Wananchi mbalimbali wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika banda la rita, wakijifunza mabo mbalimbali hasa yale yahusuyo kuandika wosia na, vyeti vya kuzaliwa na sheria mbalimbali
Labda nikudikeze darasa kwa kwa ufupi
WOSIA
1. Wosia ni nini?
Wosia ni
tamko analotoa mtu wakati wa uhai wake
akieleza jinsi anavyotaka mali yake igawanywe au wapewe watu gani baada ya kifo chake.
2. Nani anaweza kuandika wosia?
Ni mtu
yeyote mwenye umri wa miaka 18 au zaidi
na mwenye akili timamu.
3. Faida za wosia.
-
Kuepusha watoto au mke/mume kunyang’anywa mali.
-
Kuepusha migongano
katika familia, ndugu au jamaa zake.
-
Kuepuka kumrithisha mtu yeyote ambaye kisheria hapaswi
kurithi mali yako.
- Unakupa
uhakika wa maisha bora ya baadae ya warithi wako kulingana na mali ulizo nazo
- Kupunguza
gharama/usumbufu wakati wa kuendesha mirathi.
4. Sababu za kuandika wosia
-
Kuweka
msimamizi wa mirathi na mlezi wa
watoto wako au mwangalizi wa familia.
-
Kutoa
maelekezo kuhusu mali zako kama
upendavyo na kwa kufuata sheria.
5. Wosia unaokubalika kisheria
-
Uwe na wa
maandishi au matamshi
-
Ushuhudiwe
na watu wawili ikiwa ni wa maandishi.
-
Ushuhudiwe
na watu wa nne ikiwa ni wa matamshi.
-
Uwe wosia
usiomnyima mrithi halali mali bila sababu zinazotambulika kisheria.
6. Ni nani mrithi halali kisheria?
-
Mke au
mume
-
Watoto
waliozaliwa ndani ya ndoa
-
Watoto
waliohalalishwa kisheria
-
Wazazi na
ndugu wa karibu ambao walikuwa tegemezi kwa mtoa wosia wakati wa uhai wake.
7. Hali ya mwandika wosia
Anayeandika
wosia ni lazima athibitishwe kuwa ana akili
timamu wakati akiandika au kutamka wosia wake.
8. Mambo muhimu ya
kuzingatia katika kuandika wosia.
· Majina ya wanaonufaishwa
· Orodha ya mali za mtoa wosia na mahali zilipo na stakabathi / hati za
ununuzi / Umiliki wa mali hizo.
· Majina na anuani za msimamizi
wa mirathi na mwangalizi wa watoto
· Maelezo mengine ya kuweka kwenye
wosia.
9.
Ni
wapi wosia uhifadhiwe?
-
Wosia
uhifadhiwe mahali ulipoandaliwa.
-
Kwenye taasisi za dini kama vile kanisa au msikiti.
-
Kwa
mwanasheria yeyote
-
Kwa mtu
yeyote asiyemrithi katika wosia husika na awe na sifa za kuaminika za kutunza
siri.
Hayo ni machache tu kati ya mengi ambayo
yatafundishwa katika viwanja vya mnazi mmoja Dar es salaam, jumanne ya tarehe
23 Juni 2015
Watu
wote mnakaribishwa.
MENGINEYO
KWA watu wengi wa jamii za Kiafrika, mtu kuandika au kutoa wosia juu ya mali
zake, ni kitu ambacho inachodhaniwa ni mkosi..., Pia hudhani kwamba anayeandika
wosia ni mtu anayejichulia au kujitabiria kifo cha karibu!
Ukweli ni kwamba, wosia ni mojawapo ya vitu vinavyosaidia kuilinda familia na
jamii inapotokea mtu aliyeandika wosia huo amefariki dunia. Wakati fulani,
uandishi wa talaka unasaidia sana kusaidia usuluhishi wa matatizo ya kifamilia
kuhusu mali na fedha za marehemu pindi kifo cha mtu aliye na mali akifariki
dunia .
Kwa mujibu wa kifungu cha 2 cha
sheria ya Usimamizi wa Mirathi ya Tanzania, wosia ni tamko la mwisho la mtu
anayetoa tamko hilo, akielezea jinsi gani mali zake zitunzwe au kufanyiwa kazi
pindi atakapofariki dunia. Kwa ajili hiyo, mtu aliyetoa tamko hilo, anatakiwa
kutoa tamko ambalo ni la mwisho katika matamko yote aliyowahi kuyatoa wakati wa
maisha yake juu ya mali na fedha zake zinapaswa kufanywa pindi atakapofariki
dunia. Wosia unaweza kuwa wa maneno ya mdomo na vilevile wosia unaweza kuwa
wosia uliondikwa kwa maandishi. Kati hali yoyote ile, wosia wa mdomo na wosia
wa maandishi unakuwa na nguvu sawa kisheria, ili mradi tu masharti yanayopaswa
kuzingatiwa yakitimizwa.
Hata hivyo, kwa wosia wa maandishi au ule wa mdomo, kuna masharti kadhaa
yanayohitajika kutimizwa kwa wosia huo kuwa na nguvu kisheria. Mtu anayeandika
wosia kimsingi anatakiwa kuwa na mali anayoimiliki yeye binafsi (si ya
anayoimiliki kwa ubia au aliyopewa kutokana na wadhifa wake labda kiserikali au
kampuni). Vilevile wosia lazima uoneshe nia ya mtamkaji kuhusu kutoa mali zake
(pamoja na fedha) kwa watu au mtu fulani na vilevile ndugu msomaji unatakiwa
ujue kwamba wosia utakuwa na nguvu kisheria pale tu ambapo mwandishi/mtoa wosia
huo atakapokuwa amefariki dunia.
Kwa wosia wa mdomo mpaka uwe una
nguvu kisheria, ni lazima ushuhudiwe na watu au kwa maneno mengine mashahidi
wasiopungua wanne na kati ya hao, wawili ni lazima wawe watu kutoka katika ukoo
wake. Hali hii si tofauti sana kwa upande wa wosia unaoandikwa kwa maandishi,
kwani wosia huu ni lazima ushuhudiwe na watu wasiopungua wawili na kati ya hao
mmoja ni lazima awe ni mtu kutoka katika ukoo wa mtoa wosia. Hawa wanaweza kuwa
wajomba, mashangazi, kaka au dada wa mtoa tamko la wosia.
Zaidi ya hayo, wosia hauwezi kuwa na
athari yoyote kisheria kama mtoa tamko la wosia hatatia saini yake aidha kwa
maandishi au kwa kuweka dole gumba katika karatasi yake ya wosia. Hii ina maana
kwamba mahakama haitautambua wosia huo kama hautakuwa na sahihi ya mtoaji wa
tamko hilo. Hata hivyo, wosia hata kama utakuwa na vigezo vyote vinavyotakiwa
lakini kama mtoaji wake alitoa tamko lake akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa
akili au kulazimishwa/kushurutishwa, hii ni mojawapo ya vigezo vya kukataa
kuidhinisha wosia au mirathi kwa mtu yeyote na mahakama. Wosia vilevile ni
lazima umtaje mtu atakayeutekeleza. Huyu ni mtu ambaye mtoa wosia atamchagua
katika wosia wake na ndiye atakayepewa majukumu yote ya kuangalia jinsi gani
matakwa ya mtoa wosia yatavyotimizwa. Ni kweli kwamba mtu anaweza kuandika
wosia na kuufuta wakati wowote na mara zote anazotaka. Sheria haina pingamizi
juu ya jambo hilo.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba
mtoa wosia anaweza kubadilisha mawazo yake wakati wowote ule. Hata hivyo,
wakati wowote mtu atakapokuwa anaandika wosia, ni lazima aandike kwamba wosia huo
ni wa mwisho kabisa kati ya wosia mwingine aliowahi kuuandika. Hata hivyo,
mahakama imepewa uwezo kisheria kutengua au kubatilisha wosia wowote kama
haukidhi vigezo vya kisheria kuufanya uwe halali. Katika hali kama hii, familia
itatakiwa kumchagua mtu asimamie mirathi kana kwamba marehemu hakuacha wosia
wowote kwani wosia wake hautakuwa na nguvu yoyote kisheria. Ikiwa baada ya kifo
cha mtu aliyeandika wosia, kutakutwa wosia mbili tofauti na ulioandikwa siku na
tarehe tofauti, basi wosia wa tarehe ya mbele ndio utahesabika kuwa halali na
si wa tarahe ya nyuma yake. Hapa sheria inatumia busara kwamba mpaka wosia
mwingine uandikwe ina maana marehemu alibadili mawazo yake na ndiyo maana
akaandika wosia mwingine.
Wosia unapata nguvu kisheria pale tu aliyeandika akifariki dunia. Hii ina maana
kwamba, hata kama mathalani, mtoto wa marehemu ndiye aliyeandikwa atarithi
shamba la marehemu, mtoto huyo hatakuwa mmiliki halali wakati mwandishi wa
wosia huo atakapokuwa hai, ila tu pale atakapofariki dunia ndipo mtoto huyo
ataweza kuwa mmiliki halali wa shamba hilo. Kimsingi, ni haki ya mwandika au
mtoa wosia kubadilisha wosia wake wakati wowote autakao. Vilevile ni haki yake
kumpa urithi mtu yeyote atakayekuwa amemchagua katika wosia wake. Hata hivyo,
mwandishi wa wosia ni lazima azingatie watoto ambao ni wategemezi kwake pale
atakapokuwa anaandika/anapotoa wosia wake.
Unafahamu masharti ya Wosia...?
- Mtoa wosia lazima awe na akili timamu.
- Awe ametimiza miaka kumi na nane (18) na kuendelea.
- Uonyeshe tarehe ,mwezi na mwaka ulioandikwa.
- Uonyeshe majina ya warithi.
- Mtoa wosia ahusishe mali zake binafsi na si za mtu mwingine.
- Wosia ni siri wanufaika hawatakiwi kuujua.
- Mtoa wosia lazima aweke saini yake, na kama hajui kusoma na kuandika aweke
alama ya dole gumba la mkono wa kulia.
- Mashuhuda lazima waweke saini zao tena kwa wakati mmoja.