Michelle Obama akiwa ameshikilia bango akiungana na dunia katika kampeni ya kuwarudisha wanafunzi waliotekwa huko Nigeria
Mamia ya watu nnje ya ubalozi wa Nigeria huko Marekani, wakilalamikia serikali kutokuongeza bidii katika kuhakikisha wanafunzi wa kike waliotekwa wamerudishwa salama
Moja ya kati
ya habari kubwa dunia, ni ile ya kutekwa kwa wanafunzi huko Nigeria baada shule
ya mabweni ya wasichana kushambuliwa katika jimbo la Borno Kaskazini Mashariki
mwa nchi hiyo huku wasichana wakitekwa nyara.
Wazazi
wanasema kuwa zaidi ya wasichana miambili wametekwa nyara na washambuliaji hao. Kampeni hiyo ikiambatana na maandamano imefanyika karibu nchi mbalimbali duniani.
Taarifa zinazohusiana
Washambuliaji
wanaaminika kuwa wanachama wa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram.
Utekaji nyara huo ulifanyika usiku wa manane katika shule ya Chibok Kusini mwa
mji wa Borno , karibu na mpaka na Cameroon.
Inaarifiwa
wasichana 300 walikuwa wanajiandaa kwa mitihani yao. Mmoja wa wasichana
alifanikiwa kutoroka na aliambia BBC kuwa walikuwa wanalala wakati walipovamiwa
na wanaume waliokuwa wamejihami.
Waliowashambulia
wanaaminika kuwa wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Wanaume
hao waliingiza magunia ya chakula katika malori yaona kuwaamuru wasichana
kupanda lori hizo.
Wasichana
15 walifanikiwa kutoroka baada ya lori walimokuwa kukumbwa na hitilafu.
Wakazi wa
kijiji cha Chibok wanasema kuwa walisikia milipuko kadhaa huku nyumba 170
zikiteketezwa.
Vyombo
vya habari nchini humo vimeripoti kuwa wanajeshi wawili waliuawa huku mali
ikiharibiwa wakati wa shamblizi hilo mjini Chibok.
Ni wito
wetu kuunga mkono kampeni hii na zaidi kumuomba Mungu ayanusuru maisha ya
wanafuzi hao.
Mungu
ibariki Nigeria,
Mungu ibariki Afrika,
Mungu inusuru Dunia na matukio ya
kutisha!
0 comments:
Post a Comment