Ebu tuangalie misingi ya utunzi wa
nyimbo
JE UNAWAJUA WATU MUHIMU KWENYE
KWAYA, BENDI AU KWA MWIMBAJI BINAFSI?
Ili wimbo uweze kukamilika huwa
unakuwa na vipengele kadhaa ndani yake.
-
Kuna maneno au mashahiri, au kwa lugha ya
siku hizi ‘mistari’ na kwa kiingereza Lyrics.
Nyimbo inaweza kuandikwa na mtu mmoja au wawili au Zaidi,
tunawaita kwa kimombo Song writers. Mwandishi wa nyimbo anayeweka maneno ya
wimbo (lyrics) eitha kwa kwa maneno ya kawaida au kwa nota huitwa Lyricict
-
Mistari huhitaji kupewa sauti ya kuimbia, Melody.
Na huyo anayebuni au kutengeneza melody huitwa Composer. Lakini kama mtu
atatengeneza vyote nilivyotaja hapo juu, kwa ufupi anatambulika kama mwandishi
wa nyimbo (songwriter)
-
Baada ya hapo hutengenezwa arrangement, au
mpangilio wa muziki huo, nini kinakuja wapi, waimbaji waimbe vipi na kujumlisha
kazi zote hizi unapata wimbo mmoja.
Kwa uzoefu wa bendi au kwaya zetu,
mara nyingi, Lyrics huletwa na mtu mmoja, anaweza akaleta mistari yenye melody
au akaleta mistari peke yake na kutaka msaada wa wanamuziki wenzie watafute
melody. Kazi inafuata ya arrangement pia hufanywa kwa ushirikiano na hatimae
kukapatikana wimbo ambao kwa utamaduni wetu huwa tunatangaza kuwa mtunzi ni
yule aliyekuja na mistari.
Si kila mtu ana kipaji cha kutunga,
japo hiyo ndio imani ya wengi kuwa kila anaejua kuimba hujua kutunga. Waimbaji
wengi maarufu duniani waliimba nyimbo zilizotungwa na wengine, na halikadhalika
si kila anaetunga anajua kuimba, watunzi hata wa mashahiri huwaachia watu
wengine waghani mashahiri yao, mtunzi akilazimisha kuimba wakati hana kipaji
hicho matokeo ni madudu tu na hali kadhalika muimbaji asiye na kipaji cha
kutunga aking’ang’ania kutunga kipawa chake cha kuimba kinaweza kisionekane
kutokana na utunzi kuwa hafifu.
Na hali kadhalika si kila mtu ni arranger, tatizo ni pale asiekuwa na kipaji
anaamua kufanya hiyo kazi, kinachotoka hakieleweki kama kinakwenda au kinarudi.
Hali hii ipo pia kwa waimbaji binafsi(solo artist), wanataka kujionyesha
wanajua kila kitu au wanafanya kila kitu, haiwezekani. Kuna wakati unahitaji
aina fulani za tungo kutuko kwa
watunzi
wazuri, una hitaji mwalimu au mtu wa kukuongoza kuwa bora zaidi, lakini pia
zaidi ya hilo, unamwitaji arranger. Kama wewe umebahatika kufanya kila kitu
basi mshukuru Mungu kwa hilo.
Kama nilivyosema awali katika bendi arrangement huwa ni mchango wa mawazo,
lakini ukifanya utafiti kidogo utagundua hata katika kazi inayoonekana ya
kikundi kuna mtu au watu ndio wanaoongoza nini kipigwe wapi. Nichukulie mfano
wa bendi zilizopita, katika kutaka kujua undani wa jambo hili, nilipata maelezo
ya kina kutoka kwa mkongwe wa muziki wa dansi hapa nchini, ndugu yetu John
Kitime. Yeye anasema “Katika bendi nilizopitia kama vile Orchestra Mambo Bado,
Orchestra Makassy au Vijana Jazz enzi hizo kulikuwa na mtu ana sauti ya mwisho
kuhusu arrangement”
Kupendwa kwa wimbo ni mkusanyiko wa haya niliyoyataja hapo juu. Nyimbo
nyingi zinazopendwa sasa hazitachukua muda kusahaulika kutokana na kuwa na
arrangement hafifu sana. Mfumo wa sasa wa waimbaji kujaza wimbo wote bila
kuweko na hata nafasi ya vyombo kutamba ni aina moja ya arrangement, lakini kwa
mtazamo wangu nyimbo hizi zitasahaulika katika kipindi kifupi.
Katika mfumo wa uajiri au utafutaji wa wanamuziki katika vikundi vyetu, umuhimu
hutolewa kwa wapiga vyombo na waimbaji, nadra kusikia mtunzi anatafutwa na
nadra zaidi kusikia anatafutwa arranger, hivyo huwa bahati tu akatokea arranger
mzuri au mtunzi mzuri katika kwaya au bendi na si kutokana na mipangilio. Pia nawajua
arrangers wengi ambao hata wao hawajui kuwa ni arrangers, hivyo ‘majembe’ kama
hayo yakifukuzwa au kuhama kwaya au bendi, basi vikundi hivyo vinaanza
kudorora, na si mara moja nimekuta hata kwaya/bendi zenyewe hazijui kwanini
ghafla kuna ukame wa tungo nzuri, pengine yule msanii aliyeitwa mzigo, kwa kuwa
hakuwa muimbaji mzuri alikuwa ndie arranger bora wa kikundi hicho!!!
Labda niseme kwa kifupi, arrangement ndio ule mpangilio wa kuamua nini
kipigwe na kipigwe wapi. Muziki unasheria za msingi kama vile hesabu.2+2=4, si
nne na nusu wala na robo, arranger anakuwa na kipaji cha kupanga nini na anaweza
kukueleza kwa nini pale kipigwe kinanda na gitaa liwe kimya au pale vipigwe
vyote na kwanini iwe hivyo.
Muziki wetu wa wa kwaya au waimbaji wa siku hizi wakiwamo pia wale wa
Bongoflava, umetawaliwa na waimbaji kwani swala la utunzi wa muziki na arrangement
(kunakotambuliwa kama kutengeneza beat), huachiwa ‘producer’. Ni wazi
ukisikiliza mfululizo wa nyimbo zinazotoka kila siku ni wazi kuwa maproducer
wachache sana wanakipaji cha kuarrange, utasikia vyombo vinalia katika wimbo
bila kuwa na mpangilio wala sababu ya kuwepo, hapa utasikia filimbi, mara
saksafon, mara rimba, mara gitaa. Ninapo yasema hayo, sijawasahau wale
waongozaji wazuri au masoloist, ambao ni watu pekee tena wenye mchango wa pekee
kwenye vikundi vyetu vya uimbaji. Hawa nao wakiondoka huachapengo kubwa sana.
ZANA ZA UTUNZI
Mtunzi au mwandishi wa nyimbo, popote alipo anashauriwa kuwa
na zana muhimu kama; Kifaa chochote cha kurekodia, daftari au notebook na
kalamu. Kwa dunia ya leo, ukiwa na simu yako ya mkononi au tablet inatosha. Kwa
lugha nyingine tunasema; I
kiwa kweli unataka kuchukua uandishi au utuzi wako wako wa wimbo kwa
umakini mkubwa, unapaswa kujenga tabiaya kubeba zana au vifaa vya utunzi/uandishi
wa nyimbo popote ulipo. (
If you want to take your songwriting seriously
and create authentic music, you should do your best to carry songwriting
materials with you everywhere).
UANDISHI WA WIMBO.
MWANZO BORA WA UANDISHI BORA WA WIMBO.
Ifahamike ya kwamba kuna aina nyingi za kuanza
kuandika wimbo, ila njia MAKINI ni ya kuanza na MADA ambayo itakupa JINA/TITLE.
UMUHIMU WA JINA/TITLE/MADA.
1. Jina la wimbo ni moyo wa wimbo.
2. Jina huelezea wimbo mzima.
3. Jina/Mada itakuongoza vyema ktk kuandika
mistari na kukufanya usiandike nje ya mada.
Unda au chagua jina ambalo ni fupi si zaidi ya
maneno matano (5) ili iwe rahisi kukumbukwa na mashabiki hata iwe rahisi
kuiomba redioni au kuisema kwa marafiki au washikaji zao. Juu ya hili unaweza
fanya uchunguzi wa kupitia majina ya nyimbo mbalimbali ili uone ufupi wa majina
ya nyimbo unavyokuwa na madhara chanya kwa mashabiki.
Endelea kufatilia hii kitu tafadhari,na uwape
habari marifiki. Wakati ujao tutaangalia kuhusu INTRO, CHORUS, VERSE, CHORUS, VERSE, CHORUS,
OUTRO
Ukitaka Huduma ya kuandikiwa au kutungiwa limbo mzuri wasiliana namimi mwalimu wak wa Sauti Afrika Masahriki.
Kocha John Shabani