faida nyingi sana za kuimba, inategemea na malengo yako ni nini. Kuimba ni
starehe, kufikisha ujumbe kwa jamii, chanzo cha kipato, kupata marafiki lakini pia
Uimbaji huweza kutumika kwa ajili Ibada.

Jitayarishe Kuimba
Jambo la kwanza na la msingi ni Kujenga Mtazamo Mpya. Inawezekana umekatiliwa
kuimba mara nyingi na wengine wamekukatisha tamaa kuwa huwezi kuimba.
Imefikia hatua ukaanza kukiri kwamba huwezi kuimba. Ili ufanikiwe katika kozi hii ni
lazima kwanza ubadilishe mtazamo wako na ujiamini kuwa unaweza kuimba. Iambie
nafsi yako kuwa “NAWEZA KUIMBA”. Mafanikio ya kitu chochote huanza kwenye
fikra na saikolojia zetu. Ni muhimu sana ukaanza na saikolojia yako.


PUMZI KWA AJILI YA WAIMBAJI
Kama ilivyo Injini kwa gari, ndivyo Pumzi kwa uimbaji. Pumzi ya kutosha itawezesha
mwimbaji kuimba mstari mzima pasipo kukwama. Inawezekana umewahi
kuimba na ukashindwa kumaliza mstari katika wimbo kwa sababu ya ufinyu wa
Pumzi. Katika sura hii utajifunza mazoezi ya jinsi ya kupumua wakati wa kuimba na
kujiongeza pumzi ya kutosha. Kabla ya kujifunza sura nyingine ni muhimu sana
kufahamu kuhusiana na pumzi; Msingi wa Uimbaji.

MAZOEZI YA SEHEMU YA KWANZA
Katika kipengele hiki utajifunza jinsi ya kupumua wakati wa kuimba. Waimbaji na
walimu wa sauti wanaposema “Imbia kutoka Tumboni”? Wanachokimaanisha ni
pumzi yako katika uimbaji ianzie tumboni Na hiki ndio kitu cha kwanza
tutakachojifunza katika sura hii

Zoezi 1
Fuata Maelekezo yafuatayo ili kukusaidia kukufahamu jinsi ya kupumua ipasavyo;
 Weka mikono juu yako ya tumbo lako.
 Kisha toa hewa kwa kutumia mdomo wako ukisema (shiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii)-kama vile
unanyamazisha kelele. Unavyotoa hewa, ndivyo ambavyo tumbo linavyoingia
ndani. Hakikisha unatoa hewa yote pasipo ya kukata.
 Kisha ingiza hewa taratibu kwa kutumia pua. Tumbo litajazwa na hewa, hivyo
litaonekana kuwa kubwa.
Ulipokuwa ukifanya hili zoezi umeona unapotoa hewa nje, tumbo linaingia ndani. Na
unapoingiza hewa ndani, tumbo linatoka nje. Rudia Zoezi 1 mara 10.

Zoezi 2
Katika zoezi hili utajifunza jinsi ya kupumua katika Uimbaji wakati wa hali mbalimbali.
Fuata maelekezo yafuatayo;
 Ingiza hewa kwa kutumia pua (mara tano pasipo kutoa hewa). Kisha toa hewa
ukiwa umefunga mdomo. Rudia mara nne.
 Ingiza hewa kwa kutumia pua (mara tano pasipo kutoa hewa). Kisha toa hewa
ukiwa umefungua mdomo. Rudia mara nne.
 Ingiza hewa kwa kutumia pua (mara tano pasipo kutoa hewa). Kisha toa hewa
kwa kuguna. Rudia mara nne.
 Ingiza hewa kwa kutumia pua (mara tano pasipo kutoa hewa). Kisha toa hewa
kwa kusema “Ahhhhhhhhhhhhh”. Rudia mara nne
Zoezi 3
Katika daraja la kwanza, hili ni zoezi la mwisho na katika zoezi hili utajifunza jinsi
kupumua wakati wa Uimbaji. Katika zoezi jitahidi uwe na saa au simu yako
ilikuhesabu sekunde unazotumia wakati ukitoa hewa. Fuata maelekezo yafuatayo;
 Ingiza hewa mpaka ambapo Tumbo litakapo kuwa limejaa hewa ya kutosha.
 Bofya “Anza” kwenye stop watch au simu yako, kisha toa hewa kwa kutumia
“ssssssssssssssssss” pasipo kukwama mpaka utakapofikia mwisho wako.
 Bofya “Simama” pale ambapo pumzi yako imekata.
 Tazama ni sekunde ngapi. Weka katika rekodi yako kwa ajili ya matumizi ya
baadae.
Kwa kawaida kwa mtu anaeanza kufanya zoezi hili kwa mara ya kwanza hufikisha
sekunde 15 – 20. Kama umefika hapo hongera sana, kama hujafanikiwa kufika hapo
pia usiwe na wasiwasi utakapoendelea kufanya mazoezi kwa juhudi utafanikiwa.
Sekunde unazopaswa kufikia ni 40 – 45, Uvumilivu na juhudi vyote vinahitajika.

MAZOEZI YA PUMZI SEHEMU YA PILI
Katika sehemu hii tutakupatia mazoezi kwa ajili ya kujiongezea pumzi ya kutosha
kwa ajili ya Uimbaji. Naamini mpaka sasa utakuwa umepitia sehemu ya kwanza na
kufanya mazoezi yaliyotolewa katika sehemu ya kwanza. Kwa sababu mazoezi
katika sehemu ya kwanza ni msingi katika tunachoenda kujifunza sasa.
Fuata maelekezo yatakayotolewa 
Kumbuka: Kabla ya kufanya mazoezi yafuatayo , hakikisha kwanza
umepasha mwili wako tayari. Unaweza kuupasha mwili wako kwa kukimbia, kuruka
kamba au kuruka ruka. Kisha fanya mazoezi utayapatiwa katika ;
1. Fungua tumbo.
2. Fungua pande za tumbo.
3. Fungua nyuma.

UTULIVU
Be comfort when you are singing, ili kupata matokeo mazuri,  mwili wako, akili yako, hisia zako, mawazo yako vyote vielekezwe kwenye hicho unachokifanya. Jambo linguine tawala sauti unayoimbia (master the sound in singing). Usipende kuimba kikawaida kawaida, shawishi wanaokusikiliza wakukubali. Lakini pia epuka sana kupayuka hata kama unaimba in high. Badala ya kuimba in  head voice be smooth, lainisha sauti.


MKAO WAKATI WA KUIMBA
li kutoa sauti nzuri ni muhimu sana kufahamu jinsi ya kuweka mwili wakati wa
uimbaji. Mwili wako unapokuwa hauko katika mkao mzuri ni vigumu kupumua
ipasavyo na hii inaweza kupelekea sauti yako kupoteza nguvu na uhalisia wake.
Jinsi unavyoweka mwili wako wakati wa kuimba kunaweza kufanya sauti yako kuwa
bora au kupoteza ubora wa sauti. Mkao usio sahihi hufanya upumuaji kuwa mgumu,
sauti kuwa hafifu na minyifu. Kwa upande mwingine, Mkao usio sahihi wakati wa
uimbaji unaweza kukuletea maumivu katika mwili wako na matatizo mengine ya
kiafya.
Katika sura hii utajifunza mkao (posture) sahihi ya kutumia wakati wa uimbaji.
Ili kuwa na mkao sahihi hakikisha vitu vifuatavyo;
1. Usiinue shingo yako juu (Never sing with your Neck up). Wengi tumeambiwa ukitaka sauti yako itoke vizuri wakati wa uimbaji inua shingo. Hapana, kee your neck streit. Kuimba sio kujiumiza au kujilazimisha.
1. Hakikisha kichwa kimetazama mbele.
2. Uti wa mgongo umenyooka.
3. Usiinue Kifua juu sana.
4. Usiinue mabega.
Katika mchoro ufuatao hivyo ndivyo ambavyo mifupa hupangiliwa pale ambapo mtu
hutumia mkao sahihi.


Kama unataka kujiona unavyosimama wakati wa Uimbaji unaweza ukawa unafanya
mazoezi mbele ya kioo ili kujitazama na kufanya marekebisho pale unapotambua
hauko sawa. Hii itakusaidia kujitathmini na baada ya muda fulani kupita utajikuta sio
jambo la kufikiria tena bali unalifanya pasipo hata ya kujitazama.
Hivyo katika mazoezi yako kipaumbele chako kiweke katika kutengeneza
mkao ulio sahihi wakati wa Uimbaji.

SAUTI
Aina za sauti
Ni vizuri kufahamu aina ya sauti yako. Yapo makundi mengi sana ya sauti
ketegemeana na kigezo cha ugawanyishi kilichotumika. Katika kozi hii
tumegawanyisha sauti katika makundi manne ambayo ni Soprano, Mezzo, Tenor na
Bass.
Soprano, ni sauti nyembamba ya juu ya mwanamke. Mezzo ni sauti nzito ya chini ya
mwanamke. Tenor ni sauti ya juu ya Mwanaume na Bass ni sauti ya Chini ya
mwanaume. Uwezo wa kuimba funguo mbalimbali hutokana na aina za sauti
uliyonayo.

Rejista za sauti - vocal register (range of tones in human voice produced by a particular vibratory pattern of the vocal folds)
Zipo rejista tatu za sauti ambazo ni muhimu kufahamu kila moja kivyake vilevile jinsi
ya kuzitumia katika uimbaji. Rejista ya kwanza ni Sauti ya kifuani (Chest Voice),
Sauti ya Utosini (Head Voice) na Sauti Mchanganyiko (Mixed Voice).

Toni ya Sauti
Waimbaji wawili wanaoimba katika ufunguo mmoja wanasikika tofauti – Sababu ni
toni ya sauti. Unaposikiliza redio ni rahisi kufahamu nani ameimba wimbo fulani kwa
kusikiliza toni ya sauti. Toni ya sauti ni muhimu sana kwa sababu hiyo ndiyo
itakutofautisha na waimbaji wengine.
Jinsi ya kutengeneza Toni ya kipekee
Mwenyezi Mungu aliweka upekee katika sauti ya kila mtu. Tatizo ni kwamba wengi
wetu wanajikuta wakiiga sauti za waimbaji wengine na hatimaye kupoteza upekee
wao. Kama utaiga sauti ya mwimbaji mwingine basi utatunyima (mashabiki zako)
ladha ya sauti yako.
Jiamini una sauti ya kipekee, fuata maelekezo tutakayokupatia ili kufungua ule
upekee wa sauti yako katika kiwango cha juu.
Zoezi la toni ya sauti (#1) - Katika zoezi hili utafungua toni ya sauti yako na
baada ya muda utajikuta ukiimba kwa kutumia sauti yako. (Fuata maelekezo
yaliyopo kwa wale  )
Zoezi la toni ya sauti (#2) Resonance – Katika kipengele hiki utaifunza sauti
yako kujaa na kuwa na nguvu. Hata kama huimbi pasipo ya kipaza sauti,
utaweza kujaza chumba kwa sauti yako
AFYA YA SAUTI
atumizi mabaya ya sauti au vitu ambavyo huleta madhara kwenye sauti
inaweza kupoteza ubora wa sauti yako baada ya muda fulani. Kama unaimba
kanisani au kwenye sherehe na matamasha kuzingatia swala la afya ya sauti ni
jambo ambalo si la kukwepa.
Vipo vitu vingi ambavyo si sahihi na watu wanafanya kisha hawaoni madhara yake
kwa wakati huo lakini ndani ya kipindi fulani matokeo hutokea. Ni lazima uwe makini
kwenye vitu unavyofanya kwa maana vinaweza kupelekea kupotea kwa ubora wa
sauti yako katika kipindi kifupi au muda mrefu.
Vifuatavyo ni vitu hatari kwa ajili ya Afya ya sauti yako
Alkoholiki: Hupanua mishipa yako ya damu, hivyo sio nzuri kwenye kodi za
sauti yako.
Moshi wa sigara: Moshi wa sigara hupeleka madhara hasi kwenye koo. Hivyo
jizue kuvuta sigara au kuvuta moshi wa sigara kutoka kwa mtu anaevuta.
Dawa: Dawa nyingi kwa ajili ya kuponyesha magonjwa mbalimbali hukausha
koo. Hii hupelekea koo kuwa kavu jambo ambalo si jema katika uimbaji.
Muulize daktari wako kama kuna uwezekano wa kubadilisha mpangilio wa
unywaji dawa katika kipindi ambacho utakuwa unatumia sauti yako sana.
Kama umekunywa dawa na unahitajika kuimba hakikisha unakunywa maji
mengi ya kutosha.
Vyakula: Baadhi ya vyakula vina matokeo hasi kwenye sauti. Vyakula
vinavyotokana na maziwa (dairy products) sio vizuri kwenye sauti kwa sababu
vinatengeneza mucus kwenye koo lako nah ii itakufanya kusafisha koo lako
kila mara ambayo haishauriwi kwa mwimbaji kufany hivyo. Ni muhimu pia
ukafahamu ni vyakula gani ambavyo vinakuwa na madhara hasi kwenye sauti
yako ili usivitumie wakati unapokuwa na uimbaji wa muda mrefu.
Kusafisha koo: Kama ni tabia yako kusafisha koo lako kila mara, leo ni vyema
ukaacha hiyo tabia. Mara nyingi waimbaji hujikuta wakisafisha makoo yao
kwa sababu ya mucus ambayo imekaa kwenye koo wakijitayarisha kwa ajili
ya uimbaji.
Vifuatavyo ni vitu muhimu kwa ajili ya afya ya sauti yako
Kuna vitu vitatu cha kwanza KUNYWA MAJI, cha pili KUNYWA MAJI na cha
tatu KUNYWA MAJI. Maji ni muhimu sana kwa sauti yako. Hakikisha
unakunywa maji ya kutosha.
Pumua kama muimbaji wakati wote hata ukiwa unazungumza na simu.
Hakikisha unakaa katika mkao mzuri kama ilivyoshauri katika sura ya pili.
Unaweza kutumia sauti yako yote pale unapotaka kusikika lakini hakikisha
hupigi mayowe ni hatari kwa sauti yako.
Hakikisha unapata muda wa kutosha wa kulala. Hakikisha una masaa 6 – 8
ya kulala.

MAZOEZI 
Mwana riadha hukimbia, Wachezaji wa mpira hucheza mpira, na wewe
mwimbaji unachopaswa kufanya ni kimoja KUIMBA. Wachezaji imara na
wanariadha makini hufanya mazoezi yakutosha kila mara. Vilevile kama unataka
kuwa mwimbaji makini lazima ufanye mazoezi ya kutosha kila wakati. Katika sura hii
utajifunza jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya mazoezi, kuchagua mahali pa kufanyia
mazoezi na jinsi ya kufanya mazoezi.
Katika kozi hii tumekupatia mazoezi mbalimbali kama vile mazoezi ya pumzi,
mazoezi ya toni ya sauti na mazoezi ya matayarisho. Fanya mazoezi haya kila siku,
asubuhi, mchana au jioni wakati wowote ambao utafaa kwako.
Fuata maelekezo haya wakati wako wa mazoezi
Kama unataka kufahamu mpangilio mzuri wa mazoezi ambao unaweza kuutumia
wakati wako wa mazoezi, unaweza kutumia mpangilio huu ufuatao:
1. Pasha mwili wako tayari kwa ajili ya mazoezi (Body Warm Up). Ili kufanya
mwili wako tayari kwa ajili ya mazoezi ni muhimu ukaanza kukimbia au kuruka
kamba (kurukaruka).
2. Fanya mazoezi ya pumzi yaliyopendekezwa katika katika kipengele cha pumzi.
3. Fanya matayarisho ya sauti (Vocal Warmup). Unaweza kutumia mazoezi
kabla ya uimbaji au mazoezi ya sauti. (Tazama Video ya matayarisho ya sauti
kwa ajili ya Uimbaji ) – katika blogu ya Swahili Vocal Course.
4. Fanya zoezi la toni ya sauti ulilojifunza kutoka sura ya tatu.
5. Fanya zoezi la kuimarisha rejesta ya utosi na rejesta ya kifua ( kama
ulivyojifunza katika sura ya tatu)
Mazoezi hayo yanaweza kuchukua dakika 20-30 ndani ya siku. Kumbuka mazoezi
hayo ni kwa ajili ya kuimarisha sauti yako, mazoezi ya nyimbo bado ni muhimu sana
kwa ajili ya maandalizi ya uimbaji mbele za watu au kurekodi.
Vitu ambavyo si vya kufanya wakati wa mazoezi;
Usifanye zoezi ambalo hufahamu linasaidia nini katika sauti yako, Usifuate mkumbo.
Hakikisha unafanya zoezi ambalo unafahamu linakusaidia nini katika sauti yako.
Nimekutana na watu wengi wanaodhani mazoezi ya kuimba ni kupiga kelele pekee
ufukweni mwa bahari. HAPANA, ni zaidi na hayo. Usipohamu kwa nini unafanya
zoezi fulani itakuwia vigumu kufahamu maendeleo yako ya sauti.

MENGINEYO
  • Imbia kwenye key yako, utakuwa huru zaidi.
  • Nenda na mapigo ya muziki bila kutoka nje ya ufunguo(key)
  • Angalia mitetemo yako (kama ni wimbo unahusu mitetemo), iwe ya kiasi.
Ushauri
Pamoja na kwamba mazoezi ya kuimba si kupiga kelele pekee ila tunakushauri uwe
na mahali au muda ambao huwezi kusumbua mtu mwingine. Vitu ambavyo
vinaweza kukutoa katika hali ya mazoezi, vitu kama vile simu, TV, Internet na
chochote ambacho kinaweza kuondoa focus yako wakati wa mazoezi .


HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP