25 November 2019

UANDISHI WA NYIMBO ZA INJILI UNAENDANA SANA NA WITO WA HUDUMA YA MWANDISHI AU MTUNZI.
#Ushauri kwa mtunzi au mwandishi wa nyimbo za Injili.
Usitumie nguvu kubwa kutaka
Kuandika Nyimbo zitakayozependwa au kukubaliwa sana maarufu kama HIT SONGS.
Andika tu nyimbo kwa kadri ya msukumo utokao ndani yako. Imba Uimbaji wako, Tumia sauti yenye upekee na si ya kuigilizia. Fanya mziki wako ambao unaupenda kutoka moyoni.
Kuwa halisi na mkweli kwa Nafsi yako (hisia, dhamira safi, shauku, ufahamu).
#Mashairi au Lyrics huja kutokana na kiwango ufahamu wa Neno la Mungu, Kiwango cha Imani, kiwango cha Ushuhuda na Uvuvio wa Roho.
#Injili ikimgusa hata mtu mmoja ujue tayari imeshafanya kazi yake.
Nyimbo kukubaliwa au kupendwa sana si maamuzi ya mtunzi au mwandishi hata kama yeye binafsi ameupenda au amefurahishwa sana na wimbo huo bado sio tafsiri kwamba watu wataupenda kwa kiwango hicho hicho...
Kuna wakati watu wanaweza penda wimbo ambao mtunzi hakuutiliana maanani sana au matarajio makubwa (hiyo nahitaga surprise).
Wimbo kuwa maarufu kuna maswala mengi huchangia ikiwemo na promotion (kuutangaza sana).
Ila wimbo kuishi muda mrefu utatokana na kitu ambacho huo wimbo umebeba. Kiasi gani watu wanaupokea na kuguswa mioyo au kubarikiwa na wimbo husika. Ile Impact ambayo wimbo umesababisha ndio husababisha nyimbo ziishi muda mrefu sana zikipendwa bila kuchuja.
Ujumbe wake na maudhui yake vina nafasi kubwa.
Kiuhalisia ni kwamba nyimbo za Injili hazipaswi kuchuja au kupitwa na wakati kwa kuwa ni Injili Kamili na Ni Neno la Mungu.
Hivyo nyimbo za Injili zinatakiwa zishibe Neno la Mungu. Zimtukuze Mungu na Kumtangaza Yesu Kristo.

Usiache pia kufuatilia masomo wangu ya Sauti na kuyazingtia. Kumbuka una kuimba kupitia kiapaji (talent), kwa kupata ujuzi (skill) na kuimba kwa uptake au kupakwa (anointing). Sasa mwimbaji wa kipaji au ujuzi anaweza akawafurahisha watu, akagusa watu lakini asiguse mbingu kwani wengi wanachofanya ni kutoa burudani lakini maisha yao ni machafu. Usishanga mtu katoka kujirusha guest house au kapigilia bia yake au kilevi chochote akita na mzuka huo akapewa nafasi kwasababu ya kujulikana kwake akaimba au kutuongoza katika  uimbaji uliojaa uzinzi na ulevi.

Lakini uimbaji uliopakwa na Mungu mwenyewe umejaa hofu, neema, uponyaji, kicho na Kibali cha mbingu.
Pamoja na upako bado nashauri waimbaji kupata ujuzi kwa watu sahihi wenye uzoefu au waalimu wa sauti, ni muhimu sana


0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP