Wimbo ni aina ya sanaa katika Fasihi ambayo
hutumia lugha teule,sauti na kiimbo maalum. Nyimbo nyingi hugawanywa katika
beti(verse) na kiitikio(chorus),pia zipo zenye kuwa na
daraja/kiunganishi(bridge) na kiopoo/ndoano(hook). Pia nyimbo hutumia Ala za
muziki kama vile ngoma,filimbi, gitaa na kinanda.
Ikumbukwe kuwa nyimbo zinaweza kuimbwa na mtu
mmoja au zaidi.
SIFA ZA NYIMBO
1. Hutumia kiimbo au sauti maalum.
2. Huweza kuendana na Ala za muziki.
3. Huimbwa na mtu au watu kwa pamoja au kwa
kupokezana.
4. Hutumia lugha ya mkato.
5. Hurudiarudia maneno ili kusisitiza ujumbe
katika wimbo.
UMUHIMU WA NYIMBO
1. KUBURUDISHA.
2. KUELIMISHA, KUFUNZA, KUONYA NA KUELEKEZA, KULIWAZA,
KUSIFIA KITU AU MTU KATIKA JAMII, KUUNGANISHA JAMII AU WATU TOFAUTI, KUDUMISHA/KUHIFADHI
TAMADUNI ZA JAMII, KUKUZA TALANTA NA SANAA KATIKA JAMII, HUTUMIKA KATIKA MBINU
ZINGINE ZA FASIHI KAMA VILE HADITHI MWISHO NYIMBO HUTUMIKA ILI KUMTUKUZA MUNGU
MUUMBAJI.
Kabla sijaanza kutoa dondoo na maelezo ya
namna au jinsi ya kuandika wimbo/uandishi,ni bora ukapata kujua baadhi ya mambo
kuhusu nyimbo zenyewe na muziki kwa ujumla.
SONG STRUCTURE/MUUNDO WA WIMBO.
Ifahamike kwamba miundo ya nyimbo ipo mingi
ikitegemea matakwa ya msanii au waandaaji wa wimbo husika.
MUUNDO WA NYIMBO ni mpangilio wa viunda wimbo
katika mfutatano wa kujirudia. Hapa naongelea
1.
ITRODUCTION/ITRO/MWANZO/UTAMBULISHO/UINGIAJI
2. KIITIKIO/CHORUS
3.VERSES/BETI
4.UTOKAJI/OUTRO/UMALIZIAJI/ENDING.
Viunda wimbo hivi hupangiliwa kulingana msanii
anataka wimbo wake upangiliwe vipi. Ifuatayo ni mipangilio miwili pendwa na
bora kutumiwa,ambayo ni;
1. Intro-chorus-verse-chorus-verse-
chorus-outro.
2.
Intro-verse-chorus-verse-chorus-verse-chorus-outro.
INTRO NA OUTRO.
Intro ni mwanzo wa wimbo, ni sehemu fupi ya
mwanzo wa wimbo ambayo mara nyingi huwa na mistari minne tu. Mara nyingi hakuna
vionjo Vingi vya midundo ni sehemu iliyo poa. Hapa ni sehemu utaaamua wimbo
wako uanze vipi.
Outro ni sehemu ya mwisho ya wimbo au mwisho
ambapo pia utaamua wimbo wako uishie vipi,mara nyingi ni baada ya
kiitikio/chorus kurudiwa kwa mara ya mwisho au baada tu ya ubeti/verse ya
mwisho inategemea na maamuzi yako msanii.
VERSES/BETI
Hiki ni kifungu kimoja cha shairi ambacho kina
uzani sawa kutokana mpangilio wa vina vyako. Unaweza kuwa na verse yenye
mashairi ya kimapokeo/yanayofata sheria za uandishi au verse yenye mashairi
huru/ya kisasa/yasiyofuata sheria ili mradi yalete maana.
Hii ni sehemu ambayo stori yote ya wimbo
huelezewa ni hapa ambapo unatakiwa kudadavua kinagaubaga ujumbe wako ukiendana
na chorus/kiitikio chako pamoja na jina la wimbo wako maana ndio hubeba taswira
ya beti/verse zako.
Mistari 16(sixteen bars) hutengeneza verse
moja katika nyimbo mbalimbali ila sana za HIPHOP. Unaweza kuwa na verse ya
misatari 8(8/eight bars), 12 adi 32,48,40/fourty bars.
Nakushauri andika mistari 16. Na mistari 8
unapoona inatosheleza mahitaji yako.
Wakati ujao tukijaaliwa nitafundisha jinsi ya
kuhesabu mistari kulingana na midundo/beats,vina(vya mwanzo,vya kati,vya
mwisho),pamoja na chorus/kiitikio.
By Vocal Coacher John Shabani
Anaehitaji huduma hii ya kuandikiwa
nyimbo,
mawasiliano yapo apo juu.
0 comments:
Post a Comment