alipokua ziarani huko mashariki ya kati
Mkuu
wa Kanisa Katoliki, Papa Francis, amewasili Roma baada ya kukamilisha
ziara yake ya siku tatu Mashariki ya Kati ambapo alisema kuwa tabia ya
baadhi ya mapadri Wakatoliki waliokuwa wakiwanyanyasa watoto wadogo
kingono kanisani inaweza kulinganishwa tu na misa ya Mashetani.
Baba
Mtakatifu alifanya ziara ambayo ilihudhuriwa na maelfu ya watu wa imani
tofauti katika eneo hilo na wachambuzi wengi wamesema kuwa imekuwa ya
kufana.
Wengi
wanasema kuwa Baba Mtakatifu kulinganisha vitendo vibaya vya ngono
walivyofanyiwa watoto na mapadri na misa ya mashetani ni lugha nzito
hasa ikitambuliwa kuwa tayari Papa Francis amewahi kuomba msamaha kwa
vitendo hivyo kote duniani.
Vitendo hivyo vimeharibia sifa Kanisa Katoliki kwa muda mrefu sasa.
Taarifa
kutoka makao makuu ya Papa yanasema kuwa kwa mara ya kwanza tangu yeye
achukue wadhifa wake anatarajiwa kukutana na wale walionyanyaswa na
mapadri kingono.
Wakatoliki
wengi walikasirishwa na vitendo hivyo na wamefurahi kuwa Papa anaweza
kuomba msamaha na kisha akutane na walioathirika na wengi wanasubiri
kusikia atakachowambia atakapokutana nao.
Chanzo BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment