Bi Warra Nnko akiwa amekumbatia kitoto kichanga kilicholetwa baada ya mama yake kufariki wakati wa kujifungua
Baadhi ya watoto wakipata kifungua kinywa
Muonekano wa jengo la Shalom Orphanage Center
John shabani akitoa mafunzo kwa watoto
Mwenyekiti wa Chama Cha Wajane Tanzania, akiwa katika hali ya huzuni baada ya kujionea hali mbaya ya baadhi ya watoto walioletwa katika kituo cha Shalom
Hawa ni watoto wanaolelewa katika kituo cha SHALOM! watoto hawa, waliookotwa vichakani hali zao zikiwa mbaya sana, kila mara baba yao mzazi ambaye ni mlevi wa kupindukia, aliwalawiti kwa zamu. Maisha yao yalikua ya kuokota vyakula vilivyotupwa jalalani, huku makazi yao yakiwa ni kulala vichakani baada ya nyumba yao ya majani kuanguka.
Watoto wakisherekea sikukuu ya Christsmass
Wageni mbalimbali hujitolea kufanya kazi za kijamii katika kituo
Moja ya madarasa
Watoto wakisherekea sikukuu ya Christsmass
Wageni mbalimbali hujitolea kufanya kazi za kijamii katika kituo
Moja ya madarasa
Baada ya kuzunguka maeneo mbalimba, hii ni ziara nyingine
ya kutembelea kituo cha watoto yatima
“SHALOM ORPHANAGE
CENTER”!
Mimi na wewe tunaweza.
Jambo moja
nililojifunza chini ya jua, ni kufanya Jambo sahihi, kwa mazingira sahihi, kwa
watu sahihi, na kwa wakati sahihi. Jambo lako, wazo lako, uamuzi wako, mkakati
wako vyaweza kuwa, sahihi lakini si kwa watu sahihi, labda si kwa mazingira
sahihi, lakini pia labda si kwa wakati sahihi.
Inawezekana
umekuwa ukifanya mambo mengi, lakini pia unataka uonekane na watu, upongezwe au
uambiwe asante! Si vibaya, lakini wakati mwingine fanya jambo katika mazingira
ambayo si ya kupongezwa wala kusifiwa bali kwako ni wajibu kama mwanadamu
ambaye uhai wako hujaugharimia chochote.
Moja ya
mambo nilioamua ni kuwaona watu wenye uhitaji haswa tena huko maeneo ya vijijini,
hilo ni jukumu letu sote. Ndio maana baada ya kuzungukia vituo mbalimba vya
watoto yatima Tanzania, ziara iliyoratibiwa na Chama cha Wajane Tanzania (Tanzania Widows Association), moja ya
kituo kilichonigusa sana ni cha SHALOM ORPHANAGE CENTER, kilichopo huko karatu,
kilomita 160 kutoka jiji la Arusha.
Moja ya
vitu nilivyoguswa navyo ni kumuona mama mjane Bi Warra Nnko, akiwa amegeuza nyumba yake kuwa kituo cha kulelea
watoto. Vipo vyumba vya watoto wachanga haswa, wengine wameokotwa wakiwa
wametupwa baada ya kuzaliwa na wengine wazazi kufariki wakati wa kujifungua.
Pia wapo watoto ambao huletwa wakiwa katika hali mbaya, wangine wamebakwa na
kulawitiwa. Nilitiwa moyo kuona hata serikali ya wilaya na hata mkoa huleta
watoto katika kituo hicho.
Vipo vyumba
vya watoto wenye hali mbaya, wengine wanaulemavu wa aina mbalimbali, wengine
wameathiki na ukimwi n.k. Shalom Orphanage center ni kama Hospital, Shule, na
mji wa makimbilio. Pia nimeguswa kuona Bibi huyo ameanzisha miradi mbalimbali
ikiwemo ya ng’ombe wa maziwa, kuku wa mayai na mashamba ili watoto wapate lishe
na afya bora. Ukifika shalom lazima ulie kidogo; lakini cha kushangaza watoto
hao,kuanzia wachanga na wale wanaosomeshwa sekondari wote humwita Bibi Warra
Mama!
Mimi kama
mwalimu wa sauti na uimbaji, nikiwanimeambatana na mwenyekiti wa Chama Cha
Wajane Tanzania na baadhi ya watu, pamoja na kila mtu kutoa kile alichokuwanacho,
lakini pia niliamua kuanzisha mpango wa kuibua vipaji vya watoto.
Wito wangu
kwako, ni kukuomba tuungane kwa pamoja safari hii tena, kwa chochote
ulichonacho tukawaone watoto hao mwishoni mwa mwezi huu wa Novemba. Pia
ikumbukwe kuwa karatu nisehemu nzuri ya utalii wa ndani, utajifunza mengi pale MTO
WA MMBU, lakini pia kutembelea mbuga za SERENGETI, NGORONGORO, pamoja na
kutembelea kwenye misitu na mapango ya mawe wanakoishi waadzabe.
Unaweza
ukaleta nguo, chakula, pesa yako na chochote ulichonacho kisha ukakabidhi
katika ofisi za Chama cha Wajane Tanzania zilizopo maeneo ya kinyerezi.
Kwa
mawasiliano zaidi tupigie: 0754 366 530, 0713778778
0 comments:
Post a Comment