Chama hicho kijulikanacho kwa jina la Chama cha Wajane Tanzania
(Tanzania Widows Association - TAWIA)
lengo lake kuu ni kuwaweka wajane pamoja, ili kutambuana, kufahamiana,
kujua changamoto mbalimbali anazopitia mjane, na kutafuta ufumbuzi wa kutatua
changamoto hizo. Ikiwemo kusomesha
watoto, elimu ya sheria, afya, saikologia, biashara na ujasiriamali. Vilevile
chama kitajihusisha na kutoa elimu kwa jamii juu ya mjane, iwatambue wajane,
kuwapenda, kuwathamini na kuwasaidia kwa namna moja ama nyingine, pia kujitoa
kwa hali na mali kusaidia kupambana na changamoto anazopitia mjane.
Wajane wkieleza changamoto zinazowakabili Msaada wa nguo zilizotolewa na mfadhili
Pia chama kitasimamia sheria inayotetea haki za mjane Tanzania, ikiwemo
hati ya mirathi na usimamizi wa mali za familia baada ya kifo cha mume wa
mjane. Hivyo chama hiki kitarejesha
matumaini mapya kwa mjane, na wajane watarajiwa. Pia kwa namna moja au nyingine, kujihusiha na
haki za mgane na watoto walioachwa na wazazi (yatima).
Zipo changamoto nyingi
zinazotokea pale mwanamke anapofiwa na mume wake. Huo kwake ndio wakati
anaohitaji sana kupendwa na kutiwa moyo na jamii iliyobaki. Lakini kinyume
chake, umekuwa ndio wakati wa kutengwa, kunyanyaswa na ndugu, jamaa na marafiki
waliokuwa wakaribu kabisa kabla ya kifo cha mume wake. Ikiwa ni pamoja na kunyang’anywa mali zilizokuwa za familia,
pamoja na kufukuzwa katika nyumba aliyokuwa akiishi na mume wake. Mjane amekuwa mtu wa kuonewa na kuumizwa
katika jamii, wengi wamenyanyasika kijinsia pamoja na kuathiriwa kabisa
kisaikologia, na hata wengine kupoteza maisha, muda mfupi baada ya kufiwa na
mume wake kutokana na mkandamizo na msongo wa mawazo.
Ikumbukwe kuwa Nchi mbalimbali duniani limeanzisha
vyama vya aina hii. Kwasababu ya kuona changamoto anazopitia mjane, ndio maana
tarehe 22/12/2010, Umoja wa Mataifa uliridhia kila ifikapo tarehe 23 mwezi wa
sita, siku hiyo kuadhimishwa kama siku ya wajane duniani (Iternational Widows
Day).
Hapa chini ni ujumbe wa katibu mkuu wa umoja wa
mataifa kuhusu siku ya wajane duniani:
Message from Ban Ki-moon, Secretary-General, United Nations
On International Widows’ Day, 23 June 2013
We
commemorate the third International Widows’ Day for the hundreds of millions of
women in the world who suffer exploitation, deprivation and exclusion when
their husbands die. Today, we call for stronger action to end widespread
discrimination against widows because no woman should lose her rights when she
loses her husband.
Every human being has the right to live in dignity with
equal rights and opportunities to realize their potential. Yet women and girls
continue to face gender-based violence and discrimination, and this is the case
for many widows around the world.
Many widows are denied their rights—from being evicted from
their homes because they cannot inherit property or the land they live on to
being forced into exploitative and risky sex work to support themselves and
their families because they have no income and nowhere else to turn.
An estimated 115 million widows are currently living in
poverty, and 81 million have suffered physical abuse, some from members of
their own family. Adolescent girls, many of whom have been married off too
early to much older men, are at great risk with very little protection.
It is our collective duty to ensure that widows of all ages
and their children are treated as full and equal citizens, with equal
opportunities for education, participation in the economy and decision-making,
and a healthy life free of violence and discrimination.
We must recognize the role of widows as not only victims of
poverty, conflict and natural disasters but as peace-builders and re-builders
of families, communities and societies. National laws and policies that
protect and promote the rights of widows should be guided by the Convention on
the Elimination of Discrimination against Women and the Convention of the
Rights of the Child.
UN Women works in partnership with governments and with the
private sector, to support the economic empowerment of widows in Asia, Africa
and Latin America.
Moja ya mambo ambayo chama kimeanza kuyatekeleza
mapema tu baada ya kusaidiwa kupata ofisi ya muda, ni mafunzo mbalimbali
yanayotolewa bure kwa wajane na watoto wao.
Mafunzo hayo ni pamoja na kujifunza
kompyuta, ushonaji, lugha, mapishi, ujasiriamali n.k. Mafunzo hayo yanatolewa
bure hapohapo ofisini. Pia wajane wenye mahitaji madogomadogo kama mavazi na chakula
wamekuwa wakisaidika mara moja. Pia mkakati wa watoto wa wajane kupata elimu
bora ni moja ya malengo ya chama.
Chama kinawashukuru watu ambao wamejiguswa na
changamoto za ujane na kukubali kujitolea kusaidia. Pia uongozi wa chama
unawashukuru wale wote wanaoendelea kutoa ushauri wao ili kukiboresha, pamoja
na wale wote wanaoendelea kupongeza wazo hili la kuanzisha Chama cha Wajane
Tanzania.
Ili kufahamu mengi kuhusu Chama cha Wajane Tanzania, au
labda ungependa kutoa mchango wako wa hali na mali, ushauri, au wewe ni mjane,
mgane, mtoto wa mjane au una ndugu, jamaa na rafiki wa aina hii, unaweza
kuwasiliana na uongozi kwa simu namba 0716 214 680/0754 366 530, pia
unaweza ukatembelea ukurasa wa facebook wenye jina “Tanzania Widows Association”
Umoja wetu ndio mafanikio yetu!
0 comments:
Post a Comment