Mheshimiwa Ajnjela Kairuki, mgeni rasmi katika maadhimisho ya kwanza Tanzania, ya siku ya wajane Duniani.
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Angela Kairuki anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya
wajane Duniani.
Tunategemea pia kuwa na
wadau mbali mbali, kama vile viongozi wa serikali, viongozi wa kidini,
wawakilishi wa taasisi mbalimbali za serikali na binafsi, waandishi wa habari
pamoja na wasanii mbalimbali, wamesema.
Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika Juni 23 mwaka
huu, yaani siku ya jumanne, ambapo kimkoa yatafanyika katika Viwanja vya
Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza na waandishi leo Jijini Dar, Mwenyekiti
wa Chama cha Wajane Tanzania (TAWIA), Rose William Sarwatt na katibu mkuu wa
chama hicho, bwana John Shabani, wamesema, siku hiyo itawakutanisha wajane wote
nchini. Katika
maadhimisho hayo pia wataweza kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili
pamoja na utatuzi wake.
Maadimisho hayo ambayo yanafanyika Dunia nzima kwa
hapa nchini yatabeba kauli mbiu isemayo, “Andika
wosia kuepusha migogoro isiyokuwa na lazma”. Yataanzia stendi ya stesheni
hadi sehemu husika. “Kauli mbiu hiyo imekubalika na takrbani ya wajane
wote nchini, kutokana na changamoto zetu kufanana, ikiwemo ya kushuka kwa
uchumi ndani ya familia pindi mume anapofariki,” amesema Sarwatt.
Aidha amesema, changamoto kubwa wanayoipigia kelele
wajane wengi nchini ni uchumi kuporomoka pindi wakiondokewa na wenza wao, hivyo
tatizo hilo pia huongeza idadi ya watoto yatima mitaani.
Mbali na kupata changamoto hizo Sarwatt amesema, uwepo
wa TAWIA umekuwa msaada mkubwa na kimbilio la wajane wengi kwani kimekuwa msari
wa mbele kuwasaidia. Licha ya wajane wengi kuonekana kukata tamaa ya
maisha, TAWIA ilianzisha miradi mbalimbali ya kuweza kuinuana kimaisha ikiwemo
ya kufanya biashara ndogondogo. Na kwamba biashara hizo na michango mbalimbali
imewasaidia kuwapeleka watoto shule pamoja na kujikimu katika maisha yao.
“Tuchukue fursa hii kuwakumbusha wadau mbalimbali
ambao wanaweza kutusaidia, ili tuweze kuwafikia wajane wengine waliopo vijijini
ambao hatuwezi kuwafikia. Pia tunaomba serikali itusaidie kupata takwimu ya
wajane wote nchini, ili iwe rahisi kuwafikia,” wamesema.
Mwisho, watanzania wote wanaalikwa kuhudhuria siku
hiyo, kwani licha ya maadhimisho, Pia, kutakuweo na elimu mbalimbali kama
sheria, afya, uchumi n.k. Pia, kutakuwepo na bidhaa mbalimbali kutoka kwa
wajane.
0 comments:
Post a Comment